Vizuizi vikubwa vya Ndoa

Vizuizi vikubwa vya ndoa

1.MAAGANO YA MIZIMU NA UKOO

Hapa ndiyo  asilimia themanini (80%)  ya watu wanapo kwama! Na upuuzi wa hawa jamaa, unaweza hata kuhudumu hata madhabauni kabisaa na ukatumika na Mungu wao lakini waka kaa kimyaaa!  hawana shida na wewe! Huanguki! wala Hupandi lakini unashikilia Maagano yao!,  Mimi mwaka huu niliambiwa na madeni ya Mizimu! Nikumtumikia mtumishi! Nikajua kabisa ni descern Error!  SIKUJISHUGHULISHA! Hakika nimeona mwaka unaisha mambo yapo vile vile hivyo nimeanza mfungo wangu usio na kikomo!,  Jana Roho-Mtakatifu kaniambia jambo hilo hilo! HAKIKA NIMECHOKAAA! Kwa sababu nimejua jambo limeishaaa! Nishamalizana nao! Sasa wengi haya mambo hamyaamini in that SERIOUS LEVEL! na ndiyo maana lina-watesa muda mrefu sana! Mnahangaika na mengine lakini  yale ya msingi  mna ignore! na  sababumuna ignore  haya mambo huwa yanameza matokeo yenu yote!

Mila nyingi vitovu anachukua bibi, anavipeleka wapi?JE NI KWA MIZIMU ?, na wa-africa tuna mila chafu sanaa! zinazo husisha kuozesha watoto wadogo kwa wafu!,  Kuna Kabila mtu akifariki hajaoa wana-muozesha mke ili kumtuliza.Na mara-nyingi mtoto mdogo! na hawa-kwambiii! kumbe unahangaika na mume wakati kwenye ulimwengu wa Roho usha olewa!

Kuna mila za kuchinja na kula vyakula vile vilivyo apizwa! na Mara nyingi baada ya misiba! ndiyo maagano yanapo fanyika! na kuwa renewed!, Kuna maagano ya ukoo wenu na mizimu yao! Hasa Familia za ki-Chief! unakuta kuna makubaliano ya kuwa kuna vitu vinatakiwa vifanyike ili watoto waolewe! Sasa unakuta aliyeachiwa Mkoba kakimbilia Dar! Mtajijua! Hivyo mnajikuta HAMUOLEKI! Hata mwanaume awe king’ang’anizi vipi ! atakubali tu Show! (tendo)

Mambo ya mizimu ni mengina kila ukoo una mambo yake mazitooo!

UTAJUAJE KAMA UNA KIZUIZI CHA MIZIMU NA UKOO!

1.Patterns!

Unakuta watu wa ukoo wenu kalibia wote mna-kumbwa na jambo moja kila mtu kwa wakati wake! yaani wote hamuolewi kuanzia First-Born hadi Lat-Born au Mkijitahidi sana mnaishia kupata Posa tu na Wanaume wanapotea! au Akiolewa mtu lazima aachike au azike mume, Au wakati mwingine nyote mnaolewa lakini mnaishia kuzalishwa majumbani na kwa kuvutwa tu sogea tukae kisha mnatelekezwa!.

Mpendwa Ngazi ya tatizo lako inategemea na chanzo cha tatizo lenyewe! Wengine ni Familia yenu tu!, Wengine ukoo wote mpaka kwa mashangazi, mama wakubwa ,wajomba ! Kote kote!, SASA HAIWEZEKANI WOTE KUTOKUWA NA BAHATI! JAMANI?

MPENDWA KOO NYINGINE MPAKA UZAE NYUMBANI NDO UTAPATA NDOA!, BILA KUZAA NDOA HAKUNA! NA SHIDA HATA UKIKUBALI KUZAA BADO NDOA WATAKAYO KUPA MIZIMU NIYA MIYEYUSHO TU! UTATESEKA WEEE! MPAKA UIPATE FRESHI! YAANI HAWANA JEMA!

