NIFANYE MAOMBI GANI KWA SASA?

Wapendwa hili swali linaonesha ubabaifu wa asilimia 100% ?, Linaonesha mtu ni mvivu wa ibada na amekosa direction, Wapendwa Mtumishi yoyote ukimletea hizi swaga anaacha kukupokelea simu na anakutupa anajua biashara hamna hapo kwako.

Watu wengi mnapenda QUICK FIX lakini kuna mambo ya akubali quick fix kutegemeana na muombaji, Kama ajira kama huna vifungo Program moja tu upo ndani ya payroll, Biashara pia, Sababu Mungu kukupa riziki nijambo ambalo yeye ameahidi na Bwana YESU alisema tu muombe MKATE wetu wa kila siku tukiomba, Kuna Mambo yanahitaji MSHIPA kutoboa, It’s not just you ni hiyo entire industry unayo-ombea, Kama MAHUSIANO, AFYA, DELIVERANCE NA UZAO.

Umeomba QUICK FIX, It didn’t work,THEN WHAT? Wengi you tray harder kutafuta another QUICK-FIX, Hujiongezi kwamba Quick-fix ya kwanza imebumaa??.

Quick-fix ya kwanza kuto kufanya kazi ni majibu tosha, THIS ISSUE IS DEEPER! na inatakiwa ujipange upyaaa na ku-reinforce majeshi yako.

 

MTU UMESHINDWA KUVUKA WEWE UNAKAZANA HUYU MTUMISHI KASHINDWA; SASA UNAENDA KWA WATUMISHI WENGINE MNAANZA UPYA, BADALA UKOMAE HAPO HAPO MPAKA MFIGURE OUT KWANINI UNA MZEEKEA HAPO?

NA MTU A-QUALIFY KWAMBA NI MTUMISHI WAKO KIMWILI NA KIROHO LAZIMA UWE UNALIPA ZAKE KWAKE!, NI SHERIA MUNGU NDIYO KAIWEKA KWAKO NA WATOA HUDUMA YAKE!, SO HATA KAMA MIMI NIKIPOKEA ZAKA YAKO NIKA ILA NA NIKAGOMA KUKUSAIDIA UNA HAKI YA KUNISHTAKI KWA MUNGU AKANIWAJIBISHA.

HATA IKITOKEA NIKASHINDWA KUKUSAIDIA OF WHICH KUGOMA NI VOLUNTARY TU KWAMBA IPO NDANI YA UWEZO WANGU ILA NDIYO SITAKI KUSHINDWA NI KWAMBA IPO NJE YA UWEZO WANGU, WEWE UKILALAMIKA KWA MUNGU ATA NIONGEZEA UWEZO WA KUKUSIADIA, MWANZO NILISHINDWA GHAFLA NITAWEZA!

MIMI KUNA ISSUE MTUMISHI ALISHINDWA KUNISIADIA ILA HAKUSEMA AKAWA ANA BUMBA-BUMBA MPAKA MIMI NIKAISHTUKIA LIVE KWAMBA HAPA ANA BET!

Nika muomba Mungu kwamba amfunulie Mtumishi kama kunifunulia mimi sitaweza ku-discern vizuri na kweli bwana after a week Mtumishi akaniambia njoo nimejuaa shida iko wapi!; Kama hulipagi zaka kwa mtu yoyote ujue ni MUUMINI HURU, You are responsible for yourself sio kitu kibaya, ni COST SAVING lakini itabidi sasa uwe VERY HARDWORKING KUJIHUDUMIA ili uwe kuhani wako mwenyewe.Uweze KUMSIKIA Mungu mwenyewe na kumuelewa, INAWEZEKANA BUT IT DOESN’T COME EASY!

Wewe mtu humpi zaka hata sh 10 /=  ya zaka kitu ambacho Mungu mwenyewe ameagiza, alafu unakuwa mkali kama pilipili, Hujui Mtumishi anakula wapi wala ana lala  wapi wala wanae wanaishije mjini alafu unataka kumpelekesha ? Na seriously Unahisi atapeleke-sheka?, EVERY SAINT HAS A PAST, Ndiyo utagundua kabla ya kuwa Mtumishi alikuwa kijumbe wa uswazi!

