
“BEHOLD I WILL DO A NEW THING”
Isaiah 43:18–19
18 “Remember not the former things, nor consider the things of old. 19 Behold, I am doing a new thing; now it springs forth, do you not perceive it? I will make a way in the wilderness and rivers in the desert.”
Isaya 43:18–19
“Msiyanganganie mambo yaliyopita, wala msifikirie vitu vya zamani. Tazameni, mimi ninafanya kitu kipya. Kinafanyika sasa hivi, nanyi mtaweza kukiona. Nitafanya njia nyikani, na kububujisha mito jangwani.”
Achaneni na mambo yaliyopita aaa!
Mungu anataka utazame, ufocus, uone kwamba anataka kufanya jambo jipya kabisa kwenye maisha yako. Brand new! Sio ku-edit yale ya zamani au kupaka rangi same old bullshit. Jambo jipya kabisa. Na hataki kulifanya kwa siri; anataka kulifanya hadharani lionekane. Sio kiroho bali kwa macho.
Na jambo analoongelea hapa sio jambo dogo. Sio jambo la wasiwasi au la kawaida. God intends to go all out kwenye hili jambo jipya analotaka kulifanya maishani mwako.
Isaiah 43:19
“Behold, I am doing a new thing; now it springs forth, do you not perceive it? I will make a way in the wilderness and rivers in the desert.”
Achana na Swahili version, imejikoroga. Pambana na Muingereza.
“I will make a way in the wilderness and rivers in the deserts.”
Kwenye Kiswahili wamekoroga translation: mito nyikani na njia jangwani, wakapoteza maana kabisa. Hapa nabii Isaya specifically alimaanisha Mungu anataka kufanya jambo lisilo la kawaida. Jangwa na mto ni vitu tofauti kabisa. Jangwa ni ukame; maji ni shida mpaka shida tena. Sasa Mungu anasema anataka apitishe mito. Sio mvua, sio chemu chemu. Mito! Na mto ukishapita maana yake hapataitwa jangwa tena.
Mungu anataka kuling’oa hilo jangwa kwenye maisha yako kwa kupitisha mito, maana yake sio mto mmoja.
Kama umekulia mkoani, specifically vijijini, unajua nyikani maana yake ni msituni, hakuna njia. Miti imeshonana, kupotea ni dakika tano. Lazima uwe na mtu mzoefu au utumie devices kama Google Maps na trackers. Wilderness maana yake hakuna njia wala mpangilio.
Mungu anakwambia atapitisha njia za kutosha kwenye hiyo nyikani. Na sehemu zikishapita njia, maana yake it is no longer wilderness. Civilization itakuja tu kwa kasi.
Mungu hapa he is not playing small at all. He is going all out for you, doing the extraordinary. He wants not only to do a new thing, but also that thing to be mighty. Na hajamaliza; anataka hilo jambo lichipue na lionekane kwa macho, sio mambo ya rohoni. Macho kwa macho tulione. Na lazima ulijue wewe kiumbe mzito uliefanyiwa. Hakuna 50/50 wala coincidence.
Kila mtu anataka hili jambo jipya. Mwaka mpya mwenza wake mambo mapya. Lakini kila mwaka unaanza kwa matumaini na tarambe kama zote, mpaka jana December 31. Mungu amesema na imeandikwa, lakini usipokuwa makini hutoliona hata jambo jipya, hata la zamani kukamilishwa.
Mambo yanayosababisha Mungu asifanye jambo jipya kwenye maisha yako:
-
Focusing on the past.
Huwezi kuwa unataka Mungu afanye jambo jipya wakati akili yako yote imeganda kwenye mambo ya zamani. Kukomaa na past, iwe nzuri au mbaya, ni hatari. Past nzuri inaweza kukufanya complacent; past mbaya inaweza kukufanya uishi kwenye lawama.
“Remember not the former things.”