HUWEZI KUKABILIANA NA UONGO WA SHETANI BILA KUJUA UKWELI WA MAANDIKO

Mpendwa watu wengi wanakuja kwa mama nina matatizo, hata mimi najua una matatizo laasivyo usinge hangaika na  issue sio hilo tatizo ila issue ni kwanini likupate wewe ? kwa sababu Mungu wako ni mdogo sana ndani yako. Mama Mimi nina  miaka arobaini (40) sina Mume, sina familia! Sawaa! Ukitatua chanzo cha wewe kuwa hivyo at 41 everything will be history, Ukija na akili timamu hizo past yrs hatutaweza kuokoa but God  can surely change your future!.

Kama Mungu ni mdogo ndani yako na UNAONEWA na nguvu za giza, way out ni kumuongeza Mungu ndani yako! Lakini wengi wenu hamtaki kutubu tatizo mnapenda PANADOL!

Wewe mtu huna injili hata moja (1), hujui lolote, Mtumishi mbabaifu atakwambia NJOO TUOMBE! Mkiomba dakika 20 haziishi, anakwambia MAMBO YATAKUWA MAZURI, Unaacha laki mwenyewe kiroho safiii, Baada ya miaka  miwili (2) ndiyo akili zinakurudi una  miaka arobaini na tatu (43) workdone =O, Ukirudi Mtumishi anaanza kuku kwepa.

Sasa hapo UMEDANGANYWA au UMEJIDANGANYA mwenyewe? KWELI TATIZO LA MIAKA 20 LITATULIWE NA MAOMBI YA DAKIKA 20 KWELI HATA KAMA ULIFELI MATHS?

Mtu ananiambia Mtumishi NIOMBEEE WEWE tu mimi muda sina, Mimi ninaye ingia madhabauni muda mmoja na wanga huu usiku wa manane, wana nishangaaaa kwanza, Yaani kitu ushindwe kujifanyia, uamini kabisaa Mtu atakufanyia kwa moyo kuliko ambavyo ungejifanyia? Tunarudi pale pale MNAJIDANGANYA WENYEWE.

Yesu alitatua matatizo ya muda mrefu kwa dakika chache, Ni kweli lakini alimtatulia nani? Wengi walikuwa Wayahudi konki na wanaijua TORATI nje ndani, Sheria ya Musa ili lala mahala pake, Kwa hiyo YESU alichofanya ni KUKAMILISHA MAANDIKO kwa kuya unganisha hence on the process ALIFUNGUA PASSWORDS za ku deal na shetani na kumshinda, Hata watu wasiokuwa wayahudi walipo taka msaada wa YESU ilikuwa ngumu kuwapa, KWA SABABU TORATI WAS NO IN THEIR HEAD.

The fact shetani kakufunga eneo lolote la maisha yako ujue kuna ukweli hu-ujui au una-ujua nusu haujakamilika NA ILI WEWE UVUKE PERMANENTLY INABIDI UUJUE HUO UKWELI NA NDIYO UKUWEKE HURU!, Mpendwa unaweza kuji-uliza UKWELI GANI? Ukweli gani UTATA tegemea ni UONGO gani shetani alio-kufunga nao, Ukweli tu uki-ujua ndiyo itakusaidia ku-overcome uongo wa shetani ulioishi nao muda mrefu kwa miaka 40 hadi 50, Chezea shetani wewe kwa uongo wenye viwango!, Mfano mimi tatizo kubwa nalo deal nalo na  AGE GO NI KUJIKATIA TAMAA, Mtu anaona kufika 40 bila ndoa hilo swala ndiyo limesha shindikana kabisaa, KIVIPI SASA ?

Kwamba kwa sababu  uko na miaka arobaini (40) ,Shetani ndiyo ameshika mamlaka ya Mbinguni ? Au Mungu amesha zeeka ndiyo basi tena ?  Yani hizo 40 years zako kwenye ulimwengu wa Roho means ABSOLUTELY NOTHING na sana sana zina washangaza GIRL WHERE WERE YOU ALL THIS TIME ?

