Mungu ameweka wazi kwamba ana wapenda watu wote wote lakini KUJIBU MAOMBI NI KWA WALE TU WATAKAO TIMIZA CONDITIONS ZAKE TU!, Sasa mtu conditions hutimizi alafu unajishangaza kwanini Mungu hakujibu?, Anakujibu vipi sasa?
KILA AHADI MUNGU ALIYOTOA LAZIMA INAKUWA BACKED NA CONDITIONS, AHADI YA UPENDO TU NDIO UNCONDITIONAL PEKE YAKE, HATA MSAHAMA WA MUNGU UNA CONDITIONS KWAMBA UFANYE TOBA YA DHATI NA KUDHAMIRIA KUACHA KABISA.
SHIDA YETU WATUMISHI NI MOJA TUNA KATA CONDITIONS NA KUWASOMEA AHADI ZA MUNGU TU ILI MFURAHI NA KUFUNGUA POCHI HIZO! HALI NGUMU JAMANI, KUJIONGEZA MUHIMU LAKINI BILA CONDITIONS KUTIMIA AHADI KUTIMIA NI UONGO MTAKATIFU.
Kumbukumbu 28:3-13
3.Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. 4.Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako,na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.
5. Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.
6.Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. 7BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubari kia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.
9.BWANA atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; Utakaposhika maagizo ya BWANA, Mungu wako, na kutembea katika njia zake.
10. Na Mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la BWANA, nao watakuwa na hofu kwako.
11.BWANA atakufanya uwe na wingiwa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako kwamba atakupa.
12.Atakufunuli a BWANA hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe.
13.BWANA atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapo yasikiza maagizo ya BWANA, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya;
Mfano hili andiko linasomwa sana makanisani na karibia makanisa yote na cha kusikitisha linasomwa robo ili kuwa furahisha, wakati robo tatu iliyobaki ndiyo backbone ya hio robo kutumia. Ukisoma hiki kupande walichokata unaona
MUNGU SI NDIO HUYU SASA NA DINI SI NDIO HII SASA, MFANO NINGEPOST HIKO KIPANDE TU AMEN ZINGEKUWA KAMA MIA (100), Picha linaanza aya hio-hio ya
Kumbukumbu 28: 1-2
1. Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; 2. Na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako.
MPENDWA CONDITION IPO NA NI NZITO SANA, NA MUNGU YUPO WAZI KUTUMIZA KWAKE AHADI KUNA ANZA NA KUTIMIZA CONDITION, NO FULLFILLING CONDITION NO DEAL, YAANI ITAKUWA UTAKAPO SIKIA SAUTI YA BWANA MUNGU WAKO KWA BIDIU UPOO?, SAUTI UMEISIKIA HATA ACHA HIO BIDII.
Tuje mbele baada ya lile 1 million blessings type of scripture, MUNGU ANATEMBEZA ONYO KALI BALA SIO LA NCHI hii.
KUMBUKUMBU 28:15-21
15. Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapo kujilia laana hizi zote na kukupata.
16.Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani. 17. Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia.
18. Utalaaniwa uzao wa tumbo lako,na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.
19.Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo.
20.BWANA atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako,uliyoniacha kwayo.
21.BWANA atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki.
NI MWENDO WA LAANA MFULULU KUDADADEKI UKISIKIA FULL LAANA AU WAARABU WANA KWAMBIA LAANA TULAAH YAANI LAANA YA MUNGU IPO JUU YA MJA WAKE NDIYO HII.
AYA MOJA YA 28 LAKINI INA PANDE MBILI (2) ZA SHILINGI CHAGUA KUSHIKA KICHWA AU MKIA, NA HAPA MUNGU BADO HAJAMALIZA.
UKIENDELEA KUSOMA IT GET EVEN DARK AND WORSE AND SCARY!
KUMBUKUMBU 28: 22-27
22. BWANA atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie. 23. Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma.
