Je, Uko tayari kwa Ndoa?

Wengi mpo tayari kwa Ndoa kiroho ila kimwili hampo tayari, yaani Kiroho mmevuka kitambo sanaa lakini Kimwili Bado Hamjajiandaa Kabisa. Mungu anangoja Muwe Tayari  Kimwili Pia.Aidha Kama Mambo yako yameshajibiwa Kiroho kuendelea kuomba mambo hayo hayo huweza kuleta ukimya.

Mungu yupo tayari anakungoja wewe umakinike kimwili ili aachie ushuhuda. Mambo haya yapo pia kwenye biblia fuatilia nami sasa:

Character / Tabia yako ya Ndani.

Kuna Tabia  (Character) kwenye biblia amabazo Mungu ameweka wazi wawe nazo Wake bora. Mpendwa unaweza Prayer Warrior ( Mwana Maombi  wa Ngazi ya Juu ) unapiga saba (7) kazu  ila character / tabia  ikakufelisha. Unaweza kuhisi una mapepo ila kumbe umewekeza kwenye Kiburi na kutoambiwa kitu.

Mpendwa shetani mara kwa mara hutumia silaha zilizomo ndani yako kufyeka mahusiano yako. Kwa kutumia Fyekeo lililopo ndani yako shetani huweza kukupa mitihani midogo kama majani kwani hufahamu huwezi kupinga, utafyeka kila kitu.

Mpendwa Tabia ya HESHIMA NA UTII zimetajwa sana katika Biblia na nipende kukusihi usizipuuze. Ndoa za Kikristo ni ni 1 life 1 wedding hivyo Mungu anajali sana na kufatilia kiundani juu ya hiyo ndoa unayoiomba! , anaikagua hiyo Happly Ever After kama una maanisha (uko serious nayo) akiona kama mambo hayako sawa hatoi kibali.

Ufahamu Mwenendo mzuri wa Mke.

1 Petro 3: 1- 6

Nanyi Wake, jiwekeni chini ya mamlaka ya wanaume wenu, na kama hawaamini katika neno la Mungu, wafanyeni wapate kuamini kwa kuuona Mwenendo wenu. Tazama kwa kufanya haya haitakuwa lazima kwenu kusema neno, kwani wataona jinsi mwenendo wenu ulivyo safi na wa kumcha Mungu, Ila yafanyeni yote kwa Moyo wa kweli.

Aidha katika kijipamba kwenu msitegemee mambo ya Nje, Kama vile mitindo ya kusuka nywele, Kujivalia vitu vya dhahabu na nguo maridadi. Bali, Uzuri wenu unapaswa kutokana na hali ya ndani ya utu wa kweli, uzuri usioharibika wa wema na utulivu wa roho, amabao ni wa thamani kubwa mbele ya Mungu. Na Hivyo ndivyo walivyojipamba hapo kale wanawake waadilifu waliomtumainia Mungu, wakajiweka chini ya mamlaka ya ya waume zao kwa mfano Sara alimtii Abrahamu na kumwita yeye bwana.

Pia msiweke nguvu kwenye Lace Wig na Nguo za Turkey, Weka nguvu kwenye utu wenu wa ndani, Mungu anakagua ndani. Ndio maana unaweza jiuliza kaniacha mimi kaona nini kwa yule mama lishe kumuoa? Hajui ata kuoga?, Ni utu wa ndani mpendwa.

Fahamu Sifa za Mke Mwema

Mithali 31-10 – 31

Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana thamani yake yapita thamani ya majirani. Moyo wa Mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato. Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake. Hutafuta sufu na kitani, hufanya kazi yake kwa moyo wote, anafanana na Merikebu za biashara, huleta chakula chake kutoka mbali, Tena huamka, kabla usiku haujaisha, hwapa watu wa nyumbani kwake chakula na wajakazi wake sehemu zao, huangalia shamba na akalinunua , kwa mapato  ya mikono yake hupanda mizabibu, hujifunga nguvu viunoni kama mshipi, hutia mikono yake nguvu, huona kama bidhaa yake inafaida, Taa yake haizimiki usiku, hutia mikono yake katika kusokota na mikono yake huishika pia, huwakunjulia maskini mikono yake, Naam huwanyoshea wahitaji mikono yake na Hawahofii theluji watu wa nyumbani kwake.

Wapendwa nimeikata na kuandika sifa hizi kwa ufupi naamini nimekupa muongozo, ili uweze kufatilia zaidi soma katika kitabu cha Mithali 31 :10 -31.

Aidha Wapendwa Mke kusimama kwenye uchumi wake ni nguzo muhimu sana ya ndoa, tangu zamani hizo, soma mwenyewe hapo. Uchumi wa kudanga danga ukingoja Mungu akufungulie mlango wa ndoa ni uongo. Msihi Mungu akufunulie macho uinuke vipi kiuchumi usiende kuwa mzigo na kuchokwa ukweni.

Amri ya Mungu kwa Mke.

Waefeso 5:33

” Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende Mkewe kama anavyoipenda nafsi yake mwenyewe, na Mke lazima amheshimu Mumewe

Mpendwa neno kuu ( key word ) hapo ni LAZIMA Mungu aliona mbali sana ndio maana akaweka baadhi ya mambo hiari na baadhi AMRI. Mungu anaweza akakuletea watu wa kutosha kwenye nia yako lakini wewe ukakosa maarifa ya kidogo ukaangamia. Katika maisha yetu ya kila siku utasikia ” Nilikuwa na Mtu mwanzo alikuwa na nia ya kunioa ghafla akabadilika”, Mpendwa sio ghafla kaona kuipata heshima ndani yako ni mapambano na akachoka kupambana. Mpendwa wanaume wameumbwa kupenda heshima na ni amri kutoka kwa Mungu wanawake / wake kuwaheshimu wanaume , hivyo msijaribu kupindua vitu mtapinduka wenyewe.