MTU UNAKUTA ANANIFOKEA KABISA NIPO HAPA SIKU NYINGI!, SO? MBONA SIVUKi? HUNI SAIDII HUANGAKI NA MIMI?, NAMUULIZA SWALI MOJA ? MIMI NI MTUMISHI WAKO ? UANIPAGA ZAKA ? HAPA SASA NDO UKALI UNAISHA  NA SABABU ZA KWANINI HALIPI ZAKA ZINAANZA!

ZAKA KAMA ZAKA NI NGUZO KUBWA SANA YA IMANI ZOTE ZA UKRISTO NA UISLAMU, NI AGIZO LA MUNGU, SASA WEWE PICHA LINAANZA UNA KIUKA KWA MAKSUDI AGIZO LA MUNGU ALAFU UNATAKA MUNGU HUYO HUYO NA MTUMISHI WAKE ULIE MTOA DRY WAENDE ABOVE AND BEYOND FOR YOU! SIO KWELI, UNAWEZA KU PLAY VICTIM CARD UKA MMANIPULATE MTUMISHI LAKINI MUNGU HUTO MSOGEZA HATA NUKTA.

KUNA WAKATI TULIENDA KWA WATUMISHI NA MWENZANGU, AKASEMA WATUMISHI WANAPENDA SANA PESA TUWADANGANYE HATUNA KAZI WATUSAIDIE BURE, JEEZ! MIMI NILIONA NI TOTAL NONSENSE, MAANA YAKE MUNGU NDO ANASAIDIA SI TUTAJIDANGANYA WENYEWE, UNAWEKAJE MSINGI WA UONGO UTEGEMEE MATOKEO YA KWELI NA UHAKIKA? NILIMUONA HANA AKILI.

WAPENDWA NDIYO YALE YALE MTU ANATOA ZAKA YA 50K, MAMBO ANAYOTAKA MUNGU AMFANYIE AFIKE MSHAHARA 6M, MANAKE HAPO MSHAHARA NOT LESS THAN 4M ILA ANALIPIA ZAKA ONLY HIO LAKI 5, ILA BARAKA ANAZOTAKA ZA 4M, SASA HUU NI UBATILI MBELE ZA MUNGU MKUBWA SANAA NI BORA UKALA ZAKA OYTE UKAPIGA KIMYA KULIKO KUWA MNAFIKI.

Mimi kuna kipindi kikubwa cha maisha yangu nilikuwa NAKULA ZAKA YOTE uso mkavuu, Na nilimwambia Mungu sijapata Mtumishi sahihi wa kuniongoza! So najiongoza mwenyewe! NISAMEHE, Siwezi mpa zaka mtu hanipi huduma! Mpaka Siku nikapata Mtumishi alie ni vusha Babeli na namlipa zaka constant, Nipate natoa hiyo, nisipate natoa hiyo hiyo. KUDADADEKI!

FANYENI MAMBO WITH CLEAR UNDERSTANDING, MIMI NILIGOMA KULIPA ZAKA KWA UELEWA KAMILI NIKIJUA NINI NAFANYA KWA KUJUA MAANDIKO YA KITABU CHA WALAWI, NA OFCOURSE ILIKUWA MAKOSA MAKUBWA NDIYO MAANA NILITUBU KABISA ILA NIKAMPA MUNGU HOJA ZANGU ANIREHEMU.

SASA TUJIFUNZE KWA CAIN!CAIN HAKUWA NA NIA YA KUTOA SADAKA AKAJILAZIMISHA BILA KUWA NA CLEAR UNDERSTANDING YA ACTIONS ATAKAZO FANYA MBELE YA MUNGU, BORA ANGE GOMA KUTOA ILE SADAKA KABISAA AKA MUTE, MAYBE ANGE ADHIBIWA VICHACHE! LAKINI JARIBIO LAKE LA KUMPA MUNGU MAKAPI LILI BACK-FIRE BADLY.

SASA KWANINI UMCHOKONOE MUNGU WAKO KAPOA ZAKE MBINGUNI? KULA TU HIO ZAKA NYAMAZA PIGA KIMYA KULA NYAMA NYAMAZAA WANA KWAMBIA WATOTO WA MJINI, SASA ZAKA UME IMANGA NA BARAKA ZA MUNGU KWA WATOA ZAKA UNA TAKA TENA UNAFISISIO UBATILI HUO?, MUNGU SIO MWEPESI WALA HU-MMUDU!

