Yohana 10:27-28
27 Kondoo wangu husikia Sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata. 28 Nami ninawapa uzima wa milele. Hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka katika mikono yangu.
KEY WORD IS HEAR MY VOICE/ HUSIKIA SAUTI YANGU.
MPENDWA SAUTI YA YESU NI MAANDIKO MATAKATIFU!, JE UNASIKILIZA YANACHOFUNDISHA AU UNAJITIA KIZIWI WA MWENDO KAZI, UKISIKILIZA SAUTI YA MAANDIKO HUTAANGAMIA LAKINI UKISIKILIZA SAUTI YA BANGI ZAKO ZINAVOKUTUMA SELF DESTRUCTION IS INEVITABLE.
SHIDA INAKUJA UNA IGNORE MAANDIKO ALAFU SELF DESTRUCTION MODE IKIANZA UNATAKA MAANDIKO ULIO JIFANYA KIZIWI YAFANYE KAZI JUU YAKO GHAFLA SANA, LIKE HOW?
Kuna watu wengi nime waongoza miaka na mimi kwenye Uzinzi sina kona kona. Lakini mtu anasikia mafundisho ila hapo kwenye zinaa anasikilizia sauti ya UPWIRU.Teke -teke anaendelea nao kimya kimya, Mama nina miaka 3 simjui mwanaume, Mmmmh! We binti wewe huna haya wala hujui vibaya, Mimi namuona kwa Macho ya rohoni yupo kwenye dimbwi la ZINAA tena na Mume wa mtu, Tena ananuka janaba bichi kabisa!.
Hiyo Trailer, Vina muda basi? Picha kamili kamimba kwenye konaaa shwaa, Kwanza Mume wa mtu nyumbani ana mitoto minne (4), Na school-fees za Feza, Hataki kusikia neno ADA.
Sasa Ukimwambia una mimba ni kama death sentence ya huo ubatili wenu. Hakutaki tena na mtoto hamtaki, Sasa hapo ndo unarudi kwa Mungu na miguu miwili, Unataka MAANDIKO YAANZE KUANDIKARING JUU YA HATMA YAKO AMBAYO NI MATOKEO YA SELF DESTRUCTION YA KUSIKILIZA SAUTI YA TAMAA YA MALI NA UPWIRU.
Maandiko yamesema CRYSTAL CLEARLY LIPA ZAKA KILA MWEZI, Unajifanya kiziwi una manga zaka yote kwa raha zako, Tena unajimbia nalipaje?
Zamani sawaaa Moto ulishuka ku-consume zaka au Moshi ulienda juu walau Mungu alisikia harufu Ya zaka yangu, Zama hizi Mbinguni hamna Federal-Bank wala MobiLe Money, Hizi zaka zote zinaliwa huku huku duniani!, MTU ANASEMA SITOI KWANZA NINA MAMBO KIBAOOO SIJAWEKA SAWA.
The thing usipolipa zaka SIO kesi, Wala Mungu hawezi kukutokea ndotoni kukuliza HIO ZAKA VIPI SASA NDiIO UMEMONA UNIZULUMU DRY ?, Wala watumishi tunaojielewa hatuwezi kukulamba miguu leta hio zaka basiiii kipenzi. Shida ni kwamba KINGA yako inakuwa ndogo sana, UKIJIFANYA KIZIWI ENEO FLANI MAANDIKO YA HILO ENEO HAYATA APPLY KWAKO!.
Mal 3:10-12
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkani-jaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi, Mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au laah. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu;,wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi na mataifa yote watawaiteni heri, maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.
Mtu zaka hutoi na upo serious kabisaa unataka kufunguliwa madirisha ya mbinguni na Ikiwezekana mibarakaa umwagiwe, Like how??? Una utani na mbingu, Sauti ya kutoa zaka husikii na kamweee huwezisikia lakini ya madirisha ya mbinguni kufunga unasikia tena headphones za dr dre kasauti kamejichuja hatari.
