Next Level

Wapendwa msema kweli ni mpenzi wa Mungu, sijapata encounter yangu ya Exodus! Siku ya 2 ibilisi alinikalia kooni na kufanya blander moja matata. Na kati ya mfungo huko alinikalia kooni nikawa nafanya blander ndogo ndogo endelevu. Akaunajisi mfungo wangu wote.

Kupata nimepata vingi sana tu lakini kuna gharama za kushindwa kufikia expectation so what I wanted most sikupata kwa wakati. Unfortunately! Haimanishi nimekosa ila itanigharimu muda Zaidi kusubiri.

Kuna option ya kuendelea kusubiri, of which am not patient person. Na kuna option ya Kwenda NEXT LEVEL .You can only go to next level kama teari uko level Fulani. So kama ulifanya exodus matokeo hujarizika nayo karibu unisindikize kwenye NEXT LEVEL.

HATUFUNGI! NI 15 DAYS OF DECLARATIONS, AFFIRMATIONS NA MAOMBI YA KUMTUKUZA MUNGU KWA MAPENZI YAKE ANIVUSHE. TUNAOMUOMBA MUNGU MAPENZI YETU YAWE MAPENZI YAKE.

Day 1 :Next Level

Isaya 41:10

Usiogope, kwa maana mimi ni Pamoja nawe; usifadhaike,kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

NEEMA INAYOKUPA BREAKTHROUGH SIO NEEMA ITAKAYO KUFANYA UDUMU

Watu wengi wanapata breakthrough na kufunguliwa, wanaoshuhudia ni tone tu. Wengi mambo yakishanyooka wanna unfollow! It is very okay. Lakini shetani ni yule yule. Anapata kazi hasemi, mimi ni furaha yangu kutokukuona DM believe me. Anaenda kazini anagundua shetani la kazini ni shenzi kuliko la nyumbani.

Anakumbuka huduma, anaanza mamy unajua ile kazi nilipata 2 months ago lakini……..! Mmmmh! Kuna mtu march alikuja kwa Habari ya kazi. Kapata kajikausha. Katolewa kazini anataka tuzime moto. Too late.

Mtu sahihi watu wengi walipata watu wa maana. Baadhi walisepa, baadhi walikaa kidogo kusikilizia, maana it was too easy. Mtu haamini ndo hivi tu. Kiraisi raisi tu. Wachache waliobakia wengi wako stage nzuri za utambulisho, mahari tarehe zimetoka. Waliozima data wanaludi nyumbani, Wamegundua neema ya kumpata mtu sahihi sio neema ya kudumu nae.

Sisemi muwe tegemezi hata msiende chooni bila kuniambia,  I am a cool pastor! Ukipata aim for the next level.

Neema ya kukupa kazi sio neema itakayokufanya udumu kazini, wala uwe boss. Neema iliyokupa vyeti sio itakayo kupa kazi.

Neema itakayokufanya upate mtu sahihi sio itayofanya mdumu, wala sio itayofanya uolewena sio itayofanya ndoa idumu.

Wengi mkipata mtu sahihi, mnajua apa deal done. Vyote nilivotaka in a man is okay.Basi Anasahau mtu kumtoa madhabauni, anakimbilia uzinzi, na kupeleka mambo kmjini! Sisi Watoto wa mjini og , kino moko tunakushangaa, siku 4 ushampa kujitafunia kaona havina maajabu anakulamba block! Ashaona mke hamna apo. Unaludi mamy yule mwanaume hanitaki . Kwanini? Hamna sababu.

Wanaume wakitaka sex fro m you sometimes ni mtego tu, Kujua je wewe maji mara moja au mtu na heshima zako, Unaona jamani kitambo, Ngoja nichague kidogo. Miaka 6!

Unakubali mnachachuana ana kublock! Unaanza kusingizia madhabau za kwenu. Mizim undo ilikutuma ukachachuane? Unaikemea inasema wee mwanaa wee! Unachotutafuta has ani nini?

Wengine pia wanapata mtu sahihi ila power game hawawezi kuziresist. Na drama. Yaani kuna waty wanakuja kutaka maombi nawachamba huna tatizo lolote acha utoto.

Eti mtu kafunga skiku 7 mwanaume amutafute, mwanaume kamtafuta siku 3 hapokei simu ya mwanaume, kisan a mkasa mwanaume haoni thamani yake. Mwanaume kutembeza block! Pastor nimechanganyikiwa na kudata. Niombe maombi gani. Is there a limit to the drama? Mpaka kwenye mfungo.

Yesu alitabiliwa muda mrefu kwamba ujio wake utakuwa wa neema. Nabii Isaya alizungumza hilo. Akawa anangojewa.

Yesu anazaliwa lakini Helode anataka kumuuwa. Pamoja na kutabiliwa na kungojewa kote bado anahitaji neema ya kuokoka kwenye mikono ya Helode.

Yesu anaanza kazi kwa kupata neema ingine ya ubatizo. Na kuwa anaendelea na kazi zake akikaribia mateso wanatokea Mussa na Elia kumtia moyo juu kilimani.

Akiwa anajiandaa kuteswa Malaika anashuka juu kuja kumtia moyo, na kumpa neema ya kukabiliana na hiyo stage.

So utaona Pamoja na kukabiliwa na kila kitu Yesu kila hatua alikuwa anahitaji Neema Zaidi za kutiwa moyo. Mpaka akakamilisha safari yake.

Hivyo hata wewe neema itakayokuvusha sehemu sio mwisho. Utahitaji kutiwa moyo na neema Zaidi Kwenda mbali zaidiii.

Jenga Uhusiano Wako na Mungu

Naelewa baadhi ni wachaga kiimani, na hakuna aliyezaliwa anajua wote tunajifunza. Ila tupunguze drama. Kwa upendo tu.Mpendwa aliyae anza mapema kabisa kuijua hii stage ni February 2022! Na serious imeanza march. Sasa roughly ni 3 month kama ulikuwa wa mwanzo kabisaaa.Mpendwa 3 month hizi mtu ashaomba na alishakata tamaa kabisa kabisaa!!!! Jamanii!!!! Tuwe realistic hizi 3 month ndo za ku rule out umekosa kabisa kweli.

Yaani hizi 3 month akutane na mtu na atamke ndoa. Inawezekana na imewezekana kwa baadhi . DO YOU HAVE THE FAITH TO BACK UP YOUR REQUEST?

Wengi mnamlaumu Mungu sababu hammjui wala hamtaki mkumjua. You just want things from him. Husband, job, children, riches, power, health, etc,,. You are in for the things you will get.

Na kibaya Zaidi dini ni trend saiz. It is all about followers, likes,  comments and ofcourse THE MONEY! Who makes more. Which pastor is Dop, and has style , who is finer than the others.

