
BREAKTHROUGH III IWE HALISI INAHITAJI NAFSI 3 KUWEZA KUPITISHA MAJIBU YAWE HALISI.
- Lazima kwanza mtu aamini katika Mungu na mbingu kwa ujumla.
- Lazima mtu aamini katika vessels / watu Mungu anao watumia kupitisha upako na majibu.
- Lazima wewe unae ngoja majibu uwe tayari.
- Kikipwaya kimoja tuuu hapo hamna matokeo wala mjukuu wa matokeo.
Wapendwa sio kwamba watu hamuombi au hamjitutumui kufanya ibada lakini mambo madogo madogo kama haya yanakausha mafuta na kuwaacha mme kata tamaa kwa kukosekana majibu.
-
Lazima uamini katika Mungu na uamini Mungu atafanya hiko kitu.
Hebrews 11:6
But without faith it is impossible to please him: for he that cometh to God must believe that he is, and that he is a rewarder of them that diligently seek him.
Nimesha cover sanaa kwanini watu wengi hamuamini kwamba Mungu atafanya.
Leo focus na una aminije Mungu atafanya?
- Sikiliza ushuhuda wa watu waliofanyiwa uta kujenga sanaa.
- Soma maandiko ujionee kazi za Mungu. It will be hard for you to doubt His abilities.
- Lazima uamini katika vessel / watu Mungu atakao watumia.
Wengi tunapenda ku deal na Mungu moja kwa moja lakini sio rahisi. It requires years of training and learning.
Nabii Samweli akiwa mtoto chini kuhani Eli, Mungu anamuita anakimbilia kwa nabii Eli kuitika. Mara tatu Eli anamwambia mbona mimi sikukuita? Sababu Eli ni mkomavu anamwambia akikutana tena itika hivi! Ndo Samweli akili inamfunguka.
1 Samuel 3:1–10
The boy Samuel ministered before the Lord under Eli. In those days the word of the Lord was rare; there were not many visions.
One night Eli, whose eyes were becoming so weak that he could barely see, was lying down in his usual place.
The lamp of God had not yet gone out, and Samuel was lying down in the house of the Lord, where the ark of God was. Then the Lord called Samuel. Samuel answered, “Here I am.”
And he ran to Eli and said, “Here I am; you called me.” But Eli said, “I did not call; go back and lie down.” So he went and lay down.
Again the Lord called, “Samuel!” And Samuel got up and went to Eli and said, “Here I am; you called me.” “My son,” Eli said, “I did not call; go back and lie down.” Now Samuel did not yet know the Lord: The word of the Lord had not yet been revealed to him.
A third time the Lord called, “Samuel!” And Samuel got up and went to Eli and said, “Here I am; you called me.”
Then Eli realized that the Lord was calling the boy. So Eli told Samuel, “Go and lie down, and if He calls you, say, ‘Speak, Lord, for Your servant is listening.’”
So Samuel went and lay down in his place. The Lord came and stood there, calling as at the other times, “Samuel! Samuel!” Then Samuel said, “Speak, for Your servant is listening.”
Wengi mnadandia vitu ukubwani na mnataka kuvi operate kwa imani za kubumba bumba. Matokeo yake mnakwama padogo sanaa mnaishia njiani.
Mnataka kupaa kabla ya kutambaa. Na mkipaa kama ndege za kubet mnaishiwa mafuta kati kati ya anga na kuporomoka. Wakati ilikuwa issue ndogo tu ya kushupaza fuvu kidogo tu na kuongea na sisi wakubwa zako tukupe password za kuongeza mafuta juu kwa juu.
Mimi naongoza watu hapa kila siku. Mtu anafanya deliverance anapata mtu, akipata tu mtu ananikata. Asilipe zaka. Safi sana na mimi sikanipunguzia kazi. Wanaenda sehemu ndogo tu anamkosa yule mtu. Attack ndogo ndogo tu za mashangazi kwa vifungo vyepesi sanaa. Anarudi kule kule alipoanzia.
Wengine wanabakia na mtu dakika 2 anaoa dakika 2 hao! Sasa si upo na sterling sitishwi nyau mimi na nguvu za giza. Nakwambia acha wogaaa! Hili limeishaaa! Pita huku! Fanya hivi! Tokea kule! Mpaka mambo yanakaa sawa. Ahadi za Mungu lazima zitimie kwako mja wake. Hata wazibe vipi if you have the stomach for it tunatimiza.
Kuna bibi harusi wangu ndoa ina miezi 3 mwanaume jogoo hawiki kwa mkewe. Afu binti mdogo sasa anaishije bila mambo hayo?
Sisi age go tunaishi sanaa tu! Hormones zenyewe zishaanza kukauka mwilini. Mavazi yashaanza kuisha. Binti mdogo 20 na kitu anaishije bila vile vituu? Harusi haina miezi 6?
Kaja hapa jambo tukalimaliza week hio hio! Ndoa ina miaka 2 na mambo lele lele. Na mjukuu nishapata. Ndoa inaachaje kujibu? Ndoa ilitoka kwa Mungu?