Una kwambia mtu mpaka umefika umri huu kuna sehemu yule muovu kakushika, KUNA UKWELI HUUJUI! Kinatakiwa kwanza USOME INJILI ZOTE, MPOKEE YESU, OKOKA, BATIZWA KWA ROHO! PROCESS YOTE HII NI KUMUONGEZA MUNGU NDANI YAKO NA KUKU-EQUIP KUPAMBANA NA SHETANI UJIWEKE HURU NA UONGO WAKE.

MTU ANAONA NI TOO MUCH WORK,  ANATAKA YALE YALE MAOMBI YA DAKIKA 20, BORA YAWE WELL REFERENCED, KWAMBA KWA ANDIKO  FLANI NA DECLARE KITU FLANI!, LAKINI YALE YALE ACCAPELLA AKA DUA LA KU-BET! MTUMISHI ANATUMIA UTUNZI WAKE BINAFSI UFUNGUE POCHI HILO CHAP-CHAP MAANA ANAONGEA  UNAVYOTAKA KUSIKIA! UNAVYOTAKA NA YEYE NDIYO ANATAKA.

ACCAPELLA HIZI ZINA BOOST IMANI SANAA ILA KWA MUDA MFUPI SANA, SHETANI ATAKUWEKA TU SAWA, MAANA YULE NDIYO PRINCE OF THIS WORLD! UMEAMBIWA MAMBO YATAKUWA MAZURI NDIYO KWANZA UKIFIKA NYUMBANI TU PICHA LINAANZA UNAKULA  KIBUTI CHA NGUVU HUTAKIWI DADA NENDA MWANA  KWENDA, UNAUMIA KINACHO KUUMA HUELEWI NI  KIBUTI AU ILE LAKI ILIYO ENDA MADHABAUNI HUNA UHAKIKA.

Laiti kama ungesoma INJILI Kama nilivyokwambia dhoruba ikija unajua tu, huyu mpuuzi shetani tu na hila zake, Hana lolote, Hata akudanganye vipi kwamba UNASHINDWA wewe una UHAKIKA MAISHA YA USHINDI KATIKA KRISTO NI LAZIMA, Hata ionekane unashindwa vipi unajua Mungu atafanya Njia pasipo na Njia, NA THIS IS THE KIND OF ATTITUDE YOU NEED TO WIN SPIRITUAL BATTLES! Sababu kiukweli mashambulizi ni FATAL sana.

Kama huna neno ndani yako, na imani yako kwa Mungu sio ya kusua sua HUTOBOI kwenye uongo wa shetani, Mjinga game ya uongo anaiweza!

MIMI NILIWAAMBIA NIMEMALIZA MWAKA NA NOTICE MBILI (2) NA SIKU STUKA, WALA SIKU BABAIKA KWA SABABU NAJUA MUNGU NDANI YANGU NI MKUBWA SANAA KUBABAIKA NA ENEO A BIASHARA, NILICHEKA TU NILIVYO PEWA!

JUZI WENYE NYUMBA WAMEJITEKENYA WENYEWE NA KUCHEKA WENYEWE WAMESEMA WEKA MPUNGA TUNAENDELEA KODI ILE ILE! SIKUTAFUTA ENEO LOLOTE, NILIKUWA NA UHAKIKA NITAONDOKA HILO ENEO SIKU MUNGU MWENYEWE AKIONA SASA IMETOSHA NENDA SEHEMU INGINE NA WEWE NAWE HUJA JENGA HAPO

Ukubwa wa Mungu ndani ya mtu hai ongezeko kwa WIFI au BLUETOOTH, Ni kwa KUMJUA MUNGU ZAIDI NA UKIMJUA MUNGU KADRI ALIVYOJIFUNUA NI RAHISI SANAA KUMUAMINI HATA MAZINGIRA YASIPO MUAMINISHA.

WAPENDWA NI NGUMU KUMUAMINI MUNGU USIYE MJUA AU UNAEMJUA KWA JUU JUU! SHETANI AKIJA KUTIKISA MISINGI YA IMANI YAKO  HUTOBOI YAANI NDIYO ILE UMEFANYIWA SASA MAOMBI YA DAKIKA 20, UMETOA SADAKA YAKO YA KILO NZIMA, MIEZI 8 HUJATONGOZWA HATA IMANI INAANZA KUSHUKA YENYEWE, MMMHHH! MTUMISHI FAKE YULE NISHA CHUNWA LAKI KWEUPE.

