MUNGU SIO MGUMU, MAMBO SIO MAGUMU, BALI MOYO WAKO NDIO MGUMU (SUNDAY WORD)

Waebrania 4:2

Maana Habari njema imehubiriwa kwetu kama vile ilivyohubiriwa kwa hao watu wa kale. Lakini  ujumbe huo haukuwafaa chochote,maana waliusikia lakini hawa-kuupokea kwa imani.

 

MUNGU SIO MGUMU!, MAMBO SIO MAGUMU!, MOYO WAKO NDO MGUMU!

 

Waebrania 3:8

msiifanye Mioyo yenu migumu, kama mlivyofanya katika uasi, wakati ule wa kujaribiwa jangwani.

 

UNAWEZA KULIJUA NENO LA MUNGU MSTARI KWA MSTARI, AYA KWA AYA , KITABU KWA KITABU! LAKINI LISIKUFAE CHOCHOTE!

 

Na unaweza kujua maandiko MACHACHE tu, lakini ukayajua kweli kweli, kuyapokea, kuyaamini na kuyaishi kikamilifu na yakakufaa hasaaa hasa!

 

Ndiyo maana mara nyingi mtu mfano Malaya mchafu, akajipata tu na kusema ana-acha!, Anapata matokeo makubwa sana!, Mpaka ukaona mbona Sisi tumeokoka mudaa na hamna kitu, Huyu si kaja janaaa tu jamani!. Mpendwa huyu Mzinzi anakuwa ame-acha kweli kweli, Yaani amestaafu   rasmi, Kama  alivodhamiria  kufanya umalaya akaupiga KWELI KWELI Dar mpaka Zanzibar mpaka  Dubenga!, Siku akisema ameachaaa!, Ujue ameacha!, HATA SHETANI AMPE NINI HAMPATI! YAANI INAKUWA KAMA KIFANVIO KIME EXPIRE!, MAGOMENI  TUNASEMA   UMALAYA UMEMKATAA RASMI!, HATA YEYE AKIJIFOSI MWILI UNAGOMA!

 

Mtu kama huyuuu, Game yake ya kupokea mafundisho na maandiko ni 100%!, Imani yake niyakuhamisha milima! Na Focus yake haipo 50/50!, Akili yake ipo clear kujifunza na kusikiliza mafundisho!, Ameji-tune kuyapokea kama yatakavyoletwa, Ubabai wake ame u-control, HARUHUSU ULE UBABAIFU U-DILUTE YALE MAFUNDISHO,    Probability ya mafundisho kumfaa sana ni kubwa sababu yanapokelewa kama yalivyotolewa.

 

MPENDWA WENGI MNAJUA MAANDIKO ROBO-ROBO,  SIO KWAMBA HUJUI LAKINI UNACHOKIJUA UNAKIJUA JUU-JUU TU, NA DHAMBI HUFANYI KWA SIFA LAKINI HUJINYIMI, SIO MALAYA MCHAFU ILA HUJINYIMI MZINZI MZURI TU, NI KAMA MTU YUPO SERIOUS ANA MUAMINI MUNGU KUMPA NDOA ILO TOKA MBINGUNI LAKINI HAPO HAPO ANA ZINI NA WANAUME  WAWILI  AU MMOJA.

 

NAMUAMINI MUNGU SANAA SANAA ENEO LA KUMPA MUME LAKINI HAMUAMINI KABISA ENEO LA AMRI YA SITA (USIZINI!), MAANDIKO ANAYAJUA LAKINI UBABAI WAKE UNA YA DILUTE TO THE EXTENT HAYAWEZI KUMFAA CHOCHOTE.

 

WATU WENGI MNAAMINI NA KUTO-KUAMINI AT THE SAME TIME!, MKO 50/50 SANA NA INAWAGHARI MU!, UNAKUTA MTU ANAFUNGA  KABISA KUMUOMBA MUNGU KAZI LAKINI KUTOKANA NA HIYO KAZI HAIJAPATA MUDA,  MOYONI MWAKE HANA IMANI NA MUNGU HATA KIDOGO KWAMBA MUNGU ATAMPA KAZI!, ANACHO AMINI NI MAMBO YATAKUWA YALE YALE, NA  MPENDWA YANAKUWA YALE YALE KUTOKANA NA MAPOKEO YAKE.