NJIA RAHISI YA KUJIOKOA  NI  KUANGALIA UKOO WAKO!  JE, HII SHIDA NI YAKO PEKE YAKO AU KIFO CHA WENGI NI  HARUSI? NA UKIKUTA WENGI MNA-PATTERN HIYO HIYO FAHAMU TU WAUNGWANA WAME-BLOCK NIDA YAKO NA NDOA YAKO WAMEIFUKIA WAO! NA WANA MADAI YAO YA MSINGI YANAYO WAPA UHALALI WA KUSHIKILIA MATOKEO YAKO! NA DAWA NI KUVUNJA MAAGANO NA KUJITENGA NAVYO! , SASA KWENYE MAOMBI UTA-FOCUS HAPA!  MPAKA MBINGU ZISEME!

2.Laana

Laana  nikama spell tu! ambayo mtu ameiachilia na imepata uhalali! Mpendwa LAANA INATEMBEA VIZAZI  VINNE 4! , Maandiko yapo tutayapitia! Katika Biblia takatifu tunaona Yoshua ana ulaani mji wa Yerico kuwa atakaye ujenga upya ataweka msingi wake kwa kufiwa na mzaliwa wake wa kwanza na malango kwa kufiwa na mzaliwa wake wa mwisho!

Yoshua 6:26

Wakati huo Yoshua alitamka apizo rasmi mbele ya watu akisema,”Atakayeujenga tena mji wa Yeriko, na alaaniwe na Mungu, Yeyote atakayeweka msingi wa mji huo, mzaliwa wake wa kwanza na afe.Aidha Yeyote atakayejenga lango la mji huo, mwanawe kitinda-mimba na afe.”

1Wafalme 16:34

Wakati wa utawala wake, Hieli kutoka Betheli aliujenga upya mji wa Yeriko na sawa kabisa na neno la Mwenyezi-Mungu alilonena kwa njia ya Yoshua mwana wa Nuni, Hieli alifiwa na mzaliwa wake wa kwanza Abiramu,wakati wa kuiweka misingi ya Yeriko na akafiwa pia na mwanawe mdogo Segubu wakati wa kuyaweka malango yake.

PAMOJA NA HIELI KULIPA GHARAMA YA LAANA YA YOSHUA BADO MJI UNABAKIA NA GUNDU LILE-LILE !UNAKUWA UNAZAA MAPOOZA! MPAKA WAKATI WA YOSHUA NDO ANA-UTIBU!, MPENDWA WALIO MUUZI YOSHUA NI WENGINE! NA WALIOZIKA WATOTO NI WENGINE! NA HATA WALIO-ZAA MAPOOZA NI WENGINE! PIA.

2 Wafalme 2:18-22

18.kisha wakarudi kwa Elisha aliyekuwa anawangojea huko Yeriko, Elisha akawauliza,”Je, sikuwaambieni msiende?”19.Aadaye watu wa Yeriko walimwendea Elisha, wakamwambia,”Bwana,kama uonavyo mji huu ni mzuri,lakini maji tuliyo nayo ni mabaya na yanasababisha mimba kuharibika.”20.Elisha akawaambia,”Tieni chumvi ndani ya bakuli ji pya,kisha mni etee.” Nao wakamletea. 21. Elisha akaenda kwenye chemchemiya maji,akatupa chumvi hiyo ndani na kusema,”Mwenyezi­ Mungu asema hivi:Nimeyafanya maji haya kuwa yenye kufaa;tangu sasa hayatasababisha vifo au kutoa  mimba.” 22. Na maji hayo yamekuwa ya kufaa mpaka Leo, kama alivyosema Elisha.