Maandiko yako waziii washkajizangu mnajua kusoma, Kama daz-nunda walivoimba somaa mwenyewe uone barua hiii, wewe soma mwenyewe uone andiko hili. “nNitamkemea alae !!!!!, Wala hataharibu mazao ya ardhi yenu, Maana yake huyu alae asipokemewa ni swalala muda tu, ataanza kukula huko kwenye mapato yako. Huyu alaye ni hatari sana, Maandiko hayamzungumzia sana, Yani yame beep tu kuwa liko sasa hajaweka wazi kama ni li spirit, au li demon, au shetani mwenyewe, au ni likitu gani hasa lakini maandiko yametaja tu kwa jina la alaye.
Alaye is an under-stament, Mpuuzi anafyekaa mapato yako yote, Alaye haoni. Anaondoka na jungu zima, Hutaamini macho yako!, Na kaziza huyu alayeeee zimenyooka! Akipita kwenye maisha ya mtu anamuacha anatoka unga tu! Wakati once upon a time alikuwa mtu na utukufu wake! Kama ulikuwa humjui utamuona, Muongo jinsialivyo fyekwa na alaye!
MUNGU AMESEMA AKILIPWA CHAKE HALALiI, KILA MWEZI SIO SHIDA ZAKE KUMKEMEA HUYU ALAYE, THUBUTU YAKE, HATA ONJA HATA 10 YAKO.
Watumishi wanapenda sana zaka, NI KWELI! Na hilo andiko tuliandika sisi Mwaya enzi za walawi kukutapeli pesa yako mwaya.
WEWE JIZIME DATA NI SWALA LA MDA TU UTAKUTANA NA ALAYE NA NJAA IKIWA IMEMBANA USO KWA USO ALAFU KINGA YAKO NDOGO NA WA KUMKEMEA USHA MTAPELI MPAKA BASI, NDIO UTAJUA KWANINI HUYU ALAYE HAKUWEKEWA UFAFANUZI KWENYE MAANDIKO NA KITU PEKEE CHA KUMSTOPISHA NI ZAKA AMBAYO UMEILA NA KUIMALIZA YOTE! SIKU HII NDIO UTAJUA MAISHA NI SAFARI NA NAULI UMEKULA YOTE.
MIMI NILISHANGAA WAZAZI WETU MTU KAFANYA KAZI MIAKA 30 HANA YANI HANA CHA KUONESHA CHEZEA ALAYE WEWE, NA KlBAYA ZAIDI AMEANZA KUKULA NA MIAKA 30 YAKO, MTEKE NA LAINI MWENYEWE, ALAYE ANAKUFAIDIJE.
Mimi nime-deal na serious case za ALAYE, Unakuta mtu analipwa pesa nyingi hata Million 4 kwa mwezi na ana miaka 10 kazini hata kagari IST hana, Anapanga upande, ana madeni, ALAYE yuko sambamba na huo mshahara, Ukitoka tu, Mama kameza shoka, Mtoto kashikwa degedege, Mjomba kabaka, Mpaka UISHEEE WOTE! Ikawa miezi ikawa miaka na Zaka Hatoi hata 10!, Madai yake hana ya kutoa.
Nikamwambia huyu ni ALAYE, DAWA YAKE NI ZAKA TU, Akaona yaleee yale, Shoga angu unajinadi unamtumikia Mungu aliye Hai nakutafuta unisiadie unataka kunikwara 10% ya msharaaa, Thubutu, Akiondoka, Vina muda basi! yakatokea matatizo kazini nusu afukuzwe Akarudi, Nikamwambia ALAYE ALAYE, ANAONDOLEWA NA ZAKA TU KWENYE MAISHA YA MTU, NIKIKWAMBIA VINGINE NITAKUWA MUONGO, TOA HATA MIEZI 6 TUONE ITAKUWAJE MAANA KUZULUMU ZAKA NDO UMEISHINA JITU LILALO MPAKA LINAKUMALIZA. Alitoa zaka, na matatizo yanaanza kupungua, Mpaka yakaisha kabisa Mpaka kaanza kuuona mshahara wake.
THE MINUTE ALIVYOANZA KULIPA ZAKA MUNGU ALIMFURUSHA ALAE NA MIZIGO YAKE YOTE!, Akaanza kubakia na hela za saving!, Akapata million 12 ananiuliza Mara 10 ninunue Gari eeeh! Gari lenyewe IST, Namwambia with that kind of Salary nunua lakini uje U-upgrade to 4 by 4 walau HAREER au VANGUARD.
