Wewe ni Wife Material na hakika Mume wako yupo!

Haijalishi mazingira yanakwambia nini lakini amini wewe ni wife-material na Mume wako yupo hakika. Tuone katika Biblia mifano ya wanawake tofauti-tofauti na mazingira mbalimbali waliyoyapitia na Mungu akawapa  Wame zao, Itakuwa Wewe!!!.

Esther alikuwa mzuri sana wa Sura na Umbo lakini alikuwa yatima, Biblia inasema mjomba wake Modekai alipambana kumuingiza kwenye Jumba la Kifalme ili aweze kuushinda Moyo wa Mfalme tajiri Ausero!

“Mungu wetu wa haki  akupe kibali cha Ester , Katika huo ushindani wa  Ma Girl-Friends ukaonekane Mke, hata kama mko wengi kiasi gani nakutia moyo kina Esther ni wengi na Biblia haitaji idadi. Mungu aliye juu akuinulie Modekai wako atakaye kupambania upate Mwenza.”

Tazama Mungu anamuonekania Ruth kwa mara ya pili na kumpa Mume Boaz kiwepesi kabisa. Hakufunga hata moja kavu. Hivyo Naomba nikutie Moyo hata kama wewe ni mjane mpe Mungu  nafasi atakutendea makubwa ya kushangaza

Tazama Gomeri binti wa Diblaim Biblia inaweka bayana alikuwa mzinzi. Haisemi kama alifunga kavu au alifanya diet kali. Lakini Mtumishi wa Mungu Biblia inasema, Nabii Hosea anaagizwa na Mungu akaoe mwanamke mzinzi azae watoto wa ulinzi. ( Usibase kwenye kipengele hiki tu soma kitabu kizima kwa wakati wako)

Je ikiwa Mungu Baba alimuona Gomeri akambariki na kumpa Mume tena mtumishi wake , Vip kuhusu wewe ambaye ni bora kuliko Gomeri na unalishika neno lake ?.

Sipora binti wa Kuhani wa Midian kwao walikuwa mabinti saba (7), na ndio walitunza mifugo na kusimamia uchumi wa famila. Biblia inasema Musa aliwaona wakinywesha mifugo na kuwasaidia kisha akakaribishwa nyumbani kwao na baadaye akapewa Sipora kama Mke!.

Mungu anaona ulivyo banwa na kazi, unavyotegemewa kwenu kiasi cha kukosa muda wa kutafuta mwenza, Mungu wa Sipora atakuletea Musa wako hapo kazini kwako na Kazi iendelee!!.

Raheli alikuwa binti wa Labani mjomba wake Yakobo. Biblia inasema Yakobo alimpenda sana Raheli  hadi kukubaliana  na Labani afanye kazi miaka Saba (7) ili apewe Raheli kama Mke,Miaka saba inaisha hadi inafika Miaka kumi na nne (14) ndio Raheli anakuja kumpata Mumewe baada ya kumgojea miaka kumi na nne (14) kutokana na siasa za Baba yake Mzazi , Ila alifanikiwa kuolewa na kuwa Mke wa pili wa Yakobo.

Mpendwa yamkini kwenye familia yenu kuna changamoto za magonjwa, shirki, umaskini, wazazi watata, na vikwazo vingine vinavyofanya usifikie lengo lako la kuwa Mke, Mungu wetu aliye juu akuinulie Yakobo wako atakayekuvumilia changamoto zote hizo hata ikimchukua muda mrefu akufanye Mke.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top