24. BWANA atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie.
25. BWANA atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; Nawe utatupwa huko na huko katika falme zote za duniani.
26. Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza.
27. BWANA atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa.
MBINGU ZILIZO JUU YAKO ZITAKUWA SHABA KUDADADEKI, BWANA ATAKUPIGA NA KIFUA KIKIU, HOMA, UKURUTU, KUWASHWA KWA HALI YA MOTO (NDO KUWASHWA GANI HUKU TENA JAMANI TOBAA!) UPANGA, UKAFU NA KOGA! KHAA! ?, SASA UTABAKIA HATA MAJIVU KWELI BAADA YA HAYA? MASKINI, MUNGU HAPO NDIYO KWANZA ANAANZA NA WEWE KUDADADEKII.
KUMBUKUMBU 28:28-34
28. BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazila moyoni. 29. Utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe siku zote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.
30. Utaposa mke na mume mwingine atalala naye; utajenga nyumba usiikae; utapanda mizabibu usitumie matunda yake.
31.Ng’ombe wako atachinjwa mbele ya macho yako, usile nyama yake; utanyang’anywa punda wako mbele ya uso wako kwajeuri, usirudishiwe; kondoo zako watapewa adui zako, usipate mtu wa kukuokoa.
32Wanao na binti zako litapewa taifa lingine, na macho yako yataangalia, na kuzimia kwa kuwatamani mchana kutwa; wala hapatakuwa na kitu katika uwezo wa mkono wako. 33. Matunda ya nchi yako, na taabu yako yote, vitaliwa na taifa usilolijua; utaonewa tu, na kupondwa chini daima. 34. Hata uwe mwenye wazimu kwa yao-nwayo na macho yako, utakayoyaona.
WENGI MSHAPIGWA HILI BUMBUWAZI LA MOYONI, MNAKWENDA KWA KUPAPASA PAPASA MCHANA WA JUA KALI,WALA HAMFANIKIWI KWENYE NJIA ZENU, SIKU ZOTE UTAONEWA TU KUDADADEKI, WALA HAPATAKUWA NA MTU WA KUKUOKOA, JESUS CHRIST!
UTAPOSA MKE AU MUME NA WATALALA NAYE WENGINE! HALOOO, MTASHA NILETEE JAHAZI MODERN TAARAB, ASO NA KASORO NI MUNGU TUUU! ALOOOO! BALAAA ! HILII.
KUMBUKUMBU 28-45-48
45. Nalaana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza. 46. Nazo zitakuwa juu yako kwa ishara na ajabu, najuu ya uzao wako milele. 47. Kwa kuwa hukumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa furaha na moyo wa kushukuru, kwa ajiliya ule wingiwa vitu vyote. 48. Kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta BWANA juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza.
WEWE SI UMEGOMA KABISA KUNTUMIKIA BWANA MUNGU WAKO UNAITUMIKIA ZINAA, UNATUMIKIA SHIRKI, UTAMIKIA WIZI NA UDOKOZI KAZINI, UNATUMIKIA MABUZI, UNATUMIKIA KILA MTU NA KILA KITU ISIPOKUWA MUNGU, BASI SAWA!.
SASA BASI KWA TAARIFA YAKO UTAISHIA KUWATUMIKIA ADUI ZAKO ATAKAOWALETA BWANA JUU YAKO, OOH NO NA HUTAWATUMIKIA IN LUXURY NI KWA KIU, NJAA, KWA UCH….., SUBHANALLAH, GOD HAVE MERCY!.
Kumbukumbu 28:54-57
54. Mtu mume kati yenu aliye mwororo na laini sana, jicho lake litakuwa ovu juu ya nduguye, najuu ya mke wa kifuani mwake, najuu ya masalio ya wanawe waliosalia naye. 55. Hata asitake wao mmoja wapo apewe katika nyama ya wanawe atakaowala, kwa kuwa hana kitu kilicho msalia kwake; katika mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika malango yako yote.