MPENDWA UNAWEZA KUWA UNATESEKA LAKINI NI LAANA FLANI TU NDO INA-KUTESA! YAMKINI WAKATI UNASOMA MAMA YAKO ALILOPOKA  AKAWAUDHI WATU KWAMBA MWANANGU YUPO CHUO!AKITOKA ATAOLEWA MASAKI! SITAKI AOLEWE NA VIJANA WENU! WATU WAKA-LAANI!, AU ALITAMBA MBELE ZA WIFI ZAKE NA HAIKUWA KWA UBAYA ! LAKINI KAKA YAO KAMDHIBITI KWELI! NA KOSA NDO UNA LILIPIA WEWE!, AU ALIPISHANA NA MAMA MKWE ! KISA KANGA TU ZA URAFIKI ZILIVOKIWA NZITO! NA BIBI WA WATU KAFA KAACHA LAANA ! HAKUNA MTOTO WA FLANI ATAKAYE OLEWA ! KIWEPESI TU! NA IKAPITA ! WALIO-GOMBANA WAMESAHAU!LAKINI  LAANA LINA RINDIMA ULIMWENGU WA ROHO!

LAANA HAIJALI MUDA GANI UMEPITA!, VIZAZI VINGAPI VIMEPITA, INACHOJALI  NI UHALALI WA KWAMBA HAIJAVUNJWA!! NA UKIVUNJA CHAPU NA KUIOMBEA  UNAPATA REHEMA! YAANA JAMANI MIMI SIO NILIYOFANYA HAYO MAKOSA! IKAFUTWA! MAMBO YANAENDA! SOMETIMES WALIO LAANI WAPO NA ALIYECHOKONOA YUPO! MNAWEZA PATA UJUMBE MKAOMBE MSAMAHA! AU MLIPE FIDIA! LA MSINGI NI KWAMBA LAANA ZINA SOLVIKA! NA UJIO WA YESU ULILETA MASULUHISHO MEPESI! SIO KAMA ENZI ZA YERICO!  MPENDWA KESHO TUTAENDELEA NA VIZUIZI VINGINE!

3.Uchawi na Uganga

Hapa zimetumika nguvu za giza kufunga mambo! Uchawi ni MCHAWI mwenyewe anatumia uchawi kukufunga!wakati Uganga ni mtu anaenda kwa MCHAWI au mtaalamu kununua huduma yake ya nguvu za giza kukuangamiza wewe!

Mpendwa pia kuna uwezekano wewe mwenyewe umeenda kwa mganga kutaka usaidizi wa nguvu zake za giza kwenye mambo yako aka-kuchanja au kuku-unganisha na SADAKA na maagano ya nguvu za giza! HAYO MAAGANO NDIYO YANAKUFUNGA!, Uchawi mbaya ni=wa mafundo fundo ambao unahusisha kutumika kwa kitu chako kufungwa fundo na kufukiwa au kutupa baharini ili samaki alimeze fundo! Mambo ya Wapemba hayo!, Mambo ya kupoteza chupi, pads, nguo, ndo hayaaa! yaani Mtu anatumia hivo vitu kufunga ndoa yako au kazi! Inshort usipo Focus kuvunja na kuharibu HUU uchawi wao utakutesa mda mrefu!, Mtu anakuuliza hivi mama yako anaitwa nani? Na wewe unataja tu kijinga! Ndo wanatumia Jina la Mama kulogea!

WACHAWI SIO LAZIMA UWAFANYIE KITU! WENGINE NI ROHO MBAYA TU NA WIVU! WANAONA KAZINI UNAJISHAUA  HIVYO WANAFUNGA UKOSE WA KULA NAYE HIO PAY-CHECK KUBWA NA UKOSE RAHA NA AMANI BASI! BURUDANI WAMEKUWEZA!

