STRATEGY ZITAKAZO KUSAIDIA KWENYE KUPATA VICTORY 2025

1.SOMA MAANDIKO!

Mpendwa the more you know the word the easier your path will be!, Maandiko sio kujua story iliendaje alafu basi ni kuweza kumsikia Mungu anazungumza nini na ku-draw day to day inspiration za ku-survive your day to day challenges (mapito).

Mimi kuna mambo mazuri ya kufurahisha nafsi yangu Mungu alinipa unabii 2021, The minute after kila kitu kikaenda south kukanusha ule unabii kabisa yaani kama nisingekuwa najua maandiko kingeniramba lakini najua maandiko ya Joseph kwani alipewa unabii mambo yakawa meusi tii, pressure! hivyo na mimi when times get worst inspired by Joseph son of Jaccob nashupaza fuvu, yaani I ignore all the shenenigns and vivid evidence kwamba ule unabii will never come to pass, na natembea kwa imani kuwa Mungu siyo mwanadamu anidanganye au mwana wa binadamu aseme atafanya atafanya kitu na asifanye!.

Mpendwa three (3) years of shupazaring fuvu is not a joke na moja ya unabii wa 2021 umetimia mwaka jana na kunipa epic win lakini kama ungeniuliza mwaka 2022 ungeona I’m Delulu is not a Solulu, on serious note myself, si imeandikwa na kuna muda narudia kusoma just incase sikusoma vizuri or I missed something.

Mpendwa itafika muda kwenye safari yako ya kiimani things will not makew sense!, people will not make sense!, The government will not make sense, us preachers will look like hypocrites tunao payuka payuka tu, The only thing that will make sense will be the scriptures na kama hujui ni kwisha kazi.

Mfano mtu huna kazi hapo ulipo, wazazi wako walio kuzaa wanaokuona mzigo wa miba yaani hubebeki unakuta una miaka thelathini (30) lakini unavizia pension zao, Inafika wakati hadi mpenzi wako anakuona mzigo yaani anakupenda sawa lakini kuendana na gharama za maisha jinsi zilivyo juu inabidi tu akupe offer ya nafasi ya mchepuko ili nafasi ya mke akae bosslady wasaidiane zigo ambalo ni wewe, you take it personally na serikali inakwambia jiajiri sasa sijui ujiajiri kwa mtaji gani?, kila mtu anakutelekeza hapo ukafie mbele, at this point only  Jesus make sense.

Mathew 11:28-30

28″Come to me, all you who are weary and burdened, and I will give you rest.29 Take my yoke up on you and learn from me, for I am gentle and humble in heart, and you will find your souls.30 For my yoke is easy and my burden is light”

Unaona watu tunakomaa na dini mpaka zituue na unazubaa zubaa!, shauri yako mjini hapa. Mpendwa kama unajua maandiko mtego wea un-employment ukikufayatukia, trust me you won’t break a sweat, unajua wa kukupa pumziko na nira laini. aminia

Wapendwa kuna mwanangu kanyooka, zaka mezani ni kila mwezi, hawaja renew mkataba, akaniambia December ile nikamwambia hiyo gratitude leta mbuzi mmoja hapa watoto wale, We laughed and joked about it, The same un-employment issue inayokufanya una- haha.

Wapendwa akaniambia mwakani sijui hata nitakuwa industry gani, tukabet laki-laki, Mimi nikasema banking, Yeye akasema FCMG, Juzi kasaini na Bank na kanipa laki yangu.

Tushavukaaa! kwenye imeandikwa au Mungu ameahidi au atampa Neeme ya kazi, Level tuliyo sisi ni kazi ni Uhakika and guaranteed, kuisha kwa mkataba mmoja ni kuanza kwa mkataba mwingine, sometimes mikataba inagongana hapo ujue ka-sign na zungu lenye ratiba kali lilikuwa na fright usiku, siku gani ya week, no body gives a damn!, Wapendwa level tulizopo siyo za kwanini apate kazi rather ni kwa nini akose kazi?, Anaanzaje? Kivipi?, Muda huo mbingu zipo wapi?, Yeye kukosa kazi inabidi maandiko mengi sana yapinduke which is impossible sababu imeandikwa neno ” Mambo yatapita lakini Neno litasimama”

Hakuna aliye zaliwa anajua maandiko, Wote at some point tulianza kusoma na tukawa consistent mpaka kesho!, Na kadri tulivyo consume neno ndiyo our path become lighter and lighter!.

