UFUFUO WA KRISTO – SUNDAY WORD

 

YESU HAKUWA MTU WA KWANZA KUFUFUKA KWENYE BIBLIA!
WATU WALIANZA KUFUFUKA AGANO LA KALE NA YESU KAMA YESU ALIFUFUA WATU KADHAA PIA KABLA YA KIFO CHAKE.

πŸ“– 1 Wafalme 17:17-24 – Nabii Eliya anafanya muujiza na kumfufua mwana wa mjane kule Sarepta kutoka kwa wafu.

πŸ“– 2 Wafalme 13:20-21 – Hadithi inasimulia kuhusu mtu aliyefufuka kwa miujiza baada ya kutupwa kaburini kwa Elisha alipokuwa amezikwa.

 

BAADHI YA UFUFUO KATIKA AGANO JIPYA

  1. Binti wa Yairo – Marko 9
  2. Mwana wa mjane wa Naini – Luka 7
  3. Lazaro, rafiki wa Yesu – Yohana 11

TOFAUTI YA UFUFUO WA YESU NA WENGINE

Hao wote waliokuwa wamefufuliwa, walikufa tena na wakapumzika na wazee wao.
Lakini ufufuo wa Yesu ulikuwa wa milele kwa sababu baada ya kufufuka alipaa kwenda mbinguni.

YESU HAI KWA SASA.
Ameketi kuume kwa Baba yake na anaishi hadi leo.

Upendo wake bado upo, kusudi lake halijabadilika:
Kukuweka huru kutoka kwa nguvu za giza kwa gharama yoyote!
Na kazi ya wokovu imeboreshwa kwa kiwango kikubwa zaidi!

 

JE, UFUFUO WA YESU UNAKUAMBIA NINI?

πŸ‘‰πŸ½ Death is not final!
Chochote kitakachokufa kwenye maisha yako sio mwisho wako!
Kuna nguvu ya ufufuo iliyomfufua Yesu kutoka kwa wafu ambayo hata wewe unaweza kufufuka na kufufua mambo yako.

Death can strike you but Jesus made sure that after death strikes it doesn’t have to be final!
He made sure there is an option to rise again.

 

WENGI WANAVULIWA NA VIFO VYA MAISHA

Wengi wetu tunamezwa na huzuni ya vifo vya maisha β€” kupoteza kazi, mapenzi, familia, afya β€” na tunaishia kwenye kukata tamaa.

Hata wasomi wa maandiko, wanaozijua aya zote, huzidiwa na vifo vya nafsi zao.
Wanaishi huku wakiwa roho zao zimekufa siku nyingi sana.

πŸ‘‰πŸ½ Watu husema: “We live only once.”
Mimi nasema: We live every day and die once.
Lakini wengine wanaishi wakifa kila siku kwa kurudia tukio moja lililowaumiza.

 

VIFO VYA MAISHA: MFANO HALISI

Kama ulifukuzwa kazi 2015, na hadi leo bado hujaachia tukio hilo, basi una relive hiyo siku kila mara.
Ulikuwa msomi, mwenye vyeti, uzoefu, IQ kubwa β€” lakini kila unapoamka, fikirani mwako ni: “Kwanini walinifukuza?”
Na siku nzima inaharibika! Unakuwa depressed, unakunywa pombe, hujishughulishi tena.
Umeshapoteza dira ya maisha.

Mahusiano yakikufa, wewe nao unakufa.
Ndoa ikivunjika, unakufa ndani kwa ndani.
Penzi likifa, linakuwa mzimu unalilia miaka 5 hadi 10.

Wengine bado wanavaa pete za ndoa miaka mingi baada ya kifo cha mwenzi wao.
Wengine wanaongea na marehemu usiku kila siku.
Hii ni milango ya nguvu za giza.
Yesu yu hai β€” Ongea naye, sio na wafu.

 

MFANO WA MAISHA: HUYU DADA ALIYEKATAA KUFA

Dada mmoja ambaye tuliishi wote kama wasichana wa kazi, alifikia maisha mazuri sana β€” alikuwa na biashara zake mbili, mwanaume, na mtoto.
Lakini baadaye mambo yakaporomoka β€” akaachwa, biashara zikafa, madeni, akaishia kuwa msafishaji wa ofisi Dar.

Lakini bado ana roho ya maisha bora!
Bado ni mrembo, bado ana ndoto.
Amejifunza kuvumilia huzuni na kifo cha maisha yake ya zamani.
Na sasa anaendelea kuweka mipango mipya β€” hata ameanza kupewa kazi jikoni kwa uzoefu wake wa kuendesha bar.
Roho yake haijafa!

UFUNUO MKUU: KUBALI KIFO, UPATE UFUFUO

πŸ‘‰πŸ½ Dawa ya kifo chochote kwenye maisha yako β€” iwe kazi, biashara au mapenzi β€” ni kukubali kuwa RIZIKI IMEFIKA MWISHO.

Kisha pitia aibu yake, kama Yesu alivyo aibishwa msalabani.
Ukikubali, ufufuo uko karibu!
Watu waliokuzika watashuhudia ukinyanyuka tena, ukiwa bora zaidi!

Huwezi kufufuka kama hukubali kufa.
Usiishi na marehemu ndani ya maisha yako.
Usipinge kweli kwamba mahusiano fulani, kazi au ndoto zimeisha.
Kubali. Lia. Pona. Kisha fufuka kwa jina la Yesu!

HITIMISHO

Yesu alikufa, akafufuka, na yu hai leo.
Na wewe pia unaweza kufufuliwa kutoka eneo lolote lililokufa ndani yako.
Utaamka tena!
Utaishi tena!
Utafanikiwa tena!

“They killed you and you died. Yet you are back, stronger and mightier, just like Jesus who is behind you!”

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top