1 Wakorintho 16:9
Kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao.
Mungu anaweza kuwa ameshakufungulia mlango mkubwa na wa kufaaa sana, lakini wako wengi wakupingao kupita kwenye huo mlango. Mpendwa Day 3 unamalizana na wote wakupingao wewe kupita hilo eneo, Hakikisha leo-leo mnamaliza na mnakubaliana kwamba kifuatacho ni wewe kupita, Usitake kujua nani na kwanini wanakupinga, Wewe unachotakiwa ni kukiwasha yoyote akupingaye hana bahati siku ya leo!.
Prayer points
Baba ninakushuru kwa rehema na neema yako isiyo na kifani kwangu. Ninakushukuru kwa neema ya wokovu kupitia mwanao Yesu Kristo. Umeachilia mlango Mkubwa na wa kufaa sana mbele zangu eneo la ndoa/ kazi/ uzao/ ( ulicho andika) lakini wapo wengi wanipingao kupita katika hayo malango.
Kama kuna dhambi zozote zangu au za mababu zangu zina simama kama kizuizi cha kupiga mimi kupita katika hayo malango naziungama sasa toka ndani ya moyo wangu nakuanguka mbele ya kiti cha rehema nikiomba urehemu Baba na kuziondoa siziendelee kunipinga nisipite. Niweke huru Baba nivuke hayo malango leo hii.
Nguvu zozote za giza zinazo-pinga mimi kupita katika huo mlango mkubwa na wa kufaa naziteketeza sasa kwa moto wa Roho Mtakatifu, Kwa mamlaka ya jina la Yesu nazifunga sasa na kuzitupa kuzimu, Najifunika damu ya Yesu na kujiweka huru kutoka vizuizi vyoteee vinipingavyo kupita katika huo mlango kwa jina la Yesu.
In the name of jesus idecree and declare breakthrough !supernatural breakthrough katika hayo maeneo niliondaka. In the name of jesus idecree and declare divine favor katika hayo maeneo nilio andika, In the name of jesus I will walk through the mighty door God has created for me.