Yesu amponya mtu kwenye Bwawa la Bethzatha.
5 Baada ya haya, Yesu alikwenda tena Yerusalemu kuhudhuria sikukuu mojawapo ya Wayahudi. 2. Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, pana bwawa moja ambalo kwa Kiebrania linaitwa Bethzatha ambalo lina baraza tano zenye safu za matao.
3 Wagonjwa wengisana,vipofu,viwete,na waliopooza walingojea kwenye baraza hizo. Walikuwa wakisubiri maji yatibuliwe, [4] kwa maana Malaika wa Bwana alikuja mara kwa mara akayatibua maji na yule aliyekuwa wa kwanza kuingia bwawani baada ya maji kutibuliwa alipona ugonjwa wowote aliokuwa nao.
5 Mmoja wa wagonjwa waliokuwepo alikuwa ameugua kwa muda wa miaka thelathini na minane(34).
6 Yesu alipomwona amelala hapo,na akijua kwamba amekuwa katika halihiyo kwa muda mrefu, alimwuliza,”Unataka kupona?”
7 Yule mgonjwa akajibu,”Bwana,sina mtu wa kuniingiza bwawani maji yanapotibuliwa. Ninapoanza kwenda bwawani, mgonjwa mwingine huniwahi akaingia kabla yangu.”
8 Yesu akamwambia, “Simama,chukua mkeka wako, utembee!”. 9 Mara moja yule mtu akapona, akachukua mkeka wake,akaanza kutembea!
Key points za kukufunua ufahamu kwenye maandiko haya ni hizi zifuatazo:
1. kuteseka na issue mda mrefu haimaniishi Mungu imemshida au hana nia Ya kukusaidia au hasikii maombi yako.Yule mtu alie pooza alikuwa pale akiwa ame pooza kwa miaka 38!, THIRTY EIGHT YEARS! Mda aliokaaa pale akiugua nizaidiYa umri wako unaouficha-ficha!, LakiniYesu finaly anamponya tena ana-mponya Siku Ya Sabato ambayo sio ya kuponya!, Anavunja desturi ya wayahudi kumponya huyu mtu!.
Mpendwa hata wewe kwenye hilo jambolakolililo ota ndevu Jesus willcome through for you. Tena atavunja desturi zote kukuvusha!.
2. Njia wa nayo pita wenzio wewe imekushinda kabisaaa na imekukataaa! Yesu bado anaweza kukuvusha kwa njia zake!, Yule mtu aliyepooza alikuwa eneo watu wanapona kisaaa!, Akishuka malaika ukawahi kujitosa wa kwanza umeponaaa!, Lakini yule mlemavu kutokana na hali yake alishindwa kwa miaka 38!, llimlazimu abakie anashuhudia uponyaji wa wenzie kwa miaka 38!.
Mpendwa yamkini ni miaka 10 tangu u-graduate hupatagi kazi, wenzio wanapata na kubadilisha, ni miaka 20 tangu ufukie umri wa ndoa ila huolewagitu,unashuhudia wenzio wakiolewa Mwaka hadi mwaka!
BADO YESU ANAWEZA KUKUBADILISHIA STORY YAKO MWAKA HUU KAMA ALIVO MBADILISHIA YULE MTU ALIE POOZA!
3. JE UNATAKA KUPONA ??????!!!!!, YAMKI NI UMEPOOZA KWENYE UCHUMI WAKO KWA MIAKA NA MIAKA MPAKA KWENU WAMESHAKUKATI A TAMAA KAMA UTAINUKA TENA ENEO HILO?
YAMKINI UMEPOOZA ENEO LA MAHUSIANO KWAKO NI MIKOSI JUU YA MIKOSIYAANI LIMEKUFAAA KABISAA SIO TU KUPOOZA! JE UNATAKA KUPONAAA HII 2024????
JAPOKUWA HAKUKUWA NA SABABU YA YESU KUULIZA HILi SWALI KWA YULE MTU ALIE POOZA SABABU JIBU LILIKUWA WAZI LAKINI ALIULIZAAAA! SABABU LINA MAANA KUBWA KIMAANDIKO!.
JE UNATAKA KUPONAAAAA????!!!!SWALI LAKO LA MWAKA 2024!
NA YULE MTU ALIYE-POOZA ANASHI NDWA KULIJIBU DIRECT ANA ZUNGUKA MBUYU KWELIKWELI !, SASA WEWE USI ZUNGUKE MBUYUUUU! JIBU NA TOA JIBU DIRECT! AFU AMBATANI SHA MATENDO YAKO NA JIBU LAKO!
Yule mtu badala ya kujibu kama anataka kupona au la anajielezea kwa kina kwanini YEYE kupona haiwezekani na haijawezekana miaka 38 iliyopita itakuwa Siku hiyo?.
JE UNATAKA KWENDA KAZINI ? UNATAKA KUVUKA ENEO LA NDOA 2024?, UNATAKA UZAO?, UNATAKA KUVUKA ENEO GANI ULILO KWAMA MIAKA NA MIAKA ???!!!
MWAMBIE BWANA YESU MWAKA HUU 2024, KAMA ULIVYO MUULIZA YULE MLEMAVU KAMA ANATAKA KUPONA, NAOMBA UNIPONYE ENEO FLANI!.
Mwenyezi Mungu, naitaji kupona kwenye mahusiano yangu. Naitaji mume nitakaeweza kuanzisha nae familia atakae kua prayer partner wangu mume na rafikiangu awe baba wa wawangu. Awe kiongozi kwangu.
Mwenyezi Mungu najua kila jambo kwako lawezekana basi ata kwangu litawezekana.
Amen Mtumishi, Mungu ni Mwaminifu.