Ufufuo ni dhana inayogusa moyo wa kila mmoja wetu. Tunaona mzunguko huu wa maisha na kifo kila mahali tunapogeukia, kutoka katika ulimwengu wa mimea hadi kwa maisha ya binadamu. Lakini Je, Tutaonaje Ufufuo katika changamoto zetu za maisha kama ufufuo wa Kazi / Mahusiano/ Uchumi na Ndoa zetu zinazo tutatiza? Tufatilie kwa Pamoja :
Day 1 : Ufufuo Program
Yohana 11:41
“Basi, wakaitoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.”
Sala
Baba tunashukuru kwa kuwa unatusikia,Tunashukuru kwa kuweza kufanya Programu hii. Aidha tunakushukuru kwa majibu uliyo yaachilia kutokana na programu hii. Kwa Jina la Yesu Tunaomba.
Ezekiel 37 : 1 -10
1 Mwaka wa ishirini na tano wa utumwa wetu, hapo mwanzo wa mwaka, siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa nne, neno la Bwana likanijia, kusema,2 Mwanadamu, mfanye mfupa uwe wazi; nami nitaweka nyama juu yake, na kuifunika ngozi, nami nitatia roho ndani yenu, nanyi mtakuwa hai; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.
3 Basi nikaingia, nikaingia kati ya mifupa hiyo; na tazama, palikuwapo mifupa mingi porini, imekaushwa sana.4 Kisha akaniambia, Mwanadamu, je! Hawa mifupa watakuwa hai? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wewe wajua.5 Ndipo akaniambia, Haya, tabiri juu ya mifupa hii, ukawaambie, Enyi mifupa miovu, lisikieni neno la Bwana.6 Bwana MUNGU asema hivi kwa hizi mifupa, Tazama, nitatia roho ndani yenu, nanyi mtakuwa hai.
7 Nami nitaweka mishipa juu yenu, na kuotesha nyama juu yenu, na kuifunika ngozi juu yenu, nami nitatia roho ndani yenu, nanyi mtakuwa hai, nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.8 Basi nikatabiri kama nilivyoamriwa; na hata nilipotabiri, sauti ikatokea, na tazama, kulikuwa na mshindo mkuu; mifupa ikakaribiana na mifupa.
9 Nikatazama, na tazama, kulikuwa na mishipa juu yake, na nyama ikaota, na ngozi ikafunika juu yake juu, lakini roho haikuwa ndani yake.10 Kisha akaniambia, Tabiri roho; tabiri, mwanadamu, ukawaambie hawa roho, Bwana MUNGU asema hivi, Njoo kwa roho, toka pepo, ukaiingilie hii mizoga, ukaifanya iwe hai.
11 Ndipo nikatabiri kama nilivyoamriwa; na roho ikaingia ndani yao, nao wakaanza kuwa hai, wakasimama kwa miguu yao; ni jeshi kubwa mno sana.12 Ndipo akaniambia, Mwanadamu, hawa mifupa ni nyumba yote ya Israeli. Tazama, wanasema, Mifupa yetu imekaushwa, na tumaini letu limepotea; tumekatiliwa mbali kabisa.
Prayer Points 3
1. Enyi Mifupa mikavu, Ya Mahusiano yangu/ kaz.i yangu/ Uzao / Uchumi au Changamoto yako sikilizeni neno la Mwenyezi- Mungu.sikilizenni neno la Mwenyezi- Mungu. 5 Bwaba Mwenyezi-Mungu awaambia hivi : Nitaifanya pumzi iwaingie, nanyi mtaishi.6 Nitawatia mishipa na nyama, nitawafunika ngozi na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. Hapo mtajua kuwa mimi ni Mwenyezi- Mungu
2. Bwana Mwenyezi – Mungu anasema hivi : Ewe upepo njoo kutoka pande zote nne na puliza Mahusiano / Uchumi/ Afya na Uzazi/ ( Changamoto yako !) iliyokufa ili ipate kuishi.
3. Ee Mwenyezi Mungu funua makaburi yangu yote na kufufua toka kaburini kazi yangu/ Mahusiano yangu/ Uzao wangu/ Ndoa yangu. Nirudishe Nyumbani kwako katika nchi ya Israeli.