56. Mwanamke kati yenu aliye mwororo na laini, ambaye hange hatirisha kuweka wayo wa mguu wake nchi kwa umalidadi na ulaini, jicho lake huyu litakuwa ovu juu ya mume wa kifuani mwake, najuu ya mwanawe,najuu ya binti yake. 57. Najuu ya mchanga wake atokaye katikati ya miguu yake, na juu ya wanawe atakaowazaa; kwa kuwa atawala kwa siri, kwa uhitaji wa vitu vyote; katika mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika malango yako.
UBAYA UBWELAAH!, WEWE NA MUME NA WATOTO WAKO HAMTA ONA AMANI, MTAMALIZANA WENYEWE KWA WENYEWE MWANZO MWISHOOO! UBAYAAA UBWELAA!, FAMILIA NYINGI ZIPO HII STAGE YA UBAYA UBWELAA, MPAKA MTU ANAONDOKA NYUMBANI ANASEMA YEYE YATIMA.
KUMBUKUMBU 28:58-63
58. Kama hutaki kutunza kufanya maneno yote ya torati hii yaliyoandikwa katika kitabu hiki, upate kulicha jina hili la fahari na utisho, BWANA, MUNGU WAKO;
59. Ndipo atakapofanya BWANA mapigo yako yawe ya ajabu, na mapigo ya uzao wako, mapigo makubwa kwa kweli, ya kudumu sana, na magonjwa mazito ya kudumu sana.
60. Naye atakurejezea maradhiyote ya Misri juu yako uliyokuwa ukiyaogopa,nayo yataambatana nawe.
61. Tena kila ugonjwa, na kila pigo yasiyoandikwa katika kitabu cha torati hii, atakutia nayo BWANA juu yako, hata utakapokwisha kuangamizwa.
62. Nanyi mtasalia wachache kwa hesabu, ninyi mliokuwa mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi; kwa kuwa hukuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako.
63.Tena itakuwa, kama vile alivyokuwa akifurahi BWANA juu yenu kwa kuwatendea mema na kuwafanya kuwa wengi, ndivyo atakavyofurahi BWANA juu yenu kwa kuwapoteza na kuwaangamiza; nanyi mtanyakuliwa katika hiyo nchi mwingiayo kuimiliki.
OGOPA MAANDIKO YANASEMA NDIOO BWANA ATAKAPOFANYA MAPIGO YAKO YAWE MAKUBWA KWA KWELI (SIO UONGO MAANA YAKE) NA YA KUDUMU SANA TU! DAAAH MY WANGU.
KUMBUKUMBU 28:64-67
64.BWANA atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hiiya dunia; nawe huko utatumikia miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako, nayo ni miti na mawe.
65. Wala katika mataifa hayo hutapata raha iwayo yote,wala hutakuwa na kituo cha wayo wa mguu wako;lakini BWANA atakupa huko moyo wa kutetema, na macho ya kuzimia,na roho ya kudhoofika.
66. na uzima wako utakuwa na wasiwasi mbele yako; nawe utakuwa na woga usiku na mchana,wala hutaamini kamwe maisha yako.
67. Asubuhi utasema, Laiti ingekuwa jioni, najioni utasema, Laiti ingekuwa asubuhi, Kwa kicho cha moyo wako utakavyokucha, na kuona kwa macho yako utakavyoona.
68. BWANA atakurudisha tena Misri kwa merikebu, kwa njia ambayo nilikuambia, Hutaiona tena popote; nanyi huko mtajiuza nafsi zenu kwa adui zenu kuwa watumwa na wajakazi, wala hapana atakayewanunua.
JAMANI HALI NI MBAYA SANA MNO- MNOOO, TUFANYENI TOBA YA KWELI NA KUMTUMIA BWANA KWA KUTII MAAGIZO YAKE YOTE.
I real love your writing skills very nice and entertaining while learning truth kihusu MUNGU wetu ?
Amen @Alex, May Lord be with you!