THE GRASS IS ALWAYS GREENER WHERE YOU WATER IT, UNATAKA MATOKEO YAJIFANYIE KAZI

 

Kuna mtu alikuwa hana kazi akaniambia anaenda kumuona mtumishi mkubwa kwa sababu hiyo ya kazi!, mmmh! akatumia fortune ya hela ambazo hana mpaka kukutana na mtumishi, akawekewa mkono, sasa akawa anatusimulia na mdada mwingine ambaye hana hela, akawa anatamani, Mimi nikamwambia kabla sijaokoka kiukweli kazi zilinisumbua sana ila sasa naweza kuzibadili kama nguo, akawa very interested kisha akaniuliza naokokaje? wapi? nafanyaje? chezea njaa wewe! kiukweli alinisumbua na mimi niko busy! akaja kuniambia nishapata kanisa nimeokoka na nishabatizwa kwa maji mengi, ikabidi sasa nimwambie asome injili zote nne (4), akasoma kisha nikamwambia rudia, nikaona kuna progress, sasa nikaanza kumfundisha Deliverance kwa sababu anania akafanikiwa na kupata kazi nzuri sana.

Yule aliyewekewa mikono wakati naanza kumuelekeza huyu alinyalii, alivyo ona mwenzie yupo kazini mambo yake ng’arii ng’arii akaja kuni-intimidate kwamba kama najua njia kwanini simpi na yeye, simpendi tu, anafosi nimwekee mikono, nika muuliza ule mkono uliowekewa uliishia wapi?, siyo kwa ubaya, sasa kama ule umedunda huu wangu utasaidia nini akapanic hivyo matatizo yangu makubwa sana?, Yeuwii!

Nikamwambia uvivu wako ndiyo mkubwa sana, We kabla ya kuwekewa mkono na mpaka sasa ni mwaka hujasoma injili hata moja, hujui wokovu ni nini?, hutaki kujifunza, mwenzio kashabatizwa mpaka kwa maji mengi, kafyekaa agano jipya kama hana akili nzuri, alikuwa mpagani ila anajifunza hii dini kwa moyo sana kwanini asipate matokeo, hata ukiwekewaq mkono hujui Yesu ni nani? na alikuja duniani kufanya nini? na hata kwanini tunasema kwa jina la Yesu! kiukweli hata uwekewew mkono na papa hakuna kitakacho badilika kwenye maisha yako.

Yaani wewe hujui chochote kuhusu mbingu and you want to command the heavens, sister please kujifunza hutaki, akili timamu unazoo!, afya unayo tele, kwanini hutaki?, Jeuri tu, unaona kazi yote ya nini? let me have someone else to do the commanding to me, mbingu siyo nyepesi hivyo.

Transformation inaanza kichwani kwako kwa kujua mambo ambayo huyajui, Yapo na unayajua, Yapo na Yalipo andikwa unajuaa! ila nia na moyo wa kusoma ndiyo hunaa!, Basi as long as huyajui shetani atakukalia kooni, The only way ya kumtoa kooni password zipo kwenye maandiko ambayo hutaki kusoma, pambana na shetani mpaka akuue!.

Maana mimi sijui maandiko!, Kuna mtu alizaliwa na Biblia kichwani?, hamnaa! kila mtu alianza kusoma mstari mmoja mmoja, unless uamue kusoma lakini tofauti na hapo hutakaa ujue maandiko, maandiko hayawekwi kichwani kwa mtu kupitia bluetooth au WiFi bali the more books you know the more arsenal you have against the enermy! more is always prefered to less, mfano mtu uwe fiti vitabu vitano(5) vya sheria ya Musa ( Unatoa mimacho Musa aliandika vitabu vitano (5) lini tena jamani?) uwe fiti kwenye vitabu vya manabii yaani Major and Minor! uwe fit kwenye Gospel, ugonge Pauline Episles, Yaani ther is no way ukawa unateseka na imani. Unateseka kwa imani kwa sababu wewe ni mjinga mkubwa yaani kubwa jinga to be precise, una miaka ishirini (20) plus kwenye imani ila hujui kitu na ni mbabaifu wa kujifunza.

Mtu ambaye ni mweupe, mpuuzi kama wewe, mvivu na mbabaifu akapambane na shetani aliye walaghai mpaka malaika superiorbeings, akafanya uasi mpaka mbinguni akabattle na mwana wa Mungu, na amepoa duniani kama prince of flesh relim, hivi huoni kama CV ya Shetani siyo nyepesi kushindwa na kiumbe wewe mdhaifu mwenye ubabaifu, You are no match for him, usipo badilika kupata matokeo kwa shetani ni uongoo.

Kabla hujakurupuka kichwa kichwa ku-battle na shetani, battle kwanza na nafsi yako na pambana na ubabaifu wako yaani unakula zaka za Mungu bila haya upo serious na Mungu akupandishe cheo, hata shetani anakuhurumia maana yake anaona something is not right in your head, the audacity!

Wewe hujui hata vipande tu vya injili walau hata kuthibitisha imeandikwa kweli?, What if tunakudanganya? hakuna kilicho andikwa, tumetungaa, achana na doctorines na theology nyuma ya maandiko hata tu imeandikwa. Mtu ana bachelor degree maana yake kasoma kwa tabuu na ma-tabu ila pages kadhaa tu za injili hawezi kusoma, kaa na ujinga wako kwani sh.ngapi?