 

Proverbs 4:18

But the path of the just is as the shining, That shineht more and more unto the perfect day.

Wewe hapo upo na bby wako na mna mipango yenu wenyewe na most of all una mpenda  na una malengo naye ya kuanzisha familia ili uweze ku-focus na mambo mengine ya kimaisha lakini ghafla hutaki tena na kibaya anakuambia kabisa hujafanya chcochote na siyo wewe ni mimi ndiyo mwenye shida sikutaki lakini hapa aibu tunaona sisi wasomaji.

At this point mapenzi yenu ni uchizi hata sisi wasomaji tunafunga Novel yenu, Novel  gani kama Russian Roulette mpaka wasomaji tunakuwa heart broken, kwako hai make sense kabisa sababu you didi everything mpaka praying for him and fasting, He doesn’t make sense maana mna connection na wewe siyo mjings kumpenda mtu hakupendi, chemistry ipo na he was realy nice sometimes haya mabadiliko ya ghafla vipee??, He doesn’t make sense, nothing!! yaani absolutely nothing makes sense at this point, unawaza sijui uwe sister tu wa jimbo au washirika potelea potee!, au ugawee hovyo hovyoo maana ulio watunzia hawakitaki so ukitunze sokoni kwa bei za promotion.

Ungekuwa umesoma maandiko usingepepesa kope, Mary  a whole virgin alitaka kukimbiwa na Joseph kwani mwamba hakutaka drama alitaka ile ya ku-slide kimya kimya, Kuyeyukaa! yaani Mary asingepewa Courtesy ya kupewa risala kama wewe kwamba kuanzia sasa penzi stop engine! ghaflaa tu ajikute single mother!, siyo hii mikimbio haijaanza sasa ipo tangu enzi za Yosefu Selemala.

Wapendwa na Yosefu hakuwa anamkimbia bibi kwa ubaya, He just needed answers ambazo even if Mary provided still the plot would have sounded as  shameless diabolical lies, unless God provided D the divine answers in  A divine way there was no way out for MARIA!.

So hata BBY wako, siyo kwamba hakupendi, things got complicated yaani dark Vuduu, Magic may have been used against you!, Anachokiona juu yako na anacho oneshwa kwenye ulimwengu wa roho hata wewe ukipewa nafasi ya kujitetea like Maria no way out for you unless God provides those devine answers in a divinely manner and style.

Like God tackled and Sorted Josephs doubts to the extent akaamua kuendelea na the holy plot, kama unajua haya maandiko he can sort out   doubts and reservation z a Bby wako to the extent atarudisha fito zake kuja ku-propose kama siyo yeye aliye leta story za kukuacha, kivipi sasa? na Aende wapi? na Wewe ubakie na nani?

Kurudisha kiwili wili chake atarejeshaa, It is not for discussion, Ni suala tu la when exactly kama ikibidi Mungu amtumie malaika mchana saa saba (7), Ofisini akiwa katikati ya presentation anamwambia utamuoa mwanangu au umuoi, for him to proprose atatumaa!.

Mpendwa mwanaume akikwambia yule siyo chaguo langu lakini nimemuoa na jeuri ya kumuacha sina miaka 8000 muwe mnaelewa, It is 100% Truth, na ni kweli nafasi iliyopo ni ya mchepuko tu msifosi mambo, Girl Byee!!

 

2.AMINI KATIKA  MUNGU NA JIKABIDHI KWA MUNGU KWENYE KILA KITU.

Kujua Mungu yupo na kuamini katika Mungu ni mambo matano (5) tofauti, Wengi tunajua kama Mungu yupo na tunajua hell is real na Mungu ukimuuzi vizuri hasubiri hata mpaka ufe, anaanza kuku roast hapa hapa duniani tu kwani sh ngapi?

Kuamini katika Mungu ni kuamini with your every move and intention kwamba Mungu yupo, na ni Mungu wako na Most of All ni Muhimu sana kwako kuwa on his good side, Why exactly?, sababu una pambana ku-qualify as mwana wa Mungu, You wanna join the heavens gang, kwenye msafara wa Mamba Kenge ujipenyeze.