Mwingine walimwambia hatozaa! Wakaapa! Ana zaa kama kuku! Kila mwaka! Nimemkanya ndoa za sasa kwa umri wake watoto wa 2 wanatosha! Akae kwanza miaka hata 5 kama mwanaume bado yupo kwenye mstari ndo aongeze. Nyota ya kijani muhimu. Lakini uzazi wa paka umepitwa na wakati. Kikazi walimfunga kweli ila nimemfungua. Sio kujua tu principles za ulimwengu wa roho.
Wengi hampendi kuwaamini watumishi. Hampendi kuwalipa stahiki zao halali za kimaandiko walizopewa na Mungu. Mnapenda huduma za bure bure. Shetani kawashika hapo kwenye ubahili. Pesa unayo lakini unateseka nayo.
Kwa urefu wa pesa yako ulitakiwa uwe una hudumiwa na maaskofu tuuu. Lakini unaokota watumishi waliochoka hatari ili usigharamike. Ukiambiwa kuna mtumishi unauliza ana gharama kubwa?
Ana gharama kubwa sababu anajua thamani yake na ananua anachofanya.
Ubahili mtu anaamua nitaomba mwenyewe na Mungu atanisikia tu vile vile! Ni kweli! Lakini itakuchukua miaka 10 iliyowachukua watumishi ku master neno la Mungu. Do you have 10 yrs?
Kwenye bonde la mifupa mikavu Mungu alimtafuta nabii Ezekiel aje aprophesy! Ndo muujiza ukatokea wa ile mifupa kuishi kuwa jeshi kubwa sanaa.
Kuwatoa Waisrael Misri Mungu alimtafuta Musa!
Hosea 12:13–14
And by a prophet the Lord brought Israel out of Egypt, and by a prophet was he preserved.
Afu wewe mmoja unataka uwe delivered kutoka huo upweke bila nabii bila maandiko na Mungu ndo afanye hiyo deliverance ya mchongo vile vile.
How far my dear daughter? Miaka inakimbia hatari lakini progress = 0! Your life your choices.
Modus operandi ya mbinguni inataka nabii lazima asimame hapo kati kupitisha upako. Hawataki ku deal na mtu mbabaifu anae baluzaa baluzaa vitu.
Mungu hajaweka utitiri wa watumishi kimakosa. Ni kukupa wewe options na gubu lako. Yaani hata uchague vipi na kubagua usikose nabii wa kukamilisha tripartite ya wewe kupata breakthrough.
God works through the hands of men. If you ignore these men hapo sasa umeshindwa wewe tena.
Wengi mnakua mpo vizuri ila hamna manabii wazuri au hamna kabisaaa. Matokeo yake mnafanya mambo kama vipofu kwa kupapasa na kubahatisha. Kipofu hawezi kumuongoza kipofuu.
Mna jua hata mtu wa kukwambia unakoseaaa ni bahati. Asikuinue wala asikutie moyo. Akuambie tu unakoseaaa. Amekufungua macho na kukuokolea muda.
Lakini ukienda mwenyewe mpaka ujikwamie ndo ujue hiyo sio njia. Utafika kweli?
2. Muumini uwe tayari.
Mungu anaweza kuwa yupo tayari na mtumishi kajipanga hatarini lakini wewe ukiwa mbabaifu hakuna biashara ya matokeo yoyote.
Na sio uwe tayari kwa matokeo, uwe tayari kuyafanyia kazi kupatikana kwa hayo matokeo. Hamna ambaye hayupo tayari kwa matokeo ya bure bure. Kuyafanyia kazi ndo wengi hampotayari.
Mimi binafsi nimewapa mikeka ya deliverance watu miezi 6 na wamefunga kweli na wamechoka kufungwa kwa hili nawatetea. Ila kunyoosha kusoma hiyo mikeka na kuiomba miezi 6 consecutively ndo wameshindwa.
Yakobo 2:17
Vivyo hivyo, imani peke yake bila matendo imekufa.
Utayari unataka matendo na matendo yaliyo nyooka.
Mimi nikikupa maombi ukiomba najua na usipoomba najua. Kwanza naweka mitego naruka mtiririko maksudi kama kweli unaomba utaona na utauliza mbona hapa umeruka?
Pili ukiomba japo mwezi tu ile back to back lazima nguvu za giza zitareact na mambo yataanza kutokea kwenye maisha yako na utanuliza nitajua kwanini.
Wewe miezi 6 hamna kilichotokea na hata ile error hujaiona. Najua hamna muumini hapa. Nakupa tu zaka ya bure.
Na kinachokufanya ukae mwezi au miezi wala usiombe ni sababu huamini. You don’t believe my dear.
Either uijue modus operandi ya mbinguni na unyooke nayo au ukose matokeo kwa ubabaifu wako.
Mark 11:24
Therefore I tell you, whatever you ask for in prayer, believe that you have received it, and it will be yours.
Hii ndo modus operandi ya maombi.
- You ask in prayer.
- You believe first.
- Receiving and having.
After believing receiving and having comes automatically kama move ya Mungu kujithibitisha kwako baada ya kumuamini.