Gethsemane Prayers :Day 1
Mathayo 26:36-56
Kisha Yesu akaenda pamoja nao bustanini Gethsema ne, akawaambia wa nafunzi wa ke, “Kaeni hapa nami niende pale mbele kusali.” Akawachukua Petro na wa na wawili wa Zebedayo, akaa nza kuwa na huzuni na mahanga iko. Hapo akawaambia, “Nina huzuni kubwa moyonihata karibu kufa. Kaenihapa mkeshe pamoja nami.” Basi, akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akasali:”Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki kinipite;lakini isiwe nitakavyo mimi,ila utakavyo wewe.” Akawaendea wale wanafunzi, akawa kuta wa melala. Akamwa mbia Petro, “Ndio kusema hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? Kesheni na kusali iii msije mkaingia katika majaribu.Roho inataka lakini mwili ni dhaifu.” Akaenda tena mara ya pili akasali:”Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kipite bila mimi kukinywa, basi,utakalo lifanyike.”
Akawaendea tena, akawakuta wamelala, maana macho yao yalikuwa yamebanwa na usingizi. Basi, akawaacha, akaenda tena kusali mara ya tatu kwa maneno yaleyale. Kisha akawaendea wale wanafunzi, akawaambia, “Je, mngali mmelala na kupumzika? Tazameni! Saa yenyewe imefika, na Mwana wa Mtu atatolewa kwa watu wenye dhambi. Amkeni;twendeni zetu Tazameni! Anakuja yule atakayenisaliti.”
Luka 22:39- 44
39Yesu akatoka, na kama ilivyokuwa desturi yake, akaenda katika mlima wa Mizeituni;wanafunzi wake wakamfuata. 40Alipofika huko akawaambia, “Salini, msije mkaingia katika kishawishi.”41 Kisha akawaacha, akaenda umbali wa mtu kuweza kutupa jiwe, akapiga magoti, akasali: 42″Baba, kama wapenda, ukiondoe kwangu kikombe hiki; hata hivyo, mapenzi yako yatimizwe, wala siyo yangu.” 43Hapo, malaika kutoka mbinguni akamtokea iii kumtia mayo. 44 Akiwa katika uchungu mkubwa, alisali kwa bidii zaidi na jasho likamtoka kama matone ya damu, likatiririka mpaka chini
Mpendwa Yesu ni Mwana wa Mungu na anaenda kwenye bustani ya Gethsemane na wanafunzi wake kusali Kama kawaidaaa Yao kusali pamoja. But this day was different.Yesu anakuwa na huzuni na mfadhaiko. Ana waambia kabisaa roho yangu ina huzuni mpaka kifo. Ni highest level ya huzuni. Yaani Hilo jambo linamnyima raha kabisaaa. Yaani mpaka anawaomba wanafunzi wake wakeshe nae kwenye maombi.Mpendwa Hili likufundishe kwamba huzuni ipo Yesu Ali pata huzuni mpaka akahisi kufa. So hio huzuni Unahisi moyoni mwako ni normal kabisaa. Pili ikufundishe maombi ya kukesha ni muhimu na yana nguvu.Ndo maana Yesu anawaomba wakeshe. Sasa wewe ulie Lala unataka ufanye maombi ya kukesha jua Kali shauri zako. Na Yesu alikesha mara nyingi tu. Ongeza ratiba za Mikesha kwenye maombi yako.
Content ya Sala ya Yesu
My Father, if it be possible, let (H)this cup pass from me; (l)nevertheless, not as I will, but as you will.”
Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki kinipite; lakini isiwe nitakavyo mimi, ila utakavyo wewe.”
Mpendwa Anarudia sala ujumbe huu huu mara 3. Mpangilio wa maneno ndo unabadilika ila ujumbe ni ule ule kikombe baba! Kikombe Ukiwezakana kimpite. Ila si kama atakavyo yeye Bali kwa mapenzi ya Mungu.Mpendwa Tuna kunywa Vikombe vingi vichungu mnooo. Tushasikitika mpaka basi. Yaaani. Na Mungu tunae mtumikia tunamjuaaa.Haiwezekani kabisaa iwe mapenzi yake sisi kunywea hivo vikombe vya kipuuzi Puuzi. Haiwezekani asilani. Haiwezi kuwa mapenzi ya Mungu ukae bila ndoa unazini tu iii hali yeye kasema kabisa ni Amri sio Hiari. USIZINI! Haiwezekani ikawa mapenzi ya Mungu Uzeeke kwenu na upweke, watu wakuseme vibayaaa vibayaaa wa kati umeokoka na unamtumikia. Hiko kikombe sio mapenzi ya Mungu kabisaaa. Haiwezekani yawe mapenzi ya Mungu usome usipate kazi. Uishi maisha ya kunyanyasika na kuteseka. Hiko kikombe sio mapenzi ya Mungu asilani. Mungu tunaemtumikia tunamjuaaa! Tuna ahadi nae kwenye maandiko.