Faith is a two sided sword, the more you take the heat the sooner God and his army will take the heat for you, unathibisha imani yako kwa Mungu pale mwanaume unampendaa, una muelewa, upwiruu level 200 lakini sababu una amini katika Mungu na unajua zinaa ni chukizo you say “Hell Noo” alafu baada ya hapo you feel like shit, unaliaa wewe alafu unatulizia na ganja, literally speaking, huwezi kusema naamini kwenye Mungu alafu unajitegesha style ya popo kanyea mbingu, holy crap!, sio kwamba unazini una zini na mbingu kabisaa in the action, its not a laughing matter!.

Unasema una amini Mungu alafu unaiba kazini, your career is cemented with grand theft, intellectual theft, Junior wakileta ideas unazibinafsisha, destiny theft, ukiona mtu tishio kum-surrender sio shida zako, una mtuliza kabla hajakutuliza, Wewe huyo huyo unalipa zaka kubwa hoping zaka itazipooza mbingu dhidi ya ufadhuli wako, thubutuu!.

Kama kweli una muamini Mungu huwezi kuiba wala kudokoa dokoa maofisini, mngewajua wewe hayo maofisi walivo washirikina wameweka mitego kibao, wamezindika fortune zao, na wame zilaani pesa zao, ndio utashangaa mbona kama hawana nia ya kuku kamata mpaka fourty (40) yao ifike yenyewe?, They are making zero (0) efforts, sababu wanataka kukufanya collateral, damage, utamalizana na majini na mashetani ya zindiko, unachoiba wewe ni kidogo lakini kwa ujinga wako unatoa uhalali wao kuchukua vitu vikubwa sana kwako.

Mimi watu wote nilio fanya nao kazi hawajawahi kufanya biashara ikatoka, hela za waarabu zilikuwa na mazindiko, wana dokoa pesa ya kula kula tu ila waliacha nyota zao waarabu wanatumia mpaka kesho, wamehangaika kwa waganga wakaulizwa hakumchua pesa?, Tulichukua basi ndiyo mmeuza nyota zenu kama chief mangungo, sisi waaminifu tulionekana majingaa tumeondoka na clean sheet, nyota zetu tunazo na tuna tamba nazo.

Watu waaminifu ndio Mungu anawabariki wanafaya kazi mpaka miaka yao ya nguvu za kufanya kazi inatimia, akitoka hapa Mungu anampeleka kule, hawakosagi kazi, majizi! hayadumu kazini na akidumu ni kazi isiyo na baraka ni ya kupiga magoti, siku zote na kulaga loga, mshahara wote unaishia kwa waganga kutuliza mambo na kuwafumba akili maboss.

Mimi mwenyewe nafanya biashara zina maagano kama yotee na maapizo, Ukizingatia Mimi mwenyewe mtumishi vitu na navipika mwenyewe siyo kwa ubaya ni katika kulinda changu, I take zero (0) risk, picha linaanza siajiri ndugu hata mmoja, na Nawaambia kabisaa biashara kabisa biashara ina mkono wa bwana mzito hii sasa shobokeni kudokoa dokoa.

After sometimes nikiona kijana mikosi ina muandama najua tu ni mkono wa Bwana umeanza kuwa mzito juu yake, sometimes siwafukuzi ila wenyewe wanakimbia, sasa sawa utakimbia ila maagano ndiyo usha ya activate dhidi yako na yatakuandama maisha yako yote. Unless uje uniambie nilikuibia na unilipe, only then ndiyo nitakutafutia maagano na nadhiri juu yako, kufuta agano active is very expensive ukizingatia linafanya kazi vizuri sana, naanzaje?, Muwe  mnajiongeza mbona pesa nashika mimi na siyo ndugu zakee? alafu muwe waaminifu?

Back to Topic!

Wapendwa unaposema unamuamini Muingu jiulize to what extent and at what context, and in what time???,

Wapendwa siyo namuamini Mungu juu ya Mume, Ukiwashwaa ushakunwa, Kazini ni Mwizi, Muongo, Na kila kitui imani yako kwa Muingu ni ya mchongo, Ila juu ya Suala la Mume ipo Vey Very!, Mpendwa lazima Uliombee kwa Mungu walau mara nne (4).