Kwa kuwa mimi mtu wako nimetambua kuwa wewe ni Mwenyezi Mungu!. Funua kaburi langu na fufua mahusiano/ kazi/uchumi/ ndoa na vyote vuyang vilivyoporwa na adui! Tia roho yako ndani yangu nami nitaishi. Hapo nimetambua kuwa wewe Mwenyezi Mungu umesema, nawe utafanya hayo. Wewe Mwenyezi Mungu Umesema.
Maelekezo Muhimu
- Rudia somo hili angalau mara tano (5)
- Na katika uwepo wa kusifu na kuabudu utarudia hizi PRAYER POINTS Tatu (3).
Day 2 : Ufufuo Program
Yohana 11:25-26
“Yesu akamwambia, Mimi ndimi ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi. Na kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki haya?”
Mpendwa katika programu hiii unatumia akili nyingi kwani kuna Password ( Siri ) nyingi zimo katika maandiko. Hii ni moja ya Mistari ambayo huwezi kuelewa kwa kuipitia juu juu lazima ufahamu chimbuko lake lililoko nyuma sana , na kwa ufupi ilikuwa ni katika context ya Yesu kumfufua Lazaro.
Yesu alikuwa anaongea na Martha ( Na Martha alikuwa kama wewe mpendwa alifahamu ufufuo upo kabisa , lakini ni siku za mwisho ) yaani Parapanda na ndio fikira za wengi wetu.
Bwana Yesu alimfafanulia Martha na Anakufafanuia pia wewe Mpendwa jioni ya Leo.
Yohana 11 : 25
“Yesu akamwambia, Mimi ndimi ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi.”
Mpendwa alichosema Yesu ni kweli, Vitu hufa kwenye maisha ya Mtu , Watu Hufa Pia. Hamna jipya katika hiki hakika Kifo ni sehemu ya Maisha ya Mwanadamu na kuna vifo vya aina nyingi lakini vimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Vifo vya Kiroho na Vifo vya kimwili . Lakinipia vifo vifo vingine kama vifo vya hisia, vifo vya maono, vifo vya mipango ,vifo vya ndoto , vifo vya mahusiano etc.
THE GOOD NEWS, BWANA YESU ANASEMA YEYE NDIO UFUFUO NA UZIMA, MTU AKIMWAMINI YEYE HATA AKIFA ATAISHI TENA!
Hivyo Mpendwa haijalishi changamoto yako ( Kifo chako ) ni cha aina gani ,kimetokea mwaka gani na kimekutesa kwa kiasi gani, Hakika nipende kukwambia “YESU NDIYE UFUFUO WAKO NA UZIMA”
Na ukimuamini sasa hivi hizo changamoto zako ( Vifo vyako ) katika Mahusiano/ Uchumi/ Uzao/ Afya/ Ajira vitaishi tena. Aidha ukiishi katika kuamini hautokufa tena.
Prayer Points 3
- Bwana Yesu natambua wewe ni UFUFUO na UZIMA, naomba ufufue mahusiano yangu, Ajira yangu, uchumi wangu, Afya na maeneo yote yaliyokufa kwenye maisha yangu.
- Bwana Yesu nakuamini kama wewe ndio UFUFUO na UZIMA na naamini kwa kukuamini wewe changamoto zangu katika Mahusiano/ Uchumi/ Ndoa/ Afya/ Uzao/ Etc. vilivyo kuwa vifo katika maisha yangu vitaishi tena kupitia wewe Bwana.
- Bwana Yesu safari hii nitakuamini moja kwa moja na viivyofufuka kupitia wewe vitadumu milele havitakufa tena.
Maelekezo:
Mpendwa Sali kupitia Point hizi kwa kiwango na wingi unao weza hakika changamoto zako zitafunguliwa.
Day 3 : Ufufuo Program
Isaya 25 : 8
“Naye atameza mautini milele, na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na kufuta aibu ya watu wake katika dunia yote; kwa kuwa Bwana amesema.”
Mpendwa huenda unapitia nyakati ngumu , Changamoto zako zinakutatiza sana umeomba lakini hupati majibu , nipende kukutia nguvu kuendelea na vita ya maombi kwani Bwana anasema kupitia neno hili kuwa ata-angamiza vifo vyetu milele, atatufuta machozi katika nyuso zetu na kutuondolea aibu.
Mpendwa kifo siku zote hufuatiwa na aibu kubwa ambayo husababisha machozi na huzuni kubwa mfano kifo cha mahusiano yako kinaweza kusababisha watu wakuone unaupungufu fulani, huna bahati au huna nyota ya kupendwa kabisa, Japo moyoni unafahamu haya mambo yote hayana ukweli wowote, na ukiwaza na kufikiria inakuumiza na kukusononesha sana.
