Luka 5:12-16 (The Leper Encounter)
BIBLIA NI MOJA! Hakuna toleo la “watafutaji” na lingine la “watazamaji.” Sote tunasoma hiyo hiyo. TOFAUTI IKO KWENYE EXECUTION!
Wewe unasoma Biblia kama gazeti, sisi tunaisoma kama maisha. Luka 5 haikuwa story ya mkoma kuponywa tu. Ni SIRI YA UPONYAJI WA KIUNGU! Ukitaka uponywe, ukitafuta kutakaswa, YESU YUKO TAYARI—ila je, WEWE UKO READY?
✊ MKOMA HAKUJA KUSIKIA HOTUBA—ALIKUJA KUFANYA BIASHARA!
Hakumwambia Yesu:
“Bwana, nimehangaika sana, sijala siku tatu, mke wangu kaniacha…”
NO!
Alishajimaliza kichwani—hakuwa na muda wa story! Alimwangukia Yesu kifudifudi, aka declare moja kwa moja:
“Bwana, UKITAKA, waweza kunitakasa.”
🎯 Hakumwuliza Yesu kama ana uwezo. Hakutaka references. Hakutaka CV ya miujiza. ALIAMINI TU YESU AKITAKA, BIASHARA IMEISHA.
Yesu hakubishana. Hakumwambia, “Rudi kesho nikupange deliverance.”
NO! YESU AKAMGUSA. YESU AKASEMA: “NATAKA! TAKASIKA!”
🔥 Na ukoma UKAMUACHA PALAPALA. Hakukuwa na guess work. Hakukuwa na delay. Hakukuwa na process ya miezi 3 ya “cleansing classes.” ONE TOUCH. ONE WORD. BIASHARA ISHA!
🤯 UKIONA HAUPOKEI MIUJIZA—JIULIZE, JE UKO KAMA MKOMA?
Mkoma hakutaka validation ya huduma ya Yesu. Hakutaka statistics. Hakutaka kukusanya “feedback kutoka kwa watu wengine.”
ALIJISURRENDER.
Wewe bado unafuatilia reviews, unatafuta “case studies” kabla hujaamini mtu. Mpaka unajiuliza:
- “Huyu mtumishi kawasaidia watu wangapi?”
- “Anaweza kweli changamoto za aina yangu?”
- “Ni deliverance ya level gani anafanya?”
😒 Wakati huo huo unashikilia changamoto zako kama diploma!
KIBURI TU! Unataka mtumishi awe “proven” wakati shida zako hazijathibitishwa popote.
💔 Wengine hata kwa YESU hamuendi moja kwa moja!
YESU AMESHAPONYA MIKOMA, AMESHAFUFUA WAFU, BADO UNAMTEST.
Unasema:
- “Labda YESU apate chance ajithibitishe kwangu.”
- “Sina uhakika kama ataweza kuniokoa kwenye hii relationship mbovu.”
Sasa kama huamini YESU anaweza kukutakasa, UNAFA NYUMBANI ULALE NA UKOMA WAKO. Hakuna cha kuficha!
💡 DELIVERANCE YA KWELI INANZA NA MINDSET!
Mkoma alikuja na MINDSET YA MSHINDI.
Aliweka IMANI yake kwenye:
- Tabia ya Yesu (compassion).
- Uwezo wa Yesu (power).
- Nia ya Yesu (willingness).
Hakutaka chochote kingine. Hakutafuta huruma ya watu. Hakutaka like wala comment. ALITAKA KUTAKASWA. FULL STOP!
💣 NENO LA LEO NI HILI:
“BWANA YESU, UKITAKA, WAWEZA KUTAKASA….”
💥 Mahusiano yako yaliyooza.
💥 Kazi ambayo haikui.
💥 Biashara isiyo na faida.
💥 Mwili uliovunjika kwa magonjwa.
💥 Akili iliyojaa misukosuko.
💥 Roho iliyochoka na iliyokata tamaa.
💥 Imani iliyoyumba kama meli ya mitumbwi mitatu.
YESU AKISEMA NATAKA, TAKASIKA—LINAISHAAAA!
🙏 MEDITATION YA KESHO:
“Bwana Yesu, sihitaji historia ndefu. SIHITAJI APPROVAL. SIHITAJI STORY.
NATAKA KUTAKASWA!
Kama yule mkoma, najisalimisha. Najishusha. Najua uwezo unao. Najua nia unayo.
Sasa YESU, UKITAKA, waweza kunitakasa.”
🛡 DECLARATION YA LEO:
Kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO,
Ninaamuru:
✅ TAKASIKA kwenye kila hali ya maisha yenye UKOMA.
✅ TAKASIKA kwenye upweke usioisha.
✅ TAKASIKA kwenye kukataliwa, kufeli, kukwama, kushuka moyo.
✅ TAKASIKA kwenye ndoa isiyo na amani.
✅ TAKASIKA kwenye akili iliyopoteza mwelekeo.
✅ TAKASIKA kwenye miili yenye maradhi sugu.
✅ TAKASIKA kwenye finances zako!
✅ TAKASIKA KILA ENEO LINALOKATAA KUKUA KWA JINA LA YESU!
SUNDAY WORD: NAHITAJI KUTAKASWA—SIO STORY.
NATAKA YESU.
NATAKA UPONYAJI WA KWELI.
NATAKA KUONA NGUVU YAKE LIVE.
Ukiamini kama yule mkoma—SIKU YAKO YA UPONYAJI NI LEO!
🔥🔥🔥
TAKASIKA!
TAKASIKA!
TAKASIKA!
Kwa jina kuu la YESU KRISTO.
Amen.