MTU MUNGU ANAYEMUITA SIO — ANAYEMPAKAAFUTA

📖 1 Samuel 13:14

But now thy kingdom shall not continue: the Lord hath sought him a man after his own heart, and the Lord hath commanded him to be captain over his people, because thou hast not kept that which the Lord commanded thee.

THE LORD SOUGHT FOR A MAN!!!!

📖 Psalm 89:20

I have found David my servant; with my sacred oil I have anointed him.

BUT THE LORD ANOINTED “DAVID HIS SERVANT” — and not “DAVID A MAN.”

Kwa hiyo, ili Daudi apakwe mafuta, ilibidi kwanza awe “MTUMISHI WA BWANA.”

🔥 ISSUE SIO KUITWA NA MUNGU

Issue sio kwamba una wito au huna!
Issue ni hii: Je, umeitikia kuwa His humble servant?
Kwa sababu usipoitika, He will never anoint you!

Wengi Mungu amewaita kwenye karama na callings mbali mbali — nzuri nzuri!
Ameita watu kuwa management material, wafanya biashara wakubwa, viongozi wa viwango!
Lakini shida ni kwamba mmekataa kuitika.
Ndiyo maana mafuta ya kufanya Mungu alichokuita hufanyi kazi!
Unapishana nayo mchana kweupe! 😩

👑 DAUDI ALIITWA KUWA MFALME…

Lakini tangu aitwe na Mungu hadi siku ya kutawazwa ilikuwa miaka 18 ya mishike mshike!
Miaka 18 ya kuishi mapangoni, kukimbia mkono mrefu wa Sauli — mkwewe mwenyewe!
Imagine — umeitwa kuwa mfalme, umeisha pakwa mafuta na nabii,
lakini unaishi porini kama nyoka! Una lala macho!
Na bado unaamini Mungu hakukosea.

Ukiwa wewe, ungefikiria, “Hapana, hapa kuna misunderstanding!”
Kuna mafaili yamechanganyika! 😂

💰 WITO WA BIASHARA

Mungu anakwambia:

“Nimekuita uwe mfanyabiashara mkubwa sana Tanzania.
Lipa zaka, finance kingdoms, acha mashaka!”

Lakini wewe…
Unajikung’uta visenti kanisani maskini! 😅
Hauoni biashara ikienda popote!
Baada ya miezi mitatu unasema: “Bwana eeh, wachungaji wezi tu.”
Umeharibu wito wako mwenyewe!

🏢 WITO WA UONGOZI

Mungu amekuita uwe CEO hapo kazini!
Picha linaanza, unakojolea kambi. 😂
Zaka hulipi, sadaka hutoi, hu-finance huduma yoyote,
halafu unataka mbingu zipiganie nafasi yako ya CEO?!
Kwa kipi hasa? Kwa utii gani? Kwa ibada gani?

Wakati mwenzako Daudi yupo pangoni anaandika Zaburi za kumsifu Mungu,
wewe upo godoroni Dodoma unasoma tu Zaburi kaziiii…
KWENDRAAAAA MWANA WA SAUL! 😆

⚡ MFANO HALISI

Kuna mwanafunzi wangu mmoja, destined to rule!
Nikamuambia:

“Kama vip, wewe utakuwa CEO hapo! Maana una support sana huduma.”

Akaanza uoga.
Akaona kama natengeneza propaganda.
Nikamuuliza:

“Unataka Mungu aseme mwenyewe? Uta-stahimili?”

Akanuna.
Nikamuambia:

“Sawa, wiki hii kaa mkao wa roho ngumu — usije ukazimia ofisini.”

Akaona kama mzaha.
Haijapita wiki!
Barua ya promotion ikaja —
Nafasi tatu juu ghaflaaaa! 😳

Akatetemeka! Akasema, “Kumbe haya mambo yapo kweli?”
Watu kazini wanamwogopa kama ukoma.
Wanahisi “chawa wa mama!”
Maana sio kawaida! 😅

Lakini haikuwa rahisi.
Haikuwa “walk in the park”!
Wala haikuwa “abracadabra — nimekusema, vyeo vikapanda.”

🔥 KILICHOMFANYA AINULIWE

Alikuwa anaweka ibada za kutosha.
Maandiko anacharaza kama kesho hakuna.
Zaka analipa.
Sadaka anateketeza kwa yatima, kwa huduma, kwa maskini.
Ni mtu wa Mungu kindakindaki — “Servant of God.” 🙌

⚠️ PROBLEM YA WENGI

Wengi mnamfanya Mungu servant wenu!
Hamfanyi ibada, hamlipi zaka, hamtolewi kwa huduma —
watumishi wanateseka, ninyi mnageuza macho pembeni.
Alafu mnataka Mungu aende above and beyond for you?!
THUBUTUUUU YAKO! 😤

🚨 MWISHO WA HABARI

Mungu hana bavu!
Ukitwa ukaleta za kuleta — anaita mwenzio na kumpa ufalme wako mchana kweupe!

KAZI IENDEEEEE!!! 🔥🔥🔥

🕊️ “For many are called, but few are chosen.” — Matthew 22:14

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top