Kuweza kupata niche tumejikuta ma pastor tunatumia chupli chupli. We promise what we cant deliver, ukitaka kitu Fulani njo uku. Mimi ndo na upako, Hata matangazo ya makongamano focus ni vitu. Nyota ya mahusiano, kazi nzuri, kufunguliwa biashara…… chambo yule yule.

Mapastor tuna manipulate scriptures to your liking. Yaan Nakata pale tu panaposema utapata kazi, Nakumezesha, na nyinyi mlivo wavivu hamludii kujua ndo hivo tu!  Mara kibao nakosea ku reference wakishtuka wengi ni wa 3 NA like ziko 100+1

Ndo maana hampati matokei, Habari tunawapa nusu nusu na nyie mnaomba nusu nusu.

Kumbukumbu la Torati 28:6

Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.

Mnalibeba juu juu je mnajua chimbuko lake?

Kumbukumbu la Torati 28;1-2

Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidi, kutunza kuyafanyaa maagizoyake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani.

2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.

Kwenye msingi hupajui unajua apo juu tu.Tena unalalamika kabisa andiko halina nguvu. Andiko unalijua nusu. Litafanyaje kazi. Kwenye part yako umejizima data sasa Mungu anatekeleza vipi party yake? Neno ilikuwa 2 ways.

Wekezeni kumujua Mungu, Kujenga nae mahusiano. Kuelewa process zake. Ndipo mtapata matokeo makubwa Sanaa. Hizi chupli chupli zita wa frustrate tu. Mtakuwa heart broken Sanaa.

Ukimjua Mungu kiundani huwezi yumba kiimani. Sababu unajua mambo kwa uhakika. Ikitakiwa kupata kitu unajua kama neema haijatosha unajua.

Hata kama huoni Mungu akifanya kitu kama unajua neno unajua tu yuko behind the scene ana set mambo sababu unajua kabisa Mungu ni mwaminifu for a fact. Ila kama hujui simu isipo ita siku 3 basi shughuli hamnaa! Pastor maombi gani niombe.

Results is a process. For sure hizo hatua ndogo ndogo unazopiga kila siku zitakuja kulipa. Kidogo kidogo situation yako badilika.

Kubali kutambaa kabla hujataka kupaa. Weka nia ya kukomaa na Mungu mbaka kieleweke. Utaona mabadiliko.

Acha kujidekeza na kujiendekeza. Wenzio wanafunga wee umesusa. Wanakesha we unajiendekeza na depression yako. Wanapanda bado unajiendekeza kukata tamaa. Sasa ukikata tamaa haimlazimishi Mungu akupe hiko kitu.

Mungu mwenyew amesema ukinitafuta kwa bidi utauona uso wangu. Wekeza kwenye kutafuta uwo uso. Sio unakalia kujiendekeza mbona Mungu hanioneshi uso wake. Serious?

Pia kuna watu wanaenda mbele na kuludi nyuma. Unashinda njaa siku 7, ya 8 unapata breakdown na kufuta credit zote za siku 7, ya 9 unajuta. Unatakiwa kujikaza kikike. Don’t back down mbaka upate majibu.

Ukitaka kuback down je jiulize UNAWEZA KUISHI BIRA MUME/KAZI/WATOTO?? Kama jibu ni APANA! Mkemee shetani. Endelea kukaza. Kuna kudeka mmoja alikuwa kila siku anakuja DM anajilazimisha mambo bado magumu. Siku 30 nyingi. Nikamuuliza kwahiyo umekubalia kabisa kuwa single mother? Maana muda huna nab ado unaleta mzahaa. Basi nakutakia kila lakheri. Nikamwambia waza kama wee kutokuolewa ni option unaweza kui consider. Alifunga siku 30!  Wakati haikuwa kufunga. Alikuwa commited kama chizi . Saizi amepata mtu washatambulishana maana wote watu wazima hawana haja ya kuzungusha mambo.

Mwingine alikuwa anafilisika tu. Yaani anapata mahasara non stop. Nikamuelekeza kwa pastor mwingine maana niliumia kwamba nimeshindwa kumvusha . Kule hakujibiwa ndo utajua Maisha ni safari na nauli umekula. Akasema enough is enough yale yale maombi niliyompa akawa anajilegeza akayafanya kwa uchungu Sanaa. Yaani alikomaa either atoleweee au hamna kingine ni kuchomolewa tu.

Navo waambia hapa ndoa yake imerudi imara na biashara zake zimeludi top! Kaniahidi ana gazeti la ushuhuda.

Hizi shuhuda ndogo ndogo za saizi ndo shuhuda kubwa za November na December!  Wenzio wakianza kuvaa shela usipate tu BREAK DOWN! Maaana wanamtolea mahari, wanatambulishwa, hizo ni PROCESS, na zinasogea, wanarudiana na wazazi wenza.

Wewe toka kwenye ako ka self pity party kako. Umekaa apo muda gani? Ukiona hupati matokeo ongeza nguvu. Kanyaga mafuta ya kutosha. Kuna level unakuwa serious mpaka mambo yanakubali. Unakuwa commited KWELI  kweli. Unatafuta uso wa Mungu kisawasawa. Hii level ndo inaleta miracles

Kumgoja Mungu Kwenye Jambo Lako.

Sio kitu chepesi kabisaa, kipengele Kizito sana. Watu tunapenda matokeo basi atleast ishara . Wayaudi mara kibao walimtega Yesu kama vipi basi awape ishara toka mbinguni, Basi na wewe ni kiyaudi kidogo kidogo,. Maana unataka ishara kama utaolewa au laah? Ndie mtu sahihi au sie? Wewe tena!

When the time is right! The Lord will make it happen. Isaya 60:22!  Wewe sio wa kwanza kusubirishwa ahadi zako wala sio wa mwisho. Mtumishi mimi nimeokoka! Sawa unamshinda Daudi?

Daudi alingoja miaka 15 kukaa kwenye kiti cha ufalme. Anamuua Goliat akiwa teenager na kupewa binti mfalme kama mke. 1 samuel 16:13 alipakwa mafuta na Samueli mbele ya kaka zake. Mungu ndio anamuelekeza Samueli.

Ingekuwa weee ushapakwa mafuta na Nabii Samueli, na mke umepewa mtoto wa Mfalme ungewaza kuna nini cha kusubiri tena jamanii? Mambo yashaivaaa. Lakini imachuku Daudi miaka 15 kabla ya kukaa kwenye kiti kama mfalme nah apo alipigia mabalaa mengi mnoo.

