
Yesu alikuja duniani ili tuwe na uzima na tuwe nao teleee.
Hakuja ili tuwe stuck in dreams, visions, wishes, imaginations nor any other forms of spiritual results that are not tangible.
John 10:10
“The thief comes only to steal and kill and destroy; I have come that they may have life, and have it to the full.”
Anything short of “life to the fullest” isn’t Jesus. It is devil all over. Inakuwa kuja kwa Yesu miaka 2000 iliyopita hakukuwa na maana yoyote kwako wala hakukuwa na impact yoyote.
Jesus did not die on that cross so that you can be half happy, half satisfied, or half anything. Zingatia “have it to the full.” It is either the full or nothing baby. Jesus left no middle ground, no gray areas.
It is either you have life or results to the full or you don’t. Don’t get sentimental with Jesus. He set the record straight.
I was not raised pentekoste, mostly pagan and a little bit catholic and lutheran. I joined pentekoste. I learnt to read at 5 years, nobody encouraged me to read the Bible nor discouraged me.
Nothing good ever came from growing up pagan zaidi ya kurithi roho michafu tu na maagano lukuki. Lakini katika kitu upagani ulinifundisha ni kuweza kutofautisha kuwa na matokeo halisi na kutokuwa na matokeo clearly.
I hear pentekoste always talking about things being already done in spirit and I’ll be like maybe because I was not born pentekoste I am not pentekostal enough yet. “Done in spirit?” What in the broad daylight lies edition is that?
Because we can’t see in spirit and judge for ourselves ndo mnataka kutubeba ufala? You bring us to the gray areas so as you can defeat us with endless theories and no results whatsoever. People of God please.
Jesus miracle results were instant. They didn’t need a three-month gestation period. Seen in broad daylight by all, not only the spiritually capable. Why your own only you can have a sneak peek spiritually or only in your wildest dreams?
Kuna mtu nimetoka kuchambana nae muda si muda, kaniandikia ametoka kuona maono ya siku yake ya mahari very detailed. Lakini in reality yupo stupor single ile single to stupor. Ananiambia nimpe maelekezo juu ya hayo maono. You know me people, I can never lie in the name of the Lord.
Huyu mwanangu amefanya deliverance tatu so far na bado yupo single vile vile. Okay to be fair, maeneo ya ajira amevuka sana sana. Ana kazi mbili serikalini nzuri. Kwenye nchi hii kupata kazi moja tu ni issue. Ndiyo maana yupo stuck with me. Kwanini kwenye kazi kuitike na kwenye mahusiano yagome?
Issue kubwa huyu mwanangu ni mjua-ji hatari na msomi. Msomi huwezi kumpelekeasha dada. Unahitaji facts na reference kama una-defend paper ya PhD kumshawishi. Kwenye uchumi nilimkuta daft maana watumishi wa pentekoste si wakali wa uchumi. So kumfundisha ilikuwa rahisi. Alikuwa hajawahi fundishwa na yeyote.
Huku kwenye mahusiano ashapita kwa watumishi wa kutosha. Kichwa kimejaa mafundisho kama yote na kibaya zaidi hayafanyi kazi. Deliverance unaona tatu ni nyingi ila kiukweli ni moja nilimpa. Hakufanya zilizofata. Naendelea kum-extend afanye lakini hafanyi kwa sababu zake. Tumefika tatu.
Deliverance ya juzi alikasirika. Ni muumini mzuri sana na si mbabaifu kwenye matoleo. Sio mtu mtumishi atakayependa kumpoteza. Lakini mimi matoleo yako hayawezi kunifanya nikuweke kama msukule ilhali hupati matokeo halisi. Haina maana. Bora nikakosa matoleo. I work for a living so I can afford being honest.
Alikasirika akaamua kuomba mwenyewe anavyoona. She is experienced maana ameokoka miaka kumi na zaidi. She knows the ropes. Sikukataa. Akaniambia Mungu amemuonesha ana karama ya kuombea watu. Mtu aliyeshindwa kujiombea deliverance hata moja tu anafanyaje watu wengine deliverance? Nikasema ngoja nijuone mimi. Kuishi kwingi kuona mengi kama haya.
