Wapendwa kuna mambo yamekwama na kuna mambo YAMESHINDIKANA, It’s is in-fact a DEAD END! YAANI BIASHARA IMEKWISHA!, Mfano umepewa talaka na mtu ambaye mna watoto watatu (3) Na amesha OA, mtu mwingine na wamezaa watoto wengine tayari, NDOA YAKO IMESHINDIKANA!
Mpendwa Kukaa ungoje labda yule Mke mpya Afe au Bwana augue gonjwa baya au apate ajali mbaya uhitajike wewe kuja kumuuguza IT IS HOPLESS, Hata ukirudi hutakuwa Mke utakuwa NESI!, Mtu una miaka 40 shela badooo hujafanikiwa kuvaa!! Looh!.
Na Isitoshe huna hata mtu, IT IS DEAD-END, Mtu unaitafuta 40 kazini hujanusa na vyeti vimepigwa vumbi kabatini vimejaa mavi ya mende, IT IS A DEAD-END, Unaikimbiza meno-pause huna mtoto! Miaka kumi (10) ya ndoa, Mwenzio kazaa nje, Watu wanakwambia USIKATE TAMAA! KIVIPII? WANA UTANI!, KUNA MAMBO YAMESHINDIKANA! TOTAL DEAD END!.
MPENDWA KAMA DEAD END HAIJAKUKUTA PERSONALY HUWEZI KUIELEWA!, WATU WANAPENDA KUTOA MAJIBU MEPESI KWA HOJA NZITOO! NI YALE MANENO YETU “USIJALI MWAYA MUNGU ATAKUTENDEA NA WEWE “, LINII? NA WAPII? NA SAA NGAPI ?
WAPENDWA JUZI-JUZI HAPA NILIPITIWA NAKOZ TO NAKOZ FLANI MPAKA NIKAWA NATEMBEA NA MSTARI WA BONGO FLEVA MAANDIKO YOTE YALINIPONYOKA NIKASIMAMA NA BONGO FLEVA VERSE, VERSE YENYEWE YA WIMBO WA MWANA-FA ILE YA “INGEKUWA VIPI” NA MSTARI NILIOTEMBEA NAO NI HUU “NAWAZA MAMBO KWA KINAA NA BADO MAJIBU SINAA, UWEZO WA MUNGU UNAONEKANAA ANGEAMUA INGEWEZEKANA”; HAPO “UWEZO WA MUNGU UNAONEKANA ANGEAMUA INGEWEZEKANA” SWADAKATAAA!, I WAS LIKE MUNGU AMUA BASI, AMUAA! LAKINI AAMUE WAPIII? NIPO KWENYE DEAD-END, NIMETULIZWA NAYO, NA NATESEKA NAYO KAMA KAWAIDA.
MAANDIKO YANASEMAJE KUHUSU HIZI DEAD END SITUATIONS?
WAPENDWA MUNGU HAKUSEMA HAYA MAPITO HAYATAKUWEPO BALI ALICHO AHIDI NI KUKUPA USHINDI DHIDI YA HAYO MAPITO. Wapendwa Mapitooo yapo kama kawaida na kila mtu atapita ya kwake il Alicho ahidi Mungu ni KUKUPA USHINDI DHIDI YA HAYO MAPITO.
1 Corinthians 15:57
57. But thanks be to God, He gives us the victory through our Lord Jesus Christ.
Romans 8:37
37. No, in all these things we are more than conquerors through him who loved us.
WAPENDWA WENGI MNA MUULIZA MUNGU NA KUMLAUMU NA KU-PANIC KWANINI MNAPITIA HAYO MAPITO? SASA MLITAKA APITIE NANI? KILA MTU ANA MAPITO YAKE. SWALA LA NYINYI KUPAMBANA KUMUULIZA MUNGU NI USHINDI ALIO AHIDI KWENYE HAYO MAPITO UKO WAPI?
WAPENDWA HAKU AHIDI HUTAPITIA MAPITO! WATU WOTEE HATA WAKARIBU YAKE WALIONJA MAPITO MPAKA WAKAJIMALIZA KWENYE MAANDIKO KUANDIKA UTAMU WA MAPITO WANAYOPITA.
John 11:35
35. Jesus wept.
YESU Mwana wa Mungu anamwaga machozi, Chezea mapito wewe! yaani Masiah mzima!, Anashindwa kujizuia! Hii ni kabla ya JASHO LA DAMU.