Ndo maana nawambia mkiona giza kwenye issues zenu mkomae kikike. Haya mambo yapo. Unapimwa character yako je unafaa kuwa mke. Au ndo utakuwa Mrs ma BLOCK! Issues ndogo ndogo una block ukoo mzimaa.

Musa alisubiri miaka 40 kuitwa kuwaongoza waisraeli. Aliuwa akakimbia miaka 40. Anaitwa akiwa na miaka 80! Sasa wewe unakata tamaa ya nini? Mbona mapema sana kusema Mungu haJakujibu?

Mfalme wa yuda Yekonia aliwekwa gerezani miaka 37, Kwanza alitekwa na Kwenda kufungwa ugenini Babeli wakati uvamizi wa Babylonians chini ya Nebukadneza. Ambapo Yuda wanatawaliwa na Zedekia. Ambaye naye mabalaa yamemkuta, nae huyu Zedeki anaenda kufungwa Babeli, na mji wa Yelusarem unabarikiwakabisa na watu wengi wanapelekwa Babeli utumwani. Yuda inakuwa tena sio ufalme bali ni koloni la Babeli.

Yekonia yuko zake kwenye Prisons of Babylons kitambo, anatumikia tu,. Miaka 37 utawala wa Babylon/Babeli unabadilika na mfalme mpya wa Babeli anamtoa Yekonia jela na kumkaribisha mezani pake na analipwa posho ya Ufalme siku zote za Maisha yake zilizobakia. 2WAFALME 2:26-30!

Sasa wewe siku 2 au vimiezi 6 vya kususa na kuzira kuacha ibadaa. Mungu hakusikii? Kweli uko serious. Ndo maana nawaambia nyie Mungu hammjui afu mnataka kumtumi akufanya makubwa. Mjueni kwamba vizuri ndo mtakuwa na adabu na hekima na mtaacha mzaha mzaha.

Yeremia alikuwa anahubiri na ukumbuke aliyemtuma ni Mungu anatoa unabii unawauzi watawala anatupwa gerezani. Anapoa huko vizuri Sanaa. Baadae anatupwa kwenye matope afe kwa njaa. Anazama kabisa. Baada Mfalme Zedekia anaagiza asiuawe ila arudishwe gerezani akapoe tena. Anakaa gerezani mpaka siku Jerusalem anapovamiwa na Babeli na kuangamizwa kabisaa.

Hamuoni Yeremia akilegea hata mara moja. Au kurudi nyuma na kususa kwamba kama vipi na yeye Mbabylon vile vile. Hata alipokuwa amezama kwenye matope ame kaza uzi. Alijua Mungu ni muaminifu hato acha  age kwenye matope. Na kweli Mungu anamgeuza moyo Zedeka anaagiza atolewe.

Wewe majaribu kidogo una susaa. Una breakdown KAMA toto vile nakwambia. Unarudi nyuma hatua 10. Kudeka na kukosa ukomavu wa kiimani. Na Shetani kazi yake ni ukupanikisha day in day out. Yupo commited kukupiga mapicha mapicha.

Unatakiwa ujiulize je Yeremia angedeka hivi navodeka hivi? Mi sijui Imani yenu ni wapi na unajiaminisha kabisaa na mazaha huo utapata matokeo. Na una panic mbona sipati matokeo? Utapata vipi? Ilihali unaleta mzaha?

Kuwa serious na hatima yako! Mungu yupo wazi sana na amejifunua mnoo mno kwenye maandiko. Msome na muelewe utaratibu wake wa ku operate.

Fikia viwango vyake anavyohitaji. Utamshuhudia kwa ukubwa. Fact kwamba humuoni wala him siku kwenye hilo jambo maana yake pandisha kiwango.

Mungu ana njia zake. Na njia za Mungu sio za mwanadamu. Ukiona huzielewi elewi hizo njia. Jitaidi umuelewe mungu. Njia za Mungu sio za mwanadamu.

Usijiendekezeee. Kaa kwa kutulia ukimuheshimu Mungu na maandiko. Na mungu atajisibitisha mbeleni.

Day 2 & 3 : Next Level

Tutarudia na Kutafakari Maneno ya Mungu ya Siku ya Kwanza yaani Day 1

 Day 4: Next Level

NI MKESHA

JIANDAE TU MAELEKEZO SAA 4 USIKU

TUMIA NENO LA MUNGU KUSEMESHA CHANGAMOTO/KIFUNGO CHAKO. USIKU KUCHA! Wee koroma kesho uje Dm. mchana ulifeli hata usiku?

Start declaring, decreeing and claiming God’s promises over your life and your situation. You will see changes. Sasa hapa kwa Kiswahili fasaha nimekwama BILA kupoteza tafsiri HKL/HGL help.

Usiku wote unalala una raha gani, na una DECLARE, DECREE na KU CLAIM ahadi za Mungu juu ya situation yako, mfano mahusiano!

Wewe mahusiano yangu, sio mkuu kuliko Mungu,sikiaaa,nakuamuru sikia katika jina la Yesu, Neno la Mungu linasaema (Tumia kifungu) si vyema mtu kuwa peke ake nitamfanya wa kufanana nae. I claim hili neno juu yako mahusiano yangu. I decree and declare sitakuwa mpweke. Nitakutana na wakufanana na mimi katika jina la Yesu, sikia neno la Mungu wewe mahusiano.

Kukutanishwa na Mtu Sahihi

Mwanzo 2:18-24

BWANA Mungu akasema, si vyema huyo mtu awe peke ake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

Isaya 34:16

Tafuteni katika kitabu cha Bwana mkasome; Hapana katika hawo wote atakaye kosa kuwapo, Hapana mmoja atakayemkosa mwenzake; kwa maana kinywa change kimeamuru na roho yake imewakusanya.

Isaya 30:18

Hata hivyo, mwenyezi Munguanangoja awafadhili, atainuka na kuwaonea huruma maana mwenyezi Mungu ni Mungu atendaye haki. Heri wote wale wanaomtumainia.

KAMA HUJAFANYA EXODUS USIRUKIE NEXT LEVEL! INABIDI UWE NA NGUVU KIIMANI TOKA KWENYE MFUNGO UWEZE KU COMMAND MATOKEO! KAMA UPO DOWN SPIRITUALY CHANGES MAOMBI YATAKUSHINDA NGUVU!

RUDI FANYA EXODUS NDO UJE NEXT LEVEL

Hatua Kweye Mahusiano yaliyostuck

Habakuki 2:3

For still a vision awaits its appointed time; it hastens to the end – it will not lie. If it seems slow, wait for it; it will surely come; it will not delay.

Habakkuk 2:3

Maono haya yanangoja wakati wa kufaa; ni maono ya ukweli juu ya mwisho. Kama yanaonekana kuchelewa, uyasubiri; hakika yatafika, wala hayatachelewa.

