Wapendwa wengi wenu changamoto ndiyo zina direct aina ya ibada unazo fanya, aina ya watumishi unaoji-associate nao, aina ya mahubiri unayo-fuatilia!
Wengi ukisikia sehemu CV zitaombewa na mta kanyaga mafuta ya kazi hao, Mahusiano yanafanyiwa deliverance na hatma za ndoa zitaombewa hata nauli utakopa, Lakini ukisikia kusifu na kuabudu unaona hio haikuhusu ni kwa waliotoka kimaisha!.
Wapendwa It is very wrong, UNACHOTAKIWA KUPAMBANIA NI KUUJUA UKUU WA MUNGU IN GENERAL, MUNGU NI NANI NA AMESEMA NINI!, WAPI NA KWANINI!, VINGINE VYOTE UTAPEWA TU KAMA ZIADA!.
Mathayo 6:33
Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia.
Mtu anakuja kwangu nataka mwezi wa Kumi (10) usiishe sijapata Mume, Nasema moyoni, I love the Audacity! Well okay!, Namuuliza?
1.UME OKOKA ?
2.INJILI ZIMO KICHWANI UKO FITI?
3.NYARAKA ZA MITUME?
4.UMEBATIZWA KWA ROHO MTAKATI FU?
AKIPIGA HAPANA KOTE, NAFUNGA BIBLIA NAJUA HAMNA BIASHARA!, SIO TU MWEZI WA KUMI (10) HATA ZIPITE KARNE TANO, MAISHA NI SAFARI YA NDEGE NA PASSPORT SINA ACHA VISA, SANA SANA NITAMWAMBIA ANZA KUSOMA SOMA INJILI DEAR, YA MATHAYO! MAANA YA YOHANA SIO FOR BEGINNERS.
LAKINI AKIJA MTU YUPO VERE VERE, KUMBE FAMILIA? ; 1. UMEOKOKA ? “SWALI SIO NIMEOKOKA NINA MUDA GANI KWENYE WOKOVU? MPAKA MVII “, 2. INJILI? “, “ZOTE 4 NIMEFUTA NA KURUDIA” , 3.NYARAKA ? “ZIPII?, KAMA ZA PAUL NIMEKAUSHA!, ZA YOHANA NA PETER NIKO FITI KALIKITI, MPAKA TIMOTHEO, YAKOBO NA YUDA NIMESOMA JUST INCASE; NABAKIA WHO IS THIS GUY JAMANI? MBONA KAMA KAPANIA SANA.
Watu wengi mmekaaa NIFUNGULIWE!, NIFUNGULIWE!, for the rest of your life una Ole KESHEA na changamoto tu!
Wapendwa Juzi kuna mfanyabiashara mwenzetu katoa shukrani Tabata huko kwa Pastor!, Everybody is talking about that pastor!; He made her famous! Na kila mtu anataka kujua if he is really that good!, Ushuhuda wenyewe umewekewa sponsor ads, Well si katai ni ushuhuda na Bi-dada nyota iliwakaa.
Lakini Mimi navomjua she was born again way before, Aliokoka kitambo mno-mnoo, Mi nimemkuta kwenye wokovu, And like she was raised in Apostolic churches, Na anapenda mambo ya dini balaa, It’s a hobby!
Kwenye biashara ali-shine mwaka wa kama sio wa Saba(7) niwa nane (8), tangu mimi nimjue, For years alikuwa ana hustle, Na ameokoka na anamtumikia Mungu kwa moyo, Ni wale wapo front kanisani.
Wewe tena, Shoga kidawa, Uone ushuhuda huyo Tabata mojaaa, Kingdom secrets za utajiri!, Mmh!, Hutaki kupitwa!, Huna injili hata moja kichwani, Hata Mwanzo tu hujaisoma ukaimaliza, Achilia kutokaaa, Upo serious hatari na kingdom secrets, Utaona Mungu yupo kimya na watumishi wakishirikiana na waumini wote waongo-waongo tu, Hamnaaa lolote!
Unafanya ibada sanaa kweli lakini ibada zenyewe za kuendekeza NJAA na UPWIRU, Mwaka mzima maombi yako MUMEEE, MUMEEE!, Sio Upwiruuu huo unakupeleka puta mtu mzima mwenzetu?