Imani kwa Mungu works best kwama ukiifanya 360 degrees, una muamini asubuhi mpaka jioni, Jumatatu mpaka Jumapili, January to December.

Wapendwa sometimes nawaelewa Mungu anakuwa haaaminiki hivi, una mgoja kwa Moyo wote na hatokei ng’oo, una panic na unakata tamaa, it’s frustrating. Unatakiwa kuelewa jambo moja, njia za Mungu siyo nia zetu na mawazo ya Mungu sio mawazo yetu na most of all ujifunze kumuamini Mungu blindly hata kama hujui njia zake zitaelekea wapi.

 

Isaiah 55:8-9

Maana mawazo yangu siyo mawazo yenu, Wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadjhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu yako juu sana kuliko mawazo yenu.

Ugumu wa Dini na Imani unakuja pale unapo lazimika kuziamini njia za Mungu na mawazo ya Mungu na wewe nundaa! hutaki huambiliki lolote, unataka Mungu afate njia zako na atekeleze mawazo yako!, Thubutuu!, Mungu anasema usintanie!, hivyo matokeo yake unaangamia jumla jumla!.

Unakutana na mwanaume una mparamia wima wima, humuulizi Mungu na humuulizi  yeyote, yaani unaziuliz nyege zako na kuruka naye kichwa kichwa, sasa vina muda basi??, ukipanda uovu lazima uvuneee!!!, suddenly mzinzi mwenzio hakutaki tena bibi wewe, kwanini?? basi tu ahakuona huna jipya na huna maajabu, aidha huna thamani, just like that honey bae anageuka your worst nightmare yaani akikuona ni kama na kaona duduwasha jinsi unavyo mkeraa.

The bad news is he broke your heart, he sqanddered your dignity, he abused your trust and made things alot worse, but the good news is engine bado unayo mwenyewe na una imiliki ni kuifanyia tu repair za hapa na pale na another good news mwanaume duniani siyo peke yake bado wapo billion saba (7), tena wana maisha kuliko yeye.

The important lesson to learn from all this is never trust humans, just trust your God Only!.

Lakini hapanaa!, You go around doing yourself worse than before, Wewe umeruka na wanaume kumi (10) wote na wote hawataki kukuoa, badala ya kuona constant factor  ambayo ni wewe ujishughulikie na kufungua mabano, mwanaume wa kumi na moja (11) unajinasisha mimba, sasa kukataliwa wewe na mtoto cha kusikitisha hapo ni kipii?, sababu wewe una historia ya kukataliwa an innocent kid won’t be able to erase that dark history, matokeo yake you drug an innocent kid unto your shit!.

Wengi mnahisi mtoto ata feel in the gap ya upweke ulio kuwa nayo lakini kiukweli mtoto atafanya things kuwa more worse na upweke utakuuwa kabisa. Mwanzo ulisikia upweke kwa sababu ya maneno ya watu believe me pale walikuwa hawaja anza kusema, maana wali-hold back 70% maana bado ulikuwa msichana mzuri uliye kamilika Mungu angeweza kuwashangaza kupitia wewe.

Sasa the minute tumbo likionekana all hell is let loos, sasa mkeka umechanika na wana uhakika na maneno yao, na the worst part kila mtu kuanzia nesio mpaka mwenyr nyumba watakuwa wanataka kujua Mimba niya nani na yuko wapi and if you are happy or just a miserable, It only get worse!.

Mtu kweli age go na anatamani familia na kuwa mume wake na nyumba yake and things are not working out, mna anza deliverance vizuri, unamtia moyo as long as We are pushing in the right direction ni swala la muda tu, Hang On!, Kaza kamba komaa.

The minute Deliverance ikianza kufanya kazi kosaaa!, sababu kashazoea rude man, akija nice man from tons and tons of prayer and fasting utasemaa hapa sasa kapata Moyo wa kuimaliza safari kwa ushindi lakini thbutuu!.

Wapendwa njia za Mungu siyo njia zake tenaa, njia za upwiru ndio njia zake, njia za kujipatishja mimba ndio njia zake, Mlokole Binti is Old School , Zinaa sio issue! Okay!, Wenzio tulijifunza kwa njia ndefu!.

Issue siyo mwanaume hakuwa sahihi, ila wewe hukuwa sahihi kwa yule mwanaume, Mungu anakuletea mwanaume ambaye ni mja wake akitegemea hata akikushawishi utashinda vishawishi.