Yeremia 29:11
Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye.
Ee Yesu mnazareti, unaijua ile huzuni uliyokuwa nayo Gethsemane inavo umizaaaa na kufadhaishaa. Kabisaaa! Yesu wetu Kuna vikombe wanao tumenywea mda mrefu pasipo na msaada wowote. Yamkini ni katika mahusiano. Yamkini ni kwa habari ya kazi, Yamkini ni kwa habari ya ndoa, Yamkini ni kwa habari ya biashara, yamkini ni kwa habari za madeni sugu, Yamkini ni kwa habari ya cheo au uzazi Bwana Yesu tunajua Uliupenda sana Ulimwengu na wanadamu Mpaka ukatoa uhai wako kwa ajili yetu. Bwana Yesu tazama vikombe tunavunja nyweshwa na Yule muovu na si mapenzi ya Baba yako kabisaa. Bwana Yesu ametushikilia hapo mda mrefu ana tunywesha vikombe vya huzuni na uchungu mkuu. Yesu wewe ndo unajua jinsi hivo vikombe vina Ongeza uchungu maishani mwetu tunasimama na maombi yako ya Gethsemane tunaomba uungane na sisi kama ikiwapendeza Mbinguni KlKOMBE HIKI CHA (TAJA KlKOMBE CHAKO) KINIEPUKE. Mbingu zifanye jambo kwa habari yangu (TAJA JINA LAKO)
Yamkini Bwana Yesu tulikosea sisi mahala flani katika maisha na kutoa huo uhalali kwa Yule muovu kutushikilia hilo eneo na kutunywesha hiko kikombe. Leo hii tunanaguka miguuuni pa kiti cha enzi tu kuomba Rehema. Ee Mungu baba uketie enzini rehemu makosa yetu na baba na babu zetu. Kumbuka Rehema Mungu. Ni Rehema zako tu ndo zitakazo tuvusha hapa.Uturehemu kwa Damu ya Yesu. Yamkini tuna madeni au baba na babu zetu wana madeni kwa Yule mwovu ndo yanatoa uhalali wa sisi kunywea hiko kikombe mda mrefu tunaomba DAMU ya Yesu irehemu na kulipa hayo madeni yote baba katika Jina la Yesu. Mungu wewe ni Mungu wa haki siku zote. Mungu umeona haki yetu imepokonywa au kunyimwa au kucheleweshwa na Yule muovu. Usikae kimya Mungu watu uketie Mbinguni kwenye kiti cha enzi. Mungu wa Ibrahim, Mungu a lsaka na Mungu wa Ya kobo usikae kimyaaa. Tunaomba Rehema za ko. Sawa sawa na maandiko ya sala alioa Ali mwanao kipenzi pale Gethsemane ikikupendeza kikombe hiki ( TAJA KIKOM BE) kiniepuke ila si kwa mapenzi ya ngu mimi bali mapenzi yako. Kama Mungu ushivo nikavuke Leo na iwe habari ya kupita si ya ku control maisha yangu.
Mungu baba fanya ja mbo jipya kwa habari ya hiko kikombe (TAJA KIKOM BE CHAKO). Tuma malaika zako wa Mbinguni wakatengue kila kinachosababisha hiki kikombe (KITAJE) kisiondoke na kuniachia amani na furaha! Kama ulivo tuma Malaika wa ko toka Mbinguni akamtia Bwana Yesu nguvu pale Gethsemane. Tuma malaika wa ko ataebadilisha matokeo na kuleta majira mpya. Wewe Mungu ndo unajua kinacho kwamisha na malaika ga ni ata solve.
Mungu baba hakuna jambo linaloshindika na kwako kamwe. Hata hiki kikombe baba hujakishindwa. Tu nazidi kusimama na maandiko ya sala ya Bwana Yesu pale Gethsema ne lkikupendeza kikombe hiki (Taja kikombe) mimi (taja jina lako). lkakupendeze baba yangu ulie Mbinguni sio Kwasababu nasatahili au ni haki yangu ila kwa sababu ya Ukuu wako, utakatifu wako na upendo wa ko juu ya wa nao. Utukufu wako ukaniepushe na hiki kikombe baba. Katikati ya ghadhabu na machungu ya hiki kikombe kumbuka Rehema Baba na ukanirehemu kwa Damu ya mwanao Yesu Kristo
Psalm 77:14 (Zaburi 77:14)
You are the God Who performs miracles; You display Your power among the peoples. Mungu wewe ni Mungu wa miujiza na nguvu. Baba tenda muujiza kwenye hiki kikombe kiniepuke. lkupendeze nikavuke sio kwa juhudi zangu bali kwa muujiza toka kwako.
