Yohana 14 : 16
Nami nitamwomba Baba, naye atawapa msaidizi mwingine ili akae nanyi hata milele.
Yohana 14 : 26
Lakini huyo msaidizi, huyo Roho Mtakatifu amabaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha yote na kuwakumbusha yote niliyo waaambia.
Yesu anaona kabisa siku akiondoka duniani mitume na sisi wengine bila Roho Mtakatifu hakuna atakayeweza kufika popote.Hata Wanafunzi wake yamkini waliwaza sana mwalimu kaondoka itakuwaje? kwani Yesu alikuwa ni Mungu, Mwenye Nguvu, Mkamilifu na Mtu wa Busara. Yesu aliona kabisa watu hawa kwa wingi wa udhaifu wao nisipowapa msaidizi Mwovu atawavuruga.Hivyo Yesu ana-ahidi kumuomba Mungu atupe Roho Mtakatifu akae nasi milele na Yesu anagusia tena huyo Roho Mtakatifu atawafundisha yote na kukumbusha yote Yesu aliyosema.
Je Roho Mtakatifu nikimuhitaji Leo hii, Saa hii nampata vipi?
Luka 11: 13
Basi, ikiwa ninyi mlio waoviumnajua kuwaa watoto wenu zawadi nzuri, Je, Baba aliyembinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?
Hivyo kumbe huwezi kumpata Roho Mtakatifu kama bahati tu au ikatokea tu Roho Mtakatifu akakufata, Kwani neno liko wazi Mungu atawapa Roho Mtakatifu hao WAMWOMBAO. Hivyo ndiyo lazima muwe wana maombi na Muombe msaada wa Roho Mtakatifu.
Je Roho Mtakatifu anakaa wapi?
1 Wakorintho 3: 16 – 17
Je, hamjui kwamba ninyi ni hekalu la Mungu na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Basi, Mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu; Maana hekalu la Mungu ni takatifu na hekalu hilo ni ninyi wenyewe.
1 wakorintho 6: 19 SRUV
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu,mliyepewa na Mungu? Wali ninyi si mali yenu wenyewe.
Wapendwa hivyo Roho Mtakatifu tayari yupo ndani yetu. Sio wa kumtafuta.Yupo ndani yako anakwangalia tu unavyofanya uasherati, unavyosengenya, hajibani kwa dhambi.Lakini ili uwe na uhusiano na Roho Mtakatifu inatakiwa kwanza uwe msafi wa roho na mwili,Utunze hekalu la Roho Mtakatifu.Huwezi kukuta mtu mlezi ,mzinzi au mhuni anajazwa Roho Mtakatifu.
Je Roho Mtakatifu anakusaidia vipi? na ukiwa na uhusiano na Roho Mtakatifu unafaidika vipi?
1 Wakorintho 12 : 4 – 11
Basi kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni mmmoja.5 Pia kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni mmoja.6Kisha kuna aina tofauti za kutenda kazi, lakini Mungu ni yule yule anayeongoza kazi zote kwa kila mtu.7.Roho mtakatifu hudhiihirishwa kwa kila mtu kwa faida ya wote.
Maana mtu mmoja hupewa neno la hekima na huyo Roho, na mwingine hupewa neno la ufahamu kutoka kwa Roho huyo huyo.9 Mtu Mwingine hupewa imani na Roho huyo na mwingine hupewa karama ya kuponya.10.Huyo huyo Roho humpa mwingine uwezo wa kufanya miujiza, mwingine unabii, nwingine uwezo wa kutofautisha kati ya roho mabalimbali, mwingine aina za lugha, mwingine uwezo wa kutafsiri lugha.11Lakini Roho huyo huyo mmoja anayefanya haya yote, naye hugawa karama kwa kila mtu, kama yeyey mwenyewe apendavyo. Hivyo wapendwa kila mtu anakitu chake ambacho Roh Mtakatifu anampa kadri yeyey atakavyoona hata wewe kijenga mahusiano na Roho Mtakatifu atakupa kitu chako.
Unajengaje Mahusiano na Roho Mtakatifu?
- Tambua uwepo wake kwenye maisha yako.kama unavyotambua uweppo wa Mungu Baba na Yesu Kristo.Dont Sweat it or Doubt it.Yesu aliahidi Mungu ataleta msaidizi atakaye kaa na sisi.Sasa msaidizi huyo ndio huyu.