Huenda kifo cha Career yako kimesababisha uishi maisha ya aibu, imefikia kipindi umekuwa mpole na muelewa lakini ni kwasababu huna jambo la kufanya, unaishi kwa aibu. Re-Union za shule huendi, hadi Gathering za Classmates unaskip yaani unaishi maisha ambayo hayakuwa mpango wako.
Mpendwa haijalishi ni hhali gani unaipitia ( Whatever Situation ) au unaona mabo yako yanakufa, huna matumaini tena na unaona kubakia kwa uzuni na machozi maishani mwako. Mungu amesema kupitia andiko hili la Isaya 28 : 5 kuwa atakiangamiza kifo milele, atafuta machozi katika nyuso za watu wote na kuwaondolea watu wake aibu duniani kote.
Mpendwa Mungu atakiangamiza kifo hata kwenyechangamoto yako, atakufuta machozi na kukuondolea aibu.
Prayer Point 3
- Bwana angamiza kifo cha mahusiano yangu, uchumi wangu, afya yangu , uzazi wangu n.k sawasawa na neno ulilolisema kupitia nabii wako Isaya.
- Bwana nifute MACHOZI yangu na kuniondolea huzuni.
- Bwana niondoleee aibu zangu zote.
- Kwa kuongezea : Bwana fanya jambo jipya juu ya mahusiano yangu, uchumi wangu n.k na jambo lako lionekane
In the might name of Jesus I pray !
Day 4: Ufufuo Program
Isaya 49 : 15
“Lakini Mungu ataikomboa nafsi yangu kutoka kuzimu, kwa maana ataniokoa. Amenihifadhi salama, ili nisipate kuanguka shimoni.”
Psalm 49 : 15
15 But God will redeem me from realm of the dead; he will surely take me to himself.
Hapa Mzaburi anazungumzia realm of the dead ( Kufufuliwa au kuondolewa katika ulimwengu wa wafu ) ,Zaburi hii iliandikwa na Sons of Korah ! ukitulia na ukatafakari utaona mzaburi kuwa yupo hai, ndio maana akaandika zaburi hii.
Mpendwa kumbe unaweza kuwa hai lakini mambo yako hayaendi kwa kuwa umehifaziwa katika ulimwengu wa wafu.
Mzaburi anamsihi Mungu amuokoe kutoka realm of the dead ( Ulimwengu wa Wafu ) , na ampokee kwenye ulimwengu wa watu wake.
Prayer Point hapa ni moja tu :
God redeem me from the realm of the dead, niokoe na wafu wa mahusiano, wafu wa uchumi, wafu wa afya , wafu wa ajira n.k na unichukue kwako katika ardhi ya wanaoishi. Yafanye mahusiano yangu, uchumi, ajjira, ndoa etc. kuwa hai tena kwa jina la Yesu.
Day 5 : Program ya Ufufuo
Job 14 : 14 – 15
“14 If a man dies, shall he live again? All the days of my service I would wait, till my renewal should come. 15 You would call, and I would answer you; you would long for the work of your hands.”
Ayubu 14 : 14 – 15
“Naye akifa mwanadamu, je! Atakuwa hai tena? Mimi nitalingojea siku zote za vita vyangu, hata badilike hali yangu. Wewe utaniita, nami nitakuitikia; utaiona kazi ya mikono yako.”
Andiko hili liliandikwa na Ayubu akiwa hai. akini alikuwa anapitia mazito. Yuko hai lakini aliwaza kama mtu anayekufa kutokana na changamoto alizokuwa anazipitia. Wapendwa tukirudi nyuma kidogo katika mstari wa 14 ( Ayubu 14 : 13 ) neno linasema ” 13 Laiti ungenificha kuzimuni, Ukanilinda kwa siri, hata ghadhabu zako zitakapopita, na kuniandikia muda ulio-amriwa, na kunikumbuka!”
Job 14 : 13 – 15
“13 if only you would hide me in the grave and conceal me till your anger has passed ! If only you would set me a time and then remember me”
Ayubu anawaza kama ingewezekana kama Mungu angemficha kwenye kaburi, na kumkinga mpaka hasira yake ipite. Mpendwa Ayubu anajaribu kuwaza kama Mungu angemtaarifu kuwa atateseka kwa kipindi gani hadi kukumbukwa, haya ni mawazo ya ayubu katika hali ya ubinadamu kama mimi na wewe hasa wakati tunapopitia kipindi kigumu au changamoto.
