l SAMWELI 5
Sanduku la Agano huko Ashdodi na Ekroni 1, Baada ya Wafilisti kuteka Sanduku la Mungu,walilichukua kutoka Ebenezeri mpaka Ashdodi .2 Kisha wakaliingiza lile Sanduku ndaniya hekalula Dagonina kuliweka kando ya huyo Dagoni.
3 Watu wa Ashdodi walipoamka asubuhi na mapema kesho yake, kumbe,wakamkuta Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la Bwana.Wakamwinua Dagoni na kumrudisha mahali pake.
4 Lakini asubuhi iliyofuata,walipoamka kumbe, walimkuta huyo Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la Bwana! Kichwa chake na mikono vilikuwa vimevunjwa navyo vimelala kizingitini, nikiwiliwili chake tu kilichokuwa kimebaki.
5 Ndiyo sababu mpaka leo makuhani wa Dagoni, wala wengine waingiao katika hekalu la Dagoni huko Ashdodi hawakanyagi kizingiti.
6 Mkono wa Bwana ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi na vijiji jirani, akaleta uharibifu juu yao na kuwatesa kwa majipu.
7.Watu wa Ashdodi walipoona kile kilichokuwa kikitokea, wakasema,”Sanduku la Mungu wa Israeli kamwe lisikae hapa pamoja na sisi, kwa sababu mkono wake ni mzito juu yetu na juu ya Dagoni mungu wetu.”
PRAYER POINTS
1. Baba yetu ulie Mbinguni shughulika ,kuharibu na kutokomeza Miungu yote ilio nyuma ya vifungo vyangu vyote kama ulivyo shughulika na Dagon wa Wafilist huko Ashdodi, Shughulika na Ma Dagon yanayozuia mahusiano yangu, yanayo zuia uchumi wangu, afya yangu, biashara zangu, ajira zangu na changamoto yoyote unayotaka kuyasukuma.
2.Baba yetu ulie Mbinguni niweke huru na utawala wa Miungu na Madagon yote yanayoshikilia hatima yangu, kama ulivyo waweka wa Israel huru kutoka kwneye uonevu wa Miungu ya ki-Filist! Nirejeshee hatma yangu mikononi mwangu.
Una meditate juu ya hili jambo alilofanya Mungu kwa Wafilist, Na unamsihi alifanye juu ya hatima yako.