MPENDWA MTUMISHI SIO FAKE WALA MAANDIKO ALIYOTUMIA SIO DHAIFU WEWE NDIYO MBABAIFU! MCHANGA KWENYE IMANI, HUJUI HATA PROPHETIC DECREE INA THAMANI GANI YAANI NI KAMA MBUZI KUMILIKI PASSPORT YA KUSAFIRIA WAKATI HANA UFAHAMU WA KWENDA POPOTE.

Laiti ungesoma maandiko kidogo ukajua thamani ya Prophetic decree, ungakufa nayo Mimi mara nyingi watu wananiambia nilipewa unabii nitaolewa lakini hamna kitu, Nili amina yule ndio wa kwangu nikapata mpaka ishara lakini ndiyo kaoa juzi!

YALE YALE YA KUWA UNAUJUA UKWELI NUSU NA NUSU AMBAYO NI VITAL YA HUO UKWELI HUNAAA! SO HAUTAWEZA KUKUWEKA HURU, Sawa unajua kuna prophetic Decree! JE UNAJUA CHIMBUKO LAKE ? WAPI KWENYE MAANDIKO REFERENCE YA HII DOCTORINE IPO?, UKIJUA ILIPO ISIPOTIMIA MAANDIKO YALIWEKA WAZA UDAI VIPI MPAKA ALICHO TAMKA KITIMIZWE, IF YOU KNOW YOU KNOW HAPO HUDEAL TENA NA PROPHET UNA DEAL NA MUNGU OFFICIALLY KWANI PROPHET ASHAKUPA GO AHEAD!

UBABAIFU AU UHAKIKA WA MATAMKO YA KINABII KUTIMIA AU KUTO TIMIA  KWA KIASI KIKUBWA INATEGEMEA NA MAPOKEO YA ALIYE TAMKIWA, KAMA HAMDUDU HAMDADA VITA TAMKWA NA VITA YEYUKA KAMA UPEPO! KAMA KONTAWA WA MAANDIKO NDIYO KATAMKIWA LITATIMIA MPAKA NENO LA MWISHO, MAMBO YOTE YATAPITA LAKINI NENO LITASIMAMA AU SIYO WANANGU?, LINAACHAJE?

Juzi baba yangu wa kiroho kaniambia Kaota biashara yangu imeneemeka, Kanipa huo unabii Mimi mpaka ndoto zangu binafsi siziamini kabisa, Lakini za Baba Mtumishi nazi-amini 100%! kwa sababu alishafatwa na mtu wa Mgodi, anachimba hapati!

Geologist alimwambia achimbe kulia! Mtumishi akaota achimbe kushoto, Akachimba kushoto alipata madini hatari, Na hakunipa Baba hata senti tano kupande vijukuuu vya Yuda ni vingi. UNABII UTATIMIA  LABDA KAMA SIO MIMI NILIYE PEWA.

KUEGESHA MAMBO NA KUJARIBU KUFANYA MAMBO MAKUBWA KIIMANI BILA MSINGI WA NENO UTAPATA DEPRESSION YA DINI!, LEVEL YA NENO IKIWA KUBWA NDANI YAKO LIKE UTAKUWA NA UFAHAMU WA MAANDIKO YA KUTOSHA MAMBO MAGUMU YATAAANZA KUWA MEPESI SANA KWAKO!

KAMA HILI LA NOTICE KWANGU NAJUA BWANA YESU KAFUFUA MPAKA WAFU, BIKIRA KAPATA MIMBA, YEYE YESU KAPAA KWENDA MBINGUNI, MUNGU ALIGAWA MTO AKAFANYA NJIA ITAKUWA KA ENEO MIMI MJA WAKE KUFANYA BIASHARA? TENA KODI NINAYO? AAH! KWA MUNGU NINAE MJUA NI VITU VIDOGO SANA.

