Watu wengi mnaona kama kuna vibe la kuokoka linalotembea—ni kama movement flani, revival ya kipekee. Mtu akiingia humo, hawezi kutoka kirahisi. Hata kwa “grader”! Ni kama hawako kwenye mfumo ule wa zamani tena—they’re not the same people anymore!
Unapouliza, unaambiwa ni Biblia tu inayowabadilisha. Lakini na wewe unayo Biblia, unaisoma—chapters mbili, tatu kwa siku. Sio haba. Lakini mbona huo uamsho haukupati? Huo vibe wanaupata kitabu gani? Unaweza kuanza kudhani wanadanganya. Lakini matokeo yao—their fruits—hayadanganyi! Hapo ndipo unapata kuvurugikiwa kichwa kabisa.
Biblia ina maagano mawili: Agano la Kale na Agano Jipya. Mtumishi mmoja aliita Agano la Kale kuwa “Agano la Wafu.” Na kiufundi, kuna ukweli humo! Tazama: mbali na Eliya, wengi walikufa na “kulala na baba zao.”
Lakini Agano Jipya? Lote linamhusu mtu mmoja tu: YESU KRISTO, Mwana wa Mungu aliye hai! Kuanzia Injili hadi Ufunuo—ni Yesu tu anaongelewa.
Na huyu Yesu? Yu hai! Ameketi kuume kwa Baba yake Mbinguni. Alishinda kifo fully, na akatupa password zote za kuushinda ufalme wa giza! Na hakutuacha yatima—alituachia Roho Mtakatifu, ambaye yupo 24/7 kutuwezesha ku-access mbingu LIVE!
Agano Jipya ni agano la walio HAI. Ni agano la live interaction na Mbingu. Sio kama zamani ambapo mbingu zilikuwepo tu kwenye mawingu, sasa zimekuwa karibu kuliko unavyofikiri. Kila mtu anaweza kuzi-access—ni uzembe wako tu!
Na hii access? Haitolewi kwa rushwa, michongo wala shortcut. Inakuja kupitia ibada zilizo nyooka na endelevu. Kama nilivyosema: Kila kitu katika Agano Jipya kinamzunguka Yesu Kristo. Yeye ndiye PASSWORD. Ukimzunguka Yesu, huendi popote.
John 14:6
“I am the way and the truth and the life. No one comes to the Father except through me.”
Ukisoma Wagalatia, Warumi, na nyaraka za Paulo, ndipo unaelewa kwa undani YESU alimaanisha nini.
Warumi 3:21–26
21 Lakini sasa, njia ya Mungu ya kuwahesabia watu haki pasipo sheria, ambayo sheria na manabii huishuhudia, imekwisha dhihirishwa.
22 Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa kumwamini Yesu Kristo.
23 Kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
24 Wote wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa ukombozi ulioletwa na Yesu Kristo.
25 Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake…
Wengi wanajaribu kuishi imani nje ya maandiko. Hakijui kilichoandikwa, hivyo hafuatilii kilichoandikwa. Anaishi kwa general knowledge—ambayo haijui hata imetoka wapi! Lakini general knowledge haitoi matokeo. Sababu? Unachokijua si kile ambacho Mungu ameahidi, na kilichoahidiwa hujakijua kwa sababu hujasoma maandiko!
Mungu alisema utaolewa, ndiyo.
Lakini aliagiza pia usizini!
Ule upande wa “don’t sin” hujali, lakini bado unadai ahadi? Huo si upofu tu, ni ubabaifu wa kiroho!
Sheria ya Mungu ni ngumu—ni nzito. Soma Warumi 1, 2, 3… utahisi maandiko yanakusuta live! Lakini ukifika Chapter 3, ndipo unapewa PASSWORD! Kwamba imani bila Yesu ni next to impossible!
Yesu alikuja kutimiza yaliyokuwa pending. Alikuja kusahihisha misconceptions juu ya Mungu. Alikuja kufungua portal kwa watu wote kumkaribia Mungu.
John 4:23–24
“But the hour cometh, and now is, when the true worshippers shall worship the Father in spirit and in truth…”
Mtume Paulo aliweka wazi mambo matatu makubwa:
- Kuna njia ya mtu kuhesabiwa haki pasipo sheria.
- Njia hiyo imekuwepo tangia Agano la Kale.
- Njia hiyo ni kumwamini Yesu Kristo.
Sheria za dunia na za ukoo wenu zinasema hamuwezi kupata mema. Lakini hii njia mpya inavunja hiyo sheria. Inashinda “pattern” ya familia yenu!
Mtume Paulo anasema:
Warumi 3:22
“Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa kumwamini Yesu Kristo.”
HALLELUJAH!
Wengi wanasema: “Namuamini Yesu!” Lakini hawajawahi kusoma Injili hata moja. Unamwamini nani ambaye humjui? Unaamini kitu gani ambacho hujawahi kusoma?
Unaweza kusoma digrii nzima, lakini Injili nne tu unashindwa? It is diabolical. Shameful!
The devil keeps trying you, and you keep failing—yet still, you won’t read any Gospel books!?
Maisha ni rahisi. Ugumu mnaoleta nyinyi. Hakika:
“Haki hiyo hupatikana kwa kumwamini Yesu Kristo!”
Hicho vibe, hiyo movement, huo uamsho unaousikia? Uko hapo! Ndani ya Yesu.
Romans 6:14
“For sin shall not have dominion over you, for you are not under the law, but under grace.”
We are under grace, honey! Not just any grace, but the grace of the Living God!
Nimeamua kumfuata Yesu—SITARUDI NYUMA!
Kuna nabii mmoja mwaka mzima anatoa “prophecies za giza” kwa familia yetu—doom after doom! Lakini kwa sababu najua maandiko, nikabatilisha kila upuuzi huo! Nikatangaza mimi ni nani ndani ya Kristo, nikajifunika na Neno.
Proverbs 4:18
“But the path of the just is as the shining light, that shineth more and more unto the perfect day.”
Ujinga wake ni kuuliza kama nimeshaanza kufilisika! 😤
Anashindwa kuelewa kwamba ninapumua Neno la Mungu!
I breathe the Word of God.
ubarikiwe sana mtumishi wa Mungu,hiyo roho iliyondani yako ije mara dufu juu yangu na kutenda kazi zaidi,udhihirisho NAPUMUA NENO LA MUNGU,NA NDANI YANGU KUNAWAKA MOTO.
Napokea hiyo roho kupitia hili fundisho.
Amen