MPENDWA AYUBU YUKO HAI LAKINI MAMBO YAKE MENGI YALIKUFA YAKIMUACHA AKIWAZA TU KIFO NA MAKABURI.
Ayubu anamuomba Mungu ikiwezekana amfiche kaburini, lengo ni asitirike. Mfu wa mambo hana stara anadharirika mwanzo mwisho.Mpendwa aibu yako ni yako mwenyewe.
Ayubu anapima changamoto yake na kaburi anaona bora kaburi kwani changamoto kama zake hazina muda elekezi kwa kuisha. Ayubu anafikia kiasi cha kumuuliza Mungu , JE MTU AKIFA ANAISHI TENA ?
Swali hili nila msingi sana Mpendwa kwani Ayubu aliona jinsi mambo yake yalivyokuwa yamekufa kabisa ilihali anamuamini Mungu Sana lakini Mambo ya Ayubu hayakuwa mazuri kabisa. ikambidi Ayubu apime na kujiuliza sana JE NITARUDIA UTUKUFU WANGU KWELI ?, JE MTU AKIFA ATAISHI TENA KWELI ?
Mpendwa Ayubu hayuko peke yake katika hili swali. Najua kuna wengi kati yetu wanaojiuliza JE HAYA MAHUSIANO NITAVUKA KWELI NA UMRI HUU ?, AGE COUNT NI 35 , BREAKUP NI ZA KUTOSHA MAUMIVU NA KUKATISHWA TAMAA NI VYA KUTOSHA. NITAVUKA KWELI ? HAYA MAHUSIANO YATAISHI KWELI NA KURUDIA TENA UTUKUFU WAKE?.
Mpendwa huenda unajiuliza sawa tuko Day 5 ( Siku ya Tano ) lakini huoni utukufu katika changamoto yako ya kazi. JE KAZINI UTAENDA KWELI ?, KWELI UTAKANYAGA KUTA ZA OFISI ? , JE UTASIGN PAYROLL ? AFTER ENDLESS JOB SEARCH KWA MIAKA 15! NOT SELECTED KWENYE ORAL INTERVIEW. JINA HALICHAGULIWI KWENYE ORODHA ZA UTUMISHI NA BINAFSI. UMEOMBA UMETOA SADAKA LAKINI HUPATI MAJIBU KABISA.
Mpendwa nipende kukusihi siku hizi saba zikipita kama Mungu aishivyo utaingia kwenye Payroll na Career Mfu yako itaishi tena na kurudia utukufu wake.
Ayubu 14 : 14 – 15
Siku zote za kazi zangu ngumu nitangojea kufanywa upya kwangu. 15 Utaniita nami nitakuitikia.
Ayubu anasema, Siku zote za huduma ngumu, atangoja Kufanywa upya kwake. Halleluyah!!! Ayubu hajakubaliana na hali anajua Mungu lazima ipo siku Mungu atamuita na yeye atamuitikia. Lazima ipo siku Mungu atafanya jambo jipya kwenye maisha yake.
Mpendwa hata wewe Mungu atakuita na wewe utamuitikia, atakukumbuka, atakufanya mpya na kufanya jambo jipya kwenye maisha yako.
Prayer Points 3
- Remember me Lord, Weka ukomo wa ufu wa mahusiano/ kazi/ajira/afya na uzao. Remember me Ooh Lord.
- Niite Bwana nami nitakuitikia, Nifanye Mpya eeh Bwana, ambaye hata teseka na kuaibishwa na Mahusiano/kazi/ajira/afya/Uzao/Ndoa etc.
- Fanya jambo jipya juu ya mahusiano yangu/kazi/biashara/uzao/afya/ndoa na lionekane kwa macho.
Day 6 : Ufufuo Program
1 Wakorintho 6 : 14
14 Mungu alimfufua Bwana na atatufufua na sisi pia kwa uwezo wake.
1 Corinthians 6 : 14
By hhis power God raised the Lord from the dead and he will raise us also.
Mpendwa neno hili linaonesha kuwa kuna Power / Nguvu nyuma ya Ufufuo na Nguvu hio ni ya Mungu.