 

Juzi niliwapa ushuhuda wa Binti aliekuja kutaka kazi ya 1.5M na SADAKA yake akataka nimfanyie ukuhani!, Nikamfanyia na akapata hiyo kazi with-in muda ule ule.

 

BAADA YA HAPO HAMNA RANGI SIJAONA, KILA MTU HATAKI KUFANYA IBADA ANATAKA  MIMI NIFANYE MAGIC APATE KAZI YA MASHAHARA ANAOTAKA. MSICHOKIJUA YULE  BINTI GAME YAKE YA MAANDIKO NI EXTREMLY STRONG, NAWEZA SEMA DEADLY NI KAMA MTU ALIE ENDA KWA FUNDI NGUO NA MSHONO WAKE KABISAA KWAMBA NATAKA MSHONO HUU, ASHAFANYA DUE DILIGENCE YA KUJUA CAPACITY YA FUNDI NA KAMA ULE MSHONO ANAUWEZAAA?  NA HATAKI USHAURI WA FUNDI, ANATAKA MSHONO ANAO UTAKA! GHARAMA ZA FUNDI SIO SHIDA ZAKE ! LENGO LAKE NI MASHONO TU.

 

YULE BINTI ALIKUWA ANAJUA MAANDIKO YA KU BACK UP HITAJI LAKE, AKAYA STUDY MUDA WA KUTOSHA, SABABU YANATAKA SADAKA KUBWA! AKAYAPOKEA NA KUTAFUTA HIO SADAKA KUBWA, IKABAKIA PART NDOGO TU YA KUHANIKUHITIMISHA HIO IBADA, NDIYO AKAJA KWANGU!

 

MIMI HAKUHITAHI KUNIAMBIA ANACHOTAKA, NILIYO RESEARCH WORK ALIYO-INVEST KWENYE HILO JAM BO NA LEVEL YA IMANIYAKE ILIKUWA SUFFICIENT ,UELEWA WAKE WA MAANDIKO ULIKUWA OUTSTANDING, IT WAS A DONE DEAL! HAKUKUWA NA SABABU YA MIMI KUKATA ALICHOHITAJI NI NISIMAME KWENYE NAFASI YANGU TU, NAKATAAJE?

 

SASA WENGI MNATAKA IBADA KAMA HIZI ZA MIUJIZA LAKINI HAMPO TAYARI KUFANYA GROUND WOR K, HAMPO TAYARI KUJIFUNZA MAANDIKO YA KUSUPPORT HIO MIRACULOUS RELEASE OF POWER,YANI INSHORT HAMTAKI KUWINDAAAA ILA MNCHOTAKA NI KULA NYAMA-PORI!, MY FRIEND SONGA TU TEKE TEKE BUCHANI.

 

Juzi kaja mtu Dm anataka nimuongoze maombi Mungu ampe Milion 7 , miraculous na katika hiyo Milion 7 atafanya nadhiri, siwezi kumsaidia kupata hio pesa anitoe dry! How sweet!.

 

Mimi nikamuuliza tu swali dogo,  Hio ibada UNAYOTAKA by any chance kuna SCRIPTURAL reference?, Yaani kuna mahali imeandikwa labda Mungu anatoa hizo Cold Cash ?, Nilitaka kujifunza, We learn everyday, Labda mwenzetu kapata revelation.