Wapendwa mimi nina mwanangu, Aunty yangu she is twenty years old (20), kali okoka lakini umalaya wa magomeni bado upo ndani yake  kama wote, sio shida zetu kugawa gawa hovyo!, Wazaramo sisi, kufika church kakutana na A very good boy from a very nice family ambayo they have a reputation to up hold, He is twenty four (24) years old, Katoka nje, yaani bora angetuomba ushauri kudadeki.

Yamkini kwenda kule kwa kijana akaona mom is cool, wana swimming pool na personal cheff siyo mbaya akajoin the family, She pulled A Magomeni Style ya unajibebesha Mimba, Hehehe! akajua yule mama anavyo chekacheka ndiyo atachekacheka hivyo hivyo, thubutuu!, Mama kamwambia watamlipia abortion, They abused her on a every angle, yaani wamemfukuza kama Mbwa, The boy kamwambia amtafute amtafte after abortion, alafu ni walokole!.

Mpendwa kwa sisi wa magomeni hatujashangaa, kwanza wangemchukua ndiyo tunge shangaa, wewe unakuta familia ya watu, watoto wote wamezaliwa kwenye ndoa eeh, Wazee wa kanisa!, Kijana kiongozi wa vijana!, They have all image and respect with in the churchj alafu wewe kirahisi rahisi tu uwaharibie bright future for your self reasons, lazima kita kuramba.

Wapendwa Aunty yangu akataka kuvictimise akasahau sisi wa magomeni wenzie, tukamwambia cut the crap, hata kama ulifanya kuna P2, Ungeweza kucheza na Calender, Umejinasisha bwana na kimekuramba another unsolved mistery going down in your history, yaani sio shida zetu ni zaa hapa tutalea! Wewe baba yako alikulea?, Si umekua?, Tena ondoa mawazo kwamba mtoto watampokea na kumpenda thubutuu!, Kwao ni mtoto wa aibu.

Watamtafutia mchumba mwingine kanisani, atamuoa na kuanzisha familia kwenye channel zinazo eleweka, Wewe Mungu alisha kupa yule mwanaume ukakosa subira na kutumia magomeni style watch him atakavyo kunyanganya na kumpa mwanamke mwenzio anaye jielewa na ambaye ataenda na kufata njia zake.

Watu wengi hapa ndiyo mna kwama ns kuharibu maisha. Wengi wanaume wanaotakiwa kuwaoa mshakutana nao au wapo ndani ya maisha yenu tayari ila hawaja make their grand move, Ni wametulia wana usoma mchezo, na Wanangoja right timing. Sasa shida yenu kubwa pamoja na kusalii, Kufunga, na Programs bado hamuamini Mungu mnatumia akili zenu na kufanya blander za kijinga.

Mimi maandiko nayajua na Mungu namjua, Mtu anakwambia nimeacha zinaa tangu 2022, Una mwambia tulia kidodo tu Mungu atafanya jambo kwako, Kwenye odds za ndoa quality msichana mabaye hajazaa ni rahisi zaidi kupokelewa ukweni na reputable family, Unamwambia tulia tulifanikishe hili, ili uweze kupata reputable family , sasa ndugu yangu anaenda kubeba li mimba la majanini?

Kisha anarudi anavuja maziwa kwa kunyonyesha alafua anauliza hivi Mungu anaweza kunipa Mume nikiwa nanyonyesha?, Told you!, You will Cry louder than the baby himself, anaanza pressure nataka Mume by june, Nataka Mume huu mwaka usiishe, Ulimuweka?, Yaani yale yale anataka Mungu afate njia zake na script zake, Thubutuu!.

Nawaambia tena na tenaa, Hata kama kwa muda huo njia za Mungu hazieleweki amini Muingu ana nia njema na wewe, na pamoja na hizo njia zake hatakama wewe huzielewi mawazo anayo kuwazia nia kukupa tumaini siku ya mwisho.

 

Romans 8: 28

28 And we know that all things Gods works for the good of those love him, who (a) have been called according to his purpose.

