“For to be carnally minded is death; but to be spiritually minded is life and peace.”
— Warumi 8:6
SEHEMU YA KWANZA: TATIZO LA UKRISTO WA MCHONGO – IDENTITY CRISIS
Kuna watu wengi sana wanaojiita Wakristo, wamebatizwa, wamepokea Ekaristi, wanaenda kanisani kila Jumapili lakini bado ni wapagani kabisa kwa matendo yao. Hii inatokana na tatizo kubwa la utambulisho wa kiroho (identity crisis). Hawajui ni nani ndani ya imani yao – hawaelewi nafasi yao mbele za Mungu, hawajui wamesimama wapi. Wapo kanisani kimwili lakini rohoni wapo mbali sana na Mungu.
“Mimi ni Mkristo” sio kauli nyepesi – ni tamko la uzito mkubwa. Linahitaji uelewa, imani, na matendo yanayothibitisha huo Ukristo. Vinginevyo, ni mchongo tu!
SEHEMU YA PILI: AINA ZA WATU KATIKA IMANI
-
Believers (Waamini): Wamepokea Injili, wanamwamini Kristo kama Bwana na Mwokozi, wanatenda imani yao kila siku.
-
Non-Believers (Wasiomwamini): Wameisikia Injili lakini hawajaitii, hawamwamini Yesu wala hawana mpango wa kuokoka.
-
Pagans (Wapagani): Wanaabudu miungu mingine au wana changanya Mungu wa kweli na miungu mingine (hii ni kinyume na Amri ya Kwanza).
Tatizo ni kwamba watu wengi wanaishi kati ya hizi tabaka zote – hawajui kama wao ni waumini kweli au ni wafuasi wa dini kwa jina tu. Hii inawafanya washindwe kuona matokeo ya kiroho kwenye maisha yao.
SEHEMU YA TATU: MAARIFA NDIO UFAFANUZI WA UTAMBULISHO WAKO
Huwezi kusema unamfuata Kristo halafu hujawahi hata kusoma Injili hata moja! Ufuasi wa kweli wa Kristo unaanza kwa kumjua Kristo kupitia maandiko.
Kwa kuanzia, soma Injili ya Marko – ni fupi na inakwenda moja kwa moja kwenye mambo ya msingi:
-
Yesu abatizwa
-
Yesu anaponywa watu
-
Yesu anahubiri
-
Yesu anapokea ushuhuda kutoka mbinguni (“Wewe ni Mwanangu mpendwa, nimependezwa nawe” – Marko 1:11)
Ukishaelewa Injili ya Marko, utaanza kujenga msingi wa kuwa believer halisi.
“You can’t follow someone you don’t know – and you can’t command spiritual results with spiritual ignorance.”
SEHEMU YA NNE: UKISTESHA MZINGA USITEGEMEE ASALI
Ukristu wa kweli unataka kazi, maarifa, na roho iliyo hai. Si wa kubahatisha, si wa kuomba kazi siku moja kisha kesho unaacha. Ni lazima ujifunge na Neno, ujifunze tabia ya Yesu, na ujue mamlaka yako kama muumini. Hapo ndipo unaweza kusema:
“Yes, I am a believer, and I know what I stand for!”
Ukisoma Injili na ukaamini kwa kweli, utaanza kuona mafanikio hata katika mambo ya kawaida:
-
Kama Mungu alimpa Bikira mimba bila mwanaume (Mathayo 1),
-
Je, ni nini kinamzuia Mungu akupatie kazi, ndoa, au muujiza wako?
“Do not be afraid… the child is conceived by the Holy Spirit.”
(Mathayo 1:20)
Hilo andiko linaweza kuwa silaha yako ya kiroho ya kila siku. Ukiliamini, roho ile ile ya Mungu iliyomjalia Mariamu inaweza kukuweka kazini, kukupa mume/mke, au kukuweka huru kutoka vifungo vya kiroho.
SEHEMU YA TANO: KAMA SI BELIEVER – HUTAVUKA!
Ukienda kwa mtumishi na kusema, “mimi siamini,” au “sijawahi kusali,” hutapata msaada wowote! Lakini ukiamua kuokoka na kuwa muumini mpya (new believer), unafungua mlango wa msaada, rehema, na muujiza.
Lazima ujue sheria ya kiroho:
“Failure to know the law is not a defense in court.”
Usiende kwenye maombi au vita ya kiroho bila kujua nafasi yako. Ujinga wa kiroho ni kama kupigana na simba ukiwa mtupu!
SEHEMU YA SITA: MAISHA YA MUUMINI WA KWELI NI KUJIFUNZA, KUSOMA NA KUELEWA
Mwalimu kama Mwakasege ana miaka 30 akihubiri bado anasoma Injili kila siku. Na wewe unasema unahitaji kazi au ndoa lakini hujawahi hata kupitia Injili ya Mathayo? Kazi haitoki kwa drama, inatoka kwa maarifa na uaminifu kwa Mungu.
Soma Neno. Tafakari Neno. Omba kwa Neno.
“Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.”
(Yohana 8:32)
HITIMISHO:
JITAMBUE – UKIJITAMBUA, UMEFUNGUA MILANGO YA MBINGU.
Wewe ni nani katika imani yako?
Unasimamia nini?
Je, unaelewa mamlaka yako ya kiroho?
Je, umemjua Yesu au unatumia jina lake tu?
Kama hujui jibu la maswali haya, anza leo kusoma Injili. Jua Neno. Kubali kuwa muumini wa kweli. Na utashangaa ni kwa namna gani baraka, mabadiliko, na ushindi vinakuja kwa kasi kwenye maisha yako.
Mungu ni Mungu wa walio na msimamo – sio wa wavuguvugu.
📖 Yeremia 1:12
“Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize.”