Weka Nia ya Kesho

 

Kuna wakati umeomba sana lakini hupati mabadiliko yoyote, Umepambana kwa muda na changamoto zako ila bado jitihada zako zimeshindikana. Imefikia wakati umekata tamaa ya kuomba tena na kuipa Mbingu Mgongo, Umeacha Mbingu ifanye uamuzi wa kukupa au kukunyima na yote umeifanya sawa kwako kwani Mbingu imeamua.

Mpendwa unapotia nia ya kufunga kesho zungumza na Mbingu kwa mara nyingine na uliza ni nini tatizo ? Mbona inakufanyia hivyo ? na Je ufanye nini ili ione una maanisha ?. Ongea na Mbingu kuwa umetia nia kwa mara nyingine tena ya kuvuka  changamoto zako na kusihi kuwa kesho isikukalie kimya kisha Mtukuze Mungu na sifu utawala wa Mbinguni. Toa sifa za kutosha kwa moyo wa kweli na Uliza tena Mbona Mbingu imekutenga ? ,Mbona kuna wakati ulikuwa mtu wake. Aidha Omba Kesho Mbingu iweke Mapungufu yako pembeni na ushuke utukufu  na ukamilifu wake kukuokoa.

Mpendwa unapotia nia  ya kufunga  na kujadiliana na Mbingu ukifanya kwa moyo wako wote na kweli ya dhati na kwa  kuamini hakika utajibiwa na wengi wanajibiwa katika njia hii. Wengi waliozingatia nia hizi wamevunja KUTA zinazowazuia kusonga mbele na kushinda changamoto zao.Na Mpendwa, KUTA kwenye ulimwengu wa roho ina maana ya maagano ya kiganga, spiritua husbands!, na hao ndio wafunga njia za mahusiano mengi. Hivyo leo kazi ilikuwa ni moja tu kubomoa KUTA na kuweka njia.

Watu wengi hatushindi vita nyingi katika maisha yetu kwa sababu Mungu hapigani upande wetu. Tukirejea katika Biblia Waisraeli mara nyingi walikuwa wanamuuliza Mungu yupo upande gani kwanza, Ili waweze kufahamu kabisa wanasimama upande gani na Je Mungu anaenda vitani au haendi? na kama Mungu haendi au hayuko upande wao walikuwa wanaenda kinyonge wakijua fika wanaenda machinjioni na hawatoshinda vita hivyo.

Mpendwa kama vita zako za nyuma ulikuwa unakurupuka na kwenda mwenyewe ( Jeshi la Mtu Mmoja) hii ndio sababu kubwa ulikuwa unashindwa vita hizo. Na wengi wetu baada ya kushindwa ndio tunaanza kuomba msaada wa haraka kutoka Mbinguni ! na Mbingu zina huruma sana zinawapooza adui zetu kidogo.

Mpendwa leo ukiweka imani yako msihi Mungu  kwa moyo wa kweli na imani japo Mara hii tu apigane upande wako, Msihi ukisema “Mungu wa Majeshi, Alfa na Omega kesho twende wote vitani kupambana uso kwa uso na changamoto zangu hizi zinzonisumbua kwa muda mrefu”

Msihi Mungu kuwa siku hizi 3 umepambana kwa imani kubwa sana lakini kesho ni siku ya changamoto zako kujua Mungu wako ni nani yaani zikashuhudie kikamilifu Ukuu wa Mungu, Uweza wa Mungu, Nguvu za Mungu, Utukufu wa Mungu mpaka zisujudu mbele ya Mungu wa Israeli.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top