Reference: Luka 4
Watu wengi sana wana wonder mbona nikisali ndo majaribu yanazidi! Wanaacha kusali! Wakati ni jambo limeandikwa kabisaaa. Ndo hiyo unaijaribu kupeleka dini vipande vipande.
Baada ya kubatizwa na kushukiwa na Roho Mtakatifu (ambapo tulicovers Chapter 3), Chapter 4 inaanza na Yesu akiwa amejazwa Roho Mtakatifu. (Kama una dandiaga maandiko direct Chapter 4 utaona Yesu akiwa amejazwa Roho Mtakatifu ila hutajua alijazwa vipi)
Yesu alitoka Yordani alipobatizwa akiwa amejazwa Roho Mtakatifu, akaongozwa nyikani siku 40! Hakukurupuka kuanza huduma on the spot! Alienda kwanza nyikani kujipangaaa!
Wewe hufungi hata tatuu tu kavuu afu unamvaa boss wako kichwa kichwa!
Shwaaaaaa! Lazima uliwe kichwa shoga angu!
Yesu anafunga siku 40 kavuuu! No water, no food! Max ya wanaume kuishi bila maji na chakula ni 4 days, kwa vibonge maybe 7! Wanawake kwa mbinde sanaaa 10!
Yesu alipoga 40!
Ile anatoka nyikani, kama ni upakooo tunasema wa motooo motooo, wa kwanza kukutana naye mwamba huyuu hapa – Shetani akiwa amejizatiti!
Yesu na Shetani wanajuana mbinguni wakiwa roho wote kabla Shetani by then akiwa Lucifer, anaongoza safu ya kusifu mbinguni – hajafanya jaribio lake la kupindua mbingu.
Lakini kwa duniani hii, ni mara yao ya kwanza kukutana uso kwa uso na kufanya duet!
Shetani ana balls!
Anajua kabisa mwamba katoka juu ila he couldn’t resist to tempt Him. He had to take his chances.
Imagine trying the Son of God! He took 3 shots at God incarnate.
That was bold! Just bold.
His timing is never whack! Always perfect!
He timed Jesus at His weakest! When the flesh was flesh-ing!
Ubinadamu ndo unampelekaaa na njaa haswaaa.
Na jaribio la kwanza anamjaribu na mkateeee! @@@! Taking advantage of His hunger.
Hata wewe, at your weakest is when the devil shows up!
Umefika miaka 40, you are desperate – menopause inakujiaaaa!
Anakupa mume mleviii na malaya mbwa!
When you are at your weakest, he strikes.
Kumkataaa ni gizaaa nene.
Ndo utaelewa wazo la kugeuza jiwe liwe mkate halikuwa wazo bava kivile la kutishaaa.
Huna kazi miaka 8! Mtu anakwambia ofisini kwetu kuna kazi ya ukarani ya Form 6 leaver – na wewe una Masters yako. Ukiangalia mke anakaribia kukukimbia. Kila mahali umekopaaa.
Unaona familillah inakuja kufanyaaa!
He just screws your mindset.
Watu uliotakiwa wewe uwaongoze – wanakuongoza wewe.
Kudadadeki zako.
Unakuta kitoto Gen Z without qualification kinakufokea kama kimekuzaaa.
Na wewe kama kubwa jinga unakaa pale – dawa ina kuingiaaa mtu mzima!
At your weakest the fool strikes.
Koo’i imeishaaa, mwenye nyumba anakutoa, analeta mbaba anataka papuchi akulipie koo’i!
We know sis, if it was any other time you would have stood your ground! We know!
It is not that kwamba Yesu asingweza kugeuza lile jiwe liwe mkate at His own preference – angewezaaa!
Hata kuligeuza cake kabisa or any other delicacy!
Na dhambi isingekuwa kugeuza kitu kuwa chakula – dhambi ingekuwa kutii matakwa ya Shetani.
Ku-partner na Shetani kufanya kile anachotaka – regardless kwamba muda huo unakihitaji!
Kulipiwa koo’i na mbaba sio dhambi!
Dhambi ni ku-sex, kuzini, regardless ulipate koo’i au la!
As God incarnate, how can Jesus take orders or advice from the devil?
JARIBU LA PILI
Shetani ana offer milki ya dunia hii!
Shetani ndo prince of this world kweli, and he owns all the riches and luxury!
Hata mbeleni Yesu ana-acknowledge hio title yake (Yohana 12:31)
Sasa anapompa Yesu nafasi hiyo – ni kwamba Yesu aachane na mbingu, amiwachie dunia hii aitawale atakavyo.
Na kampeleka kileleni – acheki mzigooo kwanzaa!
“Authaminisheee ulivyo wa motooo!”
Mali ya uhakikaaa!
Chance of a lifetime.
Vote haya ndani ya dakika moja!
Hakutaka kumpa muda wa kutafakarii.
Ile dili la chapchap – umooo au haumoo!
Kuku pumbaza akili.
“We nisujudie tu – nakupa kila kitu. Si unajua kama mzigo ni wa kwangu kihalalii? Na ipo kwenye nafasi yangu kumpa nipendaee?”!!!
Jaribu hili kwenye maisha yetu ni DAILY!
And sadly, the devil doesn’t even try hard.
Wewe kumuacha Mungu sababu ya hela ya kula tuuu, sio shida zako.
Sponsor tu linakupiga mechi kwa laki!!!
Kilo inakutoa utu wotee!
Yesu alipewa milki nzimaaa, akakazaaa kumuacha Mungu!
Wewe laki tu – miguu wwaaaahhh!
Na gono juu!
Bora laki kubwa – sometimes mtu anakupa maneno tu matupuuu.
