Luka 8:40–51
ISSUE ZA MDA MREFU ZINADRAIN IMANI SANA!
Issue za mda mrefu zinachosha sanaaa imani ya mtu.
Na hapa ndo shetani anatupigiaaaa!
Issue unayopambana nayo ikikaza kidogo tu —
kwani kukata tamaa sh ngapi?
Unaanza kuavoid hata kwenda mbele za Mungu!
Sometimes hata mbele za watumishi unaona unawachosha,
mafuta ya watu unayakausha bure!
MWANAMKE ALIYETOKWA NA DAMU — 12 DAMN YEARS!
Huyu mama mwenye issue ya damu…
Tatizo lake lilikuwa miaka 12 damn years!
Na si tu kwamba alikuwa mgonjwa —
alifilisiwa kila kitu!
Waganga walimkwangua mpaka pa mwisho
na bado tatizo halikupepesa kope!
Sasa unaweza kujiuliza —
Why sneak on Jesus?
Kwanini asingeenda kama wenzie walivyofanya?
Omba kistaarabu? Apewe upako in peace?
Kwa desturi za Kiyahudi, huyu mama alikuwa najisi.
Alitakiwa akae mbali na wanaume na mikutano.
Aliogopa — maybe Yesu angemhukumu
kwa kuvunja taratibu.
SHE PLANNED THE IMPOSSIBLE HEIST
The risk was huge.
The penalty was hard.
But that didn’t stop her!
Ilikuwa mission planned kabisa:
“Nikimfikia tu, nadokoa upako na kusepa fasta!”
Nothing was going to stop her:
-
Not the sickness
-
Not Jewish traditions
-
Not the penalty
Being this vigorous after 12 years of failure?
Hii ni level nyingine ya imani!
WENGI WENU MNAJIENDEKEZA KUKATA TAMAA KIJINGA
Just because ulifail before doesn’t mean anything!
Unaanza na risala:
“Mtumishi, shida yangu… Dunia nzima wameshindwa! Sijui hata mbinguni…” 😒
Unataka nini sasa?
Kumtisha mtumishi? Kumtetesha?
Ushamkausha mafuta!
Bora ungem-surprise tu! 😂
Mimi akija mtumishi mpya, nawasha mbio na wapangia wenzangu kabisa:
“Today we are not the usual suspects.
Let the man or woman of God waooh us!”
Don’t kill the vibe! 😤
WE DIDN’T LIE, WE JUST WITHHELD MAJOR INFO 😅
Sometimes tunabackfire, watu wanasema tumemdanganya mtumishi.
Lie? HELL NO!
Withholding info? YESSSS!
Si kusema ni kudanganya — we just left out some minor (maybe major) info 😇
MNA SUSA ILI MUNGU AKIMBIE SAA ZENU
Mwingine ulikuwa unataka kuolewa at 26, ikashindikana,
at 29 — nayo imepita, sasa unasusa!
Na haususi kwa sababu hautaki tena kuolewa —
unasusa kwa sababu unataka kumpeleka Mungu atoe kile unataka kwa wakati wako.
Which is:
-
Diabolical
-
Ungodly
-
Unscriptural
UNA MUNGU UNAMPANGIA?
Mungu alishasema:
-
Atakachofanya
-
Muda atakaofanya
-
Jinsi atakavyofanya
Na kaandika wazi kwa maandiko ambayo hujasoma
wala huna mpango wa kusoma!
Wewe kila siku unajaribu kumpangia Mungu,
na kila ukimpangia — anapangua.
Una n’gaka siku 3 — then unarudia jambo lilelile.
“MDA MREFU” SI SABABU YA KUPWAYA KIROHO
Mtu anakwambia:
“Mama hili jambo ni la mda mrefu.”
So what??
Kwa ulimwengu wa roho it means nothing!
Na tukiforce — ina mean we are lazy, blind, na hatuna imani!
Otherwise, how do you explain your consistent lack of results???
UFALME WA MUNGU HAUFANYI KAZI KWA HISIA ZAKO
“Mama nasikia uchungu sanaa…”
In the spirit world — that means NOTHING!
Other than screaming:
“I’m a weakling, demons will finish me sooner or later!”
