THERE IS A TIME FOR PREPARATIONS, AND A TIME FOR GOD TO ANNOUNCE YOU! – SUNDAY WORD

 

Yesu alikuja duniani kwa kazi ya miaka mitatu tu, akaikamilisha. Lakini kabla ya hiyo miaka 3 ya huduma, alikaa miaka thelathini akijiandaa – akiwa seremala wa kawaida, akihudhuria masinagogi, akikaa kimya, bila kujitangaza wala kuonyesha ule utukufu wake! Miaka yote hiyo alikuwa undercover! Lakini muda wa Mungu ulipofika – ndipo akaonekana kwa nguvu!

SOMO? Watu wengi wanataka kutangazwa kabla ya kujiandaa! Wanataka kuitwa leo, na kesho waonekane hewani wakifanya miujiza! Hakuna kitu kama hicho. Kila unapokwepa season ya maandalizi, unachelewesha season ya kutangazwa. Mungu hawezi kutangaza mtu ambaye hajaiva!

 

Daudi alipakwa mafuta akiwa kijana. Akaitwa kuwa mfalme. Lakini haikumaanisha kesho yake aliingia ikulu! La hasha! Alikaa miaka mingi nyikani akipambana na Sauli. Mungu alimwandaa kwa njia ya mateso, vita, kujificha – hadi alipokomaa.

Kama ni leo unapakwa mafuta, kesho unataka iwe viral TikTok? Uwe na record ya Live anointing? Hapana. Usikimbilie kutangazwa. Kimbilia kuandaliwa!

 

To be called is one thing… but to be ready to walk the calling is another.

Wengi wetu tumeitwa, lakini hatujaitikia. Au tumeitikia kwa maneno, lakini hatujafanya maandalizi yoyote. Mungu hawezi kumtangaza mzembe, mgaigai, anayepuuza neno, anayekaa mbali na uwepo wake, anayekataa kufundishika. Hata kama aliitwa, bila maandalizi – hiyo huduma haitazaliwa!

 

USHUHUDA WA NGUVU

Mwandishi wa ujumbe huu alikataa wito. Alifanya maisha yake, akaishi kivyake, aka-enjoy ujana! Lakini ghafla ajali ikatokea – akarudi akiwa na magongo. Akaanguka ndani ya giza la depression, akahisi kifo kinamvamia. Akamrudia Mungu kwa machozi na toba ya kweli, akasema:

“Nimejua sasa, siwezi kufa kabla ya kutimiza kusudi!”

Na Mungu alimrudishia afya yake kimuujiza! Lakini bado, alirudi maisha ya zamani! Hadi mateso yalipomrudia kwa nguvu ya pili! Hapo ndipo aliingia kwenye maandalizi ya kweli – akaingia makanisani, akaanza kusoma neno, akaingia usiku na mchana kwa uwepo wa Mungu hadi chooni! Akaiva!

Na sasa? Ujumbe huu una nguvu kwa sababu umetoka kwenye mtu aliyevunjika, akaponywa, akaandaliwa, na sasa – anatangazwa!

 

KUHUSU WITO WA KUWA WAKE WA WATU

Kama unajua unataka kuwa mke, na unamuomba Mungu akutangaze kwa mmeo – jitayarishe kuwa mke wa BWANA, sio mke wa IG!

Huwezi ukawa na wito wa kuwa mke, lakini uko ndani ya uzinzi usioisha, flirt na wanaume wote, ukizoea kuchukuliwa kama booty call – alafu bado unamwomba Mungu akutangaze kama mke? Haitatokea! Mungu hawezi kuharibu jina lake kwa sababu ya tamaa zako.

Uamuzi unahitajika. Leo, achana na umalaya. Achana na mindset ya tamaa, achana na kuwaza shortcut za maisha. Anza kuishi maisha kama mke wa kweli – mwenye heshima, mwenye hofu ya Mungu, mwenye malengo halali. Mungu hawezi kutangaza kile ambacho hakijajengwa kwa misingi sahihi.

 

Ujumbe wa Leo kwa Kifupi:

  • Kuitwa sio kutangazwa.
  • Muda wa maandalizi ni muhimu kuliko muda wa kutangazwa.
  • Bila toba ya kweli na maandalizi halisi, wito hubaki tu kuwa ndoto inayosumbua.
  • Mke kutoka kwa Bwana ana akili tofauti, maono tofauti, na mtazamo tofauti wa maisha.
  • Usitake vya kunyonga kwa uvivu wa kuchinja – baraka huja baada ya kupita katika tanuru la maandalizi.

MWISHO:
Kama unaona huu ujumbe ni wako, usiishie kuguswa – badilika! Usiwe mtaalamu wa kushangilia mahubiri mazito ilhali huishi chochote unachosikia!
Kama uliitwa – itikia!
Kama umeitikia – jiandae!
Na Mungu mwenyewe atakutangaza kwa utukufu!

 

2 thoughts on “THERE IS A TIME FOR PREPARATIONS, AND A TIME FOR GOD TO ANNOUNCE YOU! – SUNDAY WORD”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top