Restoration

Kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo, Biblia inasimulia maelfu ya mahusiano – kutoka kwa vifungo vinavyopendwa vya familia hadi mienendo tata ya urafiki na nguvu ya kuunganisha ya jumuiya. Maandiko haya matakatifu yanafunua uzuri na utata wa mwingiliano wa wanadamu, pamoja na mpango wa Mungu katika kuponya mahusiano yaliyojeruhiwa na kukuza roho ya umoja. Tutazama katika mafundisho ya kina na hadithi zinazopatikana ndani ya Biblia zinazoangazia njia ya kurejesha mahusiano yaliyopotea.

Mfano wa Magugu

Mathayo 13:24-26

24 Yesu akawaambia watu mfano mwingine: “Ufalme wa Mbinguni unafanana na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake.25 Lakini watu wakishakuwa wamelala, adui yake akaja,akapanda magugu kati ya ngano na akaenda zake.26 Basi, mimea ilipoota na kuanza kuchanua,magugu pia yakaanza kuonekana.

Day 1 : Relationship Restoration

Luka 15:17-18

Alipozingatia moyoni mwake alisema, Ni watumishi wangapi wa Baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na Mimi hapa ninakufa kwa njaa. Nitaondoka, nitakwenda kwa Baba yangu na kumwambia Baba, nimekosa  juu ya Mbingu na Mbele yako.

Day 2 : Relationship Restoration.

Yoeli 2:25-27.

Day Activity / Shughuli ya Siku.

“Chukua simu yako Andika SMS kwa Mzazi Mwenzio/ Mume/Mchumba/ Mpenzi ambaye unataka RESTORATION ifanyike kati yenu kwa kutumia maneno yako (Kikubwa Umwambie, Ulikuwa unajitahmini na unaomba radhi kwa kila kitu ( You’re Sorry for Everthing) ambacho kwa kujua au kutokujua ulifanya kikamuumiza na unachukua majukumu ya mchango wako mpaka kuvunjika kwa mahusiano yenu. Aidha unaweza taja hivyo vitu kama una ujasiri mfano I was a DRAMA QUEEN, Nilikuwa na Kisirani, Mbinafsi na Mchoyo Etc.”  Ukishaandika kwanza simama na huu mstari.

Nitawarudishia Miaka ile iliyoliwa na nzige, kila kitu kilicholiwa na tunutu, parare na matumatu, hilo jeshi kubwa nililowaletea! Mtapata chakula kingi na cha kutosha;Mtalisifu jina la Mwenyezi Mungu , aliyewatendea mambo ya ajabu. Watu wangu kamwe hawatadharauliwa tena.Mtatambua kwamba mimi nimo miongoni mwenu, enyi Waisraeli; Kwamba mimi Mwenyezi Mungu, Ndimi Mungu wenu wala hakuna mwingine.[Yoeli 2 : 25 – 27]

Day 3 : Relationship Restoration

1 Wafalme 18:30-39

30 Kisha Elia akawaambia watu wote, Nikaribieni mimi, watu wote wakamkarbia. Akaitengeneza madhabahu ya Bwana iliyovunjika.31 Elia akatwaa mawe kumi na mawili, kwa hesabu ya makabila ya wana wa Yakobo,aliyejiliwa na neno la BWANA na kuambiwa, Jina lako litakuwa Israeli. Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la BWANA; akafanya mfereji, kama wa vipimo viwili vya mbegu,ukiizunguka madhabahu.

Kisha akazipanga zile kuni, akamkata yule ng’ombe vipande vipande, akaviweka juu ya kuni.Akasema, Jazeni mapipa manne maji, Mkayamwage juu ya sadaka ya kuteketezwa na juu ya kuni.

34 Akasema, Fanyeni mara ya pili. Wakafanya mara ya pili.Akasema, Fanyeni mara ya tatu.Wakafanya mara ya Tatu(3).35 Yale maji yakaizunguka madhabahu akaujaza mfereji maji.

Ikawa, Wakati wa kutoa dhabihu, Nabii Elia akakaribia, akasema,Ee BWANA, Mungu wa Abrahamu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako.37 Unisikie, Ee BWANA,unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie.

38 Ndipo moto wa Bwana Ukashuka ukaiteketeza Sadaka ya Kuteketezwa, na kuni na mawe na mavumbi, ukayaramba yale maji yaliyokuwamo katika mfereji.39 Na watu wote walipoona hayo yote, wakaanguka kifudifudi; wakasema Bwana ndiye Mungu, Bwana ndiye Mungu.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top