Hatima nyingi sana zinauawa na mapito. Mungu anaweza kukupa ahadi, akakupa mpaka vision na ukaona na ishara ila yaka ibuka mapito makali ukaona Mungu ni muongo na alikuwa tu anachezea hisia zako. Shetani ni mkali wa mapichapicha. Atakupiga telemundo moja Leo umetolewa mahari kesho upo singo mpaka umtukane Mungu ndo akupe break.
Mungu alipomuumba mwanadamu,alimuumba pamoja na MAPITO/NJIA (paths) ambazo anatakiwa kutembea katika hizo iii aweze kuishi katika dunia hii kwa makusudi ambayo Mungu amemuumbia.
Katika MAPITO/NJIA hizo ndipo Mungu ametuwekea yote ambayo tunayohitaji au tungeyahitaji katika maisha yetu tukiwa hapa duniani.
Katika MAPITO/NJIA hizo ndio kuna afya yako, ndoa (mume/mke}, biashara, nyumba, magari,watoto,utajiri, heshima n.k.
Lakini Mungu ameamua kutupa NENO LAKE litakalotusaidia kututoa kwenye mateso mbalimbali ambayo Shetani ameya penyeza kwenye maisha yetu kupitia mlango wa MAPITO/NJIA za kiroho.
Biblia inatuonyesha mambo MANNE (04) ambayo ya naweza kufanyika juu ya maisha ya watu wa Mungu.
- MAPITO yanaweza KUPELELEZWA
- MAPITO yanaweza KUPOTOSHWA
- MAPITO yanaweza KUUWAWA
- MAPITO yanaweza KUTIWA GIZA
MAPITO YANAWEZA KUPELELEZWA
Ayubu 33:11 “Hunitia miguu ya ngu katika mkata le, na mapito ya ngu yote huyapeleza.”
Mpendwa kwa kuwa maisha yetu yako wazi kwenye ulimwengu wa roho, na Shetani ana uwezo wa kuchungulia na kuona, hivyo atapambana kuhakikisha hufikii hiyo hatua ambayo unatakiwa kuifikia kwenye maisha.
Kumbuka, Mamajusi walipoiona nyota ya mashariki (Mathayo 2:2) walitambua kuwa aliyezaliwa ni Mfalme wakaenda na tunu, dhabihu, uvumba na manemane. Alitambulikaje, kwenye ulimwengu wa vitu vyote vilikuwa wazi na mambo yake yote kwenye maisha yake.
Hivyo, adui anaweza kuyapeleleza mapito yako na kukuzuia kufika hatma yako. Ulikuwa karibia kuolewa ghafla ndoa inaota mbawa, ulikuwa unataka kufungua biashara ghafla mtaji ulikuwa nao unaisha, una mimba ghafla inaharibika, etc.
Kwa jina la YESU tunayafunika MAPITO/NJIA ambazo Mungu ameyaweka kwenye maisha yetu shetani asiweze kuchungulia vile ambavyo Mungu ametukirimia (Waefeso 1:3).
MAPITO YANAWEZA KUPOTOSHWA
Maombolezo 3:7-9 “Amenizinga pande zote hata siwezi kutoka; amefanya mnyonyoro wangu mzito. Naam, nikilia na kuomba msaada, huyapinga maombi yangu. Ameziziba njia zangu kwa mawe yaliyochongwa; ameyapotosha mapito yangu”
Adui akishayapeleleza mapito yako (Ayubu 33:11) na kujua sasa ni hatua gani unayoiendea anatafuta namna ya kukufanya usiweze kufikia na anachokifanya ni kukupotosha. Kama ulikuwa na wazo ndani yako la biashara, ghafla unapopata mtaji linakuja wazo lingine la biashara na ghafla unapoifanya biashara hiyo haifanikiwi na mtaji unapotea. Nini kimetokea?, Shetani kakupotosha kutoka kwenye wazo ambalo Mungu alikupa awali ambalo lingekufanikisha na akakuletea wazo la pili la biashara ambalo linaenda kukupotezea mtaji. (Mwanzo 3:1-6)
Kila mpango wa adui ambao ameufanya kwenye maisha yako, kwa ajili ya KUPOTOSHA MAPITO YAKO ninauharibu kwa DAMU YA YESU KRISTO. Mpendwa Surprise za adui ambazo ameziweka mbele ya maisha yako iii kukupotosha kutofikia kwenye kile ambacho Mungu amekikusudia kwenye maisha yako naziharibu kwa Damu ya Yesu Kristo. Surprise za waume, kazi, biashara, pesa n.k
MAPITO YANAWEZA KUUWAWA
Ayubu 13:27 “Waitia miguu yangu katika mkatale, na kuyaaua mapito yangu yote; wajiandikia alama kuzizunguka nyayo za miguu yangu.”
Anasema kuwa ameifunga miguu kwa mikatale…na KUYAAUA MAPITO YANGU VOTE. Adui akifanikiwa kuuwa mapito yako yote hakuna chochote ambacho utafanya kwenye maisha yako kikafanikiwa. Kwa sababu kila ambacho unakiendea au unatakiwa kukifikia kiko ndani ya mapito ya mtu. Hivyo, adui akiyaua hakuna ambacho Mungu amekuwekea utakifikia.
Ulikuwa na ndoa nzuri na mume/mke anayejali ghafla anabadilika na ndoa inakufa, ulikuwa na biashara inayokuingizia faida na wateja wengi ghafla biashara inakufa na wateja wote wanakukimbia, umepata mchumba kashatoa mahari na Pete kakuvisha ghafla anakimbia n.k
Unaanza kujiona hufai kumbe adui kapeleleleza mapito yako, kayapotosha na kuyaaua. Lakini yupo Yesu Kristo anayeweza kuyafufua Tena mapito yako na kukupitisha katika njia ambayo Mungu amekuandalia.