Atleast njaa inauma vibayaaa,sitaki kuropoka kisa nimeshiba!, Njaa iashafanya nikakufuru mimi! LIVEEE! Nawaambia!, Nilimwambia Mungu Kama hanipi kazi bora anichukue nimechoka kidharaulika! Mimi nami kwa kuendekeza njaaa nilishindikana! ( DON’T GET INSPIRED, IT WAS BLASPHEMY OF THE HIGHEST ORDER) ILA NAHSUKURU MUNGU ALINIPA KAZI THE SAME WEEK!, MY POINT IS NJAA MJIKAZE KAZE, LOOK AT THE BIGGER PICTURE!
UNAWEZA KUJIKUTA HUKUI KATIKA UKRITO KWA KUENDEKEZA NJAA NA UPWIRU KUNA DIMENSIONS HUTAWEZA KUINGIA MAANA YAKE NJAA NA UPWIRUU NDIYO VILIVYO JAZA FIKRA ZAKO!, YOU CANT SER BEYOND NJAA YAKO NA UPWIRU WAKO!
UNAKUWA TOO BLINDED NA SHIDA AU HIO CHANGAMOTO EVEN TO SEE BENEATH IT, WEWE MUDA WOTE NI MUMEEEE! KAZII, FAMILIA! HUPATI HATA APPETITE YA KUSOMA MAANDIKO!, KUSIKILIZA MAANDIKO KWA MAANI BILA KUWA ATTENTION MUME ATA TAJWA HUMOO? HUPATI AMANI YA KUMUABUDU MUNGU WAKO UN-CONDITIONALY! ? UKAJIACHIA NA KUFANYA IBADA KWA RAHA NA AMANI.
Mathayo 6:25-34
“Ndiyo maana nawaambieni, Msiwe na wasi-wasi juu ya chakula na kinywaji mnavyohitaji ili kuishi, walajuu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. Je, maisha ni chakula tu au zaidi? Na mwili, Je, si zaidi ya mavazi?
Ndege wa mwituni: Hawapandi, Hawavuni, wala hawana ghala yoyote. Hata hivyo, Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je,nyinyi si wa thamani kuliko hao? Ni nani miongoni mwenu kwa kuwa na wasiwasi sana anaweza kuuongeza muda wa maisha yake? “Na kuhusu mavazi, ya nini kuwa na wasiwasi?
Tazameni maua ya porini jinsi yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayasokoti. Lakini nawaambieni, hata Solomoni mwenyewe na fahari zake zote hakupata kuvikwa vizuri kama ua mojawapo. Ikiwa basi, Mungu hulivika hivyo janila shambani ambalo leo liko na kesho latupwa motoni, Je, si atawafanyia nyinyi zaidi?”
Enyi watu wenye imani haba! “Basi, msiwe na wasiwasi: ‘Tutakula nini, tutakunywa nini, tutavaa nini!’ Maana hayo yote yanahangaikiwa na watu wasiomjua Mungu. Baba yenu wa mbinguni anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo vyote. Bali, shughulikeni kwanza juu ya ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo yote mtapewa kwa ziada. Basi, msiwe na wasiwasi juu ya kesho; kesho inayo yake. Matatizo ya siku moja yanawatosheni kwa siku hiyo.
SHUGHULIKENI KWANZA NA UFALME WA MBINGUNI NA MATAKWA YAKE, HAYA SASA UNAYAFAHAMU KWA KUSOMA MAANDIKO KILA MARA WITH COMMITMENT KWAMBA NATAKA KUJUA MATAKWA YA MBINGUNI NA KUUFAHAMU KWA KINA HUU UFALME WA MBINGUNI ILI U-QUALIFY KUPATA HIZO ZIADA.
VITU MAANDIKO YALIVYOSEMA USI-SUMBUKIEEE WEWE NDIYO PRAYER LIST YAKO!, LEO NIME CHANA CHANA MIKEKA YENU YA PRAYER POINTS KAMA ZOTE!. VITU MAANDIKO YALIVYO KWAMBIA PAMBANA! KOMAA, PIGA UA GARAGAZA HAKIKISHA UNA-VIFAHAMU WEWE NDIYO HUNA MUDA NAVYO, KATIKA VITU SIO SHIDA ZAKO KABISA MOJA WAPO NI UFALME WA MBINGUNI!.
UNA MIAKA THELATHINI (30) NA UMEZALIWA CHRISTIAN BY BIRTH NA NGUZO ZOTE ZA UKRISTO WAZAZI WAKO ALIPAMBANA KUHAKIKISHA UKIKUA HUWI MPAGANI AMBAYE HANA MUNGU, LAKINI MWISHO WAKE UMEKUWA PAGANI BY CHOICE!