- Tambua nafasi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya mtu yeyote. Siku zote Roho Mtakatifu ni kiongozi lazima ukubari na uridhie yeye ndiyo akuongoze. Sio mnajadiliana kila hatua, no power games, No power struggle. Akisema mkesha sema ndio Boss. Itii sauti yake na utaona ukuu wake. Sometimes anakupa maelekezo matata sana, ila yatii.Anaweza kusema furahi tuu juu ya tatizo lako, na utashagazwa sana ila tii.
Nafasi nyingine ya Roho Mtakatifu ni mshauri. Una muuliz mambo yako anakushauri. Mfano unaweza kumuuliza Hivi hapa ninavuka vipi?, Hivi huyu Binti unamuonaje au tunapigwa? Mimi mbona sioni Mume wangu anacheruka vipi wewe unaona kitu?.Mpendwa unaweza kushangaa mtu anapiga simu anakwambia usiku nimemwona mumeo wankunywa pombe mpaka saa tisa usiku au nimemwona kazini. Anakuondolea maswali yote.Ongea na Roho Mtakatifu muda wote na useme naye kwa hakika bila shaka atakujibu.Kwenye ushauri atakuonesha ukweli ila wewe ndio utafanya maamuzi.
Nafasi nyingine wewe ni MSAIDIZI. Hapa sasa wewe ukikwama unamuomba either akusaidie karama yake moja ukamilishe jambo lako. Mjano unaweza kuomba Nguvu na Ujasiri kwa ajili ya interview au presentation. Au unaomba roho ya unabii/gift of prophecy ujue mamabo yajayo kama sisi wafanya biashara ili ujue kabisa unaweka hela au huweki. Au unaomba maelekezo unafanyaje kutatua hiyo changamoto yako.Maybe Unamombaje? Au umefungwa wapi? na ufanye vipi kwenye ulimwengu wa wa mwili.Au ukaomba intervatio yake, yeye kama yeye aende kwenye issue akasolve mambo. kuna mambo yanakuwa yamekushinda kabisa. Mfano kuna mtu umempenda kabisa mpaka unaumwa lakini ndiyo hakutaki hata kukusikia. Unamuomba tu akamgeuze moyo wake kama limbwata, utashangaa tu anabadilika.(Inategemea level ya uhusiano wenusio leo tu umeanza kumjua kesho unaomba intervention yake)
ROHO MTAKATIFU NI MSAIDIZI AMBAYE TUMELETEWA NA BWANA YESU, AENDE KUTOA USHAURI, UONGOZI NA USAIDIZXI KWA KILA MWENYE UHITAJI.
Mpendwa jenga sasa mahusiano na Roho Mtakatifu, mshirikishe mamb yako, mazuri na machungu.Muhusishe mambo yako siku nzima. Asubuhi Msalimie, Mchana na Jioni. Uhisi uwepo wake kila mahali ulipo. Badala ya kuendekeza meltdowns na depression , talk to the Holy Spirit in you. Utaona matokeo makubwa hata mwanzo unaweza kuhisi huoni kitu au kuhisi hufanyi kitu lakini utaona matokeo. Mfano unaweza kuzungumza naye kuhusu kazi, unaweza kuona kimya lakini baadaye mtu anakupigia kwa habari hizo za kazi.Au ukawaza kuweka pesa kwenye biashara yako au kutokuweka lakini akaja mteja na kulizia bidhaa ile ile ambayo unajishauri uweke pesa au usiweke maana yake anasema weka pesa hiyo na uache uoga.
Mpendwa wengi tunahisi kuwa tukiomba ngazi za juu tukajazwa Roho Mtakatifu imeishia hapo.Hapana!nRoho Mtakatifu ni Cool Spirirt.Unaweza jihusisha naye asubuhi mpaka jion.Kwa kumsemesha tu kimoyo moyo.kuhusu kitu chochote yaani ndiye mfariji wa matatizo yako.Kwanini ubebe mzigo peke yako?. Mpendwa hakna sehemu kwenye maandiko Roho Mtakatifu anabaya na mtu, muda wote ni msaada wa kukupeleka mbele.Maandiko yanasema hata ukiomba isivopasa anakurekebisha katika maombi yako yawe sawa kabisa kama ubani mbele ya Bwana.Kwanini usitake kuanzisha mahusiano naye?. Nawaambieni hizo changamoto mnazozunguka nazo kutafuta unabii, kutafuta neno la faraja, tumaini, kutafuta uponyaji, kutafuta msaada na ushauri wa binadamu wenzenu sawa wengine ni watumishi wa Mungu kweli, wengine ubinadamu unawaingia wanachukua mambo kwa maslahi binafsi, jenga mahusiano na Roho Mtakatifu, atakuwa KIONGOZI, MSHAURI NA MSAIDIZI WAKO.