MAPITO YANAWEZA KUTIWA GIZA
Ayubu 19:8 “Yeye ameiziba njia yangu nisipate kupita, na kuitia giza katika mapito yangu”
Kama nilivyotangulia kusema, kuwa Mungu alivyomuumba mwanadamu alimwandalia mapito/njia ya yeye kupita iii ayapate Yale yote yatakayomsaidi a anapoishi hapa duniani kuliendea kusudi lake. Hapo tunaona adui anaweza kuiziba njia yako yako iii usiende kupita, na haishii tu kuiziba Bali anatia giza kwenye mapito.
Kwanini anatia giza ni iii usijue unakokwenda au unalotakiwa kufanya kwa wakati wake. Ni muda wa kuolewa wewe hata huelewi, ni muda kuanza biashara uliyokuwa unatamani lakini hujui, ni muda wa kupanda au kuvuna huwezi kujua, anakuja mume/mke kwa ajili ya kukuoa lakini huwezi kujua….shida mapito yako yametiwa giza hivyo huwezi kujua majira yakupasayo kufanya maamuzi maana uko kwenye giza hujui kama ni mchana au ni usiku.
MAOMBI
Kwa jina la YESU KRISTO kila giza lililowekwa kwenye maisha yako naliondoa kwa Damu ya Yesu Kristo. Nuru ya Kristo iangaze kwenye mapito yako huku Nuru ya Nena lake ikikuongoza (Zaburi 119:105) katika jina la YESU.
Baada ya kuona mambo hayo MANNE ambayo adui anaweza kuyafanya katika MAPITO/NJIA tuangalie jambo lingine muhimu ambalo adui analifanya katika maisha ya watu na kujikuta wanahainga mchana kutwa pasipo kufanikiwa wala kuwa na matumaini.
Jambo hili, ni kwamba ADUI ANAPOYAGUSA MAPITO/NJIA ZAKO hakuachi hivyo, Bali anachokifanya ni kuhakikisha anakupandishia mapito/njia yake, Na anapofanikiwa kukupandishia njia zake utakutana na Yale ambaye amekuwekea mambo yake (magonjwa, kuachika, mauti, misiba, madeni, uchungu, huzuni, kudharauliwa etc).
Ayubu 30:12-18 “Kwa mkono wangu wa kuume huinuka kundi, huisukuma miguu yangu kando, na kunipandishia njia zao za uharibifu……..huifukuza heshima yangu kama upepo, na kufanikiwa kwangu kumepita kama wingu ……..wakati wa usiku mifupa yangu huchomeka ndani yangu, na maumivu yanayonitafuna hayapumziki, na ugonjwa wangu kuwa na nguvu nyingi…”
Neno linasema huisukuma miguu yangu kando…inasukumwa kutoka katika njia yake ambayo Mungu aliikusudia. Wakishaisukuma ndio WANAKUPANDISHIA NJIA ZAO ZA UHARIBIFU…baada ya kupandikizwa hizo njia za uharibifu unashangaa mambo yako yote yanaharibika pasipo kuwa na sababu za msingi.
Kumbe ni njia ambayo Shetani ameipandikiza kwenye maisha yako ambayo inaleta uharibifu kwenye kila jambo ambalo ulilonalo (ndoa, kazi, biashara, kilimo, mifugo,afya etc) au unayotarajia kuyaendea.
Ukisoma hiyo AYUBU 30:12-18 utaona mambo mengi yanayotokea baada kuisukuma miguu yako kando na kukupandishia njia zao za uharibifu. Mambo yaliyooneshwa ni pamoja na;
- Kuharibiwa kwa njia zako Kuzidisha misiba kwenye maisha yako.
- Vitisho kukugeukia.
- Kuondokewa kwa heshima yako Kufanikiwa kwako kumepita kama wingu Siku za mateso kushika
- Kupata maumivu ya mifupa usiku na maumivu yasiyoisha.
- Na ugonjwa uliokukabili baada ya kupandishiwa hiyo njia kuwa na nguvu nyingi.
Aidha, yapo madhara mengine ambayo yameainishwa kwenye neno la Mungu katika kitabu cha AYUBU 19:9-19. Tukianzia mstari wa Ayubu 19:12 anasema “Majeshi yake husongea pamoja, na kunipandishia njia yao, na kupiga marago kuzizunguka hema yangu”
Majeshi yanayozungumziwa hapa ni Majeshi ya shetani au mawakala wake. Wanachotafuta ni kukupandishia njia zao ambazo zitakuondolea mafanikio kwenye maisha yako ambayo Mungu ameyakusudia katika maisha yako.
Baada ya kukupandishia njia zao katika Ayubu 19:12 madhara yaliyojitokeza ni pamoja na;
- Kutengwa na ndugu na marafiki zako (Ayubu 19:13)
- Wanafamilia na marafiki kukusahau (Ayubu 19:14)
- Watu wa nyumba yako, wafanyakazi wako, mke/mume wako na watoto kukudharau (Ayubu 19:15-19) n.k
Yako mengi ambayo ninatakiwa kukufundisha kuhusiana na umuhimu wa kujifunza kuyaombea mapito yako mara kwa mara iii kuweza kufanikiwa kwenye maisha yako kwa kiwango kile ambacho Mungu amekikusudia kwenye maisha yenu.
Kwa hayo machache ninajua Mungu kupitia Roho Mtakatifu atakupa kiu ya kujifunza zaidi kuhusiana na mapito/njia alizoziweka katika maisha yetu.