Waefeso 1:7
Maana kwa damu yake Kristo sisi tunakombolewa, yaani dhambi zetu zinaondolewa .Ndivyo ulivyo ukuu wa neema yake.
Mpendwa Neema ya wokovu ni Neema ya kuokolewa kutoka kwenye utumwa wa dhambi, mshahara wa dhambi na mfumo wa dhambi kwa ujumla. Watu mnahisi ukitenda dhambi unamkosea Mungu afu basi, usichokijua Unajiongeza kwenye mfumo wa dhambi ambao unakudai dhambi zaidi ili mambo yako yaende, Na ukigoma unapokea mshahara wa dhambi zako, Mfano ukianza umalaya mdogo mdogo tu kulala na wanaume for favors!, Itafika mahala bila kulala na mtu hupati kitu.
Yaani inakuwa as if una alama kwenye paji la uso kwamba ili wanaume wakupe kitu lazima wakugonge kwanza!, Ushaingia kwenye mfumo na kuchomoka sio rahisi unajikuta mtumwa tayari wa ngono, Mijitu mibaya huipendi ila unalazimika kulala nayo.
Unaweza kuwa umeanza Wizi ofisini ki utani utani,Wizi ule Bwana unakuondolea kibali chako kabisa, Unabakia huna kibali kwa Ma-Boss wala wenzio. Hupati KITU ofisini mpaka UIBE, Unageuka mtumwa sasa wa wizi na mwisho lazima utapokea mshahara wa kufukuzwa kazi.
Unaweza kama masihara ukaanza kuwa sio muaminifu kwenye mahusiano YAKO, Ndumila kuwili dada!, Unakula huku na huku! Kibali chako kupata wanaume wazuri kinayeyuka unaanza ku-attract watu kama wewe ! WAONGO WAONGO NA MALAYA MALAYA hivyo hivyo, Hangaika unavyo-hangaika kupokea mshahara wa dhambi kupo pale-pale.
Nguvu za giza Mara nyingi tuna-zifungulia milango wenyewe kwenye maisha yetu, kwa kupitia dhambi ndogo-ndogo tu, Zikijikita na kuungana na mshahara wa dhambi mambo yanakuwa EPIC. Utaskia mtu anasema kwetu tuna shida ya Mizimu ya ukoo, sababu wote tunazalia nyumbani, As if mizimu ndiyo inawabaka usingizini na kuwa zalisha watoto, ndiyo laana ya ukoo ipo sawa, lakini wewe unaifungulia milango ichanue maishani mwako kupitia ZINAA, Mizimu haikupeleka guest na kukutanua miguu ni Tamaa zako tu, Mbuzi kafia.
Mambo yakishakuwa intense, inakuwa kama Sodoma na Gomora, Kuchomoka sio rahisi, hata kidogooo, Kwa nguvu zako kwa KWELI uongo, yaani unasali sana lakini upwiruuu ukikushika ndo unajipooza kidogo, Unaanza moja, Mwisho unakata tamaaa.
Na nguvu nyingi za giza mtaji wao mkubwa ni dhambi wanajua wewe na Mungu hamfiki mbali na huo urafiki wenu ,, Siku 3 tu utashikwa na upwiru, ukiupunguza tuuu kwishaaa kazi!, Wewe unaweza kuwa kweli unataka kuvuka kwenye kazi!, Uko serious!, Wenyewe wanakutegemea kwenye zinaa ndiy utakapo tibua bwana na kutoboa mtumbwi.
Kiukweli kuishinda dhambi in cold blood sio rahisi hata kidogo ndio linapokuja sasa swala la kuhitaji neema ya wakovu. Mpendwa neema ya wokovu haswa haswa ni kukuokoa na wewe mwenyewe kutoka kwenye utumwa wa dhambi zako, aidha mshahara wa dhambi zako.
Mfano umekuwa mtumwa sanaa wa zinaa somtimes hata hutaki lakini basi tu mambo yanakuwa si mambo unajikuta ushaachia goli wazi, baada ya hapo unasikitika mpaka kesho unaachia tena!, na kusikitika tena katika mazingira haya hapa inabidi uombe neema ya wokovu wa kuachana na zina, utubu kwanza dhambi zako na kuomba neema za mungu uvuke eneo hilo sasa, na mungu akikupa neema zake inageuka hata kama wewe unataka kuzini mwili na nafsi havitaki kabisa kabisa.
Saving grace pia inakuokoa na dhambi za mababu zako, kuna laana na malipizi zinatoka kizazi cha nne (4) nyuma yaani wewe deni umelikuta na linalipiwa na ukoo wenu, hata aliye fanya hiyo dhambi humjui wala hujamsikia lakini malipizi kama kawaida yana kuhusu.
