Mpendwa utaufata litrujia/ mtiririko huu wa Ibada kila siku kwa mda wa maasaa mawili (2) ikishindikana kabisaa walau mara moja(1) kwa siku, Usiruke siku,usilipue-lipue inshort usilete upuuzi wa aina yoyote It is your future hapa ipo in a stake. Hivyo fuata mtiririko huu kwa siku zote 10 asubuhi na jioni.
Hatua ya 1
Mpendwa sifu na kuabudu mda wa kutosha angalau kwa kiwango cha chini iwe ni nusu saa, Tumia nyimbo unazotaka na ambazo zinakuweka uweponi, Usiruke hatua hii wala kuchakachua.
Hatua ya 2
Mpendwa kiri maandiko kwa nguvuambayo Mungu aliahidi kuhusu delivarence, Yaani usitamke kimoyo moyo tamka kiasi cha kujisikia kisha simama na maandiko haya matakatifu:
Luka 10:19
19. Nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na kushinda nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu chochote kitakachoweza kuwadhuru.
Waefeso 1:7
Maana kwa damu yake Kristo sisi tunakombolewa, yaani dhambi zetu zinaondolewa. Ndivyo ulivyo ukuu wa neema yake.
Warumi 16:20
20.Na Mungu wa amani hata kawia kumponda shetani chini ya miguu yenu. Neema ya Bwana wetu Yesu iwe pamoja nanyi.
Ufunuo 12:11
Ndugu zetu wamemshinda kwa damu ya Mwanakondoo na kwa neno waliloshuhudia, Maana hawakuya-thamini maisha yao kuwa kitu sana, wakawa tayari kufa.
Wakolosai2:14
14. Baada ya kufuta kabisa hati ya mashtaka iliyokuwa inatukabili na kutupinga pamoja na masharti yake, ali-iondoa akaipigilia msalabani.
Wagalatia 3:13-14
13.Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kuchukua laana hiyo kwa ajiliyetu, kwa maana imeandikwa, ”Mtu anayetundikwa msalabani amelaaniwa.” 14.Lakini alitukomboa ili baraka aliyopewa Abrahamu iwafikie na watu wa mataifa mengine kwa njia ya Yesu Kristo. Na kwa kutegemea imani, sisi tupate kupokea Roho wa Mungu.
Zaburi 91:3
Hakika Mungu atakuokoa katika mtego, atakukinga na maradhi mabaya.
2 Timothee 4:18
Bwana ataniokoa na mambo yote maovu na kunichukua salama mpaka katika ufalme wake wa mbinguni. Kwake uwe utukufu milele na milele!, Amina.
HATUA YA 3
Vunja na kuharibu Maagano, Laana na mikosi juu yake na kuondoa uhalali wake juu yako. Sasa kutegemea na Level yako ya ukomavu, Kama mzoefu jimalize kwa kuzama kwenye maombi mpaka unene kwa lugha.
Kama kifaranga bado kwenye haya maombi sali sala simple lakini kwa imani kubwa. I break all covenant and curses working against me in the name of Jesus.
Mpendwa unarudia rudia kwa kumaanisha, Navunja maagano yote na laana zote zinazofanya kazi juu yangu na juu ya mahusiano yangu, juu ya uchumi wangu kwa Jina la Yesu na unajiongeza kidogo na wewe.
HATUA YA 4
Funga Roho zote zilizo nyuma ya hayo maagano na laana. Kama uko vere vere just be vere vere kwenye maombi yako, Show them and show out yaani Kama begginer mwendo wa simple prayer lakini imani kubwa, Kwa kusema nazifunga ROHO zote zinazo fanya kazi nyuma ya hizi LAANA na maagano kwa Jina la Yesu, Naziteketeza kwa Moto wa Roho Mtakatifu hazitainuka tena juu yangu kwa Jina la Yesu na unajiongeza na wewe.
