
Mathayo 9:17
Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote.
New blessings of God can not flow in an old you!
Watu wengi wepesi wa kumuomba Mungu afanye mambo makubwa mpaka kudai na kuzirai endapo yangesubiri, lakini wanasahau kuji-update na kutengeneza mazingira ya kupokea hilo jambo.
Na hamjiandai wala kuji-update kwa sababu hamuamini kama Mungu atatenda. Na Mungu akimpa mtu unabii, anaangalia mapokeo ya yule mtu juu ya ule unabii na maandalizi atakayofanya ndio u-optimize au ubakie ahadi kama ahadi.
Waebrania 11:6
Na pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu; kwa maana kila mtu anayemjia ni lazima aamini kuwa yupo, na kwamba huwapa thawabu wale wanaomtafuta kwa bidii.
Bila kumuamini Mungu kwamba atafanya, na kupokea unabii kwa moyo wako wote kwamba itafanyika, ni ngumu sana kumpendeza Mungu. Unampendeza vipi kwa kuwa na mashaka mashaka au don’t care?
Nimesema andika maombi yako kwenye diary. Mtu hata diary hajanunua bado, wala hanunui. Yaani unabii nikupe bure, halafu bado nikubembeleze kununua diary? Kweli?
Hujanunua diary kwa sababu hujaamini wala kupokea unabii wa Mungu kufanya jambo jipya kwenye maisha yako. Mimi mwenyewe nilienda Shoppers kununua diary nikiwa nime-approximate 20k au chini kwa diary ya 2026. Nikakuta diary nzuri ni 42,000/= nikasema sinunui. Thubutuu yangu.
Nikaondoka kabisa nikakwenda kununua, among other things, Amarula ya 45k, wines na other liquors zaidi ya laki kwa sababu I’m hosting guests hii January.
Nikiwa liquor section sijibanii laki si pesa milioni deni, Roho Mtakatifu akanisema: Ina maana 42k ni ghali sana kununua diary uweke malengo yako? How much worth are those goals?
Nikawa mbishi: I have 2025 diary hata nusu haijafika. We continue.
Then nikapata interpretation kwamba Roho Mtakatifu hafurahishwi na ubahili wangu. Nikaenda kununua ile diary, na zile pombe sikurudisha. And I forgot about the diary.
Roho wa Mungu akanikumbusha kwamba unaweza kuwa mganga ukaganga watu vizuri, ila usijigange mwenyewe kwa sababu you don’t drink your own medicine. Umepayuka madhabahuni watu wanunue diary waandike malengo, halafu wewe diary iko store.
Unapolia: “Nitakuwa daraja mpaka lini ee Mola?” daraja la kijazi kama daraja.
Nia ya kujaza diary nimeiweka siku kadhaa nyuma. Ila nikasema nisiijaze tu kwa mihemko. Let me pray about it. Nimuombe Mungu anipe malengo ya mwaka halisi, ndipo niandike yale ya ukweli.
Huwezi amini kwamba simple act ya kununua diary ilisignify obedience, na Roho Mtakatifu ameninena mambo mengi sana ya breakthrough za maisha yangu mwaka huu. Vision nishapata, bado kuiandika tu.
Leo ndio naandika rasmi, mafunuo yote. Na Mungu alivyo wa ajabu, kuna mambo yatafunuliwa nikianza kuandika. Nisipoandika, imeishia hapo. Oraaaa.
Malengo ukiyaandika na kuyakabidhi kwa Mungu yanakuwa agano rasmi kati yako na Mungu. Bila kuandika, yanabaki story tu kama story nyingine.
Isaya 43:19
Tazama, mimi nifanya jambo jipya; sasa litachipuka; je, hamtalijua? Nitafanya njia jangwani, na mito nyikani.
Soma maandiko kila siku, fanya ibada, lipa zaka na sadaka.