KUNA NDUGU YANGU NI BOSS DE-LA BOSS LAKINI AKAINGIA KIJICHO KWANINI MIMI NABANGAIZA TU LAKINI KWENYE MAENDELEO TUKO BEGA BEGA AS IN HOW? YEYE ANA LARGER THAN LIFE SALARY, YEARLY BONUSES, BAHASHA ZA WATEJA, INSURANCE! MIMI NINA MAANDIKO TU.
NIKAMWMABIA MAENDELEO YA MTU HAYATEGEMEI ANAPATA NINI BALI ANABAKIZA NINI, WEWE UNAPATA KINGI LAKINI NDO ALAYE TENA ANAKUJA KULA HAPO MWISHO KINABAKI KIDUCHU KAMA CHETU!
MIMI NAPATA KIDOGO ILA ALAYE HAONI, SITUMII KWA LOLOTE SINA BIMA NA NINA MIAKA 5 HATUJAUMWA HATA MALARIA TU, SIPATI MKOSI WOWOTE ULE, CHOTE NACHOPATA KINABAKI HIVO HIVYO! USIPOJIANGALIA NAKUPITA MDA SI MDA! ALIFADHAIKA MNO.
Yohana 10:27-28
27 Kondoo wangu husikia sauti yangu nami nawajua,nao hunifuata;28 nami ninawapa uzima wa milele.Hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakaye wapokonya kutoka katika mikono yangu.
SIKIA SAUTI YA MUNGU KUANZIA SASA UPATE UZIMA WA MlLELE NA HUTA ANGAMIA KAMWE, WENZIO WAKIPEWA MIMBA NA KUACHWA WAANGAMI E NA WATOTO WAO WEWE HUTA ANGAMIAAA KAMWEE! WENZIO WAKIFUKUZWA KAZI WEWE UTABADI LIKAZI KAMA NGUOOO! WENZIO WAKIMALIZA HELA HOSPITALIKWA MATIBABU WEWE KINGA YAKO ITAKUWA KUBWAAA MPAKA WATATAMANI WAKUFANYI E VIPIMO, KUJIFANYA KIZIWI WA SAUTI YA MUNGU NI MWANZO WA SELF DESTRUCTION MODE!
KWA MNAO SUMBULIWA NA AFTER MATH YA ALAYE KWENYE CAREER ZENU TAFUTENI PROGRAM ZA CAREER HELL MJUE MLIANGUKA WAPI NA MKA MPA UPENYO, NIMEELEZA KWA KINA NA NIMEWEKA REFERENCE YA MAANDIKO NA NIMEKUJA KUTOA SOLUTION KWENYE PROGRAM YA CAREER GROWTH! UFANYE NINI KUTOKA HAPO. NA KAMA UNATAKA KWENDA EPIC UNAMALIZIA NA PROGRAM YA CAREER LEVEL UP, SASA UKIJIZIMA DATA KUFANYA LEVEL UP WAKATI BADO ALAE AMEKUKALI A KOONI UNA TWANGA MAJI KWENYE KINU, ANZA CAREER HELL! MMALIZANE NA ALAYE, NJOO KWENYE CAREER GROWTH, THEN CAREER LEVEL UP!
WATU WA KAZINI HIZO NI PROGRAM TATU ZOTE KWENU JINSI NAVO WAPENDA MSHINDWE NYIE TU WAKATI WENZENU JOBLESS NIMEWAPA PROGRAM MOJA, NA UNAENDA MWAKA WA TATU HUU! PROSPERITY BASI.
KAMA UNATAFUTA KAZI FANYA PROSPERITY! HII PROGRAM IMEWAPA MATOKEO WATU WENGI MNOOOO! NA SIJATOA NYINGINE MAANA HII NI KIBOKOOO NA INA LIFETIME, ACHIEVEMENT, WEWE FANYA HII KWA MOYO UTAENDA KAZINI KAMA UNAENDA KWA MKWEO.