Unakuta mtu mmoja umechezewa na shangazi, umechezewa na ofisni,umechezewa mtaa unao ishi! Lazima udateeee! na UZURI WACHAWI NA WAGANGA NI WATU! NA NI TOFAUTI NA NGUVU NYINGINE ZA GIZA AMBAZO NI ROHO! SO AKISHAJUA UMEMJUA TAYARI KWAMBA YEYEE NDO ANAKUCHEZEA ANAPANIKI NA KUKUOGOPA VIBAYA MNO! NA UKIVUNJA VUNJA UCHAWI WAKE NA KUJIWEKA HURU NA VIFUNGO VYAKE MAMBO YAKO YANAENDA! NA SABABU UMEWAJUA UNAWEZA KUWAWEKEA VIKWAZO VYA KIROHO WAKIJARIBU TENA HAWANA BAHATI!

Majini Mahahba/ Spiritual Husbands/ Marine Spirits

Mpendwa Somo hili nilifanya topic nzima iko katika post za nyuma tafadhari itafute kupitia blog zetu.

Mpendwa hizi ni roho chafu, zinazo Oa wanadamu, kufanya nao MAPENZI usingizini, kuzaa  na wanadamu watoto na kuwa na mahusiano nao! Source kubwa ya  kuruhusu upenyo wa kukuingia ni UZINZI, unakuta mwanaume tayari  analo anakupatia!, Hata kama mwanamke unaota uko na mwanamke mwenzio! sababu  kubwa ni alikuwa nalo Bwana wako la kike! Ndiyo mambo ya kwa East unaanza kutamani wanawake wenzio una-haha uwe connected! na PORN SITES ni portal yao nyingine mbaya sana! Unavyo angalia hizi Connections au Ma-Website ya X unajiweka vulnerable kwenye RELIM yao na ukifanya masterbation ndo kabisaaa umefungua mlango wa kuingiliwa!, Source nyingine ni Mila za baadhi ya makabila hasa ya kando ya bahari, ziwani na mitoni kuji-associate na Roho za majini! Mfano Watu wa pwani, Ziwani na sehemu za MITO ndo wana-shida sana na hizi Roho!

Shida yao kubwa ni KUUA MAHUSIANO YAKO! ya kuwa Hutakaaa uwe na meaningful relationship itakayo fika popote! LAZIMA MAHUSIANO YAKO WAYAHARIBU!, MPENDWA KUYATOA SIO KAZI SANA, KAZI NI KUFUNGA MLANGO WANAYOINGILIA!, WANAWEZA WAKATOKA ILA UKICHUNGULIA TU CONNECTION WANARUDI!

Niliweka maombi kwenye hio posts ya last year ya SPIRITUAL HUSBAND!, Maombi ya kufunga Milango! na Wengi walipona kabisaaa! Na kwa sababu hawajarudia kuangalia PORN, Hawajafungulia mlango tena! Wali -VUKA! Walio rudia kuenjoy PORN yamerudi!, Wananiambia tu mom yamerudi! KIVIPI ? Wanakanyagia.Mpendwa ukijiendekeza hawa wadudu niwabaya! Utalala mpaka na MBWA! Utalala na ndugu zako INCEST ! utalala na shemeji zako,utalala na wanawake wenzio, 3 some, mipalange! Na kiu yako haitaridhika ! NI MATESOOO!

Kuna mtu nilitaka kuletewa nika-mkataaa! mAlilala na mtu,wakavuta bangi wenyewe, yule mwanaume akamlala akamuita mdogo wake wa kiume aje akale!, akalala nao wote wa wawili (2), ikawa 3 some ya wanaume wa  wawili (2) mwanamke mmoja!, Na hayo mapepo amewekewa na hao wakaka!, Wana kazi ya kumfilisi tu! Maana ana-pesa ndefu Sana! So far washamkopa million mia moja (100)!, Hawamlipi ni kumtumikisha kingono tu!, Ni 3 some tu wanamfanyisha za wanawake wawili (2) au wanaume wawili (2)! NA  ALIKUWA NA NDOA YAKE IMEVUNJIKA!,   ACHENI UMALAYA KUNA LEVEL MTAFIKISHWA HAMZIWEZI! , HIZI ROHO WATU WENGI WAMEZIPATA KWENYE UZINZI! NA NDO ZINAWASUMBUA!  MNAKUWA HAMTOSHEKI NA DOSE KITANDANI SASA USHALALA NA SHETANI BINADAMU ATAKURIDHISHA?

