Kukwama katika maombi huweza kusababishwa na sababu mbalimbali na sababu hizi niza kipekee :
Aidha Sababu za kukwama katika Maombi ya Mwenza wakati mwingine huweza kutokea katika kipindi ambacho tayari tumeomba sana na Kukosa Matokeo;
1.TUNAACHA KUOMBA
Hii ni sababu ya kukwama katika Maombi kwani katika kipindi hiki wengi wetu huanza kunung’unika tukidhani tunaomba.
2.IMANI YAKO INARUDI NYUMA
Katika kipindi hiki wengi wetu huweza kuomba bila kujali, yaani matokeo yatokee au yasitokee ni sawa.
3.KUKATAA TAMAA
Katika hatua hii mtu huweza kutilia mashaka Biblia nzima takatifu na dini nzima kwa ujumla.
Kwanini Hatupati Matokeo?
Wengi wetu tunaomba Matokeo. Mfano katika Sala zetu za wenza, wengi wetu tunatengeneza picha ya yale tunayoyataka, Tunaweka vigezo na hata kufikia kupanga kiasi cha Muda wa kutoleana posa/ mahari.
Marko 10 : 27 “Kwa Mungu yote yanawezekana” lakini tunayo imani kubwa kiasi hicho cha kuhamisha milima? Wengi wetu tunazo imani za kawaida sana na Imani zetu, uhusiano na Mungu na uelewa wa neno lake lazima vitoshane na matokeo tunayotaka na uharaka au muda tunaotaka matokeo yatokee.
Usiombe Matokeo
Maombi ya matokeo ya ghafla au haraka ni maombi magumu sana na yanahitaji imani kubwa sana, uhusiano wa karibu sana na Mungu na uelewa wa hali ya juu wa neno la Mungu jambo ambalo ni watu wachache sana hufikia katika ngazi hii.
Aidha maranyingine huwa kuna uwezekano mkubwa maombi unayoomba hayako sawa na mpango wa Mungu kwa mfano Mpango wa Mungu unaweza kuwa upate Mume au Mke anayekujali na kukukuza kiimani lakini wewe matokeo unayo yaomba na kuyatak ni Mume / Mke mwenye sura nzuri na pesa. Hivyo unakuta unajibiwa lakini mizani yako ya kupima majibu inaona bado hujajibiwa, pia jambo hili huweza kukufanya uone kimya kirefu cha majibu au kutojibiwa kabisa.
Hivyo basi tunayohaja ya kumpa Mungu nafasi katika Maombi yetu ili aweze kufanya njia sahihi na majibu sahihi ya changamoto zetu zaidi ya kujiwekea vikwazo kwa kuomba matokeo.
Omba hatua Moja zaidi ya ulipo
Haya ni Maombi mepesi sana na yenye matoke chanya na ya haraka sana ambayo baada ya kukatisha tamaa yanakujenga kiimani zaidi na kukutia moyo kwenye safari yako ya kupata matokeo ya jumla.
Kwa mfano ” Waisraeli walimlilia Mungu kuhusu mateso ya Farao, Waka-ahidiwa kwenda Caanan, lakini tazama katika safari yao nzima waliomba maombi mengi sana kwani kila hatua waliyopita ilikuwa na changamoto yake iliyohitaji change of plan na change of prayer hata wewe kila hatua itakuja na changamoto zake na kama Waisraeli itakulazimu kuchange gear ! ( Kubadili mwelekeo). Aidha kuna hatua utavuka kwa mfungo, nyingine kwa sala nyepesi nyepesi na nyingine kwa maombi ya Getsemane.
Pia, Hawa hawa Waisraeli katika safari yao ya Caanan kila mji waliopita walipita na miongozo tofauti tofauti kutoka kwa Mungu, Mfano Muongozo wa kuiteka Yerico ulikuwa tofauti na mpango wa kuiteka Hebroni.Hivyo hata wewe muongozo wa kukupa mchumba nitofauti na Muongozo wa kukufanya ukubalike Ukweni!!! kila hatua muombe bwana Muongozo yakinifu wa kuvuka.
“Matokeo ni Safari, Safiri na Bwana Mungu wako Hatua kwa Hatua”
Hatua za maombi ya Mwenza
- Kama hauna Mwenza kabisa ( Uko Single) hunabudi kumuomba Mungu uonekane kwa watu sahihi na ije kwa kiasi yaani kidogo kidogo.
- Kama Mwenza yupo lakini haeleweki, Muombe Mungu ishara akuoneshe kama ni Mtu sahihi au Sio ili upate muongozo mmoja.
- Kama umepokea ishara au umeridhika basi Muombe Mungu ajitambulishe kwenu (Nyumbani kwenu) / akutamkie nia ya dhati.
- Muombe Mungu ukubalike ukweni na upate kibali huko.
- Chereko chereko ( Ndoa) ikaye ya kheri.