Imani Inayozaa Matokeo, Sio Maneno Pekee
Yakobo 2:17
Vivyo hivyo, imani peke yake bila matendo imekufa.
1. Andika Malengo Yako Na Uyabidhi Kwa Bwana
Usilete ujua-ji kwamba lengo langu nalijua sio lazima kuandika. Huo ni ubabaifu! Andika kwenye diary, na kila ukiomba shika diary yako iombeeee kama unapeleka upako kwenye malengo. Kila ukiomba ndani kwako chukua sadaka unaiweka kwenye page ya maombi hata mwezi mzima unaiombea na kuyaombea malengo. Afu ndo unaitoa sasa.
2. Weka Ratiba Za Ibada
Wengi unaweka malengo page 20 afu basi! Sasa sijui yatajiombea. Be practical! Weka muda wa ibada kila siku, hamna hamna kwa jitu vivuuu hasaaa mara 2 kwa siku: asubuhi na jioni. Na usiwe na nadharia nyingi — action o!
Kama ratiba yako ni kusali asubuhi na jioni, basi ukifumbua macho cha kwanza decree na ku-declare neno lako la mwezi. Kabla hujashika simu wala kwenda kukojoa. Na session zako zigawwe kabisaaaa: asubuhi kusifu na kuabudu, na jioni kusoma Neno na kushukuru.
Ainisha miezi 12 utasoma vitabu gani, with minimal ya vitabu 2 kwa mwezi kwa jitu vivuuu ambavyo vita-average vitabu 24 kwa mwaka. Almost robo ya Roman Bible na zaidi kidogo ya robo ya Protestants Bible.
Ainisha kwenye diary yako ya malengo unacho muomba Mungu na ji-commit how will you worship God to get what you want! Dondoka vitabu 24 utakavyo soma mtoto acha ubabaifu! You can mix Old and New Testament. Au hata ukiamua kukomaaa na agano moja pia sio kesi. La msingi u-put in the hours.
Ukijua vitabu angalia vitabu vina chapters ngapi. Mfano Injili ya Luka ina 28 chapters. Gawa kwa siku 15 maana yake you will be doing approx 2 chapters a day.
Usiku soma chapters zako, kesho meditate on the chapters na tailor maombi ya malengo yako ya mwaka kusimama na hizo chapters 2 za usiku wa jana. Decree na ku-declare according to the chapters ulizosoma the coming to pass ya malengo yako.
Mimi binafsi lazima niweke vitabu vya Injili na Major Prophets kwenye kila mwezi. Sio mpenda miujizaaa! Kwenye Injili kuna actions za kutosha. Wafalme napo wamo wamo. Isaya mwana wa Amozi nae yumo yumo.
Kuna vitabu ni migodi iliojificha. You can read the books over and over. Lakini don’t get it twisted — all books in the Bible zina upako sawa sawa.
Ukisoma 2 chapters per day hutakuwa the same 2026. Read the real undiluted Word of God for yourself! Ubabaifu hausaidiiii.
Mungu anaongea na wewe majibu yako kupitia maandiko unayosoma kila siku. Atajifunua kwako kupitia hayo. Kama husomiii my dear, mwaka hautakuwa na jipya huu! Kwendraaaaa!
Mungu ni Neno. So kumjua Mungu lazima ulijue Neno lake — haina comeback hii! Hujui Neno humjui Mungu, full stop.
John 1:1
In the beginning was the Word, and the Word was with God, and the Word was God.
Hebrews 10:6–8
Then said I, ‘Lo, I come (in the volume of the Book it is written of Me) to do Thy will, O God.’
3. Mpokee Yesu Kama Bwana Na Mwokozi Wa Maisha Yako
Romans 10:9–10
If you declare with your mouth, “Jesus is Lord,” and believe in your heart that God raised Him from the dead, you will be saved. For it is with your heart that you believe and are justified, and it is with your mouth that you profess your faith and are saved.
I was born Catholic, I was raised pagan Catholic, then Lutheran, then pagan again, and finally Pentekoste! Each time I will advise you to be Pentekoste.
Pentekoste as in makanisa yanayoongozwa na Roho Mtakatifu — Assemblies of God, haya mapya mapya ya watu binafsi, hata baadhi ya Lutheran churches ni za kiroho sana, hata Romans wale charismatic. Cha msingi wawe na uamsho wa usharika na Roho Mtakatifu.
Kanisa au dhehebu au mtu ambaye hana ubatizo wa Roho hii, dini ya Kikristo atakuwa tu msindikizaji na shabiki. They will miss all the action, ambiance and vibe. Dini kwao itakuwa ngumu mnoooo na very very boring.
Kuna dimension za imani huwezi kuzifikia kwa kubakia kwenye dhehebu ulilopo. Sisemi ubadili dhehebu, lakini usijibane dhehebu moja. Explore watumishi na makanisa mengine.
Sio kila Jumapili usali parokia yetu ya Sinza Makuburi! You will never grow. Padri yule yule atasoma masomo yale yale, wataimba zaburi ile ile, atacheka jokes zile zile. How will you grow kama you have been going to this mass since you were 5 years?
It is one God and one Jesus. Normalise kufanya tour makanisa mbalimbali ujifunze dimension kubwa zaidi za kiroho. The fact kanisa lako hawafundishi haimaanishi hawajakukataza kujifunza privately.
Kukiri kwa mdomo Yesu ni Bwana na kuamini moyoni kwamba Mungu alimfufua katika wafu may sound simple ila it is deeper than that.
Ukiamini Mungu alimfufua Yesu katika wafu, you will never doubt God in anything anymore in your life. Baaassss! Umevukaaaa!
There is no way uamini haya mazitoo na miujiza ushindwe kuamini Mungu atakupa mume au kazi. Wewe kutomwamini Mungu kwenye malengo kunaanzia kutoamini Injili kabisaaaa.
Wakristo wengi hawaamini chochote — wanazuga zuga tu kwenye hii dini. Ndiyo maana hawapati matokeo: they identify as Christians but are not practically Christians.
The list of being practical 2026 is long. Nimepata tu dharura nikaikatisha. Itaendelea.