Baba Kama kusali nimesali Sanaa, Kama kufunga nimefunga Sanaa, Kama sadaka nimetoa nyingi lakini Mungu hamna matokeo, na hata yakiwepo ni madogo au ya msimu. Mungu baba uketie sirini laumu na fedheha za wanadamu zimenila na kunimaliza kwa habari ya hiki kikombe (kitaje). lngilia Kati uniokoe Mungu kwa mkono wako tukufu. Bila hivo nitafia katika hii huzuni Mungu.
Yeremia 37:20
Na sasa unisikilize, Ee bwana wangu mfalme; maombi yangu yakapate kibali mbele yako; usinirudishe nyumbani mwa Yonathani, mwandishi, nisije nikafa humo.
Ee Mungu maombi haya yapate kibali machoni pako na nisinywee tena kile kikombe nisije nikafia kwenye hio huzuni. lkupendeze Hiko kikombe kinieupuke Baba yangu uketie enzini.Sitaki kuishi tena kwa huzuni, uchungu, laumu na Sikitiko.
Je kwa huzuni hio na machungu nitaweza kukuinulia ibada takatifu na za kukupendeza zisizo jaaa ubatili na laumu ndani yake. Nasimama na Bwana Yesu pale Gethsemane kuanguka miguuuni pako ikikupendeza Baba yangu ulie Mbinguni kikombe hiki kiniepuke, si kwa mapenzi yangu ila kwa mapenzi yako.Sikio lako si zito na mkono wako ni mwepesi kuokoa. Mungu baba uketie mahali pa juu wakati wakuniokoa ndo sasa wala si wakati mwingine. Mungu ukaniepushe na hiki kikombe. Saa ilia amriwa ndo sasa. Mungu ukanivushe na kuniumbia Tuamini Jipya.Kama uishivo hakuna gumu mbele zako wala usilo liweza. Nasimama na neno hili nikiomba na Kuamini kwa Jina la Yesu.
Mathayo 19:26
Yesu akawatazama na kuwaambia, “Hili haliwezekani kwa wanadamu, Lakini yote yanawezekana kwa Mungu.”
ITS A WRAP DAY 1
Wale mlio Kesha mlifaidi muongozo wa Roho Mtakatifu na tukatiii maelekezo. Na tumemshuhudia Mungu kwa level zingine. Na Tumepata msaada mzito. Tulia hitaji. Unforitunately kutokana na sensitivity ya maombi yenyewe Roho Mtakatifu ameelekeza yasikae Public sababu ni maombi hatari na sensitive yanahitaji instructions toka kwa Roho
Mtakatifu na Supervison. So nimelazimika kuyaondoa ONLY THE SENSITIVE PART. Mlioa lala kama andiko linavosema mwili ni dhaifu, Roho I radhi Leo usiku kuna mkesha mwingine. Mpambane zaidiii!
Gethsemane Prayers: Day 2
Key of King David/Ufunguo wa Mfalme Daudi
lsaya 22:22
Na ufunguo wa nyumba ya Daudi nitauweka begani mwake; yeye atafungua wa la hapana atakayefunga; naye atafunga wala hapana atakayefungua.Hiko kikombe chako Yamkini ni kitu kimefungwa usikipate. Haijalishi na nani wala kwanini. La msingi ni Hilo jambo limefungwa kabisaa.Lakini Mungu mwenywe kwenye lsaya 22:22 anaweka wazi Kuna ufunguo wa Nyumba ya Daudi. Amba o ukifungua jambo hapana anaeweza kufunga.Sasa Hiko kikombe chako tunaenda kukifungua na ufunguo wa Daudi.
ROHO MTAKATIFU ANASEMA LEO NDO TUMEMALIZA HAPA! NO DAY 3! MUNGU ANAENDA KUTUFANYIA KICHEKO KIKUBWA KILA ATAESIKIA ATACHEKA NA SISI.ONLY HIO VISION YA UNAPOTAKA KWENDA BABADA YA KUEPUKA KIKOMBE llSHI NDANI YAKO MPAKA ITIMIE. HIO NI AHADI YA MUNGU KWAKO KWAMBA AMEKIONDOA KIKOMBE ULICHOKINYWEA USIKU HUU NA KUSUDI LA MOYO WAKO LITATHIBITIKA. HALLELUYAH!