Mathayo 11:12 (KJV):
“And from the days of John the Baptist until now
the Kingdom of Heaven suffereth violence,
and the violent take it by force.”
Ufalme wa Mungu unafanya kazi kwa maandiko!
Spiritual laws zinatoka kwa maandiko.
Na hizo laws ndo zinatawala ulimwengu wa roho 24/7!
JESUS WASN’T MOVED BY HER STORY – JUST HER FAITH
Yesu alihisi nguvu zimemtoka — maana mtu ali-perfect spiritual law!
Hata baada ya kumjua mdokozi wa upako wake,
YESU HAKUONEWA HURUMA NA HISTORIA YAKE.
-
“Alikuwa mgonjwa miaka 12…”
-
“Alifilisika…”
BLAAH BLAH!
None of that moved Jesus.
Absolutely NONE.
Yesu aliguswa na imani tuu ya huyu mama!
Ndo ka-comment on that ONLY.
PEOPLE WANT TO TELL YOU THEIR STORY – NOT THEIR STRATEGY
Watu wengi:
-
Hawana interest ya kujadili solution
-
Hawana interest kuambiana what they’re doing spiritually
-
Wanataka tu tukuonee huruma
Yesu hajishughulishi na details za ordeal — HE SOLVES!
God performs HIS WORD — not your emotions!
Na Neno la Mungu si weak!
Ukijielekeza kwa weakness —
you hinder God to perform!
12 YEARS, STILL SHE DIDN’T QUIT!
Mwanamke huyu:
-
12 years of bleeding
-
Jewish rejection
-
Zero energy
-
Financially broke
Still she fought through the crowd — aka fika kwa Yesu!
She did NOT indulge in weakness —
hence she was on the faith level God could perform in.
“Moyo wangu umeinama”… 🙄
“Mama, moyo wangu umeinama kwa kweli…”
Ni sawa na kusema:
I am doomed, I am cooked!
“Tafuta shamba ukalime.”
YAIRO ALIKATAA KUKATA TAMAA
Yairo alipoambiwa mtoto wake amekufa —
YESU akamwambia nini?
Luka 8:50:
“Lakini Yesu aliposikia hayo, alimjibu,
Usiwe na hofu, amini tu, naye ataponywa.”
Wengi wenu mambo yenu yamekufa
sababu mmeacha kuamini.
Mmeamua tu kuzika hiyo issue.
“Basi, ndoa isha isha.
Kazi isha potea.
Uzazi hauna nafasi.”
Mmekubali hukumu!
Mnaishi tu kusambaza UKIMWI na stress!
UMEAMUA KUWASIKILIZA WAJA BADALA YA YESU
YESU alimwambia Yairo:
“Usiogope. Amini tu.”
Na waombolezaji walifanya nini?
Wakamcheka mpakaa!
Lakini YESU alijua — mtoto halala, hajafa!
Sasa na wewe:
YESU anakwambia:
“Ndoa ipo. Mume yupo. Tarehe ya harusi iko pending tu.”
Waja wanacheka na kusema:
“Huyu ni msaka bwana!”
Ni juu yako sasa:
Uwaamini wao au umuamini Yesu mwenye mbingu na enzi zake?
WAJA WAKIKUCHEKA – TUPILIA MBALI!
Yesu alisema:
“Usiogope. Amini tu.”
Na vicheko vya waja havijawahi kumbabaisha Yesu kamweeee!
Ukiwaamini waja —
pole zako!
Wajakuvuruga mpaka utavurugika kabisa!
Hapo ndo intro tu!
MAKE THIS DECLARATION – DAILY!
If you believe Jesus for marriage, job, healing, children, finances —
Chukua andiko hili:
Luka 8:50
“Lakini Yesu aliposikia hayo, alimjibu,
Usiwe na hofu, amini tu, naye ataponywa.”
Na tangaza hivi kila siku:
“Bwana Yesu, sawasawa na andiko hili, SINA HOFUUU!
NAAMINI…
Nitaolewa ndoa takatifu
Nitapata kazi
Biashara itakua
Maradhi yatapona
Nitapata mtoto
(wewe jaza yako hapa!)
Amen!”