2 Wakorintho 6:2

2 Kwa maana Mungu anasema, “wakati ufaao nilikusikiliza , na siku ya wokovu nilikusaidia. Tazameni, huu ndo wakati ufaao; leo ndio siku ya wokovu”

2 Wafalme 2:19-25

Baadae watu wa Yeriko walimuendea Elisha, wakamwambia, “Bwana, kama unavioona mji huu ni mzuri, lakini maji tuliyonayo ni mabaya na yanasababisha mimba kuharibika,” Elisha akawambia, “ Tieni chumvi ndani ya bakuli jipya, kisha mniletee,” Nao wakaleta , Elisha akaenda kwenye chemchemi yam aji , akatupa chumvi hiyo ndani na kusema, “ mwenyezi Mungu asema hivi, nimeyafanya maji haya kuwa yenye kufaa tangu sasa hayatasababisha vifo au kutoa mimba,” na maji hayo yamekuwa ya kufaa mbaka leo, kama alivosema Elisha.  

ENDELEA KUPAMBANA NA LAKO MPAKA MAJOGOO

Day 5: Next Level

KAZI/BIASHARA

Kuvunja Vikwazo Vinavyozuia Kazi

Mungu muda mrefu sana nimesubiria ajira. Na sijaenda kwa Miungu mingine, nimekusuburia wewe kwa uaminifu.

Nimechoka kukataliwa baba kwa sababu mbali mbali, marks, kiwango cha elimu, muonekano, umri, etc nimechoka baba na NOT SELECTED!

Let them choose me because your goodwill is upon my life. No more will I beg of bread but it will be given abundantly to me in the name of jesus.

Lord, your word says that the same God who take care of me will supply all my needs from his glorious riches, which have been given to us in christ jesus.

Nasimama kinyume na yule muovu aliekuja kuua na kuharibu. Amenitenga na baraka zangu muda mrefu. Na futa na kukemea kwa jina la Yesu! Hatachelewesha baraka zangu tena.

But I will trust in the Lord of heaven and earth for my breakthrough. Lord , you have done it all on the cross for me and no longer will I suffer the trouble of unemployment, in jesus name, Amen!

Romans 8:28

And we know that in all things God works for the good of these who love him, who have been called according to his purpose.

Kutoka 14:21-31

Mose akaunyosha mkono wake juu ya Bahari, naye mwenyezi Mungu akaisukuma Bahari nyuma kwa upepo mkali toka mashariki. Upepo huwo ulivuma usiku kucha , ukaigawa Bahari sehemu mbili na katikati kukatokeza nchi kavu. Waisraeli wakapita katikati ya Bahari mahali pakavu, kuta za maji  zikiwa upande wao wa kulia na wa kushoto.

Yehova jire fanya njia pasipo njia. BILA wewe MUSA hakuwa nan jia baharini. Baba nimehangaika sana kwenye ajira, yamkini hakuna njia ya mimi kupita nipate ajira. Fanya njia pasipo na njia katika jina la yesu. Baba nirehemu kwa kunifanyia njia pasipo na njia katika hili swala la ajira kama ulivofanya red sea!

MSIHI MUNGU MUDA MREFU AKUFANYIE NJIA PASIPO NA NJIA KWA KUTOA SABABU ZAKO JINSI KUKOSA AJIRA KUNAKUTESA NA KUKUSINYA KWA UKWELI WAKO TOKA ROHONI!

 Maombi ya Kazi Sahihi

Heavenly father, I ask that you provide a job suited for my needs this day, I ask that my talents, skills, abilities, and education will be put into practical use. That way, I can have sufficient to pay my bills, and place bread on my table for my self and my family. May I also be able to give back what is due to you, Father.

Lord, You command blessings upon me in my barns and in all that I put my hands to do, and you will bless me in the land which you give me.

Right now, I proclaim that I will receive many job opportunities that will allow me to perform at any best, remembering you in all that I do.

I speak that doors will be opened to me in every direction I turn, because your right shines upon me.

I decree and declare that unemployment is of the past and will be no more. In jesus name I pray, Amen!

Proverbs 3:5

“Trust in the Lord with all your heart and learn not on your own understanding,”

Mathew 7:7

“Ask and it will be given to you; seek and you will find; knock and the door will be opened for you,”

Hagai 1:6-7

Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamtosheki na vinywaji; mnajivika nguo lakini hampati joto; nay eye apatae mshahara apata mshaara ili kuutia mfuko uliotoboka toboka. BWANA wa majeshi asema hivi, zitafakarini njia zenu.

Baba yetu uketia mahala pa juu nimetafakari hili kwa kina na nakukimbilia kwenye kiti chako cha enzi kuomba rehema kwa damu ya yesu. Baba nakataa katika ulimwengu wa kirohoo hili halitakuwa fungu langu kwa jina la Yesu, kuanzia mkesha huu nabatilisha haya juu ya hatima yangu kwa jina la yesu.

Mathayo 7:7-9

“Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni mlango, nanyi mtafunguliwa, maana yeyote aombaye hupewa, atafutae hupata na abishae mlango hufunguliwa, je kuna yeyote miongoni mwenu ambaye mtoto wake akimuomba mkate atampa jiwe?

Baba umesema kwa neno lako niombe nitapewa. Leo hi inaja mbele zako kuomba ajira baba. Umesema mtu hawezi kuomba ajira akapewa kitu kibaya. Baba nikumbuke usiku huu kwenye ajira , kila kitabu chako cha kumbukumbu kote nilikofanya applications. Wakanikumbuke na kunipa ajira kwa jina la Yesu.

Dear lord jesus, I come before you at this moments in the area of job, Thank you for providing employment for me. Father , cover my calcilum vitae (CV) with the blood of Jesus Let the heaven of my job breakthrough be opened into me,Good job is my portion this month. I decree and declare that good connection, unmerited favor and good news call shall locate me in the name of Jesus. Those who rejected me will soon open doors for me in the name of jesus.

Lord, my mate have been secured with a better job, mine shall not pass me by this month,. Nothing will be impossible for me because I am in christ and through him, I can do all things (Read -Phillippians 4:13)

This month and this year , God’s oil of devine favor flowing all over me and my credentials/documents.

I shall no more experience the attack of joblessness and begging. I speak mercy and power of God into my credentials., to begin to works for my good Father , let there be quick intervation of job breakthrough in my life, whether it is convenient for my enemies or not, this month am getting myself in a good company.

Those that are divinely positioned to help me to secure this job will not rest until they fullfil God’s promises in my life. The place that I have submitted my credentials, let your blessings begin to speak for me aloud, Lord, let me be at the right place (organization) at the right time.

