Nguvu ya Mungu katika Kukata Tamaa

Hata maombi yawe na ufanisi kiasi gani, au yatolewe na Nabii gani kama umekata tamaa ndani yako hayawezi kufanya kazi. Hivyo Utabadili makanisa lakini bado matokeo yatakuwa hafifu au yasiyoridhisha.

Ndani ya Biblia wengi walikata tamaa mara moja au zaidi! Tuangalie rejea chache!

Mfano wa Habakuki

Habakuki 1 : 1- 17

” Ee Mwenyezi Mungu,nitakulilia mpaka lini, nawe unisikilize na na kunisaidia? Kwanini nalia: ‘Dhuluma’ nawe hutuokoi?”

Habakuki amepewa jina weeping phrophet maana aliandika kitabu cha manung’uniko. Katika Aya yote ya kwanza (1)  Habakuki amesononeka kwa kukosa majibu kwa Mungu na kikubwa hasa  alichonung’unika  Habakuki ni utawala wa kionevu wa Wakaldayo uliodumu kwa muda mrefu , pasipo Mungu kufanya lolote dhidi yao lakini Good News Mungu ana mjibu Habakuki kwenye aya ya 2! ( Alijibu nini? nakupa homework kajisomee….).

Na Mungu hakujibu maombi ya Habakuki  bali alijibu kunung’unika kwake na Maombi  yalibaki pending ( yakisubiri) ila manunguniko yalijibiwa kwa haraka!!!. Hivyo,  Naomba nikutie moyo  mpendwa hatakama umekata tamaa kiasi gani usiondoke kwenye uwepo wa Mungu na kama ukishindwa kwenda ibadani nenda kanung’unike, Maombi yako yanaweza yasijibiwe ila ukapata Ufunuo wa namna ya kutatua changamoto yako.

Mfano wa Nabii Elia

Wafalme 1 : 17,18, 19.

Nabii  Elia ni kati ya manabii waliotenda miujiza  mikuu zaidi ya kuhubiri na kwa  miujiza aliyotenda Elia aidha  uhusiano aliokuwa nao na Mungu ungeweza kusema imani yake haiwezi kutikiswa na lolote.

Elia alizuia mvua miaka mitatu (3), alilishwa na kunguru, alifanya muujiza kwa mjane wa (unga na mafuta yasiyoisha) , alimfufua mtoto wa mjane, aliita moto toka juu mbinguni ukateketeza sadaka na kuwaahaibisha manabii wa baali. Elia alikuwa nabii wa vitendo kuliko maneno.

Lakini  Elia anapojua ashamalizana na baali, baada ya kupambana nao kwa miaka kadhaa na kufanikiwa kuwashinda hadharani, akaona sasa ataweza tulia lakini  ndo kwanza akapata taarifa kuwa Jezebel amejiapiza kumuua kwa gharama yoyote yaani baada ya vita kuisha ndo ikaanza. Elia anakata tamaa kabisa kiasi cha kumuacha mtumishi wake sehemu na yeye kuelekea msituni!.

1 Wafalme  19 :4 Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake kufa, akasema ” Yatosha Sasa Ee Bwana, Uiondoe roho yangu kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu.”

Elia anajiombea kufa na kumbuka huyu ni Nabii wa ngazi za juu kiasi cha kufufua mtu. Ila tazama alivyokata tamaa! Haoni mbele wala nyuma. Na Elia hakuwa amekosea popote wala kukiuka agizo lolote alifanya kila alichotakiwa kufanya  lakini mambo bado magumu.

Malaika wa bwana walimtokea Elia na kumpa chakula lakini hawakujibu  maombi yake yaliyomkatisha tamaa wala ya Kufa. Elia akazidi kwenda msituni na ndipo Mungu anamtokea Elia na wanajadiliana kwanini Elia yuko pale, na  Kisha Mungu akampa Elia suluhu ya kwenda kutekeleza.

Naomba nikutie moyo mpendwa, Mungu wetu ni muelewa, hatoacha ufe au uangamie katika kukata kwako tamaa, rudi kwa Mungu atakupatia hitaji lako kwani  Hata watumishi wakubwa kama wakina Elia walipitia hio changamoto ila hawakuiacha imani na Elia angeweza kwenda kwa Jezebel  kujisalimisha na kumtumikia baali aokoe nafsi yake ila akaona bora akaikabidhi nafsi yake kwa Mungu na  ijulikane Mungu alimchukua kuliko alikufa kwa upanga wa Jezebel. Elia hakutaka kumpa Jezebel ushindi katika kifo chake. Rudi kwa Mungu atakusaidia vita yako kwa wakati wake kama alivyomshindia Elia.

Mfano wa Mfalme Daudi

2 Samweli : 11 & 12.

Mfalme Daudi anaanguka kwenye uzinzi, anapora mke wa mtu, anampa mimba na anamuua Mumewe, anamtwaa na kumfanya mke wake kiasi cha kusahau kabisa matendo yake na Mungu anamtuma Nabii Nathan Kwake na  Daudi anakubali uovu wake wote na kutubu. Mungu anamuahidi  Daudi kuwa hatokufa ila mtoto wake atakufa kisha Mtoto  wa Daudi anaanza kupoteza afya na Daudi anafunga kavu na kulala akimlilia Mungu sana na katika Siku ya saba (7) mtoto  wa Daudi anakufa. Daudi anapojua mwanae kafariki anaenda kwake, anasali kwa Mungu, anakula na kuendelea na maisha yake. Mungu anakuja kumpatia Daudi mtoto mwingine ambaye  ni Suleiman kwa yule Mkewe.

Hiyo ,Naomba nikutie moyo mpendwa, yamkini ulimkosea Mungu sehemu kiasi cha kuachilia  magumu dhidi yako, isiwe sababu ya kukata tamaa!!!. Jipe moyo kama Daudi katikati ya magumu fanya toba na umrudie Mungu, naye atakupa faraja kuzidi hayo magumu.

2 thoughts on “Nguvu ya Mungu katika Kukata Tamaa”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top