2WAKORINTHO 11:23-29
23 Wao ni watumishiwa Kristo? Mimi ni mtumishi bora zaidi, nasema kama kichaa. Nimefanya kazi zaidi, nimefungwa gerezani zaidi, nimechapwa viboko visivyo na hesabu, na mara nyingi nilikuwa karibu kufa. 24 Mara tano nimechapwa viboko arobaini kupungua kimoja na Wayahudi. 25 Nimechapwa kwa chuma mara tatu. Nimepigwa mawe mara moja. Mara tatu nimevunjikiwa na meli. Nime-elea baharini usiku kucha na mchana kutwa. 26 Katika safari zangu nyingi, nimekuwa katika hatari za mafuriko, hatari za wanyang’anyi, hatari kutoka kwa Wayahudi wenzangu na hatari kutoka kwa watu wa mataifa mengine; nimekuwa katika hatari mijini, nyikani, baharini na katika hatari kutoka kwa ndugu wa uongo. 27. Nimekuwa katika kazi ngumu na taabu, siku nyingi nimekuwa bila usingizi,nimekuwa na njaa na kiu, mara nyingi nimekuwa bila chakula, katika baridi na bila nguo. 28 Na ukiacha mambo mengine nimelemewa na wasiwasi juu ya makanisa yote.29 Je,ni nani ana kuwa mdhaifu nisijisikie mdhaifu? Nani anashawishiwa kutenda dhambi nisijisikie nachomwa na uchungu?
Wapendwa Mtume Paul ana wakumbusha Wakorintho kupitia barua yake ya pili kwamba KAMA MAPITO BASI NA YEYE ANAPITIA KWELI-KWELI!. Bado kina Ayubu, bado Mitume wengine, Bado Wafalme kina Daudi na Saul bado Makuhani kina Eli, na Elia, MAPITO YAPO ILI UPITIEE.
ISSUE SIO MAPITO ISSUE NI UNAPITAJE PITAJE!, WENGI MMEPITIA MUDA MREFU KULIKO WENZENU KWA SABABU MBALI-MBALI, SASA SIONI TIJA KUANZA KUWAPA SABABU KWANINI MME KWAMA HAPO SABABU NI NYINGI LAKINI MOJA WAPO NI KITOKUWA NA NIA YA DHATI YA KUVUKA.
MIMI KUNA WATU WENGI WANANISUMBUA HAWAJAWAHI KUPATA KAZI, JUZI TUMEANZA SAKO LA NYANI KUFURUMUA KILA KINACHOFANYA USIENDE KAZINI, HAKUNA HATA MMOJA ANAYEFANYA HII PROGRAM, MMOJA NDIYO JANA KANIAMBIA ANAANZA DAY 1.
NINGEKUWA SIO MKOMAVU WA IMANI NA KUELEWA LOGIC YA KUNA WATU MUNGU AMEWAKUSUDIA WAVUKE NINGEACHA DAY 1, NILI ELEWA TU MUNGU HAKUWAKUSUDIA WAO SABABU HAWANA NIA LAKINI KUNA WATU MIMI SIWAJUI ILA ILITAKIWA NITUMIKE KAMA CHOMBO WAVUKE, NA WAMEANZA KUNITAFUTA.
WALE WABABAIFU WANGU NAWANGOJA KWA HAMU WAJE WANILETEE UBABAIFU WAO WANATAKA KUVUKA ENEO LA KAZI!, MMMH!.
Mpendwa Tuachane na kwanini hujavuka mpaka leo ,Tujiulize UNAVUKAJE HAPO?
1.ONGEZA UFAHAMU NA MAARIFA!
Unaweza kuwa unamjua Mungu na maandiko to some extent na ume-OKOKA fresh tu kitambo lakini MAANDIKO NA MAARIFA YA WEWE KUVUKA HAPO HUNA! INATAKIWA U-INVEST KUYATAFUTA, Ndipo unakuta unaombea watu wanaolewa lakini wewe bila-bila, Unakuta unaombea ndoa za watu zina imarika yako imevunjika kitambo sana na umeshindwa ukirudisha.
MPENDWA UKIONA IBADA HAZIKUPI MATOKEO PANDA VIWANGO, BADILISHA WATUMISHI, EXPLORE ZAIDI YA UNACHOFANYA, KUNA WATU WALIKUWA WANABISHA HAWAJARONGWA KWENYE CAREER!, WAMEFANYA HII PROGRAM NDIO WAMEHAKIKISHA WAMERONGWA ENEO LA KAZI, KAMA WASINGE-EXPLORE WANGEZEEKA BILA KAZI.
UMEKAA HUDUMA MIAKA KUMI (10) HUNA MAHUSIANO, HUU MWAKA WA SKUMI NA MOJA (11) HUDUMA ZINGINE HUZUONI AU ?, IT IS OBVIOUS CASE YAKO NI CHRONIC IMESHINDIKANA KWENYE MADHABAU YAO!, MIMI ROMAN CATHOLIC NA UNAZEEKA MWENYEWE WALOKOLE HUTUONI AU ?, TAFUTA HUDUMA ITAKAYO KUVUSHA.