Holy spirit direct me to the right company, right people that will aid my job breakthrough, Lord, bress me with a good (better) job so that I can bless others and pay my time and offerings regulary. From this day, I declare that, “no more looking into men for help that go with unclean motives”.

O Lord open my inner ears to see the type of job you wanted me to do or engage myself with. Father, help me not to do a wrong job that will delay my greatness, my prosperity and my marriage.

I refuse to do a job that will take away my relationship completely from you. The arrows os sitting at home while during nothing shall not succeed over my life. My God will not allow povery , shame, disgrace to be a major occurances in my life and destiny.

Father , empower me and put words into my mouth to speak confidently at my job interviews, in jesus name. I have an assurance and expectation that I will be victorius at the end in the name of Jesus, (Jeremiah 29:11). I decree that the plan of the enemy concerning my job shall scarter by fire. Every curse of thou shall not get job, operating in my life, shall break by fire.

Kumbukumbu La Torati 28:13

BWANA atakufanya kuwa kichwa, wala simkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya BWANA, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, Kuyaangalia na kufanya

DECLARE HILI ANDIKO JUU YA HATIMA YAKO USIKU KUCHA

Day 6: Next Level

MEDITATION

Uakesha Unatafakari Ukuu wa Mungu

 Kutoka 20:2-5 BHN

“Mimi ndimi mwenyezi Mungu, Mungu wako, niliyekutoa nchini Misri, ambako ulikuwa mtumwa.” Usijifanyie sanamu ya Miungu wa uongo, au kinyago cha chochote kilicho mbinguni, katika nchi au majini chini ya dunia. Usiisujudie wala kuitumimikia; kwa kuwa mimi mwenyezi mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha 3 na cha 4 cha hao wanichukiao.

Usiende Kwa Mganga

2Wafalme 1:2-4, 17

2 Mfalme Ahazia alipokuwa Samaria alianguka kutoka chumba kilichokuwa paani  mwa nyumba yake, akaumia vibaya, kwahiyo akawatuma wajumbe akawambia, “Nwndeni kwa Baal zebubu, nungu wa mji wa Ekroni, mkamuulize kama nitapona ugonjwa huu,”

3lakini Malaika wa mwenyezi Mungu akamwambia nabii Elia kutokaa Tishbe aende kukutana na wajumbe hao na kuwauliza, “kwanini mnakwenda kwa Baal zebubu, mungu wa Ekroni? Je, hakuna Mungu nchini Israeli?

4Mwambieni Mfalme kwamba mwenyezi Mungu amesema hivi, “Hutashuka kwenye kitanda ulichokipanda; hakika utakufa,”

17 Badae Ahazia akafariki kama mwenyezi Mungu alivomwambia nabii wake Elia.

1 samueli 28:6-7, 10, 13-19

Lakini sauli alipouliza kwa BWANA, BWANA hakumjibu wala kwa ndoto, wala kwa ulimi, wala kwa manabii.

Ndipo Sauli akawambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo ya utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia tazama, tazama yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori.

Naye Sauli akamwapia kwa BWANA, akasema aishivyo BWANA haitakupata adhabu yoyote kwa jambo hili . ndipo yule mwanamke alivosema, Je ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema , Nipandishie Samueli.

Mfalme akamwambia usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, naona Mungu anatoka katika nchi, naye akamwuliza , Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka naye amefunikwa wazi, Basi sauli akamwambia ya kwamba ni Samueli mwenyewe huyo. Akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.

Ndipo samweli akamwambia sauli, Mbona unanitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, mimi nimetaabika Sanaa; kwa kuwa hao wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje.

Samweli akasema, kwa nini kuniuliza mimi, akiwa BWANA amekuacha , naye amekuwa adui yako? Yeye BWANA amekutendea kama alivosema kwa kinywa change; BWANA amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa Jirani yako, yaani Daudi.

Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya BWANA , wala hukumtimilizia hasira yakekali juu ya Ameleki; kwa sababu ni BWANA atawatia Israeli mkononi mwa wafilisti; hat ana kesho wee na wanao mtakuwapo Pamoja nami; tena BWANA atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti.

Day 7: Next Level

ONGEZEKO/INCREASE

Ukilala Huna Bahati

Sometimes sio kwamba kitu huna kabisaa, unacho kidogo, All you need is for it to increase. Unahitaji hiko hiko kidogo kiongezeke. Kama Mungu alikujalia hiko kidogo kukiongeza sio issue.

2 Wakorintho 9:10

Na Mungu ampae mkulima mbegu na mkate kwa chakula , atawapa nyinyi pia mbegu mnazohitaji, na atazifanya zoite, zikuwe na kuwapa mavuno mengi ya  ukarimu wenu.

Isaya 54:2-3

Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa Kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako;

3 kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto; na wazao wako watamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu.

Zaburi 115:14

BWANA na awaongeze ninyi, ninyi na Watoto wenu.

Mwanzo 26:12

Mwaka huo Isaka akapanda mbegu katika nchi ile , naye akapata mavuno mara mia Zaidi. BWANA akambariki.

Ayubu 8:7

Tena ujapokuwa kuwa huwo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, lakini mwisho wako ungeongezekana sana.

Kumbukumbu ya Torati 1:11

BWANA, Mungu wa baba zenu, na awafanye kuwa wengi mara elfu kuliko mlivo, na kuwabariki, kama alivyowahaidi.

Mathayo 14:15-22

Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimuendea wakamwambia, “Mahali ap ani nyikani, na saa za mchana zimepita basi, uwaage watu waende vijijini wakajinunulie chakula,” yesu akawambia, “si lazima waende , wapeni ninyi chakula” Lakini wao wakamwambia.

“Tunayo mikate mitano tun a samaki wawili, “Yesu akawaambia, Nileteeni hapa. “akawaamulu watu waketi katika nyasi, kisha yesu akaita ile mikate mitano na Samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akavibariki harafu akamega hiyo mikate, akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu.

Watu wote wakala, wakashiba,kisha wanafunzi wakakusanya mabaki, wakajaza vikapu kumi na viwili, jumla ya waliokula ni wanaume wapatao 5000, bila kuhesabu wanawake na Watoto.

Day 8-14 : Next Level

KUVUNJA UKUTA WA YERIKO

Andika changamoto yako moja iliyoshindikana! yaani imeshindikanika kama mji wa yeriko imefunga kweli kweli hakuna anayetoka wala kuingia ili wewe usipenye, haisikii maombi, toba, mifungo, sadaka wala neno la kinabiii! andika kwenye karatasi afu tulia nayo siku 7 hizihuo ukuta wake tunauporomosha!