Ni Roho ngumu sana kudeal nazo,sababu zinakutumia wewe mwenyewe kujiharibia! zinakufanya kisirani na mkorofi hatari!, zinakufanya umchukie mwanaume wako badala ya kumpenda afu ukimuacha unajuta!

Dalili

  1. Kuota unafanya mapenzi nawanaume hata wanawake muda mwingine!
  2. Kuota una Mume na Familia yako, au unafunga ndoa na watu wa zamani au usio-wajua!
  3. Kuhisi una Pete kidoleni!, Ukiomba Kidole cha Pete kinaumaaa au kuwaka moto!
  4. Kuota upo baharini au mtoni umevaaa crown, au upo na malkia wa baharini/ ziwani au mtoni!
  5. Kuota watu wa zamani, Mababu umefunga nao ndoa na unaishi nao!

MPENDWA KAMA NILIVYOSEMA KUJIKOMBOA SIO KAZI, KAZI KUBWA NI KUWEZA TU KUFUMBA MACHO USIANGALIE PORN SITES! KUBANA MIGUU USIPASISHIWE WADUDU WAPYA! OTHERWISE YESU NI KIBOKO YA KUTOA HAWA WADUDU! UKISIMAMA TU NA MAANDIKO SERIOUS WANA  KUACHIA!

Tabia Hatarishi

Hapa unakutana na HASIRA, UVIVU, UONGO, MATUSl, VISIRANI,UCHOYO, GUBU, MDOMO MCHAFU, WIVU ULIOPITILIZA, JEURI, KIBRI, DHARAU, MAJIVUNO!  ETC

Ndoa basicaly ni idea ya kuishi na mtu ! Na mtu ili akubali kuishi na wewe lazima umshawishi hayo maisha yatakuwa na furaha na amani!! Sasa tabia zako zinatangaza jambo tofauti kwamba kuishi na wewe mtu awe TAYARI KUSACRIFISE AMANI YAKE NA UTULIVU WA NAFSI KU-ACCOMODATE UPUUZI WAKO!  SIO RAHISI! HATA KAMA PISI KALI, PISI YA KWENDA HIO SACRIFICE NI KUBWA SANA  BORA AISHI NA FLAT-SCREEN ILA AWE NA AMANI NA FURAHA!

Tabia chafu mtu hazaliwi nazo! Sometimes ni PSYCHOLOGICAL  inakuwa ni product ya mazingira, life   experience,trauma, Kuumizwa, Disapointments etc. Wakati wa miaka 21 HAMKUWA MAGAIDI AMINI MAMA, MLIKUWA MNAOGOPA MIJOKA YA WANAUME! UKIITWA UNAWAZA WIKI NZIMA! SAHIVI UMEKUBUHU UNAZIPIMA NA SIZE NDOGO NA KUBWA!!, Sometimes ni SPIRITUAL! Maroho yanakuvamia hasa kutokana na uzinzi na ngono zembe, haya maroho wanakuwaga nayo wanaume lakini wanaweza kuishinayo na kuya-balance kama mkemia MKUU! Lakini yaki-kuingia mwanamke ni hatari Sana!,  Mwanamke unakuwa kama dume yaani una balls za kubishana na wanaume na wakatuliaaa!.

Either way Psychological or Spiritual mateso yako palepale!,  Huwezi kuingia mji wa watu wengine ukawapanda Vichwani! Watakufurusha kwenye Miji yao kila leo!, Utakataliwa ukweni kila siku!, Jeuri wafanyie wazazi wako! Kiburi ifanyie Familia yako!, Familia za watu wataungana kukufukuza, ukigoma watakuroga!, Ukijitia nunda wanakurudisha na JENEZA!