UNAFANYA IBADA NYEPESI NYEPESI HUVUKI, PANDA VIWANGO NA ANZA KUFANYA IBADA NZITO! ANZA KUFUNGA TATU (3) KAVU, ZAMA KWENYE IBADA LIKE NEVER BEFORE.
2. AMINI KATIKA MAANDIKO MUDA AMBAO HAYA AMINIKI.
Sio rahisi,Kama nilivyosema kama hujapitia utamu wa mapito sio rahisi kuelewa, lakini nakwambia from experience SIO RAHISI LAKINI INAWEZEKANA NA INATAKA TU UWE NA ROHO NGUMU NA KUJIZIMA DATA!
Habakkuk 3:17-19
Even if the fig tree does not bloom and the vines have no grapes, even if the Olive tree fails to produce and the fields yield no food, even if the sheep pen is empty and the stals have no cattle- even then, I will be happy with the LORD.I will truly find joy in God,who saves me. The LORD Almighty is my strength. He makes my feet like those of a deer. He makes me walk on the mountains.
AMINI KATIKA MAANDIKO HATA KAMA HAKUNA SABABU ZA MSINGI ZA WEWE KUAMINI NA HIYO NDO IMANI YA KWELI, UKIAMINI SABABU UNAONA SIO MKOMAVU WA IMANI!
Mtu mwenye miaka 45 na hana Watoto na Hana mchumba na akasema NAMUAMINI MUNGU KWA HABARI YA MUME, HII SASA NDO IMANI YA KWELI.
JOHN 20:29
Jesus said unto him,”Thomas,because thou hast seen Me, thou hast believed. Blessed are they that have not seen and yet have believed.”
JIKAZE KI-KIKE,PAMBANAA! KOMAA NA MAANDIKO KWAMBA MUNGU UMEAHIDI USHINDI KATIKA KRISTO KWA KWA SISI TULIO OKAKA, UKO WAPI? NA UTAKUJA LINI?, MUDA HUO SHETANI UMEMUWEKA PENDING, HUMSIKILIZI WALA HUBISHANI NAYE, WALA HUANGAIKINAE!, USHAFANYA MAAMUZI MAGUMU YA KUKOMAA HUKU KUDAI-USHINDI WAKO!, KOMAA KWELI-KWELI MPAKA WAKUCHOKE! MWAKA MZIMA NON-STOP!
SHIDA YENU MTU ANADAI USHINDI WA MAPITO SIKU (5) NA SIKU YA SITA (6) ANABREAK DOWN NA KURUDIA UPYA KUEPELEKEWA MOTO, SIKU YA KUMI (10) ANAONA HATA HAPA NAJIKOSEA MWNEYEWE MUNGU BADO ANAWEZA, ANARUDI HUKU KUDAI USHINDI, UBABAIFU MTUPU, MIMI MTU WA HIVI SIMUONGOZI MAANA NAJUA SHETANI ATA NIDHALILISHA KUPITIA YEYE.
3. USIPOTEZE TUMAINI LAKO KWA MUNGU!
Mzungu anakwmabia WHEN HOPE IS LOST ALL IS LOST, HOPE IS THE LAST THING TO LOSE! TUMAINI NI KITU CHA MWISHO KABISA MTU ANAPOTEZA.
Hebrews 11:1
Now faith is confidence in what we hope for and assurance about what we do not see.
Romans 5:3-4
Not only so,but we also glory in our sufferings, because we know that suffering produces perseverance; perseverance, character; and character, hope.
Romans 12:12
Rejoice in hope, be patient in tribulation, be constant in prayer.
Romans 8:24-25
For in this hope we were saved. Now hope that is seen is not hope. For who hopes for what he sees? But if we hope for what we do not see, We wait for it with patience.
MUNGU WAKO UNAYEMTUMIKIA ANAKWAMBIA BADO HAJASHINDWA KUKUVUSHA KWENYE HAYO MAPITO NA BADO HAJAMALIZANA NA WEWE.
Zaburi 18:6
Katika taabu yangu nilimwita Mwenyezi-Mungu, Nili mlilia Mungu wangu anisaidie. Alisikia sauti yangu hekaluni mwake; kilio changu kilimfikia masikioni mwake.
lsaya 61:1-3
Bwana Mwenyezi-Mungu amenijaza roho yake, Maana Mwenyezi-Mungu ameniweka wakfu, akanituma niwaletee wanaokandamizwa habari njema, niwatibu waliovunjika moyo, niwatangazie mateka kwamba watapata uhuru, na wafungwa kwamba watafunguliwa. Amenituma niutangaze mwaka wake wa neema, na siku ya Mungu wetu ya kulipiza kisasi; niwafariji wote wanaoomboleza; niwape wale wanaoomboleza katika Siyoni ni taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya moyo mzito. Nao wataitwa mialoni madhubuti, aliyopanda Mwenyezi-Mungu kuonesha utukufu wake.