OMEGA PROGRAM (UPAKO WA MWISHO WA MWAKA) 2023

Mpendwa katika maombi haya tutaombea yale malengo uliyokuwa unaomba mwaka huu wote na bado hayakutimia ,MUNGU AKUHURUMIE NA KUKUREHEMU USIANZE MWAKA NA VIPORO!

Muhimu: TUTAFUNGA SIKU 7!, MASAA 12!,  TUTAFANYA MAOMBI YA MEDITATION!! KUANZIA TAREHE 6/11/2023 – 12/11/2023

Omega charity program

Mwaka jana tuliwanunulia chakula siku va christmass!!, Mwaka huu kuna kituo kipo Arusha, cha kanisa kina watoto wadogo kati ya mwaka 1 – 5 /7 yrs nilipanga kuwanunulia nguo za christmass nao wajue raha va kuvaa nguo mpya atleast wa feel its christmas kama watoto wengine!

Sasa nguo mpva sio mchezooo! !Nguo zipo juuu and on christmass its even worse! lakini Mungu nimuaminifu sanaa! Kuna mtu kanitafuta ana nguo nzuri na zenye ubora wa hali ya juu sana, na yuko katika hatua ya kufunga duka lake!, Hivyo atatuuzia bei ya kwenda  ya 25,000 Tshs flat rate bila kujali size wala design wala quality!. Tutajumua! na sadaka yake yeye atatoa 5000Tshs kwa kila nguo hivyo atatupa kwa 20,000Tshs flat rate!

MUHIMU:Kama utataka kujiunganisha na baraka hii unakaribishwa sanaaa! Namba zetu za charity ni 0713300038.

Mpendwa kitakacho-fanya ufunge kesho ni kiu yako ya kuvuka na kupata matokeo, Imani yako ndo itakayo kuponya na kukuvusha! Mpendwa sio watu wote walio-enda kwa yesu kuponywa walimuamini sanaa anachofundisha au kumuelewa sana isipokuwa waliamini kwamba anaweza kuwa sio mfalme wa mavamudi lakini shida zaooooo! Shida zaoooo anazimuduuu!

Ndio maana hata kwenve maandiko walitokea ghaflaaa tu wale wagonjwa! Mara chache walikuwa ndugu wa familia za wanafunzi wake!, Most times walikuwa wanatokea ghafla sanaaa! Sio watu wanao zurura na yesu day in day out!

Hivyo hata wewe kesho! Kama una amini Mungu hiyo changamoto yako anaiweza na imani ya kufanya kitu juu ya changamoto yako ipo dandia mtubwi wa wanao-funga!

Omega Program : Day 1

Yeremia 10:6-20

6.Ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliye kama wewe, wewe ni mkuu na nguvu yako yajulikana.

1Mambo ya Nyakati 16:25

Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana; Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.

1Mambo ya Nyakati 29:11

Ukuu ni wako, Ee Mwenyezi-Mungu, una nguvu, utukufu, ushindi na enzi.Vyote  vilivyoko mbinguni na duniani ni vyako. Ee Mwenyezi­ Mungu, ufalme niwako, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.

Omega Program : Day 2

Waefeso 3:20

Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiriya nguvu itendayo kazi ndaniyetu

Hesabu 23:19

Mungu si mtu, aseme uongo, wala si mwanadamu, ajute, lwapo amesema, hatalitenda? lwapo amenena, hatalitimiza?

Yeremia 32:17

Ee Mwenyezi-Mungu, ni wewe ambaye kwa nguvu zako nyingina uwezo wako  mkuu,umeziumba mbingu na dunia, hakuna kisichowezekana kwako.

Omega Program : Day 3

1Mambo ya Nyakati 21:13

Daudi akamjibu Gadi,”Nimeingia katika mashaka makubwa! Lakini afadhali niadhibiwe na Mwenyezi­ Mungu kwani yeye ana huruma sana. Ila nisianguke katika mkono wa mwanadamu.”

Nehemia 9:31

Ila kwa rehema zako nyingi hukuwakomesha kabisa, wala kuwaacha, kwa maana wewe u- Mungu mwenye neema na mwenye rehema.

Yeremia 32:37

Nitawakusanya watu kutoka nchi zote ambako kwa hasira na ghadhabu na chuki yangu kubwa, niliwatawanya. Nitawarudisha tena mahali hapa, na kuwafanya wakae salama.

Omega Program : Day 4

Hosea 2:21

Tena itakuwa siku hiyo,mimi nitaitika,asema BWANA, nitaziitikia mbingu ,nazo zitaiitikia nchi.

Yeremia 33:3

Niite,nami nitakuitikia, nami nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.

Ezekieli 14:4

Basi sema nao,uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi, Kita mtu wa nyumba ya Israeli atwaaye vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, na kumwendea nabii; mimi, BWANA, nitamjibu neno lake kulingana na wingi wa sanamu zake.

Omega Program : Day 5

lsaya 65:24

Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu, na wakiwa bado wanena, nitasikia.

lsaya 30:19

Enyi watu wa Siyoni, enyi watu wa Yerusalemu, hakika nyinyi hamtaomboleza tena. Kweli Mungu atawahurumia; mara tu atakaposikia kilio chenu atawaitikeni.

Zaburi 38:15

Kwa kuwa nakungoja Wewe, BWANA,Wewe utajibu, Ee Bwana, Mungu wangu.

Omega Program : Day 6

Mwanzo 30:22

Kisha Mungu akamkumbuka Raheli, akalikubali ombi lake na kumjalia kupata watoto.

1Samweli 1:19

Wakaondoka asubuhi na mapema, wakaomba mbele za BWANA, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama;Elkana akamjua mkewe Hana; naye BWANA akamkumbuka.

lsaya 49:15-16

Lakini Mwenyezi-Mungu asema:”Je,mama aweza kumsahau mwanawe anayenyonya,asimwonee huruma mtoto wa tumbo lake? Hata kama mama aweza kumsahau mwanawe,mimi kamwe sitakusahau. Nimekuchora katika viganja vyangu;kuta zako naziona daima mbele yangu.

Omega Program : Day 7

Warumi 7:24

24 Ole wangu, mimi mnyonge! Ni nani atakayeniokoa na huu mwili wa kifo?

Tito 3:5

Sikwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; balikwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa mara ya pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu.

Ezekieli36:29

Nitawaokoa kutoka uchafu wenu wote. Nitaiamuru ngano iongezeke,wala sitawaletea njaa tena.

 

 

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top