Skip to content
  • Home
  • Programs
  • Blog
  • Gallery
  • Contact
  • Home
  • Programs
  • Blog
  • Gallery
  • Contact

PART 3A

By Denis / August 26, 2023

Katika ulimwengu ulio na mapambano, maumivu, laana na vifungo suala la ukombozi kamili (Complete Deliverance)  lina umuhimu mkubwa .Biblia inatoa  mwongozo katika mchakato wa kupata uhuru kutoka katika utumwa wa dhambi, mzigo wa laana na vifungo.

Mpendwa kama laana au kifungo kina uhalali wa kukupiga kitakupiga sana hii ni hadi kipindi utakapo pokea Ukombozi kamilifu na wa kweli ( Complete Deliverance) , Katika maisha yetu ya kila siku watu wengi huamini mtu hawezi kujifanyia ukombozi ( self deliverance ) nipende kukanusha hili kwani jambo hili linawezekana lakini inatakiwa utulivu mkubwa na imani kuu wakati wa dhoruba .

Ukombozi ( Deliverance ) dhidi ya Laana na Roho zinazo zuia mambo yako umegawanyika katika hatua kuu tatu. ambazo nilazima zikamilike ili kuweza kufika  Ukombozi Kamilifu ( Complete Deliverance)

  1. Ukombozi wa Damu ya Yesu
  2. Neno la Ushuhuda.
  3.  Upako (Annointing) ya kuvunja Nira.

Ukombozi wa Damu ya Yesu

Watu wengi wanafahamu Damu ya Yesu ina nguvu na inaponya na hii ni kweli. Yamkini umemsikia Mchungaji wako anaita Damu ya Yesu mwanzo mwisho na wewe ukamfata  kwenye njia hiyo, hakika hujakosea uko katika njia sahihi ila inakubidi upate uelewa juu ya msingi wa ukombozi li uweze kupata matokeo.

Mathayo 26 : 27 – 28

Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa akisema, kunyweni nyote katika hiki, kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.

Mpendwa hili ndilo chimbuko la Damu ya Yesu, Kutukomboa na Dhambi. Yesu alifanya agano kuwa Damu yake ikimwagika italeta ukombozi.

Waefeso 1:7

Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.

Mtume Paulo akiongea na Waefeso anasisitiza juu ya Damu ya Yesu kuwa na ukombozi wetu  dhidi ya changamoto zetu.Mpendwa wengi tunatumia Damu ya Yesu bila kujua msingi wa nguvu itokanayo na damu hiyo.Huu ndio msingi mmojawapo.

Wakolosai 1:13-14

Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa Pedno lake; ambaye katika yeyey tuna ukombozi, Yaani msamaha wa dhambi; ukuu wa Kristo.

kwa hiyo katika Yesu kwa kupitia damu yake ya thamani, tumepata kuokolewa kutoka nguvu za giza. Hivyo hizi Laana na Vifungo vinavyotusumbua katika maisha yetu ya kila siku kupitia  damu yake tunaweza kukombolewa.

Ufunuo wa Yohana 5 : 9 – 10

Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake;kwa kuwa ulichinjwa,ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juuu ya nchi.

Mpendwa Yesu alitununua kwa damu yake ya thamani akalipa madeni ya kila mtu, kila taifa kutoka kwenye utawala wa shetani. Na kuwafanya wafalme, makuhani na wamiliki wa dunia. kwa hiyo madeni yetu yote yanayotoa uhalali wa shetani kuendelea kututesa na kutushikilia yameshalipwa kwa Damu ya Yesu yenye thamani kubwa. Hivyo kama tuki tubu ( Plead Mercy) na kuomba Damu ya yesu ( Blood of Jesus ) dhidi ya  dhambi na Laana zetu tutakuwa huru na kuweza kutawala na kumiliki tena duniani.

Mpendwa nipende kukusihi , Umsihi Mungu apitishe rehema zake na kukurehemu na hizo laana za kujitamkia Mfano Sina shida ya Mume, Mume wa kazi gani ?, Sishobokei Ndoa etc, Unajimaliza .  Hivyo Laana za kutamkiwa na watu, delaying spirit na roho zote zinazozuia matokeo yako arehemu kwa Damu ya Yesu. Deni lolote alilokushitaki Shetani, Damu ya Yesu irehemu. Msihi Mungu Damu ya Yesu irehemu hata makosa ya familia yako na ukoo wako na kulipa madeni  yote ili uweze kuwa huru.

Kimbilia kiti cha rehema kwa unyenyekevu mkubwa, tubu vitu vyote vilivyokufanya ulaaniwe   na kili kuwa ulikosea  kwa roho ya kweli na msihi Mungu katika ghadhabu yake akumbuke rehema na akurehemu kwa Damu ya Yesu.

Mpendwa usiende mbele za Mungu ukijihesabia haki bali msihi Mungu akurehemu kwa Damu ya Yesu na kukuokoa kutoka Nguvu za giza.Msihi Mungu Je ukifa sosnoneko la mfu linaweza kumsifu ?,  Je kuokoka kwako na haya mema ya siku 2 au 3 hizi hayahesabiki kabisa?, Je sadaka zako hazija mgusa hata kwa mbali ? na kama zimemgusa basi akurehemu kwa Damu ya Yesu na kukuondolea hiyo Nire ya Shetani upate kuwa huru.

