Mathayo 16:24-25
Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake,”Mtu yeyote akitaka kuwa-mfuasi wangu, lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. Maana, Mtu anayetaka kuyaokoa maisha yake mwenyewe atayapoteza, lakini mtu anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayapata.
This day the level of jesus honest wa brutal, He said what he said and he was too correct!. In other words alichosema ni kwamba no one will carry your cross for you! Absolutely no one, Sasa wengi your delusional kwamba kuna mtu atakubebea huo msalaba na kufanya hizo extra-miles for you! Wake up sweety.
Jesus was crystal clear beba msalaba wako nyonga hatua hizo teke-teke kumfata not the other way round, Kwamba chillax mwanangu, Nakuja kuku-sort alijua misalaba ipo ndiyo akatoa solution kuwa issue sio huo msalaba, watu wana misalaba mikubwa zaidi ya hiyo na wamemfata Yesu na mambo yameenda, Wewe husikiii aibu like watu wanashuhudia mambo makubwa ya kutishaa, Misalaba waliyo-kokota sio mchezo alafu wewe una kimsalaba kidogo na umeshindwa ku deal nacho?. Issue siyo ukubwa wa msalaba bali unyenyekevu na willingness ya kudeal nao huo msalaba accordingly!
Mimi katika shukrani nyingi za ndoa nilizo kula niza single mother, Watu ambao odds zao ni ngumu balaa, watu wana watoto 2 wadogo au 1 mkubwa wa umri mpaka wanaume wanawaza kama mwanao ana 15 utazaa tena kweli?, Hio yako likizo ya labor au kustaafu labor?, Na kids make you look older even if you are not, Let’s say ulizaa mapema Ukisema una mtoto wa miaka 13 ni sawa useme tu una-late 30s au early 40s. Sasa kwa sisi wa magomeni watu wanzaa sana 17-21 siyo kuwa 30 na mtoto wa 13 kawaida sanaa ila ukija mikocheni wanaona unajidogosha tu lakini katika huduma yangu nimeona watu wengi walio na odds ngumu ndo wana fanikiwa kwasababu wapo serious, odds zinawatetemesha utumbo mpaka wao wenyewe.
Mtu aliye kutana na betryal na deceit ya mwanaume alie-mzalia hawezi kuweka mapozi kwenye maombi anamjua shetani vizuri sana asha mkobeka mkuki wa moyo, ata sali kama hamna kesho, Atajitwika msalaba na kukimbia kwa Yesu na Nina mabinti wazuri wana odds nzuri mnoo lakini hawa-oleki simply because they are full of bullshit na upuuzi mwingi yaani Mabinti wana kazi nzuri, clean slate, no kids, no divorce, low body count, wengine no-aborti ons, In their prime 30s, Lakini hawaoleki, Niko nao mwaka wa 3 huu.
Unaweza jiuliza why? And I will tell you why, Shida sio msalaba shida ni una deal nao vipi?, Odds na kila kitu viko upande wao lakini ufahamu, Utii na Unyenyekevu viko kwa single mothers, Men see it, God see it, I see it. Wao misalaba ni midogo lakini nia ya kuvuka hakunaaa, Badala ya kubeba msalaba mtu ana anajilaza pembeni ya msalaba na kufanya drama. Wenzao misalaba mikubwa lakini wabishi wamjipata, Mtu akishindwa kujitwika ana ukokota hivyo hivyo mpaka kieleweke. Sasa jJesus was very direct, Kana nafsi yako jitwike msalaba wako nifate sanan unakuta Mtu kukana nafsi yake hataki, Ni kujiendekezaaa tu, Mpaka unajiuliza when do these whims end? Like is there an age limit or something?
Niko nao 34 and above, Utahisi sababu wako age hio wamejipata! Thubutuuu! Picha linaanza mwanzo walikuwa 200 na wali register kwa nida kabisaa, 100 hakutoa sadaka ya ukombozi, Na hio sadaka ilikuwa kama base ya program nzima, Hapo wana bakia 100, katika hawa 100 kuna ambao walitoa sadaka lakini program hakufanya, Alisema yupo busy na kazi atafanya atafanya bora atangulize sadaka mpaka kesho hio imetoka.Kadri tunavyoenda program zinaendelea mtu hafanyi, Na yupo serious visaya mno kuuliza mbona hapati matokeo, Ni mtu mzima huyo wa makamo unabakia mtazamaji, Hao 70 waliofanya wamepata matokeo, Ni expectated sababu walikomaa sasa kuya shikilia basi yakomae.
