UKIMTAFUTA MUNGU KWA BIDII UTAMUONA

Yeremia 29:13

Mtani tafuta na kunipata, mtakapo nitafuta kwa moyo wote.

 

Mpendwa Mungu alikuwa muwazi kwamba kumpata lazima u-invest moyo wako wote on the process, Hajawahi na hatopatikana kirahisi. Kupatikana anapatikana ila kwa gharama, Siyo ndogo, Umtafute kwa moyo wako wote, Je unamtafuta kwa moyo wote?

 

Wengi mnakata tamaa sababu mnahisi kumtafuta Mungu ni jambo la mara moja, unawekeza kwenye program moja usipomuona basi, Unasusa au unakata tamaa, Mpendwa Kumtafuta mungu ni process!

 

Ukisoma maandiko tofauti tofauti juu ya kumtafuta Mungu utakuta msimamo wake ndiyo ule-ule! Hapatikani kirahisi!, Mimi nimetafuta wepesi wa kimaandiko wa kupita nao lakini Hamnaaa, Sijaupata!, Nilianza na Nabii Yeremia nikaona Nabii Yeremia mnonko-mnonko ukimsoma mwanzo wa kitabu chake mpaka mwisho yupo upande wa Mungu kindakindaki, Nikaja kwenye Mithali wembe  ni ule-ule!, Nikasema nirudi kwenye Torati,wembe ule-ule! Okay naenda Agano jipya lakini bado Wembe ule ule, Basi nikakubali  show.

 

Mithali 8:17

Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.

 

Zaburi 119:10

Kwa moyo wangu wote nimekutafuta,usiniache nipotee mbali na maagizo yako.

 

Kumbukumbula Torati 4:29

Lakini huko,kama mkimtafuta bwana, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote.

 

Mpendwa Key point nikumtafuta kwa moyo wako wote, Maana yake maandiko yako wazi kabisaaa hatopatikana kirahisi, Investment ya moyo wote ina hitajikaaa!

 

Sasa ni rahisi kusema nataka kumuona Mungu kwenye eneo la kazi au ndoa au afya, Ni jambo jema sana lakini sasa hiyo investment ya moyo inakuwajeeee?, Kusema na kujinasibu ni jambo moja kufanya kweli ni Jambo lingine kabisa.

 

Tena unavyoweka deadline fupi maana uko tayari kuinvest massively ndani ya muda mfupi kwenye hiyo agenda, Kujisemesha namtafuta Mungu sana eneo la ndoa ni jambo moja na kumtafuta kweli kwa moyo wako wote ni jambo jingine kabisaaa na Je, Maandiko yanaposema kwa moyo wako woteeee yana maanisha nini?

 

Ni muda gani katika masaa yako 24 unatumika kumtafuta Mungu eneo hilo la mahusiano au kazi? Daki ka 20?, Kama muda mwingi unatumia kufanya mambo yako maana moyo wako upo kwenye mambo yako ya netflix and chill!.

 

Mawazo yako kwa asilimia ngapi yana mtafakari Mungu, ukuu wake, uweza wake, maandiko yake ? Kama unatafakari mabwana walio kuacha na kuku-umiza sasa hapo una-invest kwenye uchungu!, Imaniyako ime-egamia wapi kwenye hilo swala la mahusiano? Kwamba Mungu atakushindia na hili jambo analiweza kabisaaa na atalifanikisha? Au Mungu amekuacha njia panda, unadhalilika, na kufedheheka, unacho amini ndio kitakacho thibitika kwenye maisha yako.

 

Rasilimali zako unazitumia kujenga ufalme wa Mungu ili tu kujipendekeza kwa Mungu, sawa mambo sio mambo lakini Mungu mimi nina nia kabisa, Au unazitumia kuwahonga vingasti, Sadaka 2000!, Kingasti iphone 15 pro max!!,Kingasti akijisemesha tu amekwama ni miamala ya  nguvu, Mtumishi mate yatamkaukaaa!

 

Wewe tulia tafakari unamtafuta Mungu kwa level gani? Kwa moyo gani? Wote au vipisi-vipisi! Alafu fanya maamuzi ya kumtafuta kwa moyo wote. Mpendwa Mimi mwanzo nilijua Mungu ana upendeleo na ana watu wake, Lakini ukweli ni kwamba Mungu ni Mungu wa haki, Ukiona mtu amepata kitu jua alifikia viwango!

 

Mpendwa nilianza utaratibu wa kiwaualiza watu wanaofanikiwa ulifanya ibada gani, Hapo ndiyo kwenye utamu, Na hapo ndo nilipojua kuwa mimisipo serious hata kidogo!. Mwanzo kabisaaa wakati naanza biashara, sikuuza week nzima, Nilikuwa naomba kawaida, Bila bila, Nikamuuliza kaka mmoja nyie wenzetu mnafanyaje? Akaniuliza utawezaaaa? Nikamwambia niko fit!, Akanipa mkeka wa maombi! Unaomba dakika 5 kila lisaaa! Kwa masaa 12!, Sio mchezoooo!, Nikaenda mpaka saa 6 mchana! Nikapata oda 1, Kufika saa 12 nina oda 7! Mmmhhh!, Nikasema hili balaaaa, Nilikuja kushindwa!, Njaa  ikizidi naombaaa! Ikipungua narukaaa rukaaa, Mwisho Nikashindwa kabisaaa!, Yule kaka nitajiri sanaa!