Huko kote ulikuwa una boost spirituals charge! now you are ready! kama ulikuwa serious kuanzia exodus by now una vibrate glory of god! jana nilienda sehemu kukanyaga tu pale wateja wakafurika. sikuongea neno! utukufu tu! mbaka wakaniuliza mtumishi leo umeomba neno gani? ukiwa serious nguvu za giza zinajua!

Andika hiyo changamoto yako! andika tarehe ya mwisho wewe hutaki kuisikia wala kuiona tena?

Anza kusoma yoshua 6 yote mdogo mdogo

Usiku kuna jambo letu! giza lisiingie hujasoma hiyo aya yote! endelea kujiendeleza muda wa shuhuda uwe mpole.

DAY 1 YERICO PRAYER! : Next Level

Ile karatasi uliyoandika ukuta wako sugu, UNAIZUNGUKA MARA 1 TU1 moyoni ukimtukuza Mungu kwamba hajawahi shindwa makubwa na magumu itakuwa hako ka ukuta kwenye karatasi.

Zungumza na Mungu kwamba Pamoja na mazingira kukaa kiimpossible impossible lakini historia inajieleza Mungu hajawahi kushindwa. Na hiko kiukuta hawezi kushindwa. Mkumbushe tu umetoka exodus, mpaka hapa Yeriko nothing is moving, nothing is shaking but he is still your God!

Fee! The power of God! Sense it! Expect the power of God to move in your favor kwa Habari za huwo ukuta. Be frank as silly as it sounds navoelekeza binti mlokole kama it is what it takes ndo kama hivo unapiga rounds ya kwanza cause you realy really the wall to come down!

DAY 2 YERICO PRAYER! : Next Level

Ile karatasi ulio Andika ule ukuta wako sugu, UNAIZUNGUKA MARA MOJA TU!

Yeremia 10:10

Bali BWANA ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele;

DAY 3 PRAYER! : Next Level

Ile karatasi uliyoandika ukuta wako sugu,UNAIZUNGUKA NMARA 1 TU!

2Mambo ya nyakati 20:12

Wewe ndiye Mungu wetu! Waadhibu, kwani sisi hatuna uwezo wowote mbele ya jeshi kubwa kama hili linalotujia. Hatujui la kufanya ila tunatazamia msaada kutoka kwako,”

SPIRITUAL TEST YA KUTUMA KWA WATU WA 3 MAGOLIAT WAKO KWAMBA SOON MUNGU ANAKUVUSHA HIYO CHANGAMOTO IN DETAILS MMEFIKA WAPI?

DAY 4 PRAYER! : Next Level

UNAZUNGUKA ROUND YAKO 1 YA KIBABE.

Isaya 55:11

Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi uko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandae mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa change; halitaniludia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.

DAY 5 PRAYER! : Next Level

UNAZUNGUKA ROUND YAKO 1 YA KIBABE.

2 Wakorintho 10:3-5 BHN

Kweli tunaishi duniani, lakini hatupigani vita kidunia, maana silaha tunazotumia katika vita vyetu si silaha za kidunia, il ani nguvu ya Mungu yenye kuharibu ngome zote. Tunaharibu hoja zote za uongo na kubomoa kila kizuizi cha majivuno kilichowekwa kuipinga elimu ya Mungu; tunaziteka fikra zote na kuzifanya zimtii Kristo.

Ponya Majeraha ya Nafsi Yako

Wengi tumejeruiwa mioyo, japo unajikaza lakini bado unavuja damuuu mbichi. Kuna mambo yalitokea na yakakuachia jeraha na hukulitibu umejifunza kuishi nalo. Sasa ni tatizo kwenye mahusiano yako yajayo.

Sio tu kuomba mtu sahihi au kukutana nae, issue utaweza kudumu naye na moyo wako unavovuja damuu? Manake wanaume wanaangalia nje , ni binti au mwanamke mzurii, unamjua Mungu, lakini ndani ndo moyo unavuja damu mtupu.

Yamkini umeachwa na wanaume wengi bila sababu, yamkini ulikaaa na mtu akaoa mtu mwingine, yamkini ulikataliwa, au hujawahi kupata mtu, yamkini ulikuwa mdogo mtu akakufanyisha abortions, au mtu alikuzalisha akakuacha tu, au uko divorced au mjane. Kwa nje unapambana ila kwa ndani unavuja damuu nab ado hujakata tamaa na Mungu.

Sasa kabla hujarukia maombi mengine omba kwanza mungu akuponye moyo wako. Upendo tena na kuamini tena.lasivyo utahisi muda wote historia inajirudia. Unakuwa mtu wa kutafuta red flags. Mtu wa kungoja suuu muachane unajiset up for failure.

Unapo ngoja majibu yako jitayarishe kwa habari za hayo majibu

Wengi ni wepesi wa kuomba ila sio kupokea majibu. Tena mlio okoa ndo kabisaaa. Mnaamini kusubiri kusiko na kikomo. Hapo ndipo mnapofeli na kuludi katika depression na kukata tamaaa.

Yaani state ya mind yako kabla na baada ya maombi ni ile ile. Si tatizo hilo, woga uko vile. Wasiwasi ndo usiseme yaani hamna mabadiliko ya moyo, means bado hujayaamini maombi yako.

Unatakiwa ukue kiimani ukijiambia! Prayed for this moyo wako unapata amani ipitayo amani zote. Nitashangaa sana mtu atoke next level aludi ALIKOTOKA.

Kama umeomba mme,. YOU ARE PRAYED FOR THAT! Anza kuwaza na mumeo mtaishi wapi. Vitu vyako utamgawia nani? Maana ndo unaenda kuolewa , unataka Watoto wangapi, serious issues, Fanya maandalizi serious.

Mpaka mbingu zikikuangalia ulivojipanga na ulivo na uhakika nazo hawawezi kukuletea majibu ya DENIED au WAIT! Kama ni kazi nunua nguo kabisa na viatu sababu Mungu ni mwaminifu. Kama mtoto anza kuuliza gyneologist mzuri ni yupi? Duka gani wana staterback nzurii?

ALWAYS DISPLAY MASSIVE FAITH SABABU YOU PRAYED FOR IT!

DAY 6 PRAYER ! : Next Level

UNAZUNGUKA ROUND YAKO 1 YA KIBABE.

Isaya 58:8

Ndipo nuru yako itakapo pambazuka kama asubuhi, na uponyaji wako utatokea punde; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.

Mungu ana nguvu sanaaa! sasa mbona matatizo yako hayastukiii?

Mungu ana nguvu hilo halina ubishi usije uka beep kukufuru akuonyeshe! utajuta! ila anajiuliza sasa mbona matatizo yako hata kupepesa kope bado mbele ya hizo nguvu1 leo nawambia kwanini?

