HAKUNA MAOMBI YA MUME WALA YEYOTE YANAYOFANYA KAZI KWA MPAGANI

MPENDWA UMEFUNGA, UMEKESHA, UMESHUKA MILIMANI – NA HAKUNA JIBU? LABDA HUKU UNAKOITA “IMANI” NI UPAGANI ULIOVAA MAVAZI YA KIKRISTO!

Leo nakuletea andiko zito – la kushtua na kufungua macho – kwa wale wote waliokaa miaka mingi kwa “maombi” bila kuona matokeo. Wale wanaojiona kama Wakristo, lakini kimyakimya wanaishi maisha ya kidini bila misingi ya imani ya kweli.

Hebu tuliweke wazi…

HAKUNA MAOMBI, HATA YAKIWA YA MOTO KIASI GANI, YANAYOINGIA MBINGUNI KUTOKA KWA MPAGANI.

 

Ndiyo, umesikia vizuri. Mpagani unafunga, unakesha, unanyamazisha “mapepo” lakini Mungu hana ushirika na wewe – MUNGU HANA USHARIKA NA WAPAGANI, HAJAWAHI NA HATAWAHI!

LAKINI MIMI NI MKRISTO… AU NINAJIITA MKRISTO TU?

 

Kama hujui hata sababu ya kubatizwa, kama hujawahi kujifunza maana ya Ekaristi, kama unaandika “Nataka mume” kwenye kila karatasi ya maombi lakini hujawahi kupokea Sakramenti za msingi – wewe si Mkristo, wewe ni mpagani aliyevaa suti ya kidini.

MAOMBI HAYAJENGI IMANI – NI IMANI INAYOAMSHA MAOMBI YENYE NGUVU!

 

Wengi wanatafuta “deliverance” bila kutubu. Wanatafuta kazi bila kufahamu wa nani wao katika Kristo. Wanashika Biblia bila hata kujua vitabu vyake ni vingapi – hata Injili moja hujasoma lakini unataka kuvuka kiroho?

Je, unajua maana ya:

  • Ubatizo wa maji na Roho?

  • Sakramenti ya Toba na Maridhiano?

  • Sakramenti ya Ekaristi kama Agano la damu, si mkate tu?

  • Kipaimara kama kitambulisho chako kikuu kiimani?

  • Sakramenti ya Ndoa kama agano takatifu, si tu kupendelewa na Mungu kwa “mume mwema”?

MAANA YA UKRISTO WA KWELI SI KUHADHIRIA TU KANISA – NI KUJUA NA KUSHIKILIA IMANI YAKO KWA MSINGI SAHIHI

Unaweza kuwa na degree, lakini huna hata uelewa wa Neno la Mungu. Unamlaumu Mungu kwa kuchelewa kujibu, lakini ni wewe uliyekaa miaka mitatu hujasoma hata Injili ya Marko!

Unaomba “mume”, “ajira”, “visa”, lakini:

  • Hujawahi kutubu kwa dhati.

  • Hujui Agano jipya linamaanisha nini.

  • Hujawahi kutangaza ahadi za Mungu juu ya maisha yako kila siku.

  • Hujui wewe ni nani katika Kristo.

Hata Mungu alitamka: “Kuwe na mwanga!” – na mwanga ukawa. Wewe unataka mwanga pasipo tamko?

JUA KANUNI ZA MCHEZO KABLA YA KUCHEZA

Ukitaka maisha yako ya imani yabadilike:

  1. Tubu – toba ya kweli, sio hisia.

  2. Pokea Sakramenti zote kikamilifu.

  3. Soma Neno kila siku – tembea na ahadi za Mungu.

  4. Tambua nafasi yako katika Kristo – jua haki yako kisheria kiroho.

  5. Acha ubabaifu wa kiroho – tafuta mizizi ya kweli ya imani.

NA NDIYO MAANA WENGINE WAMEVUKA NA WEWE BADO UKO MAHALI PALEPALE TANGU 2022

 

Kwa sababu waliamua kukata upagani wao, wakajifunza imani, wakasoma Neno, wakatubu, wakajijua – wakabadilika. Wewe bado unazunguka kanisa kwa maombi ya “deliverance” ambayo si ya kiandiko.

USIANGALIE IDADI YA MAOMBI – ANZA KWA KUJIFUNZA UKWELI WA IMANI YAKO.

Kama unataka kutembea katika utukufu, si katika uvivu wa kiroho – ingia mchezoni kikamilifu. Usikariri tu maandiko; yaishi! Usitafute mume kabla ya kutafuta Mungu aliye Mtoa wa mume.

NATAMANI KILA MTU ASOME ANDIKO HILI!

Tuwe wakweli. Kama bado unaomba pasipo kuelewa, utazidi kuteseka. Lakini leo, anza safari ya kweli ya kiimani. Soma Neno. Tubu. Pokea sakramenti. Jitambue. Utavuka.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top