Biblia imeweza kuonesha mifano mbalimbali kuhusu hatua za kinabii na namna zinavyoponya na kutatua changamoto mbalimbali za watu, Katika andiko hili tutaweza kufatilia na kuona namna ufataji wa hatua za kinabii unavyoponya na aidha kuona namna viwango vya imani vinavyochangia katika upatikanaji wa majibu na utatuzi wa vifungo ,laana na vikwazo katika maisha yetu ya kila siku.
Kupokea uponyaji kwa njia ya kufata unabii ( Phrophetic Move ):
Yesu anawaponya Wakoma Kumi (Luka 17:11-14)
11 Kisha ikawa, alipokuwa akielekea Yerusalemu, aliipitia katikati ya Samaria na Galilaya. 12 Naye alipokuwa anaingia katika kijiji kimoja, kulikutana naye watu kumi wenye ukoma, waliosimama mbali. 13 Wakainua sauti zao, wakisema, “Yesu, Bwana, utuhurumie!” 14 Alipowaona, aliwaambia, “Enendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” Ikawa, walipokuwa wakienda, wakatakasika.
Katika hadithi hii uponyaji wa wakoma hawa kumi (10) instant! , Yesu alitaka wainue imani yao ndio wapate kupona! Hakushindwa kusema Ukoma Upotee na Ukapotea bali aliwafanyajia uponyaji wa kinabiii! Sawa sawa na Sheria ya Musa (Kumbu kumbu la Torati 24:8) “Angalia katika pigo la ukoma, utunze kwa bidii, kwa kufanya mfano wa yote watakayowafundisha makuhani Walawi; tunzeni kwa kuyafanya vile vile kama nilivyowaamuru wao.
Yesu anamponya mtu mwenye ukoma (Mathayo 8 :4 )
“Naye Yesu akamwambia, Angalia usimwambie mtu awaye yote; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe sadaka iyo aliyoiagiza Musa, kuwa ushuhuda kwao.”
Hapa, tunasoma kuhusu tukio ambapo Yesu amemponya mtu mwenye ukoma na anamwagiza asimwambie mtu yeyote ila aende kwa kuhani na kufuata maagizo ya Torati kwa ajili ya sadaka ya kuthibitisha uponyaji wake. Hii inaonyesha jinsi Yesu alivyoheshimu na kutii sheria za Agano la Kale, na pia inaonyesha umuhimu wa kuwa na ushuhuda wa kihalali katika jamii ya wakati huo.
Kupokea Uponyaji kwa njia ya imani kuu (Instantly):
Yesu anampoya mtu mwingine mwenye Ukoma (Luka 5 : 13)
“Naye akamnyoshea mkono wake, akamgusa, akisema, Nataka; takasika. Mara ule ukoma ukamwacha.”
Hapa, tunashuhudia Yesu akimponya mtu mwenye ukoma INSTANTLY (Hapo kwa papo). Mtu huyu alimkaribia Yesu akiomba uponyaji, na Yesu, kwa huruma yake, akamnyooshea mkono na kumgusa. Mara tu Yesu alipomgusa, ukoma ulimwacha, na hivyo kumponya kutoka kwa ugonjwa wake. Katika uponyaji huu hatuoni Yesu akimtak mtu huyu aende kujionesha kwa Makuhani ili kutakasika bali alimponya INSTANTLY yaani papo kwa papo na hii ni kutokani na kiwango kikubwa cha imani ya mtu huyu mwenye ukoma juu ya uponyaji wa yesu.
Hitimisho
Katika uponyaji huu wa Yesu kuna baadhi ya wakoma waliponywa INSTANTLY! (Papo kwa Papo) na Baadhi waliponywa kwa kwa njia ya kufata Torati ya Mussa kwa sababu KATIKA KUTIII IMANI YAO INGEPANDAAA JUU, NA KWA KUPANDA JUU IMANI YAO WANGEPOKEA UPONYAJI WAO!
Mpendwa kwa kwenda kujaribu nguo ya Harusi, na kuplan harusi IMANI YAKO KATIKA HIO CHANGAMOTO INAKUWA LEVEL ZA JUUU KABISA! na kupokea uponyaji ni rahisiiii Sana! aidha ukiachilia declaration katika level hio imani inakuwa vizuri kabisa! Inapita bila kupingwa! Hatua zako za kwenda dukani ndizo zinazo fungua uponyaji wako katika hio changamoto!
Kuna muda upinzani unakuwa mkaliii sanaaa! Mimina chumvi ya Elishaaa kwa chochote kinacho kuzuia. Iwe uchungu, self pity, nguvu za giza, Muite Bwana wa vita apige hizo dagon. Mpaka ujaribu Hilo gauni na ukamilishe ibada ya Kuplan harusi yako.
Mpendwa muda mwingine penda kuutia ulimwengu wa giza katika wakati mgumu kidogo. ni kweli wamekufunga lakini unawapa moto Siku 5 non stop! na ya 6 unavaaa SHELA mbele yao. Walilojiapiza hutavaaa mpaka kiama!
LAZIMA WASUJUDU NA WATAMBUE KWAMBA IMEKWISHA IMANI YAKO IPO LEVEL ZINGINE NA MUNGU WA ISRAEL UNAEMTUMIKIA SASA HIVI HASHINDWI KAMWE. WAKIJARIBU KUKUGUSA WATARUDISHWA KUZIMU NA KUSALIMISHA SILAHA ZAO CHINI.
LAZIMA UJUE JINSI YA KUPOKEA USHINDI MPENDWA.