“Nitakuoa.”
Duka la mzungu kwake linakuwa wazi mdaaa woteee.
Anakugonga anavyotaka, mwisho wa yote anakutukanaa.
Mradi wewe unalipwa vizuri kwenye deal lenye jasho la watu ambao hawajalipwa – una chuna kimyaa!
Kila mtu ashi nde mechi zakeee!
Au siooo?
Ukiiona haki haitendeki, upo radhi kumsujudia Shetani anaye zima haki za watu ili uendelee kunyonya titi la Shetani.
Mungu atajiongeza mwenyewe.
JARIBU LA 3
Yesu anaambiwa ajirushe toka juu maana imeandikwa – Malaika watakulinda.
Shetani anajua maandiko kindakindaki – afu unajaribu kupambana nae na maandiko ya beep beep!
Lazima kikurambeee!
Shetani anafanya gaslight Yesu apime uhusiano wake na Baba yake.
Yesu anakataa!
This is what he always does to us.
Gaslighting is his nature!
Mda wotee – anakutia ndimu umjaribuu Mungu na kumpima imani.
Mtu unajijua huna uhusiano na Mungu – you’re not even trying!
Ata ku-gaslight ufanye maombi ya kazi juu, na ku-apply sehemu kama TRA ambapo anajua kabisa sio kwa uhusiano huo wa uzi ulionao na Mungu hutoboi!
“Jirushe, Malaika watakudakaaa” – wewe tena unarukaaa umefumba macho!
191! Lazima utue na makaliooo na uvunjike mgongo!
Then he has the last laugh!
Anakwambia, “wewe nenda kwa baby tu mfirimbanee weee kama kesho kwa Mungu hamnaaa.”
Mototooo ujipoze na maumivuuu! @!
You being you unasusaaa ibada na unaona Mungu kakukoseaaa.
MIMI
Watu wanakuja kila siku – wananijaribu kwa laki 1 mpaka milioni.
Mtu mpagani kabisaaa ka-apply kazi, anataka nimpe andiko la kufanikisha apate kazi arudi kuwa mpagani na kutumikia miungu mingine.
Kiukweli – laki laki zina nitolea udendaaa hatarii!
Kuna muda rejesho lipo kooni na laki inapita mbele zangu – lakini andiko sitoiiii kwa wapagani.
Bora nilipwe faid.
Hakuna kiasi cha pesa kinachotosha mimi kumjaribu Mungu. Hakunaaaa!
Na isitoshe, sio tu kumjaribu Mungu – najua nitakupa false hopes na false doctrine. Itaishi akili mwako.
You will never learn from your mistakes and ignorance.
LAKINI…
Ukikosa hiyo kazi, akili zitakukaaa sawa – na maybe utataka kujua kwanini Mungu hajakusaidia?
Hapo sasa mimi ndo naingia – kukusaidia kuweka misingi imara na thabiti, kuhakikisha unajenga uhusiano na Mungu na mbingu solid ambao utalast you a lifetime.
WATU WENGI
Ninawakuta na mahusiano yaliyoojengwa kwa misingi ya zinaa, upagani, cheatings, havana hata harufu ya Ufalme wa Mungu – alafu mtu anataka niyabariki na kuyasimamisha mbele za Mungu yafikie ndoa takatifu.
“Mama tuyaombee haya mahusiano.” ®!
The fact kwamba hayataenda popote kila mtu anajuaaa!
You know it! I know it! God knows it! And the devil knows it!
Ni suala la muda tu!
Lakini you wanting to bring God in the middle of your hell is diabolical!
Child!! Who do you take your God for?
Alafu muda ukifika ukaachwa – unamlaani Mungu na kusema “You prayed for the relationship.”
Which relationship??
The same one you graced with lots and lots of fornication!!?
The same one you left God out and partnered with the devil?
We know the devil gaslighted you to fornicate akikuahidi kwamba atakupa huyo mwanaume awe mumeo – and you fell for it!
Mpeee tu hilo papitooo – si atakuoa!!!?
Thubutuuuu!
FINALLY…
How far you’ll go and how much you’ll achieve in life is determined by how many tests from the devil you pass.
Yesu ndo kwanza katoka nyikani – hajatumia upakooo hata robooo, Shetani akamdaka juu juu kumjaribuuu!
Kama Yesu angejaa kwenye 18 za Shetani, biashara ya wokovu ingeishia pale pale – dakika za mwanzo kabisaaa!
Wengi mnapiga ibada kwa nguvu mwanzoni, Mungu anakuwa anapanga kufanya makubwa na nyie – ila Shetani akiwajaribuuu kidogo mna jaaaa!
Mtu anafanya program ya mtu sahihi kufungua mahusiano – wakija watu wa mwanzooo wanamtia mimbaaa!
Inakuwa mahusiano kufunguka kama mkosi – tena sio baraka tena.
Mtu anapata kazi kwa maombi – akifika anakuta wenzie wana iba… ana jichanganya na veve kuibaaa.
Mda si mda anakwambia, “Mama, ile kazi ilishaaa…”
Kivipi? Hasemiii.
MWISHO
Mungu anaweza kukupa kitu – ila muda gani utadumu nacho utaamuliwa na tests ngapi utafauru.
Mungu anakupa kazi – Shetani anakughasslight usilipe zaka.
Kazi inakosa baraka za Mungu na kugeuka jela huru.
Mwisho unafukuzwa.
Kila mtu atajaribiwa kwenye kila kitu.
Revelation 2:10
“Fear none of those things which thou shalt suffer: behold, the devil shall cast some of you into prison, that ye may be tried; and ye shall have tribulation ten days: be thou faithful unto death, and I will give thee a crown of life.”