Kuna watu wanajijua zaka silipagi Lakini wanajipambania, Wana gonga Program wenyewe tu! Ikikataaa anarudia hata mara 3! Ya 4 anakuuliza TICHA hili swala nimefanya hii Program Mara 3 lakini nimepata progress hii!, Namuuliza maswali ya papo kwa papo kama kweli? Then una mwambia hii issue kubwa kuliko ulivyo expect, Una vifungo 1,2,3 ndiyo vinaweza sababisha usipate matokeo. Hapo anainuka anaenda kupambana navyo mbele kwa mbele, Consultation is free sababu ina takeless than 10 minutes.

KUJUA TATIZO IS JUST THE ICING ON TOP, NA MTUMISHI YOYOTE ANAWEZA KUKWAMBIA BUREE KABISAA, HATA WEWE UKITULIA NA KUSIKILIZA MAHUBIRI UNAWEZA KU-SELF DIAGNOSE ! ISSUE NI THE ICE BERG WITH IN HILO TATIZO,  LALALA CHANZO CHAKE WHY YOU?, WHO IS BEHIND? WHY? MNA-LISOLVE VIPI? MNAWEKAJE ULINZI LISIRUDI? ASIKUDANGANYE MTU HAPA SASA NDIYO DINI NA IMANI ILIPO, NI MTITI MTU  MMOJA (1) UNAWEZA  KUHANGAIKA NAYE HAMNA HAMNA MIAKA  MIWILI (2) AU MITATU (3) NDIYO KUPATA VICTORY YA KUONEKANA NA HAPO AWE NA NIA SANAA NA MTIIFU KWELI-KWLEI!

NDIYO MAANA WATUMISHI WENGI NA DINI NYINGI ZINA FOCUS NA KUENEZA INJILI TUUU BASI MATATIZO YAKO DILI NAYO MWENYEWE, ROMANS, LUTHERANS AND COMPANY! HAKUNA MAMBO YA DELIVERANCE WE KULA NENO TU MATATIZO YATAISHA YENYEWE, KAMA KWELI WAUMI NI WAKI CONSUME NENO LEVEL INAYO TAKIWA IT IS 100% TRUE DELIVERANCE ITA HAPPEN AUTOMATIC! WAKU-CONSUME NENO SANA WAKO WAPI ?

Wapendwa hizi ICEBERG kudeal nazo sio ngumu kama mtu ana akili timamu na nia, Shetani sio mgumu ila mioyo ya watu ndiyo migumu na ndiyo maana mimi mtu halipi zaka SI DEAL nae kabisaaa, MTU MUNGU ANA MFANYIA JEURI NA KIBRI cha waziwazi ana puuzia maandiko mchana kweupeee itakuwa mimi MTU kweli ? Lipa zaka upate Usharika na Mbingu zitusaidie sasa kuyeyusha hillo barafu hataki, Unataka  tugande  wote   au?, HOLYSPIRIT FORGIVE ME!

HATA KAMA ZAKA UNALIPA NA TUMEANZA DELIVERANCE  AU HULIPI UNA SELF DELIVERANCE PIA HILI LINAKUHUSU, DELIVERANCE PROGRAM NYINGI NI SIKU 30 LAKINI HIZO 30 NI PILOT TU, DELIVERANCE KU-MANIFEST INAWEZA KUCHUKUA HATA MIAKA MIWILI (2) HIZO SIKU 30 NI ZA KUEPENA COMPANY TU, KAMA ISSUE NI NDOGO ZITATOSHA KUMALIZA! KAMA HAIJAISHAAA USIACHIE SIKU YA 30! MKEKA UNAO ENDELEA KUJIDUNGA MDOGO MDOGO UTAFIKA.

MIMI KUNA WATU WA ZAKA TUMEANZA DELIVERANCE AUGUST WENGI TAYARI WAPO KAZINI,WAMEPATA WATU VICTORY IMEPATIKANA VERY FAST SABABU KABARAFU KALIKUWA KADOGO, MOTO KIDOGO KWISHA.

Wengine WAME DHOOFIKA! Wameishi na issues muda mrefuuu sanaa,Issue sio kubwa wala nini, ila mioyo yao imedhoofika na imani ime wakakukaaa kwa hio mapigo wanayo toa vitani ni very WEAK! Hawa wanahitaji tu KUJIPATA kazi inamalizia, Inatakiwa tu kuwajengea imani mda tu ndo sijapata! Ila I can see VICTORY!