Kabla nakukumbusha tu mungu ana nguvu nyingi na muhimu anazihitaji. chache ni nguvu za uponyaji, kurudisha majira, kuumba jambo jipya, kuokoa, kuvusha, kuongeza, kung’oa, kukuza, etc!

Kwanini hazifanyi kazi kwako?

Huna plan B ya tatizo lako! uko 50/50 huku unaomba huku una pambana kivingine. za madhabau unachanganya na za kitaa. god wont move because if he does hutojua for sure nini kimefanya kazi.

Huamini! upo 50/50 kwa kiasi chake unaamini na kwa kiasi chake huelewi elewi! upo upo! unaamini kwa kiasi cha kuto kukufuru na huamini kwa kiasi cha kuvuka.

DAY 7 PRAYER! : Next Level

UNAZUNGUKA ROUND ZAKO 7

Round ya saba ukimaliza shangilia na ufurahi toka ndani! picture yourself on the other side! na kumshukuru mungu kwa kina kwamba hatimae hizi changamoto zimeporomoka leo.

Mshukuru mungu kwa kuwa historia yako inaenda kubadilika na unaenda kuvuka kwa kishindo!

Mshukuru mungu kwa kina!

Hizi kuta sio kwamba hujawahi ziteremsha! ushaziteremsha huko nyuma  mara nyingi lakini in no time unakuta wanazijenga upyaaa!

Ushindi unakuwa wa msimu tu na mda kabla hawaja kujengea ukuta mpyaaaa mrefu zaidi. safari hii historia haitajirudia! huu ndo ukuta wa mwishoooooo!

This breakthrough shall be permanent!!! nakuja na andiko la kuseal the victory!

Mlaani ataekuinulia tena ukuta wa Yerico

Yoshua 6:21

Basi wakaangamiza kabisa vitu vyote vilivokuwa ndani yam ji, wanaume na wanawake, Watoto na wazeee, na ng’ombe na kondooo, na punda, kwa makali ya upanga.

Yoshua 6:24

Kisha wakauteketeza mji kwa moto, na vitu vyote vilivokuwa ndani yake; bali fedha , na dhahabu na vyombo vya shaba, na vya chuma, wakavitiakatika hazina ya nyumba ya BWANA.

Yoshua 6:26

Naye Yoshua akawapisha kiapo wakati ule, akasema, na alaaniwe mbele za BWANA mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa yeriko; ataweka mji wake kwa kufiliwa na maziliwa wa wakwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliyemdogo.

Mtukuze Mungu wako kwa ushindi

2Mambo ya nyakati 20:6

Yehoshafati akisimama kati ya kusanyiko la yuda na Yerusalemu, nyumbani mwa BWANA, mbele ya ua mpya; akaomba kwa sauti akisema,

“Ee mwenyezi Mungu, mungu wa baba zetu, wewe ndiye Mungu uliye mbinguni! Wewe unazitawala falme zote duniani; unao uwezo na nguvu, wala hakuna awezae kukupinga.

Change Of Plans

Kuna mtumishi kupanga yangu, na kuna Roho Mtakatifu kuongoza kwamba pita huku na huku kwa matokeo fulani.

Hizi instructions nimezipata jioni hii na naendelea kuzipata! kadri tunavokesha!

Roho Mtakatifu alinikumbusha andiko kwamba walizunguka mara 7 at once so initial plan ilikuwa contrary na andiko.

Ndo maana nikaipiga chini. na tukakamilisha maandiko yalivo elekeza. na tunaendelea kadri roho wa bwana anavo elekeza!

Omba na Ku refresh

Heavens have your audience! audience you payed highly for! umefunga 7, umekesha, umezunguka! you earned the audience sasa kilichobakia put a good performance!

Zaburi 51:16

Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa, wewe hurithi sadaka ya kuteketezwa.

Zaburi 51:17

Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika, moyo uliyovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.

Nenda mbele za Mungu na moyo uliovunjika na kupondeka, huu ni moyo unaomtegemea Mungu pekee, Ni moyo uliosubmitt kwa Mung utu na hauna plan B1 ni pale upo at your lowest! Huna connection, huna shosti huna lolote wala yeyote wa kukupa mume au kazi. Mwambie Mungu sina mwingine wa kunitoa ni wee tu yeweee! Ni wewe tu baba!

Mathayo 22:29

Yesu akajibu, akawaambia, mnapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.

Mathew 22:29

29 jesus replied, “you are in error because you do not know the scriptures or the power of God.

Roho mtakatifu tujalie usikuu huuu tuweze kuyaelewa na kusimama na maandiko nak u experience POWER OF GOD

1 Wakorintho 4:20

20 Kwa kuwa ufalme wa Mungu si maneno matupu bali ni nguvu.

1 Corinthians 4:20

For the kingdom of God is not just a lot of talk; it is living by God’s power.

Maneno matupu yanaisha usiku huu. Kuanzia kesho unaishi kwa nguvu ya Mungu ambapo chochote kinachozungumzwa kinatimia halisi kabisaaa. Hutaishi kwa matumaini bali kwa matokeo, mambo yatajithibitisha kwako.

Nguvu ya Mungu iliyohalisi usiku huu, ika manifest kwenye uhalisia chochote kinachofanya ukeshe. Kama ni kukutana na mchumba mkakitane live uso kwa uso. Kama ni kutamkiwa WILL YOU MARY ME? Akatamke ukasikia kwa masikio yako. Kama kazi ukaitwe kazini.

Yohana 11: 1-4

Palikuwa na mtu mmoja jina lake Lazaro ambaye aliugua. Yeye aliishi katika Kijiji cha Bethania Pamoja na dada zake wawili, Mariam na Matha. 2 huyu Mariam ndiye aliyempaka Bwana Yesu manukato miguuni na kumpangusaa kwa nywele zake. 3 Hawa dada wawili walituma ujumbe kwa Yesu kumwambia, “Bwana, rafiki yako ni mgonjwa sana.” 4 lakini Yesu alipopata Habari hizi alisema, “ugonjwa huu hautaleta kifo bali umetokea kudhihirisha ukuu wa Mungu. Kutokana na ugonjwa huu, mimi mwana wa Mungu nitatukuzwa”.

Yohana 11: 11-15

Baada ya kusema haya yesu aliongeza kusema, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini nakwenda kumwamsha,”.