In short mwaka umeisha. Yupo vile vile stupor single isipokuwa sasa anaona matokeo in spirit. In visions. In dreams. Makubwa. Mpaka katolewa mahari in spiritual realm. It is a milestone and I am being sarcastic.
Katika kitu nimebaki nacho kutoka upagani ni kutoendeleza haya matokeo katika ulimwengu wa roho yasiyo mature wala kumaterialise kwenye ulimwengu halisi.
Ni kitu kimoja kuona vision rohoni na baada ya muda mfupi ikawa halisi, na kitu kingine kuona mambo elfu rohoni yanayoishia rohoni.
Kuna mtu aliniambia yeye rohoni anaota anashika pesa za kigeni sana. Anaota ni mtu mkubwa sana, tajiri, ana miliki vitu vingi vya kifahari. Alipo hana hata shilingi mia mbovu. Analishwa na dada yake.
Wengine wanaona wameajiriwa na kushika nafasi nyeti kwenye maono. Wanaona ukuu, utajiri, nafasi kubwa kubwa. Usipoona utajiri unaona nini sasa?
Haya maono na ndoto ndiyo yanatufanya tuonekane walokole wote bipolar. Yes, kuna watu wanaona maono kweli wala sio bipolar. Hata mimi mwenyewe naona maono sana sana kuhusu mimi mwenyewe wala sio mtu mwingine.
Issue ya maono ni very complex. Inataka uelewa wa juu sana wa kuweza ku-decipher kwanini umeona hayo maono, logic behind ya ulichoona, na logic behind time factor ya ulichoona. Kwanini wakati huu sio mwingine?
Nabii Elisha anamwomba Mungu afumbue macho Gehazi aone maono ya jeshi la mbinguni dhidi ya jeshi la Waaramu. (2 Wafalme 6:17–20.)
Elisha alikuwa mkali wa maono. Gehazi alikuwa mgeni wa maono. Mungu alimwonesha yale maono kumtuliza wasiwasi na woga tu. Hakukuwa na mpango wowote wa kutumia lile jeshi la mbinguni hata kwa sekunde tano.
Kama Gehazi angekurupuka na yale maono angeona chariots of fire na kudhani imeisha. Kumbe ilikuwa ni show tu. Plot twist Elisha anaomba Waaramu wapofushwe na anaanza kuwachezea kombolela. Jeshi la mbinguni linaondoka bila hata mshale mmoja kurushwa. Utaelewa hujui.
Sometimes Mungu anakionesha unashika pesa za kigeni uache uvivu kazini, uache kujiendekeza, ufanye applications benki za kigeni. Wewe unaanza “I receive.” From where?
Matokeo ya rohoni ni magumu maana kuona sio kupata. Unaweza kuona na ukaishia kuona tu.
Jesus style is the best. Matokeo halisi papo kwa papo. Yesu alikuwa mtu wa kazi. Alionesha kazi, alionesha matokeo. Maneno kidogo, matokeo makubwa. Hakuna aliyepinga matokeo yake.
Matokeo ya rohoni ni old testament. We are in the new testament, agano la uzima wa milele.
John 14:12
Yesu alituambia yeyote atakayemwamini atafanya kazi alizozifanya na hata kubwa zaidi.
Sasa inakuwaje hata yale Yesu aliyofanya yanakushinda? Yesu hakuacha masharti magumu. Aliacha sharti moja tu, amini.
Kuamini nako linakuwa tatizo? Hapa shetani anawavuna kwa kuwawekea doubts tu.
Yesu amesema “don’t be afraid, just believe.” Ishi nalo.
Ukifufua binadamu, mahusiano yako yatashindikana vipi? Career yako itashindikana vipi? Yesu alifufua mtu live bila chenga. Na akatuahidi tutafanya makubwa zaidi.
Kuamini Yesu sio ushabiki. Ni kusoma Injili zote nne, Matendo, Nyaraka na Ufunuo. Agano jipya lote linamhusu Yesu.
Huwezi kusema unamwamini Yesu usiyemjua na husomi maandiko. Huo ni uongo.
Yesu amekupa assignment moja tu: just believe.
Usiogope. Amini tu.