Katika maandishi ya mahusiano ya kibinadamu, Biblia hutoa mwongozo tata na wa kina wa kutafuta mtu sahihi wa kushiriki naye safari ya maisha. Maandishi haya ya kale yanatoa kanuni zisizo na wakati na simulizi zenye kuhuzunisha ambazo huangazia sifa za mwenzi anayefaa, zikitoa mwanga juu ya kiini cha uhusiano wenye maana na unaozingatia Mungu.
Mpendwa hii ni ushahidi tosha kuwa Biblia inatabua kuwepo kwa Mtu sahihi na asiyesahihi katika safari ya mahusiano yetu. Hivyo Nipende kukusihi uweze kutembea nasi katika safari ya Maombi haya ili tuweze kuangusha KUTA zilizofunga mahusiano yetu na kuweza kupata watu sahihi katika mahusiano yetu.
Maombi ya Mtu Sahihi.
Siku ya Kwanza
28 Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaangazia njia zako [Ayubu 22:28]
28 You will also declare a thing.And it will be established for you; So light will shine on your ways. [Job 22:28]
Mpendwa simama na neno hili na fanya tamko (declaration) ya kukutanishwa na mtu sahihi unaye mhitaji popote pale alipo.Rejea ile karatasi uliyoandika! kisha omba kwa imani ukimsihi Mungu aangaze njia zako na kukupatia mtu wako sahihi. Kam tulivyokubaliana Imani ya kuhamisha milima, imani ya kumtoa Mr.Right aliko na kumfanya mkutane ,mbadilishane namba na mpendane.
Siku ya Pili
Kutoka 14:15-16 ,21-22
15 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Kwanini mnanililia?Waambie Waisraeli waende mbele”. 16 Inua Fimbo yako na kuinyosha juu ya bahari.
21 Musa akaunyosha Mkono wake juu ya bahari, Naye Mwenyezi Mungu akaisukuma baari nyuma kwa upepo mkali toka mashariki.Upepo huo ulivuma usiku kucha, ukaigawa bahari sehemu mbili na katikati kukatokea nchi kavu.22 Waisraeli wakapita katikati ya bahari mahali pakavu, kuta za maji zikiwa upande wa kulia na kushoto.
Waamuzi 5:6
Katika siku za shamgari, mwana wa Anathi, Siku za Yaeli, Njia kuu zilikuwa hazina watu; Nao wenye kusafiri walipita kwa njia za kando.
Prayer (Maombi)
“Ee Mungu fanya njia pasipo na njia, Bila wewe Musa hakuwa na njia bahari ya Shamu! Fungua mlango wa rehema na nipe kibali cha kuvuka kupata mtu sahihi.”
“Lord make a way where there is no way! If not for you Moses had no way in the Red Sea! Open the Door of Mercy, Door of Favour and Door of Breakthrough fot the right man.”
Siku ya Tatu
Mathayo 15 :24
” Mwanamke mmoja Mkaanani aliyeishi sehemu hizo akaja kwake akamlilia akasema, ” Nihurumie Bwana, Mwana wa Daudi; Binti yangu amepagawa na pepo na anasumbuka sana”. 23 Lakini Yesu hakumjibu neno.Basi wanafunzi wake wakamwendea wakamwomba, “Mwambie aende zake, kwa maana anendelea kutupigia kelele”.24 Akajibu, ” Nimetumwa tu kwa ajili ya kondoo wa Israeli waliopotea.”
25 Lakini yule mwanamke akaja, akapiga magoti mbele ya Yesu akasema, ” Bwana, nisaidie!” 26 Yesu akajibu, ” Si haki kuchukua chakula cha watoto na kutupia mbwa.”27 Yule mwanamke akajibu, ” Ndio Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yanayo anguka kutoka kwenye meza za mabwana wao”
28 Ndipo yesu akamwambia, ” Mama imani yako ni kubwa! Na ufanyiwe kama unavyotaka.” Tangu wakati huo mtoto wake akapona.
Siku ya Nne
Kutoka 14 : 14
BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
Kutoka 15 : 3
BWANA ni mtu wa vita, BWANA ndilo jina lake.
1 Samweli 5 : 3-4
Baada ya Wafilisti kuleta Sanduku la Mungu, walilichukua kutoka Ebenezeri mpaka Ashdodi.2 kisha wakaliingiza lile sanduku ndani ya hekalu la Dagoni na kuliweka kando ya huyo Dagoni.3 Watu wa Ashdodi walipoamka asubuhi na mapema kesho yake, wakamkuta Dangoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la Bwana! wakamwinua Dagoni na kumrudisha mahali pake.
4 Lakini asubuhi iliyofata, walipoamka kumbe, walimkuta huyo Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la Bwana! kichwa chake na mikono vilikuwavimevunjwa navyo vimelala kizingitini, ni kiwiliwili chake chake tu kilichokuwa kimebaki.
Siku ya Tano
2 Wafalme 19-22
19 Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza.20 Elisha akawaambia, ” Tieni chumvi ndani ya bakuli jipya, kisha mniletee.” Nao wakamletea.
21 Akatoka akaenda mpaka chemichemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema BWANA asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kupooza. 22 Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawa sawa na neno la Elisha alilolinena.
Siku ya Sita
Isaya 49 : 18
Inua macho yako, ukatazame pande zote;hao wote wanajikusanya na kukujia. Kama niishivyo,asema BWANA, hakika utavika hao wote kama pambo, nawe utajipamba kwao kama bibi harusi.
Yeremia 33 :11
Itasikika tena Sauti ya furaha na sauti ya shangwe, sauti ya Bwana harusi na sauti ya bibi harusi, sauti yao wasemao Mshukuruni BWANA wa majeshi, maana BWANA ni mwema, rehema zake ni za milele, na sauti zao waletao sadaka za shukrani nyumbani kwa BWANA.
Siku ya Saba
1 Wafalme 7 : 8 – 13
8 Wana wa Israeli wakamwambia Samweli, usiache kumilili BWANA, Mungu wetu, kwa ajili yetu kwamba atuokoe na mikono ya Wafilisti. 9 Ndipo Samweli akatwaa mwana-kondoo mchanga, akamtolea BWANA sadaka ya kuteketezwa nzima; Samweli akamlilia BWANA kwa ajili ya Israeli; BWANA akamwitikia.
10 Hata Samweli alipokuwa akiitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti wakakaribia ili kupigana na Israeli; walakini BWANA akapiga ngurumo, mshindo mkubwa sana, Juu ya Wafilisti siku ile, akawafadhaisha; nao wakaangamizwa mbele ya Israeli.
11 Nao watu wa Israeli wakatoka Mispa, wakawafuatilia Wafilisti, wakawapiga. hata walipofika chini ya Beth-kari.
12 Ndipo Samweli akatwaa jiwe, na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni, akaiita jina lake Eben-ezeri, akisema Hata BWANA umetusaidia.
14. Hivyo Wafilisti walishindwa, wasiingie tena ndani ya mipaka ya Israeli;na mkono wa BWANA ulikuwa juu ya Wafilisti siku zote za Samweli.