Ndani ya kurasa za Biblia, maombi yanatokea kama njia yenye nguvu katika mawasiliano kati ya binadamu na Mungu. Andiko hili takatifu linatoa utanzu mwingi wa mitindo ya maombi, kila moja ikitumika kama onyesho la kipekee la imani, shukrani, dua, na uhusiano na Mungu. Kuanzia mazungumzo ya kibinafsi na Mweza-Yote hadi maombi ya jumuiya na maneno ya sifa, Biblia hutoa safu nyingi za aina za sala zinazopatana na kina na tofauti-tofauti za maisha ya wanadamu.
Mpendwa unaweza kuwa unaomba sana ila ukawa unaomba maombi ya Aina moja bila kujua. Ukawa unaomba aina A ukisahahau aina B. Ukiona unatumia aina moja ya maombi na hupati majibu badili aina ya maombi. Tujifunze aina za Maombi.
Aina za Maombi
- Maombi ya Kuongea na Mungu
- Maombi ya Kumsikiliza Mungu
Maombi ya Kuongea na Mungu
Mpendwa maombi haya ni yale yanayohusisha wewe kuzungumza na Mungu wako .Unaenda Mbele za Mungu na kuzungumza naye na utakayozungumza ndio yatatanabaisha aina ya maombi unayoyafanya. Aidha Maombi ya Kuongea na Mungu pia yamegawanyika katika makundi madogo madogo amabayo ni :
- Maombi ya Sifa
Maombi haya ni mazuri kwani unaenda mbele za Bwana kwa lengo la Kumsifu tu na Wapendwa Zaburi ni Kitabu kizuri sana cha Sifa.Tumia Zaburi ya 148 – 150. Mungu wetu anapenda sifa anapenda ajue ukuu wake.
Mpendwa ukisoma Biblia utagundua watu wengi walifanya maombi ya aina hii sanaa mfano Mfalme Daudi alitumia Maombi ya aina hii sana.
Unaweza kutumia Nyimbo. Maombi ya Sifa yanahusisha Kusifu, Kuabudu, kutukuza na kuuona ukuu wa Mungu. Kuna vita ni ngumu sana na huwezi kushinda kirahisi kwa maombi mengine zaidi ya maombi ya sifa. Je, Kama ufanyi maombi haya ya sifa itakuwaje?
- Maombi ya Rehema
Maombi haya uhusisha kwenda mbele ya Mungu kutubu na kuungama uovu , makosa na kusita sita kwako au namna yoyote ile unayohisi hujamtendea Mungu sawa na kumuomba arehemu.
Inashauriwa ufanye mara kwa mara maombi ya rehema. Ambapo utataja mambo unayoyajua hayakwenda sawa au kuyasahau na utaungama.Tumia Zaburi ya 151 na 123 zaidi. Msihi Mungu arehemu vile vinanvyo kukosesha haki fulani mbele yake.
Maombi haya yanalipa madeni na adhabu za makosa yetu na kufungua milango mikubwa sana. Mfano Mpendwa umefanya uzinzi miaka na miaka bia kuwaza na unataka Mungu asahau kirahisi tu ( Just like that) na unakazana kuomba favour ya Mume, Omba rehema mpendwa milango itafunguka.
- Maombi ya Shukrani
Maombi haya yanahusisha kwenda mbele za Mungu na kumshukuru kwa mema aliyokutendea.Tumia Zaburi ya 100, 136. Mara nyingi tukivuka tunachukulia poa.Tunarukia shida nyingine na kusahau kushukuru tuichopewa kabla, hii inafunga milango.
Ukishukuru kwa wema amabao Mungu bado hajakutendea inapendeza zaidi na kuonesha imani ya juu sana. Na unampima Mungu uaminifu wake kwa kumshukuru katika jambo amabalo halijatimia. Na kwa sababu Mungu ni mwaminifu napewa haja za moyo wako kiulaini.
Mpendwa huenda umeomba sana maombi ya uhitaji na hujaona matokeo, Nakusihi ubadili aina ya maombi unayoyafanya a kuomba Maombi ya Shukrani kwa jambo lile lile ambalo halijatimia na utaona ukuu wa Mungu.
Kumtega Mungu zaidi unaweza fanya maombi haya na kuambatanisha na sadaka kwamba kwa kupokea tayari. Je kwa nini ? kwa sababu Mungu ni mwaminifu sana.
- Maombi ya Mahitaji ( Maombi Pemdwa )
Maombi haya hufanyia masaa 24/7 . Ni kupeleka shida , mahitaji na matamanio yetu kwa Mungu. Lengo hasa ni kupokea msaada wa Mungu in return.Maombi haya sio ya bure bure.
Ni maombi ya kumsihi Mungu atende jambo. au afanye kitu. Tumia Zaburi ya 5 na 17 sana. Maombi hya huwaleta watu karibu na Mungu.
Mungu mwenyewe ametusihi tuombe maombi haya sana. Na watu wengi kama sio wote wanajikuta wakiomba maombi haya sio mara moja wala 2. hivyo tujikite nayo.
Formula ( Kanuni ) za maombi haya zipo nyingi sana na mitindo ya kuomba pia ipo mingi kama kulia, kukesha, kufunga, kulalamika, kujitenga, kujipaka majivu na kuvaa gunnia. YESU alifanya maombi haya mpaka akatoka jasho la damu, Ugumu wa maombi haya sio kwako tu Mpendwa. Jitie Moyo ipo siku yako.
- Maombi ya Kuombea wengine
Hapa unaenda mbele za Bwana na kupeleka shida za mtu mwingine, ndugu au jamaa, adui , booss goliath wako etc. jambo la muhimu unaita uzingatizi wa Mungu kwa mtu mwingine. Tumia Zaburi ya 1 na 122.
Mpendwa Mungu anapenda sana ufikirie wengine usiwe mbinafsi katika maombi yako. yaani kama unavotaka manabii na mitume wakuombee hivyo hivyo na wewe waombee wengine. Huenda maombi yako hayapiti ila kwa kuombea wengine mambo yanafunguka. Ukiyafahamu haya maombiyanaweza kuwa very strategic kwenye shida zako. Pia ni mazuri kushtaki na kuomba Mungu ahukumu. Pia ni mazuri kwa kuwaombea wapendwa wenu.
Hadithi fupi ya kweli.
” kuna mtu alikwa anasumbuliwa na Boss katili tena anayemuwinda amfukuze kazini kwa nafasi yoyote atakayopata.Akaomba sana maombi ya hitaji la kuokolewa dhidi ya yule Boss dhalimu lakini hakujibiwa.Akaendelea kuteseka chini ya utawala wa Big Boss kwa muda mrefu. kuna siku akanishirikisha nikamshauri abadili maombi. kwa sababu kama asemavyo Boss ni dhalimu sana hivyo kaburi alishalichimba bado kutumbukia. Nikamwambia asijiombee yeye bali awaombee wengine yeye asijihusishe kabisa na akamshitaki kwa Mungu Boss huyo dhidi ya udhalimu anao mfanyia na amshihi Mungu ahukumu huo udhalimu sawa na haki yake na wapendwa haukupita muda mrefu ilipita audit (Ukaguzi) mkubwa na Boss yule alifukuzwa kazini.”
Outstanding story there. What occurred after? Take care!
Reiew mmy homepage –
Amen