KUSOMAA UNAJUA, MACHO UNAYO, SHULE UMEENDA UPO-FLUENT IN ENGLISH AND SWAHILI, EITHER WAY NENO USHAAMUA HUSOMII NG’OO, HATA SHETANI AKITAKA AKUUWE ILA KUSOMA NENO KWAKO NI NEVER, KILA KlPANDE CHA JUMAPILI KINATOSHA MBONA , MPAGANINO MWENYEWE KWENYE UBORA WAKO, ONLY PAGANS NDIYO HAWANA HAJA YA KUSOMA MANDIKO, SO KAMA NI MKRISTO NA NENO HUSOMI AUTOMATICALY NI PAGAN BY DEFAULT.
Wakristo wapagani wengi mimi wananikausha uzazi tu, MTU anataka Mungu amfanyie mambo makubwa sanaa!, Una muuliza swali dogo tu! ” WEWE MUNGU UNAMJUAJE? WHAT DO YOU KNOW ABOUT GOD?”, UTAJI-SURPRISE! Unapata majibu NO WONDER THE REQUESTS!, Anadandia train kwa mbele, Same applies kwa Shetani!
Wengi wapana sanaa Mimi nataka kumshinda shetani, asinizoee wakati haja invest muda kusoma na kumuelewa, Mumjue kwa kina ni nani na nini kime andikwa juu yake!?; Wengi hamjui alikuwa Malaika na alikuwa na nafasi Mbinguni na hadhi yake, Kabla hajaleta ubabaifu na kutaka kupindua serikali Kuu! So hayo maandiko wewe unayo jivuta-vuta kusoma yeye anayajua nje ndani, Hizo Mbingu wewe unaona uvivu kuzisoma yeye ali-taradadi ndani yake kwa muda wa kutosha na uongozi akashuka.
SASA JITU LA HIVI UTALISHINDA KIZEMBE KWELI? THUBUTUUU!, JITU LILILETA UASI MBINGUNI ALIPO MUNGU ITAKUWA KWENYE MAISHA YAKO YA MCHONGO MCHONGO?, UKISOMA NA KUMJUA KWA KINA HUTA MU-UNDER ESTIMATE!, THE FACT UNAJUA MPUUZI ANALIJUA NENO YOU WILL TREAD VERY CAREFULLY KABLA HAJATUMIA HILO HILO NENO KUKU-DEFEAT.
WEKEZA MUDA KUJENGA IMANI YAKO KWA MISINGI IMARA, ISIWE BASE LESS, UKIANZA LEO KUSOMA AYA TATU (3) KILA UKIAMKA AU KABLA HUJALALA NDANI YA MWAKA UTAKUWA MBALI SANAA!
SASA HIVI KUNA BIBLIA HADI KWENYE SIMU YAKO, KUNA AUDIO VERSION UNASOMEWA UNA SIKILIA KWA WENYE IPHONE ZENU, USIPO SOMA MAANDIKO UMEAMUA MAKUSUDI KABISA KUWA PAGANINO.
HUWEZI KUSEMA MUNGU WAKO WAKATI KUMSOMA UMEGOMA WAZIWAZI, BY DEFAULT UMEMKATAA MUNGU NA KUSHADADIA UPAGAN!; MUDA NA BUNDLE LA NETFLIX UNALOO! LA KUSOMA UMBEA INSTA UNALOOO!, LA KUSOMA MAANDIKO HUNAAA!
KWA TUNAO SOMA MAANDIKO TUNAJUA FOR A FACT MUNGU HANA SHIDA NA IBADA ZENU ZA UBABAIFU NA KUBEMBELEZANA, ANA JESHI LAKE LA MALAIKA SERAPHIMS NA CHERUBIMS WANAFANYA IBADA ZILIZO NYOOKA 24/7 ZENYE VIWANGO VYA MBINGU SIO DUNIA.
WEWE NENGENEKA TU,TAMBA UTAMBAVYO ILA IPO SIKU YAKO PRINCE OF THIS WORLD, KING OF THE FLESH RELIM ATA KUMINYA PABAYA SANA MPAKA MAJI UTAITA MMA NA MBINGU UTAZIONA KARIBU KULIKO ULIVYO-DHANIA.
DAY 9
Wakolosai 1:13
Naye alituokoa kutoka kwa nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wake mpendwa.
PRAYER POINT
Bwana Yesu, Roho Mtakatifu maandiko yanaesema tutaokolewa kutoka nguvu za giza na kuhamishiwa katika Ufalme wa Mwana wake mpendwa NA CLAIM HILI ANDIKO JUU YA MAISHA YANGU SASA, JUU YA CAREER YANGU, (CHANGAMOTO YAKO YOYOTE) in the Mighty Name of Jesus.