HATUA YA 5
Mpendwa shika kichwa chako na kutovu anza kujiombea ushukiwe na Roho Mtakatifu, Kwa kusema Moto wa Roho Mtakatifu waka kuanzia kichwani kwangu mpaka kwenye unyayo wa miguu yangu kwa Jina la Yesu. Hapa usikimbize Gari, Kaa kwa kutulia na Taja eneo moja moja, Roho Mtakatifu anaweza kukuelekeza maeneo ya kuomba, Unaweza kushangaaa mikono imehama yenyewe, Tulia dawa ikuingiee hata woga ukikushika kumbuka image ya maisha after deliverance jikazeee ki kike kike na endelea na Delivarence na tumia muda wa kutosha hapa.
MPENDWA UKIONA ROHO MTAKATIFU HAJI MKARIBISHE NON STOP! KWA KUSEMA KARIBU ROHO MTAKATIFU NON STOP! MPAKA AJE!.
Mpendwa anaweza KUJA akakusaidia kuomba vitu vingine ambavyo akili YAKO inataka kuomba, mfano akili yako inataka kuomba kuhusu kazi lakini mdomo una tamka mahusiano! Tuliaaaaa dawa ikuingie.
MAMBO LAZIMA YAWE MENGI MDA LAZIMA UTAKUWA MCHACHE.
HATUA YA 6
Mpendwa anza kujifunika kwa damu ya Yesu! kwa kuita damu ya Yesu inayo nena mema na inene mema juu ya uchumi wako, juu ya mahusiano yako, juu ya ajira yako, juu ya afya yako, juu ya maisha yako kwa ujumla, Mpendwa lta Damu ya Yesu iingie ndani ya mwili wako na nafsi yako na kujiweka huru na vifungo vyote. Tamka kunywa na kuji-nyunyizia damu ya Yesu iliyo-mwagika kwa ajili ya ukombozi wetu na maondoleo ya dhambi na vifungo vyote, Tamka I drink the blood of Jesus kama wakati wa mageuzi ya communion!
Mpendwa unakunywa Damu ya YESU spiritually kama kanisani tu tofauti kanisani wanageuza mvinyo kuwa Damu Ya Yesu wewe huna hio luxury so drink it spiritualy. Mpendwa tumia muda wa kutosha hapa kujikomboa kwa Damu ya Yesu.
HATUA YA 7
Hapa sasa unakiwasha si ushajifunika kwa Damu ya Yesu na kunywa manake upo covered nje na ndani na unaanza kukemea sasa ile proper!, Katika Jina la Yesu yaani Roho zozote zilizojificha na ku operate kwenye maisha yangu toka sasa, Kwa Jina la Yesu na kuwafunga na kuwaondoa kwenye maisha yangu kuanzia Sasa, Kwa Mamlaka ya Jina la Yesu niachieni sasa na eneo la mahusiano yangu, eneo la uchumi etc.
Nimefunikwa kwa Damu takatifu ya THAMANI ya Yesu, hamuwezi ku-operate tena kwenye maisha yangu, Najiweka huru kutoka kwenu kwa Jina la Yesu, Tulia kwa muda kusikiliza maelekezo ya ROHO MTAKATIFU!
HATUA YA 8
MPENDWA OMBA KUJAZWA NA ROHO MTAKATIFU UPYA, NA OMBA USAIDIZI KAMA KUNA MAENEO WEWE UMEPWAYA AJE AMALIZE SHOW YEYE!, ENDELEA KUMKARIBISHA HUKU UKIENDELEA KUABUDU NA KUSIFU.
Mpendwa Malizia kwa Parayer Point hizi :
1. OMBA UKUTA WA MOTO UKUZUNGUKE WEWE NA ENEO UNALOTAKA KUVUKA.
Zekaria 2:5
Kwa maana Mimi, asema BWANA, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake.
2. OMBA KUFUNIKWA KWA DAMU YA YESU
Ufunuo 12:11
Ndugu zetu wamemshinda kwa damu ya Mwanakondoo na kwa neno waliloshuhudia, Kwa maana hawakuyathamini maisha yao kuwa kitu sana, wakawa tayari kufa.
3 OMBA MALAIKA WA MUNGU WAKUZUNGUKE.
Zaburi 34:7
Malaika wa Mwenyezi-Mungu huwalinda wote wamchao,na kuwaokoa katika hatari.