Utii wa Mke kwa Mumewe [Sehemu ya Kwanza]

Wakolosai 3: 18 – 25

“Enyi Wake, Watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo bwana” 

Mpendwa unaweza kuwa mzuri sana kwa sura na umbo, kama Malkia Ester lakini you’re so full of your self  katika maisha yetu tunasema Wewe ndio wewe sasa Pisi kali uambiwe nini ? Au Umebarikiwa uchumi yaani tha Boss Lady na ukawa una muomba Mungu Mume ila mpango wa kumtii hauna kabisa sana sana unlohitji la yule wa kukutii wewe Pisi kali au Boss Lady.

Mpendwa nipende kukuambia hizi hila zako hata ukizificha kwenye chmba ya moyo wako, Mungu anaona na ni ubatili mtupu. Nipende kukusihi uweze kutubu na kusafisha Moyo wako na katika Maombi yako kama mchumba unaye mwambie Mungu kuwa anajua ulipokosea , na kisha ahidi katika hiyo ndoa Mungu atakayokupa utazingatia haya. Mkumbushe mara kwa mara bila kuchoka kwamba uko tayari kwa ndoa hata katika haya ya mwilini.

Utii wa Mke kwa Mumewe [Sehemu ya Pili]

Waefeso 5 : 22-33

“Wake watiini wame zenu kama kumtii Bwana”. Maana mume anayo  mamlaka juu ya mkewe, kama vile kristo alivyo na amlaka juu ya kanisa, lakini naye Kristo huliomba kanisa vivyo hvyo, Wake wawatii waume zao katika mambo yote.

Aidha Mpendwa unaweza kuwa na mtu Mungu kakuletea kwa lengo zuri kabisa la wewe kupata mwenza. Ila wewe uko radhi umtii Bwana kwa nguvu zako zote na sio yule Mume wala Familia yake. Hujui hili andiko na wala hujawahi kulisikia na aidha hujali. Hakika unafanya ubatili mkubwa katika ubora wako kwa huyo mtu ila kwa Bwana unabaki mwaminifu mpaka mwisho  lakini mambo yakienda ndivyo sivyo unaanza kumuona Mungu sio mwaminifu kwako, Nipende kukusihi uwe makini , Leo nime kupa Password.

Mume ni kichwa cha Mkewe.

Wakorintho 11: 3- 17

Wapendwa napenda muelewe kuwa Kristo ni Kichwa cha kila Mwanamume, kama vile  Mume alivyo kichwa cha Mkewe, na Mungu ni kichwa cha Kristo.

Hizi ni kanuni ( Principles) zilizowekwa na Mungu kuongoza ndoa na familia. Na katika Biblia takatifu Mungu amerudia rudia sana kanuni hizi hivyo nawasishi tuweze kuzifuata. Na tujiulize mara kwa mara tunataka Ndoa au Harusi? na Je tupo pamoja na Mungu katika Miongozo na Kanuni hizi?  kama umekubali kuzifuata na kutii hakika jiandae kisaikolojia kusika nafasi ya Mke na huwezi kamwe kuwa Mke Nusu au Pisi Kali Nusu. Na kama hii ndiyo plan yako Mungu ni mwaminifu sana atajidhihirisha kwako. Aidha Mpendwa kama unataka NDOA elewa misingi ya NDOA kwenye biblia ni ipi , kubaliana nayo na Muahidi Mungu upo tayari kuishi kwa unyoofu ukifata miongozo yake yote hakika nakwambia Mume atatokea wakati na muda usiotegemea na huto amini kama jambo dogo hivi lina matokeo makubwa sana na utagundua kuwa ulijitayarisha kiroho lakini kuna sehemu bado hukuzifuatilia.

Unyenyekevu wa Mke kwa Mumewe.

1 Timotheo 2 : 11 -1 4

11 Mwanamke unapaswa kukaa kimya na kuwa mnyenyekevu wakati wa kujifunza. 12  Mimi simruhusu mwanamke amfundishe au amtawale mwamaume; Anapaswa kukaa kimya. 13 Maana Adamu aliumbwa kwanza, halafu Hawa. 14 Na wala si Adamu aliyedanganywa; bali mwanamke ndiye aliyedanganywa, akavunja sharia ya Mungu.

Wapendwa najua katika maisha yetu ya sasa Boss Ladies wengi, Wapambanaji na Pisi kali hii ni ngumu kukubali ( Ngumu Kumeza) nipende waambia kuwa kama misimamo yenu ni tofauti na maelekezo na miongozo ya Bblia kuelewana na Mungu kwenye jambo hili ni Ngumu.

Aidha nipende kuwasihi kama njia yako uliyotumia kwa muda haikupi majibu unayo yataka basi Tumia njia ya Mungu, Muombe Mungu akutie Nguvu mpya uweze kuishi katika hio nia yako na hakika Mungu anajua bila kutii haya maelekezo talaka hazikwepeki hivyo anaona bora akuache single lady kuliko uwe Mtalaka! kwani hauko tayari kupokea ukubwa wa Mume.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top