Mpendwa ukikomaa kumuomba mungu hii saving grace , msihi akurehemu na makosa ya uko wako na akutenge na adhabu zao za ajabu-ajabu, msihi sana mungu apitishe neema na rehema zake uvuke.
Mfano ndo umekuta watu wanazalia nyumbani tu, uwe na tasia njema nyumbani utazaaa uwe gawa-gawa wembe ule ule, kumbe huko nyuma bibi yako alikuwa mwali akakimbia na shanga za kungwi, kungwi aka -laani mwali ambaye ni bibi yenu na nyinyi harusi mtaziona kwa wenzenu tu.
Mpendwa kuna maeneo kwenye maisha yako unajua yana shida lakini chanzo cha hiyo shida yamkini unakijua au hukijui ila shida ipo na unaona kabisa hilo eneo lime paralise!, despite kujaribu kuliombea na nini, mpendwa li-identify hilo eneo wiki hii yote, uwe unaliombea neema ya mungu, walau mara tatu (3) kwa siku, saa 3 asubuhi, 9 mchana na 3 usiku ( endekeza mda wa huba), unaweza omba 15 min -30 min hata zaidi yaani wewe tu.
Na katika maombi yako kiri-kuwa eneo hilo halina neema za mungu kwa sababu either unazijua au huzijui, kama ni dhambi zako, tumia huo mda kutubu kwa dhati na kumuhakikishia mungu unataka kuacha serious na muombe akupe akupe tu neema ya kuacha.
Kama huzijui mwambie mungu akihurumie na kupitsiha neema zake hilo eneo, umenyauka na umeisha kabisa akusaidie ku-experience neema ya wokovu kwa matendo.
Mpendwa kweye maombi ya neema maneno sio muhimu sana, jambo la muhimu ni roho yako kuwa na kiu ya neema na kuamini mungu kama mungu agawaye neema zake kwa watu wake atakupa na wewe.
Ukiomba neema eneo la mahusiano amini kwamba mungu atakupa hiyo neema na expect kuwa utaona mabadiliko chanya kwenye hilo eneo kuanzia wiki hii, yaani akili yako ifocus na hilo na itarajie, hayo matokeo, i expect hayo matokeo na amini mungu katika uaminifu wake ameachilia hiyo neema, you should put your soul in your prayer for saving grace sawa nimesema sali dakika 15, sio hizo dakika 15 unarudia kwenye dhambi za reja reja hutaona maajabu mpendwa,
Wiki hii sali dakika 15 kila baada ya masaa 6, lakini tumia muda wako uliobakia akili yako i-focus na kupokea saving grace kwenye hilo eneo sugu, tumia muda wako kutafakari hilo eneo na nini unahitaji mungu akufanyie, tumia muda wako kumuabudu na kumsifu mungu kwa ukuu wake huku ukimuomba achilie neema yake ya ukombozi, kukomboe na mambo unayoyajua na usioyajua, mpendwa muda wako mwingi tumia juu ya hili jambo tu,week hii yote.
Sijatoa muongozo wa maombi kwa sababu nataka utumie maneno yako zaidi utumie kuuguza kwa moyo mbele ya bwana wako, utumie feelings na real situation kujenga hoja mbele za mungu, nataka ubwage moyo wote. Yaani akili yako ishinde ikisema bwana naomba neema yako eneo la mahusiano, nimefanya program 15 sijapata hata dalili ya marriage yoyote, nimeombewa na watumishi flani na flani, sijapata hata kope kustuka, lakini naamini bwana kwa neema yako bado linawezekana, sitaki kukukatia tamaa au kujikatia mimi tamaa.
Bwana imeandikwa neema yako ni kuu sanaa, ikaniondoe kwenye utumwa wa upweke na kuniweka huru nikastawi kwenye mahusiano, bwana mimi sikutanagi na mtu sahihi, nakutana na mauza-uza, naomba neema yako ya wokovu nikawe huru kutoka nguvu zote za giza zinazo influence mahusiano yangu kukwama na kuchelewa kwa neema yako nikakutane na mwenzangu week hi, mpendwa tumia maneno yako kwa situation yako.
1 thought on “ONE SAVING GRACE/ NEEMA YA WOKOVU”
maxime alias non sed illum laborum consequatur. nihil facere modi qui autem ratione fugit beatae qui ducimus. autem et impedit sed officiis qui aut. ut iure ut cumque dolores modi vel illum eum aperia