Tumia Zaburi ya 51 kuomba rehema na kumsihi Mungu arehemu hio adhabu na kuachilia Mercy ( Msamaha ) ili upate tena uhuru wako. Nenda kwa hoja nzito ili mjadiliane. Mpendwa nenda kwa Mungu ukiwa na Moyo uliovunjika na kupondeka.

Tambua kwamba uliumiza watu kwa matendo yako, nao waka wakamlilia Mungu , na shetani akapata uhalali wa kukupiga. Tambua kwamba uliwasababishia uchungu mkuu na jutia kosa lako. ukifanya kwa roho ya kweli Mungu atakurehemu.

Mpendwa Fanya zoezi hili usiku kucha mapaka jioni, jutia, jishitaki na omba rehema ukilia Damu ya Yesu ikukomboe.

Neno la Ushuhuda

Mathayo 12:37

Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.

Mpendwa maneo unayotamka au unayotamkiwa yana  nafasi kubwa sana katika hatima yako (destiny yako ), Baadhi mnasumbuliwa na laana binafsi. Unajilaani wewe mwenyewe bila kujua. Ukiwa na  mabadiliko yako ya hali na tabia ( Mood swings and Attitude ) unaanza kujilaani kwa akili zako na unazitingisha Mbingu.

Yesu yeye kama yeye alijitamkia ufalme wake hajaanza hata kuhudumu, Angalia andiko hili :

Luka 4 : 17 – 21

Akapewa chuo cha Nabii Isaya, akakifungua chuo, akafuta mahali palipo andikwa, Roho wa bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru walioteswa, na kutangazwa mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Akakifungua Chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia maskioni mwenu.

Mpendwa Yesu maneo haya aliyasema Nazareti. Kiasi cha watu kuanza kuulizana  Huyu si Mwana ya Yusufu ?, Huu ni ushuhuda Mkubwa na Mzito na yeye hakujali. Katika kipindi hiki Yesu alikuwa na umri wa miaka 30.

Mpendwa Dhamira kuwa ni USHUHUDA WAKO na  nikuaminishe wakati wako ulioamriwa ni sasa. Mpendwa usijali  ” Tangaza Ndoa yako, Wakati ulioamriwa ni 2023, Tangaza kuwa Utavaa Shela au kuoa hata kwa kujisokomeza. Toa Neno lako la Ushuhuda.

Kama kunawatu walishuhudia kuwa wewe utazeekea nyumbani, ukishajikomboa na DAMU ya Yesu kwa kuomba rehema. Ushuhuda huu mpya utabadili laana zako kwenye ulimwengu wa roho

Annointing ya Kuvunja Nira.

Hii  Annointing ( Upako ) unakuja pale unapo unganisha ( Connect ) Mbingu juu ya jambo lako la kuvunja  Nira ( Ile kitu Ng’ombe anawekwa shingoni kumuongoza ) na ndicho hukitumia shetani kukucontrol ( Kukuongoza ). Ndio maana pattern ( Alama ) zako ni zilezile. Mpendwa shetani atakuacha ufunge siku sita (6) na ya saba anakukumbusha kushindwa ( failure ) zako zote unakula Biriani saa 5 Asubuhi.

Msihi Mungu Hii Nira ivunjwe kabisa ili uweze kuwa huru kutoka katika hizo control ( Miongozo ) ya hivyo vikwazo, laana, Vifungo na Nguvu za Giza. UKiweza Fanya hivi kila Siku, Kwa Wiki mara Moja na unaweza kusimamama na andiko hili wakati ukimsihi Mungu avunje hiyo nira na uwe huru.

Isaya 10:27

Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani wako, na nira yake shingoni kwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.

Mpendwa ikivunjwa Nira hiyo hakuna chochote utakachoshindwa kukifanikisha ( There is absolute nothing you wont accomplish ) , Utakutana na Mtu wako ndani ya miezi 3 ( in 3 Months ) na Ndoa itafungwa. Uhuru wa Kweli ( True Freedom ) , Ukiomba Maombi haya kwa muda mrefu lazima nira itavunjika.

Maelekezo Muhimu

Mpemdwa utafanya:

  • Ukombozi wa Damu ya Yesu kwa siku 14.
  • Neno la Ushuhuda kwa siku 10
  • Annointing ys Kuvunja Nira kwa siku 6

Hii itakupa jumla ya siku 30.

 

Previous

Aina za Maombi

Next

Kapime Nguo ya Harusi ! It’s a Prophetic Move !

Leave a Comment Cancel Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Copyright © Mlokole Binti2025 | Developed By Mlokole Binti ICT Unit.

Sisi ni Familia ya Mungu iliyojizatiti katika kutoa Mafunzo, ibada na huduma zinazo kuponya na kukujenga kiroho.

Useful Links

Home
Programs
Blogs
Contact

Anwani

 Dar es salaam, Tanzania
  +255 713 300 038 ( SUPPORT HUDUMA)
     +255 713 144 639 ( SADAKA AU MBEGU)

© 2025. Mlokole Binti, All Rights Reserved | Developed by Mlokole Binti ICT Department

Scroll to Top