2 wanafunzi wakamwambia, “Bwana, kama amelala bira shaka atapona,” 13 Yesu alikuwa amemaanisha kuwa Lazaro alikuwa amekufa, lakini wanafunzi wake hawakumuelewa. Walizani anasema Lazaro amelala usingizi. 14 Kwa hiyo Yesu akawambia wazi wazi , “Lazaro amekufa”. 15 Hata hivyo nafurahi sikuwepo kabla ya Lazaro kufa. Hiii itakuwa kwa faida yenu, ili muweze kuamini. Lakini sasa twendeni, “16 Tomaso aliyeitwa pacha akawaambia wanafunzi wenzake, “Na sisi pia twendeni tukafe Pamoja naye,”

Yohana 11:17-27

Yesu alipowasili alikuta Lazaro alikwisha kuzikwa siku nne zilizopita. 18 Kwa kuwa Kijiji cha Bethania kilikuwa umbali kama wa kilomita 3 tu kutoka yerusalemu, 19 wayaudi wengi walikuwa wametoka mjini kuja kuwafariji Martha na Mariamu kwa kifo cha ndugu yao. 20 Martha aliposikia Yesu amefika, alitoka Kwenda kumpokea, Ila mariamu alibaki amekaa ndani, 21 Martha akamwambia Yesu, “Bwana kama ungalikuwa hapa ndugu yangu angali kufa. 22 Na hata sasa ninafahamu kuwa chochote utakachomwomba Mungu atakutimizia.” 23 Yesu akamwambia, “kaka yako atakuwa hai tena,” 24 Martha akajibu, “ndio najua atakuwa hai tena wakati wa ufufuo, siku ya Mwisho,” 25 Yesu akamwambia ,”Mimi ndiye ufufuo na uzima; mtu akiniamini mimi, hata akifa ataishi; 26 na yeyote anayeishi akiwa ananiamini hatakufa kamwe, je unaamini haya?” 27 Martha akajibu, “ndio Bwana; naamini yakuwa wewe ndiye Kristo, mwana wa mungu, ambaye angekuja ulimwenguni,”

Yohana 11:28-37

Baada ya kusema haya Martha alikwenda akamwita Mariamu kando akamwambia, “Mwalimu amefika na anakuita,” 29 Mariamu akaondoka upesi akaenda alipokuwa Yesu. 30 Yesu alikuwa bado hajaingia kijijini, ilikuwa bado yupo pale martha alikutana naye. 31 Wale wayaudi waliokuwa wakimfariji Mariamu walivoona ameondoka haraka, walidhani anakwenda kaburini kuomboleza, kwahiyo wakamufuata. 32 Mariamu alipomuona yesu aliinama chini kwa heshima na akasema, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangalikufa,” 33 Yesu alipomwona Mariamu akilia na wale wayaudi waliokuja naye pia wanalia, alifadhaika sana moyoni; 34 Akauliza, “Mmemzika wapi?”, wakamwambia, “Bwana njoo uone,” 35 Yesu akalia. 36 Wale wayahudi wakasema, “Tazameni jinsi alivyompenda Lazaro!”. 37 Lakini wengine wakasema, “Alimponya kipofu, kwanini hakuweza kuzuia Lazaro asife?”

Yohana 11:38-44

Yesu akafika kwenye kaburi akiwa amefadhaika sana. Kaburi lenyewe lilikuwa katika pango ambalo mlango wake umezibwa kwa jiwe. 39 Akasema, “ondoeni hilo jiwe”. Dada yake marehemu, Martha akasema, “Bwana patakuwa na harufu kali kwani siku nne zimepita tangu  azikwe. “ 40 Yesu akajibu, “sikukuambia kama ungeamini ungeona utukufu wa mungu?” 41 kwahiyo wakaliondoa lile jiwe. Yesu akaangalia mbinguni akasema, “Baba ninakushukuru kwa kunisikia, 42 ninajua yakuwa kuwa huwa unanisikia wakati wote, lakini nimesema hivi kwa faida ya hawa waliopo hapa, ili wapate kuamini yakuwa umenituma,” 43 Baada ya kusema haya akapaza sauti akaita, “Lazaro toka nje!” 44 Yule aliyekuwa amekufa akatoka , mikono yake na miguu yake ikiwa imevingilishwa vitambaa. Yesu akawambia, “mfungueni awe huru!”

Mhubiri 9:7

Wewe enenda zako, ule chakula chako kwa furaha, unywe mvinyo yako kwa moyo wa kuchangamka; kwa kuwa Mungu amekwisha kuzikubali kazi zako.

Wafilipi 4:4

Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini!

THE END!!

Majibu ya Exodus/Next level

Kupokea majibu usikae chini unasubiri. Test upako upo au mambo yale yale. Ukikaa unasubiria hutaona kitu. Mambo yanaweza kuwa yamefanyika wewe unazubaaa.

Pool of Bethesda yule mlemavu, yesu anamwambia NYANYUKAAA! Manake attest upako. Ananyanyuka na kusepa zake.

Mathayo 9! Yesu anamponya mgonjwa mwingine wa kupokea. Anamwambia NYAKUKA na uondoke.

Sasa wewe toka umalize maombi umekaa unasubiri. Sasa sijui unasubiri ishara ya mama jusi au sijui unasubiri nini. GET BACK ON THE GAME! INTO ACTION! Kama ulikuwa unaomba kazi hupatagi, sasa omba utapata. Kama ulikuwa hutongozwi, sasa toka na confidence utatongozwa mpaka uombe pooh. Kama ulisema hakuoi, Muulize tena UNANIOA AU HUNIOI???

Kugoma kupokea jibu sio kuto kujibiwa

Mungu lazima anajibu. Wapo wachache kama Saul, kweli Mungu aliwalia bati, bati hasaaa. Si kwa ndoto, sio manabii, Sio kwa vyovyote. Kimya mtindo mmoja. Ukienda kwa mganga mara nyingi hii ndo inakukuta.

Lakini wengi wetu tunajibiwa ila sasa si kile tulichokitaka na kutalajia, sasa wengi apa unajizima data na kuzidi kuomba. Unajidanganya. Pokea majibu fanya mapenzi ya Mungu utapiga hatua.

Mfano mimi tangu EXODUS niliwaambiwa sijajibiwa. Na kwa mganga sijaenda! Nimepiga NEXT LEVEL! Leo nimepokea majibu tata kama nabii Yeremia. Nabii Yeremia akiwa gerezani anamlilia Mungu juu ya hiyo hali, mungu anamjibu kwa Habari ya shamba. Ndio anunue shamba la ndugu yake jamani.

Na mimi nilikuwa naomba maombi yangu mengine leo nimepokea majibu nifufue biashara yangu iliokufa. Na ilinitia hasara kubwa sana na ilinivunja moyo Sanaa. It is complex situation il ani jibu. Na mungu hakosei.

HIVYO KABLA HUJASEMA HUJAJIBIWA TAFAKARI!

2 thoughts on “Next Level”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top