 

Mimi biblia kwenye  maeneo ya  Shekeli nimeipindua juu chini katikati, Nime Research na BADO na Research miaka na miaka, LAKINI BADO hio ibada ya kureceive COLD CASH from heavens sijaipata SANA SANA THE MORE I STUDY THE MORE MAANDIKO YANANIVURUGA TU,  AFTER  HEAVY RESEARCH NILICHO AMBULIA NI THE THEORY KWAMBA  KUANZIA  NABII MUSA MPAKA KWA MITUME HUKU HAKUNA NABII WALA KUHANI ALIYE MPA MTU YOTOTE UTAJIRI!, YESU ALIWAPENDA SANAA MITUME WAKE LAKINI ALIWAACHIA UTAJIRI WA ROHO MTAKATIFU!, ELISHA ALIFOSI KINGI KWA ELIA KWELI KWELI,  ALIPAMBANA LAKINI ALICHO AMBULIA NI SHATI TU LA UPAKO WA ELIA. WAPENDWA MIMI NILIMWAMBIA TU MIMI SIO MTUMISHI SAHIHI WA HIO IBADA!.

 

UKITAKA KUPATA MILAGE KWNEYE ULIMWENGU WA ROHO LAZIMA UPOTEZE MlLAGE KWENYE ULIMWENGU WA MWILI, RELIM OF THE SPIRIT NA RELIM OF THE FLESH ZOTE ZINAGOMBANIA HAYO HAYO MASAA 24 YAKO KWA SIKU, UTAKAPOWEKEZA NDIPO UTAKAPO VUNA, HAMNA FAULO WALA UJANJA-UJANJA.

 

KUNA MAMBO KUYAPATA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO LAZIMA KWANZA KWENYE ULIMWNEGU WA MWILI UONEKANE DISHI LIMEYUMBA NA AKILI KIDOGO ZIME SHAKE. IMAGINE HALI ILIVYO NGUMU KWA HIARI YAKO UNATOA 10% NA KUMPA MTU ANAYE ENDESHA RANGE ROVER VELAR,  NDIYO MAANDIKO,  KUNA MTU AKILIPA ZAKA ANASEMA ANDIKO LINALOMJIA KICHWANI NI HILI TU.

 

Luka 19:26

“Akawajibu, Nawaambia kwamba kila aliye na kitu, ataongezewa. Lakini yule asiye na kitu, hata alicho nacho atanyang’anywa.

 

Mpendwa unaona kwamba Process ya zaka ndio WEWE  kunyanganywa hicho kidogo imeanza mapemaaa! Kidogodogo cha 10%.

 

ILI UENDE SAWA NA MAANDIKO UJINGA NA UZOBA HAUKWEPEKI, UKITUMIA TU AKILI ZAKO UMEISHA! NI KAMA UMEJIFYATUA NA MTEGO WA PANYA.

 

Mathayo 5:38-48

“Mmesikia kwamba ilisemwa: Jicho kwajicho, jino kwa jino, Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi katika shavu la kulia, mgeuzie pia la pili. Mtu akikupeleka mahakamani kutaka kukuchukulia shati lako, mwache achukue pia koti lako. Mtu akikulazimisha kubeba mzigo wake kilomita moja, ubebe kilomita mbili. Akuombaye mpe ,wala usimpe kisogo anayetaka kukukopa kitu. “Mmesikia kwamba ilisemwa: ‘Mpende jirani yako, na kumchukia adui yako. ‘ Lakini mimi nawaambieni, wapendeni maadui zenu na kuwaombea wale wanaowadhulumu nyinyi, ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni.

 

Ukisoma haya maelekezo ya Yesu kwako kwa akiliza dunia utaona ni UPUUZI PROMAX, Hivi yupo serious kweli?  (NDIO UGUMU WA MOYO WAKO UNAVO KU COST!)

 

Ukiamua kujifanya mjinga na kusema anyway Ngoja nipokee haya maandiko na kuyaishi, Utashangaa kesi uliotaka kwenda mahakamani, Mungu amekupa kazi nzuri ZAIDI ambayo ungekuwa na historia za kushtaki waajiri usingeipata, Wakikupora Bwana ukawaachia, Mungu anakuja kukupa Mume kabisaa wa maana!, Wakati unge Gombea Bwana ungelogwa ufe maskini.

 

HATA KAMA KUTII BAADHI YA MAANDIKO KUTAKUONDOLEA HADHI NA HESHIMA YA KIDUNIA, LAKINI UPATA MILAGE NA MATOKEO KWENYE ULIMWENGU WA ROHO.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top