 

Kuna kipindi ndugu yetu tulikuwa nae kajichokea, Ghafla akaanza kupata nafasi kubwa!, Mara manager, senior manager! Mara paap !Director, Tukamfata tupe mkekaaa huo! kwani Haiwezekani!, Akatuambia mimi nimeokoka sahivi!, She was bad baaad Mtawezaaa?, Tukamwambia for CEO position mbona na kwaya tunaimba kabisaaa!

 

Akaongea kabisaa na pastor wake mnigeria, Baba ana mashauzi hatari!, Alafu  kakutana na sisi vichwa Vibovu, Siku 3 tukafurumushwa na kufukuzwa, Ofcourse we were bad sheep, Lost sheep, Mnigeria was hardcore pastor! He doesn’t condone any nonsense, Hatakiku fundisha mtu miaka 3! yaani ni 3 months max na kama hupati results ana kufukuza vile-vile,Anataka A – list students and A-List only!

 

Mode ya huduma yake anataka watu wachache ambao watakaa position kubwa kubwa sana ambao zaka zao ndo zitaendesha kanisa na kwa hao watu ana invest kweli-kweli kuhakikisha wanadumu kwenye hizo nafasi na hawamzingui, Then muda mwingi anatumia kuponya wagonjwa na kutoa watu mapepo!, Healing ndo kitu alicho kuwa anapenda kukifanya sana na healing haina maslahi!, Maana mimi mwenyewe kuna ndugu yangu ( RIP) alikuwa anaumwa sanaa. Akaenda pale kuponywa na alikuwa hana nauli, akaombewa na pastor akampa elfu 30 ya kula na nauli!Maana alienda asubuhi akatoka usiku.

 

Sisi tulifukuzwa sababu alituupa vitabu vya kusoma, hatukusoma. Kuja siku alisema tubakie usiku! Ikafika saa 6 tukaondoka tuliona hatajua akaona humuuu kwetu anapoteza nguvu zake tu, Akatufukuza, Tuliumiaaa sana, For real!, Na mission yetu ingekuwaje? Tuliomba msamaha lakini wapi ??

 

Tulifadhaika sana, Nikamwambia mwenzangu tutafute mtumishi mwingine tukawe chawaa, This time mtumishi akisema ruka hamna kuuliza kwanini? Is it safe kuruka?, Jibu letu kulia au kushoto, Akisema soma kitabu cha Mwanzo! maana yake hapo break ni baada ya vitabu 5 vya Musa!, Soma Injili Humalizii Injili ipi! Unakongota zote mama. Akiuliza doctorine unaichambua angle 4 za vitabu vyote 4 vya injili!, Akisema sadaka! Tunamuuliza yeye hii itatosha au tuongeze ?.

 

Hapa tulikiwa kwelikweli tumeamua kwa dhati kumtafuta Mungu kwa mioyo yetu yote, Kuja siku tuliambiana mimi siendi na yeye kasema haendi! Tulikutana kanisani.

 

Watu wetu wakaanza hamna akili nyieeee! Tuna waambia ni kweli mwenye akili sim-meona kwenye media kawa CEO, We went same school, same class! Kweli akili hatuna ndiyo tunapamabana kufunguliwa ufahamuu, We jiunge na sisi  au utabakia mwenyewe.

 

Mwingine akasema ama kweli walokole wachawi, Nyieeee magaidi mme-okoka?, Ama kweli shetani akizeeka anakuwa malaika, Pamoja na vyote juju limetumika kuwatuliza nyiee sio bureee, Mpaka mmekuwa kondoo wa bwana ?

Tukamwmabia hamna juju lolote!, Tumejipata tumechokaaa na hali zetu unataka matokeo, Tupo serious tunamsaka Mungu, yaani hata Pastor akifa moto wetu ni huu-huu, Tushafanya maamuzi hatuwezi kurudi nyuma!

 

Mwanzo watu walichekaaa na kutubezaaa sana, Tulivyopata matokeo ukaanza usumbufu, Mbona mmeniacha jamani mbona mna-tutengaaa!, Tukawamabia nyie si mlisema sisi tuna tapeliwa?Oooh hata sisi tupo tayari kutapeliwaaa! Lakini msituacheeee Misri, We are relatives by blood.

 

Juzi hapa kuna mtu alikuwa anataka kitu Mungu amfanyie ghafla sana, Nikamwbia sali siku 3 mfululizo! Akasema mbona jambo gumu! Nikamuuliza unalotaka rahisi?, Kapiga moyo konde! Alitoboaaa! Na alipata hitaji la moyo wake.

 

Kama unataka kumtafuta Mungu usikurupuke!, Jitafute ndaniya moyo wako!, Fanya maamuzi kwa muda wa kutosha ili uyasimamie maamuzi yako!, Kukurupuka utakosa consistency! Na utakata tamaaa na kuanza upya mara kwa mara, Mwisho utakata tamaa kabisaa!

 

Bora utumie muda wa kutosha kufanya maamuzi na uelewe kwanini unafanya maamuzi hayo,na yata kugharimu vipina moyo wako ukiridhia ndiyo uyafanye sasa kamili lakini Ukikurupuka utaenda siku 2 baadae ndiyo utajiuliza  hivi kwanini nateseka hivi?, Utaacha! Baadae unajilaumu kwanini Uliacha.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top