Mpendwa shida sio Mungu au Nguvu ya Mungu au Ufufuo. Shida ni Je, unaamini kuwa Mungu ana nguvu /power ya kukufua katika hilo eneo linalokutatiza? Unaamini kuwa Mungu ananguvu?. Huenda unapitia wakati wa mashaka unawaza Je kweli Mungu nguvu za kufufua anazo?, Je kipindi unapobaki katika waiting list yake atatumia nguvu zake muda huu kukuokoa ?, Nikusihi mpendwa Mungu atatenda kwa kuwa ni mwaminifu sana na atajithibitisha kwako.
Prayer points 3
- By the powers you raised christ from the dead, Fufua Mahusiano yangu, Fufua ajira yangu, uchumi wangu , uzao wangu, umiliki wangu na viwe hai tena,vionekane kwa jina la Yesu.
- Bwana tenda jambo jipya juu yangu na lionekane kwa macho.
- Bwana unithibitishe na kwangu pia mara hii tu Bwana.
Day 7 : Ufufuo Program
Zaburi 103 : 1 – 5
Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi Mungu, nafsi yangu ilisifu jina lake takatifu!, usisahau kamwe wema wake wote.Ndiye anaye nisamehe uovu wangu wote, na kuniponya magonjwa yangu yote.Ndiye aniokoaye kutoka kifoni, na kunijalia rehema na fadhili zake. Ndiye anayeniridhisha mema maisha yangu yote, hata nabaki kijana mwenye nguvu kama tai.
Wapendwa kumshukuru Mungu wakati mambo yako yanaenda ni rahisi, lakini wakati mambo hayaendi inataka moyo sana. Kuna wakati nafsi inakwambia sasa unashukuru nini ? na ukingalia kwa haraka haraka hakuna cha kushukuru kweli. Lakini shukrani yako mpendwa na mtu aliyevuka tayari zinautofauti sana. Yeye aliyevuka au kufanikikiwa anashukuru kwa alichokiona tayari. Ila wewe mpendwa unashukuru kwa sababu unamjua Mungu ni nani,anaweza nini na una imani naye kiasi gani.
Yesu katika hali zote zilizobana sana alikuwa haombi, alikuwa anashukuru tu. Mfano kwenye ule wakati wa watu 5000 na chakula kidogo , angeweza kusali lakini ingechukua wakati mrefu sana ila Yesu alitazama mbinguni na kushukuru tu na muujiza wa Mungu ukafanyika watu wakala na kusaza.
Paulo na Silas walisifu na kuabudu milango ya gereza ikafunguka. Mpendwa Paulo na Silas walikuwa jela sio kwasababu ya uovu na dhambi bali mahubiri ya injili lakini hawakususa sababu ya Mungu kuwaacha , Mbona yuko kimya, Kwanini tunakaa gerezani. Yamkini walihisi hivyo mioyoni lakini hawakujiendekeza wakaona na chochote kitokee. Kama Duniani tumeshindwa ni bora tushindwe lakini ni heri kushindwa duniani na sio mbinguni, wakaongeza nguvu na kuendelea kusifu na kuabudu hadi milango ya gereza ikafunguka.
Mpendwa ni vema mambo yako ukayaweka pending kwanza, muda wa kujisononesha siku baada ya kesho upo wa kutosha ,Ila kwa kesho Sifu , Abudu na Mshukuru Mungu. Mpendwa kumbuka hiyo changamoto yako Mungu anaweza kuitatua, huna haja ya kughazabika wala kukosa raha kwani Mungu mwenyewe ameshajithibitisha kwako ni suala la muda mambo yata manifest.
Usifanye kosa la kumtilia mashaka Mungu kesho,ukafanya changamoto zako baada ya kesho kuanza kutokea na kuishia njiani kwani hata ibada yako uliishia njiani yaani umemla ng’ombe mzima na mkia ukushinde.Mpendwa mambo mengi yanatokea wakati wa KUSIFU na KUABUDU kwa moyo wa shukrani.
Mpendwa hatakama nafsi yako inaleta ugaidi. Usijiendekeze kamilisha program hii mpaka mwisho hivyo hivyo sala zako zikamilishe hadi mwisho, utapata matokeo.
1 Wathesalonike 5 : 24
Yeye anayewaita nyinyi atafanya hivyo kwani ni mwaminifu.
1 Thessalonians 5 : 24
24 The one who calls you faithful, and he will do it.