Kitu kidogo mtu ana vunja mahusiano! Ana kwambia mimi nishazoea kuanza upya, Siwezi kubembeleza Hapo ana 39 na haimstui, Yani kikitokea hata ki-upepo kwenye hayo mahusiano ananza ku -question kama yametoka kwa mungu kwellll? Na huyo mtu ndieee au aendelee kusubiri, Kuna drama kule nyie. Kuna mda unajiuliza wanataka kuolewa kweli hawaaa au wanataka tu kunivuruga kichwa, Basi tu wamekuta na roho ngumu kweli kweli sikati tamaa. Kwa ku left sasa, Mmoja akaniuliza Mama mbona una waacha wa left? Nikamwmabia hawapo tayari, waache waende. Moyoni nasema mtu ustahimilivu wa group tu umemshinda ndo ataweza kumstahimilia mama mkwe na gubu lake? Ataliweza gubu la mume na ukweni? Unakosewa wewe unaomba msamaha wewe,Hawezi.
Kiukweli mimi wanaoleft naona ni nafuuu kuliko mtu ambae hasali, haamini na anataka matokeo anakusumbua balaaa,jamani huu si ugaidi?, All in all my focus siku zote ni kwa wale wabishi wa ku-defy odds! Wale wakukomaaa mpaka mwisho wale wa ku-yield matokeo halisi. Hawa ndiyo na focus nao kuangalia nini walipatia na kipi cha ziada walichofanya na walipataje matokeo! Ili kuboresha teaching techniques.
Wapendwa katika Jamii siku zote mtu anayefeli sio shida zetu wala concern yetu kabisa, Ni another one tu, katika ma elfu ya waliofeli, Anaye-faulu ndiyo jamii haswa ina mstudy na kunsikiliza na kumpa ukumbi wa kueleza amefani kiwaje?, Wapendwa Mtu yoyote anaweza kushinda au kushindwa ni vile tu yeye mwenyewe atakacho-amua,If you decide to eat up this open doors program you will ace it like no can comprehend, Utafyatua hayo malango kwa fatumaaa, Na utashuhudia miezi yote iliyobakia wewe tu, Mpaka tutaomba utupumzishe.
Mpendwa Ukiamua ku-play the fools card ndiyo hivo tena,Utafanya upuuzi upuuzioctober urudi mama nimerudi tenaaaa nipokee mwanao, Mwaka wa 3 huuu una-yoyoma!
Mpaka leo hii kuna watu wana odds mbaya balaa kuliko wewe, Lakini wameji-pangaa, Malango yatafunguli wa na jiwe fatuma, Wamechoka kuwa losers na usipokuwa makini watashuhudia mbele yako wewe mwenye odds nzuri na msimu wako ukikomaaa wana tambaaa hatarlll kwa miamala.
Sasa sikia mimi I really want you to win! God knows I do! Ndiyo maana usiku mnene huu naandika waraka wa kuku inspire kweli jamani, Nikupende vipi?. Inorder to win lazima ufanye maamuzi ya kuwa winner, Ugome kujifelishaaa! Bring your a game na competition spirit, Kana nafsi yako, Jitwikeee msalaba wako, Twende kazi, We will eat this up in no time.
Kama nilivyo sema mabinti wazuri,clean slate, prime age, solid jobs but Mnashindwaje kuoleka?, How on earth? Who wouldn’t want to marry you?, It’s a shame mambo kuishia yalivo mpaka watu wanaokujia wanaumiaaa inawezekana vipi?, Haitaishia hivyo maana utaikana nafsi yako na kujitwika msalaba wako kwa Yesu kufungua hilo lango na utangangania mpaka lifunguke! You wont let you down.
Mpendwa niko hapa kuandika ushuhuda wako kama shujaaa wa 2024!, you defeated your history, your odds, your ancestors and the devil himself, A true child of God!, Ikumbukwe only winners get to tell their story, you will win ukidhamiria na story yako tutaisikiliza tu taka tusitake, Sentensi kwa sentensi. Mpendwa there is no honor in losing and remember Jesus did not die on the cross for you to live as a side-chick!, Wenzio waweze wana nini na wewe ushindwe una kasoro gani? Wote mna 24hrs! Huwezi kushindwa!, Not this time. It is your time and even if its not make it your time !