Alafu  kuna PASUA  KICHWA, Lalalala Deliverance  kwanza Mwezi wa wa 8, KASHA ACHA ALAFU ANANIULIZA MIMI TUNAFANYAJE ?, NILITOA MPAKA PRAYER POINTS MBINGU ZINA NIONALENGO LANGU MTU APIGE MZIGO MPAKA DECEMBER 31, TUONE KAMA SHETANI KATUNISHA MSHIPA FULL  AU KALEGEZA, KUTOKANA NA NITAKACHO KIONA NITAJUA TWENDE VIPI, MTU KAACHA PRAYER POINT SEPTEMBER, ANA BALUZA FREE MPAKA DECEMBER! SASA JAMANI UTASEMA MBINGU NDIYO ZINA SHIDA?, MIMI UANURY NIKIJA KWENYE FOLLOW-UP FILE ZENU NINAZO NIKIONA MIEIZ VOTE UNA BALUZAAAA NAONA HUNA NIA, NAKUTEMA.

KUNA MDADA HUMU HUMU ALIFANYA DELIVERANCE YA JANUARY YA SIKU 30 HAKUONA CHOCHOTE, HAKUPATA HATA IMPERTATION MOJAAA! SISI TUME BWAGA YEYE KAUNGA yaani kakomaaa na ile deliverance kila siku kwa miezi 6, Haoni chochote ila Day in day out anapiga mzigo! Issue yake ilikuwa ndoa, Hatongozwi kabisa, Na ni mzuri balaaa, Nimeona profile!

Mwezi wa  sita (6) akaanza kuona maono, Mama yake wa kambo anachukua pedi yake anaipeleka kwa mganga, Mama anafukia vitu walipokuwa wanaishi, Alimuibia chupi akaipeleka kwa mganga, Yani alimrogaaa hasa, Huyu Binti hana Mama maskini amelelewa na huyo Mama wa kambo, Yupo Ulaya sahivi, Lakini mama wa kambo yupo huku bongo.

Akaendelea kuomba mpaka akaja kupata maono malaika,wame mfata yule mama na kumuhoji kwanini ulifanya  hivi, anasema nilikuwa SITAKI AOLEWE, haya fukua, Akafukua kote na kuchoma, Anaulizwa hamna vingine? Anajibu hamnaaa, Ndio finally sasa VICTORY imepatikana! Ameanza kutongozwa sasa.

Na Roho Mtakatifu anatumia sasa kuombea wengine, She keeps getting visions za vifungo vya watu wengine na jinsi gani awaombeee na kuwa fungua, Mungu anaendelea kumtumia sana, ALIFANYA TU ILE DELIVERANCE PROGRAM YA JANUARY MIEIZ  SITA (6)  PEKE YAKE.

Badala ya kukaaaa unauliza ufanye maombi gani? Acha ubabaifu fanya maombi yoyote yatakayo kubariki na Uwe na consistency, Rudia hata mara  tatu (3),  Fanya na program zingine tumia muda wa kutosha ku-deal na hio changamoto!

Wapendwa ili useme umefanya program usiwe umetimiza ratiba, mHakikisha ume-elewa kwanini Umefanya hio Program, ili lengo kukujenga nini?, Maandiko gani umeishi  nayo  baada ya Program? Clear understanding imepatikana kwenye hilo eneo ? SASA TO REACH THIS LEVEL OF UNDERSTANDING INABIDI UFANYE PROGRAM HATA MARA KUMI (10).

WATU WENGI MMEFANYA MTU SAHIHI LAKINI MPAKA KESHO HAMNA CLEAR UNDERSTANDING YOYOTE WALA HAMKUNGAMUA HATA PASSWORD MOJA KUTOKA ILE PROGRAM MPAKA KESHO, NDIYO MAANA HAMJAPATA WATU SAHIHI,  MLI BALUZA BALUZA TU MKAINUA ILA WALIOPATA CLEAR UNDERSTANDING WALIPATA WATU SAHIHI WAKACHAGUA MACHAGUO YAO.

ILE PROGRAM ILITOA PASSWORD ZA KWANINI HUPATI MTU SAHIHI?, ILITOA PASSWORD YA KUDEAL NA NGUVU ZA GIZA NYUMA YA WEWE KUKOSA MTU SAHIHI ONE BY ONE, IKATOA PASSWORD YA KU CREATE UNABII WA HARUSI YAKO NA KUUSIMAMIA UTIMIE, KURUDIA UKIWA NA AKILI TIMAMU SIO UJINGA.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
× IT Help Desk