Kutokana na vikwazo mbalimbali ,Maombi yetu hushindwa kusikika hali inayofanya ukimya na kutojibiwa katika changamoto zetu, Jambo ambalo utufanya tuweze kukata tamaa na kuipa mbingu mgongo. Mpendwa nipende kukusihi usikate tamaa kwani ipo njia iwezayo kufanya maombi yako kusikika na kukupatia matokeo , Naam ni njia ya Sadaka.
Omba Sadaka yako ikapige kelele sehemu ambayo Maombi yako hayafiki.
Mpendwa Msihi Mungu maeneo ambayo Sauti ya maombi yako haifiki kutokana na vikwazo mbalimbali au kutokujua kuomba basi Sadaka yako ikapige kelele.Biblia imeonesha visa mbalimbali vinavyoonesha nguvu ya Sadaka katika Maombi yetu , Tupitie kwa pamoja.
Kisa cha Petro kumfufua Dorkasi.
[Matendo ya Mitume 9:36-42]
Huko Jopa kulikuwa na mwanafunzi mwanamke aliyeitwa Tabita au kwa lugha ya Kigiriki, Dorkasi, yaani Paa. Huyu Mama alikuwa mkarimu sana, akitenda mema na kuwasaidia maskini. 37 Hata hivyo aliugua akafa. Wakamwosha na kumlaza katika chumba cha ghorofani.38 Kwa kuwa Jopa hapakuwa mbali sana na Lida, wanafunzi waliposikia kuwa Petro yuko Lida, waliwatuma wenzao wawili wakamwambie, “Tafadhali njoo huku pasipo kukawia.” 39 Kwa hiyo Petro akaharakisha akaenda nao Jopa.Alipowasili wakampeleka hadi kwenye chumba alipokuwa amelazwa marehemu Dorkasi. Wajane wengi walikuwa wamemzunguka marehemu wakilia na kuonyesha mavazi ambayo Dorkasi alikuwa amewashonea alipokuwa hai.40 Petro akawatoa wote nje, kisha akapiga magoti akaomba; akaugeukia ule mwili akasema, “Tabita, Amka!” Dorkasi akafumbua macho na alipomwona Petro, akaketi. 41 Petro akamshika mkono akamsaidia kusimama. Ndipo alipowaita wale waamini na wajane akawakabidhi Dorkasi akiwa hai.42 Habari hizi zilienea sehemu zote za Jopa. Na watu wengi wakamwamini Bwana.
Wapendwa Dorkasi kutokana na Sadaka zake za kuwakalimu na kuwasaidia maskini na wajane, Wanapigia Kelele kifo chake. Mpaka Mtume Petro anamfufua. Hivyo mpendwa kama Sadaka imeweza kumfufua Dorkasi ,inaweza kukupatia Mtu Sahihi kwenye Mahusiano yako na Inaweza kutatua changamoto zako. Inua Sadaka!.