SUBMISSION TO GOD’S PLAN — SOMO KUBWA ALILOTUACHIA BWANA YESU IJUMAA KUU

Yesu na Baba yake walikuwa na mpango mkuu — si wa kawaida, bali wa milele. Mpango huu ulitangazwa kupitia manabii, vizazi kwa vizazi: kwamba Mwana wa Adamu atakuja, sio tu kuishi, bali KUOKOA ULIMWENGU.

Luka 22:41–43

“Akaondoka kwao kama umbali wa kutupa jiwe, akapiga magoti, akaomba, akisema, ‘Baba, kama unataka, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu bali yako yatendeke.’ Malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu.”

Hapa tunaona Yesu, baada ya kutumia muda wake duniani, akiwa na maumivu ya ndani. SI KWAMBA HAKUJUA KILICHOKUJA — ALIKUWA ANAJUA! Lakini utu wake wa kibinadamu ukaanza kuhisi uzito wa mateso. Alitaka mpango ubadilike kidogo, lakini bado alijisalimisha kwa mapenzi ya Baba.

KUSITA SI DHAMBI — KUTOKUTII NDIO DHAMBI.

Hili ndilo somo kubwa tunalojifunza Ijumaa Kuu: Submission to God’s Plan. Yesu alijisalimisha, na kwa sababu hiyo, mpango wa wokovu uliendelea. Malaika akaja kumtia nguvu — maana kujisalimisha hakumaanishi hautahisi uchungu. Inamaanisha utatii hata ukiwa na maumivu.

LAKINI WENGI WETU HATUJIFUNZI SOMO HILI.

Mungu anapotuonyesha mpango wake — kupitia ndoto, maono, sauti, au hata ushuhuda wa watumishi wake — sisi tunaanza kutumia akili zetu na tamaa zetu. Anaweza kukuambia waziwazi, “Huyu ndiye niliyemkusudia kuwa mume wako,” lakini unakuwa na mbio za kutafuta mchaka bwengo mwingine kwa sababu huyu si wa ‘ladha’ yako ya mwilini!

Wengine mnaomba mume, lakini mdomoni mna maombi, moyoni kuna mpango B. Huyo B ni ‘baby’ wa dhambi, wa mapepe, wa haraka haraka! Mpaka unafika hatua ya kupakiwa mkongo na kupelekewa moto — halafu unasema “Bwana amenisahau.” LA HASHA!

SURA YA KWANZA YA KOSA: KUTOJISALIMISHA KWA MPANGO WA MUNGU.

Mungu anapokupa mtu kwa maono, anatamani umwelewe kupitia Yeye. Usiangalie ‘vibe’ bali uangalie value. Lakini ukianza kumshtua, kumweka benchi, kuuza mechi — mwisho wa siku UTUKUFU WA BWANA UNAONDOKA.

IKABODI — maana yake: “The Glory has departed.”
Usikubali mahusiano yako yafikie hapa kwa sababu ya kiburi, tamaa, au uzinzi.

HADITHI HALISI:

Kuna dada mmoja aliniambia kabisa, “Mungu ameniambia huyu ndiye.” Nikamuuliza maswali machache, nikaona kweli ni mtu aliyemtumwa na Mungu. Lakini yule dada akaniuliza mara 20, “Nikikubali basi tusifanye zinaa?” Nikajua, huyu hajakomaa rohoni.

Akamtoa kipa goli, akaanza kuuza mechi. Kelele nyingi, matendo machafu, mwisho — utukufu ukaondoka. Yule jamaa akapata bibi mwingine, ambaye alijitunza mpaka harusi. Na yule dada akaona ndoa ikipigwa picha na akaumia! ULIKUWA MWALI WAKE — LAKINI ULIMZIDI MIPAKA!

KUMBUKA: KWA MWANAUME WA MUNGU, MAADILI NI KILA KITU.

Ukitoa kabla ya wakati — unajifuta mwenyewe kutoka kwenye list ya potential wife.
Kwa nini?
Kwa sababu wewe si wa Mungu, hauji kwa njia za Mungu, hufanyi yaliyo ya Mungu.

Ni rahisi sana:
Mke mwema hutoka kwa Bwana. Mzinzi hawezi kutoka kwa Bwana.

NA KWA WALIOCHELEWA KUOLEWA — SIKILIZA:

Mungu anajua umri wako. Anaona umeteseka. Na ndio maana huwa makini sana na mtu atakayekuletea.
Over 35? God becomes EXTRA SENSITIVE.
Anaweza kumtoa mtu kwenye maisha yako ghafla — bila sababu.
Anaweza hata kufanya mwanaume aliyekuwa anakuomba ghafla akukate. Kwa nini?
Ni rehema! Anaepusha kosa la maisha!

Ndoa ya 40s sio ya kufanyia mazoezi — ni ya kufunga safari ya maisha.
Ukiolewa vibaya kwa kuchelewa, dunia haina huruma!

USISUBIRI HADI UCHOKE — JISALIMISHE SASA!

Usiwe bado unaomba mume huku uko kwenye Ozempic!
Unajichoma sindano kwa milioni tano ili tu “uonekane vizuri” — lakini bado haujajisalimisha.
Dada, submission ni dawa ya roho, si sura. Sura inazeeka, submission haizeeki.

Omba ombi moja tu:
“Bwana, nipo tayari kwa yule uliyenikusudia. Nipe yule uliyemwandalia.”

Na ukijia mtu wa kweli — utajua.
Hatakuomba zinaa. Hatakupima kwa mwili.
Atakuongoza kwa roho na kweli.

MWISHO WA SIKU — USIKUBALI KUUZA USUKANI KWA SHEETANI.

Mungu hawezi kugombania usukani na wewe. Ukiomba yeye aendeshe, unapaswa kushuka kutoka kwenye kiti cha dereva.
Huwezi kumwambia Mungu akutafutie mume halafu wewe uko miguuni kwa mchaka bwengo!

Kama bado unafanya dhambi za uzinzi, unavunja miiko, unapata mimba na kutoa — halafu unasema Mungu hajakupa mume — je, kweli unastahili kumlaumu Mungu?

JIFUNZE KUTULIA — SUBMIT — TRUST — OBEY.

Weka ibada yako mbele. Soma Neno. Tafakari mapenzi ya Mungu.
Omba kwa unyenyekevu, si kwa kisirani.

Tafuta Bwana — si boyfriend.

Ndoa bora si matokeo ya make-up, selfies, ama skintight jeans — ni matokeo ya submission to God’s perfect will.

 

Mimi nimeishi maisha ya dunia na maisha ya wokovu — na nitachagua wokovu kila siku.
Mara ya kwanza nilinusurika kwa muujiza — sitarudia tena.

Na wewe pia — usirudie tena.

 

🕊️ Zingatia mpango wa Mungu juu yako.
Ni mpango wa uzima, si wa maangamizi.
Submit to it. It’s worth everything. 🙏

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top