Unataka uhuru wako na U-Battle na shetani ikiwezekana umfurumushe kwenye maisha yako uweze ku-access soft life package!,una mfurahishajeee?- silaha na technique zote zipo kwenye maandiko ambayo wewe hutaki kusoma, kuandikwa unajua imeandikwa lakini kusoma ndiyo hutaki!!

Wapendwa mtu ambaye ameokoka kamili ile fully anatakiwa awe ameshinda following powers;

1.Power of Sin (Usiendeshwe na zinaa, tamaa, uongo na dhambi rejareja

2.Power of Grave/Death ( Usiogope kufa, Unaogopaje kurudi kwa baba kwenye makao mazuri?, kufa sio shida zetu, sio kufa wewe tu yaani hata chochote kikifa kwenye maisha siyo shida zako.

1 Corithians 15:55-57

55. O death, where is thy sting? O grave, where is thy victory?

3.Power of Evil; Mpendwa na hizi ndiyo kiboko yaani zina roho saba (7) lakini ikijua neno la kutosha unazi defeat vizuri tu na mapema sana.

4.Power of the flesh ; Mwili usipo ushinda hufiki popote yaani uowiru utakumaliza kabla ya shetani na watumishi wa Mungu sasahivi wanaenda gym dada yaani pastor anaita mkijiendekeza mnastukaa mbingu zimefunga juu yenu kwani mshakula tunda la mtu wa kati kitamboo zimebakia vuu tu kama ushahidi wa myoya kwamba kondoo kashaliwa kitamboo, power of the flesh haihishii kwenye upwiru tu, wanajua ndiyo mambo yenu ndiyo maana nakazia sana lakini kiuhalisia inahusisha hasira, Mungu anakupa mtu sahihi unamgombeza kama umemzaa sasa anarudi kwa Mungu yamemshinda hehehe, we kuwezaa??? tamaa! mpaka unajiuliza viungo Mungu alichomamji sababu amepiga marufuku kutumika, wewe unatumika ili upate maisha bora, yaani moto wako unakuja personal tubu ungalipo!, Uvivu!! ndiyo kama hivyo kusoma maandiko ya Mungu wako hutaki unaendekeza mwili utasema kusoma injili ni sawa na kulima heka saba (7) ingekuwa hivi tungekwisha, mwili ukiuendekeza hufiki.

Acha ubabaifu acha kubumba bumba, kama hujui hujui, hata apostle awe ndugu yako kichwani hamna kitu ni hamnaa!, wewe ni natural man!, kama injili kichwani kwako hakuna hautakuwa na wakumzugaa! hao unaotaka kupambana nao wanajua fika kuwa kichwani wewe ni zumbukuku.

Sons of sceva waliona mtume paul anatoa pepo kwa jina la Yesu wasijifunze kwanini na kuna-doctirines gani nyuma yake wakapita na hiyo mishe ya kuruka kwa jina la Yesu kichwa kichwa kwanza mapepo yakawashangaa hehehe!, yakawachana live, Yesu namjua! Paul namjua! ila mbona nyie siwajui!, Siwa somii mjue alafu mnataka kunitoa humu ndani? kivipi?, Kwa mpango gani? likawatoa relay maana siyo race wakiwa utupu wa mnyamaa.

Ndiyo hapo sasa na wewe husomi maandiko, huweki misingi ya imani, hujengi mahusiano na Mungu alafu unatumia summary ya mtumishi kuruka na shetani hewani, we mwana wewe uvivu utskukost.Ndiyo mtu hutaki kusoma injili, hufanyi ibada, zaka hulipi, sadaka hutoi, hufungii, ubao wa amri kumi za Mungu unafutaa wote yaani hubakishi inshort unamfuga shetani ndani yako na anakunenepesha.

Mtu anakuja anakwambia kabisa dubwana lililo ndani yangu siyo dogoo!, ni nene alafu anakupa mtego litoe wewe! thubutuu! limekutuma!, kama upo serious tulitoe wote anza kwa kusoma injili, anza kusali mara mbili kwa siku, funga siku moja (1) kwa wiki before you know it lilikwisha kimbia siku nyingi sanaa.

Mpendwa kama uantaka kupata matokeo eneo lolote hakikisha unafanya haya kwa miezi sita (6) utakuwa na matokeo:

1.Soma maandiko!; Mpendwa hakikisha unasoma hata aya moja kila siku, yaani kitabu kimoja kimoja kwa mwezi.

2.Soma Injili zote nne (4)

3.Jifunze wokovu/salvation; Imani bila wokovu ni sawa na Gari bila Mafuta.

4.Mpokee Yesu na pambana ubatizwe kwa Roho Mtakatifu.

Mpendwa Number 1 – 4 is all you! Hakuna wa kukusaidia, Mtumishi hawezi kusema  akusomee aya moja kwa siku au injili, Wewe ndiyo kila kitu, ukiji kataa umejimaliza mwenyewe.

Ukifika stage 4 sasa hapo Mtumishi ana make-sense kukukuzaa, hata kama namba tatu (3) na nne (4) bado mchanga ila namba moja (1) na mbili (2) upo solid mnaweza kwenda sawa!

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
× IT Help Desk