TUNATAKIWA KUMTUMIKIA MUNGU — SIYO MUNGU KUTUTUMIKIA SISI!, WALA SISI KUTUMIAKIANA NA MUNGU

Yesu na manabii wote waliotangulia walifundisha jambo moja kuu: Kumfanyia Mungu ibada ya kweli, ya kila siku. Walifundisha kwa bidii namna Mungu anavyotaka atumikiwe — siyo kwa namna yetu sisi, bali kwa namna Yake.

Lakini leo hii watu wengi wamepotoshwa kabisa. Wanataka Mungu awatumikie wao! Subhanallah! Kabla hujajitenga na hoja hii ukisema “Haitakuwa mimi,” hebu jichunguze upya… Inaweza kuwa wewe tayari!

Leo mtu anasema:
“Mimi sitaki wokovu, nataka Mungu anipe kazi!”
“Mimi sitaki kuokoka, nataka Mungu anipe mume!”
“Mimi sitaki kujihusisha na mambo ya dini sana, nataka tu watoto!”

Anakuambia:
“Mtumishi, wewe omba tu! Maadamu unanena, mambo yaje!”

Lakini ukweli ni huu: Hutapata chochote kwa namna hiyo! Kwa sababu msingi wa kile unachoomba hauko sawa. Hauko katika maandiko. Na bila maandiko — hakuna matokeo.

 

MUNGU HAJAWAHI KUJITOA KUWATUMIKIA WASIOMTUMIKIA!

 

Hakuna sehemu yoyote kwenye Biblia ambapo Mungu aliahidi kuwasaidia wale wanaomkimbilia ghafla tu kwa shida zao bila kumtumikia. Lakini yule yule Mungu ameahidi mara nyingi kuwa pamoja na, kuwatunza na kutowatelekeza wale wanaomtii na kumtumikia.

Swali la msingi ni moja tu:
👉 Je, unamtumikia Mungu au humtumikii?
Maadamu humtumikii, kamwe hutashiriki katika ahadi zake wala thawabu zake.

 

UTUMISHI WA KINAFAKI – HAUJENGI!

Wengi wanakuja kwa watumishi wakiwa na shida, wanapewa maombi, wanafanikiwa. Lakini badala ya kumshukuru Mungu na kuendelea kumtumikia, wanachofanya ni kuwasambazia wengine yale maombi — hata ndugu zao ambao hawana msingi wowote wa kiroho.

Wewe unajua fika ndugu yako hajawahi hata kutoa zaka, hajawahi kusali, hajui maandiko, lakini unataka nimfanyie huduma ile ile kama yako? Haiwezekani! Ni upendo kujaribu kumsaidia, lakini kiroho hana sifa ya kupokea hiyo huduma.

 

2 thoughts on “TUNATAKIWA KUMTUMIKIA MUNGU — SIYO MUNGU KUTUTUMIKIA SISI!, WALA SISI KUTUMIAKIANA NA MUNGU”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top