Mtumishi mimi NINA HASIRA SANAAA! UTAZEEKA MWENYEWE USIPOKUWA MAKINI! Mwanaume gani anataka kufokewa na ku-deal na Drama zako?, Hamnaaaa! Aki kudate Siku 3 akiona  UNAFOKA-FOKA NA KUMGOMBEZA  KAMA UMEMZAA  ANAKUACHA   KIMYA KIMYA!, MEN HAVE A HUGE EGO!  SASA UNAMPANDA KICHWANI KIVIPI?

Mwanaume anaweza kuwa anakupenda lakini KILE ULICHOMWAMBIA  SHOGA ANGU ANAKUJA KUKUTA NI UONGO ULIOPITILIZA! yaani umemwambia una MASTERS wakati DIPLOMA!,  Hata ungemwambia una DIPLOMA angekupenda hivohivo!, KUNA WATU NI SERIAL  LIERS! unamdanganya una 27 kumbe 36! Akilifuma NIDA lako huna bahati!

Mtu anakupeleka kwao cha kwanza una WANYALI!! Kwanza hawana kitu, Hawajasoma!, Wamechoka choka! DHARAU UNAITANGULIZA!, Ujinga wenu unahisi hawazioni dharau zako!,wanazionaaa! na wanafanya maamuzi MJI HUU HUINGII!, Tabia ya kuhisi una-chitiwa muda wote!, Yamkini ulichitiwa zamani basi kila mwanaume HATA akienda msalani ujue!,  Wanaume wanakuona Binti mzuri lakini akili zako DISHI LIMEYUMBA!, Wana kukimbia!! You are a control freak!

Unavukaje?

MPENDWA IKANE NAFSI YAKO NA FANYA OPPOSITE NA MOYO NA AKILI ZAKO ZINAVO KUTUMA!, Kama nilivosema source haijalishi whether Spiritual or Psychological, ILI WATU WAISHI NA WEWE LAZIMA UBADILIKE NA UKISHINDWA KABISA ATLEAST UWATAPELI KWAMBA UMEBADILIKA AND YOU ARE NO LONGER A THREAT TO THEM!

Kama una mahasira yako hakikisha kabla hujalipuka unamkimbia mwenzio unaenda kulipuka mbele! Kama ni Muongo jifosi kufunga bakuli LAKO! Jifanye mkimya!, Maana ukilifungua tu UONGO PROMAX! USIFUNGUE, Kama ni Dharau usioneshe nje, Cheka-cheka kama mjinga vile lakini moyoni sonya kimya-kimya!, YOU NEED TO    THE MASTER OF YOUR IMPERFACTIONS.

PERMANENT SOLUTION ZINACHUKUA MDA MREFU!

ILI UVUKE JUMLA JUMLA LAZIMA KAMA NI PSYCHOLOGICAL UPONE KWANZA TRAUMA ZILIZO KUFANYA UWE HIVO! UWASAMEHE WALIO KUPUSH ON THE EDGE MPAKA UKA  EVOLVE! NA U- COME TO PEACE WITH YOUR PAST!, IT TAKES TIME LAKINI IT CAN BE ARCHIEVED!

KAMA NI SPIRITUAL! KADRI UNAVYOJIFUNZA NENO NA KUFANYA IBADA ZA MAOMBI NA SADAKA HIO MIROHO INAKUACHIA! UTAJIKUTA ULE MSUKUMO WA KUJIARIBIA HAUPO TENA MOYONI MWAKO ANAKUJA YESU NA SHETANI ANAPUNGUA  MPAKA ANAISHA!, PIA UNAWEZA KUWA UNAZIOMBEA HIZO TABIA CHAFU ZIKUTOKE NA ZISIWE NA NAFASI KWENYE MOYO WAKO NA MAISHA YAKO! OVER TIME UTAJISHANGAAA

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top