Mtumishi mimi na 40 na watoto wa 3 nitapata mtu wa kunioa kweli? Sasa mtu umeshathibitisha ji- uzazi unalo jingi na la kutosha kwanini ukase mtu?, Ukinyoosha njia zako na kuongeza level ya ufahamu wakojuu ya Mbingu utapata watu na Utachagua, Ukiendeleza UBABAIFU mtaka na shetani kudanganyana kwamba ushazeeka wewe bwana wewe badala ya kuzingatia kuwatafutia wanao wake kwa waume Unajiwaza wewe kweli upo serious? Uki-wauliza wanao kama walikaaa kikao na shetani, watakwambia Mama umri huo kuolewa si uchuro, We tulia tukuletee wajukuu ule.

UBAYA WA SHETANI UONGO WAKE ANAUSEMA KWA WATU WAKO WA KARIBU SANA SANA, IT COULD BE YOUR OWN CHILDREN, YOUR PARENTS, YOUR HUSBAND YANI BILA MUNGU MKUBWA NDANI YAKO HUTOBOI.

NAKUMBUKA NILIKUWA NATAMANI KWENDA MASTERS JUST A YOUNG GIRL, NA MAMA ALIKUWA ANA HELA ILA AKANIAMBIA WAZI WAZI PESA ZA KUCHEZEA MIMI KUSOMA MASTERS YEYE HANA, TENA NIFUTE KABISAA HILO WAZO KAMA DEGREE HAIJANISIADIA ITAKUWA MASTERS ?, SHE WAS LEVEL 10 RUDE MPAKA NIKAJIULIZA WAS I ADOPTED OR SOMETHING? LAKINI NIKAJIAMBIA SHETANI NI MUONGO, MUNGU ATANIFANYIA NJIA PASIPO NA NJIA, KIUKWELI NILIUMIA KAMA MWAKA MAANA DADA YANGU ALIKUWA ANAFANYA MASTERS NA ANALIPIWA NYUMBANI NA MY COUSINS NAO WANAFANYA! SHETANI NI MUONGO NYIE ACHENI, MMH!

BAADA YA MWAKA WA MAUMIVU LAKINI  I NEVER GAVE UP! MIPANGO YANGU ILIKUWA PALE PALE NA IMANI YANGU KWA MUNGU ILIKUWA THABITI KWAMBA KAMA MUNGU AISHIVYO NITASOMA MASTERS! KIVIPI? SIJUI YEYE ANAJUA BWANA!

SIKU SINA HILI WALA LILE NIKAKUTANA NA RAFIKI YANGU AKANIAMBIA KUNA SCHOLARSHIP YA MASTERS ANAFANYA YEYEE NA WAMETOA TENA, SIKUTAKA KU-APPLY, AKANIKOMALIA MPAKA NIKA APPLY! NIKAPATA SPONSORSHIP! NA ILE MASTERS TULIKUWA TUNALIPWA UNONO, MAMA ANAJICHEKESHA CHEKESHA TU MPAKA KESHO KWENYE HILO SWALA! MIMI NAJUA NI SHETANI TU ALITAKA KUNIDANGANYA KUPITIA MDOMO WAKE AND GOD CAME THROUGH FOR ME!

SHETANI ANAVYO KWAMBIA HUTO OLEWA, HUTO PATA KAZI, HUTO PATA FAMILIA, HUTAPONA HAYO MARADHI, HUTAPATA HIYO SCHOLARSHIP NI UONGO MTUPUUU!

SOMA MAANDIKO NA SOMA INJILI ZOTE NNE (4) ILI UWEZE KUJIZA TITI KUKABILIANA NA UONGO WAKE, MTU ANAWEZA KUKUOMBEA VYA UWONGO NA KWELI LAKINI UKIFIKA MUDA SHETANI AKAKUWEKA KWENYE MIZANI YAKE HUTO CHOMOKA KWA MAANA SHETANI UTAMSHINDA KWA HOJA YA “IT IS WRITTEN ” NA UJUE NINI WAS WRITTEN NA WAPI UKAPATA MESSAGE GANI?

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
× IT Help Desk