In all things including kuachwa kisa umegoma kutoa chiu, kuonekana kwenu maskini maskini utaolewa ufaidike na familia yako, kuonekana hujasoma not a good fit, kuonekana mzee age go, kuonekana sio pisi kali tako huna dada!. Yote kwa yote Mungu atakupa fungu lako na mtu wako wa kufanana naye.

 

Yer 29:11

Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

Hata kama mwanaume anakuacha leo kisa papuchi jitie moyo katika Mungu wako kwamba anakuwazia mema na ushindi, ni swala la Muda, Yule mwanaume atarudi na kukuta umejitunza sio una watoto wawili (2) or Better atakuja mzuri zaidi kuliko huyo anaye kuuma roho.

Hata kama njia za Mungu zina kulazimu huyo mwanaume aondoke kwanza kwenye maisha yako, Tag along!, Komaa na Mbingu mpaka zikuue, Ofcourse utaumia robo ya kufa, lakini jua jambo moja kwa hakika ” Mambo yotee yatapita lakini Neno litasimama wima” Kwa hiyo neno la kupewa tumaini na Mungu siku za mwisho lipo karibu kutimia kwako kuliko unavyo zania.

Wewe mwenyewe tafakari umekaa mpaka miaka thelathini na saba (37) huna kiraruu raruu cha mtoto ila mwaka huu ndiyo umepanic hatari, Jua shetani kaona wakati wako umefika, akikukosa sasahivi atakukosa milele ndiyo maana ka-tripple attacks, left right centre watu wana kusakama zaa, zaa na wewe kwani mayai yanaisha, Mpaka mama yako mlokole shetani anamtumia kukwambia zaa, Yote hiyo ni ilimradi ahadi ya Mungu iki mature ya mwezio kuja akukute unalimimba au unavuja maziwa inakuwa siyo riziki, yaani unaanza upyaaa! After three(3) years ofcourse maana mpaka mtoto asogee!

3.ILI USHINDE LAZIMA KWANZA UZALIWA UPYA KATIKA KRISTO NA ILI UZALIWE UPYA LAZIMA KWANZA UFE NA KRISTO MSALABANI KWA KUKUBALI KUBEBA MSALABA WAKO NA KUSULUBIWA NA KRISTO

 

Romans 6:8-18

8. Now if we died with Christ, We believe that we will also live with him.9 For We Know that since Christ was raised from the dead, He can not die again, death no longer has mastery over him.10 The death he died, he died to sin once for all; but the life he lives, he lives to God.

Wengi mnateseka na case ya kukimbia misalaba na kukwepa kwepa kusulubiwa hivyo matokeo yake mna kwama kuzaliwa upya katika kristo, mnajizungusha jangwani wenyewe na kujichelewesha. Yesu alidemonstrate jinsi gani ya ku-deal na dhambi na kuzishinda, Lazima ukabiliane na ukweli, uzikokote dhambi zako hadharani, ukubali kusulubiwa nazo na ushupaze fuvu zikuue mbele ya kila mtu, only then yesu ndipo atakuona serious na safari yako ya kuja kufufus ndipo utazaliwa upya.

Mpendwa hiyo version of you ya mchongoi, siri kama zote, ubabaifu ndiyo usiseme, in decision ndiyo kabisa haiwezi kushinda, You know it, God knows it, even the devil knows it sasa who are you kidding??.

Mpendwa Every saint has a past and every sinner has a future all that matters is what is your next move!, Ndiyo maana watu unaowaona leo wako on firee kwa Mungu ukipewa ma-file yao ya nyuma utasema “Jesus Christ” na kuna watu wa dhambi leo na kesho kutwa utawakuta kwenye makongamano hutaamini.

Wengui kujitwika misalaba na kumfata Yesu mnakwepa kwepa kwepa matter of fact misalaba maificha kama majibu ya kipimo kikubwa, mna jaribu kuitelekeza na kujizima data lakini misalaba ipo na nyinyi mpaka iwa uwe, yaani mlipo ipo yaani unachotaka na msalaba wako unataka.

Mtu kweli umri umeenda sasa watu wasiseme kweli una arobaini (40) dada mkubwa!!, lakini unakazi ya kujifanya mtoto wa 2000 yaani mashavu yanachuma kunde, ” Msinione hivi mimi nimekula shida sana” mmh!! dada kubwaa!, Wanaume wakija uko kuwaambia “Mimi ni 28″ Mwili tu  huu!, Mhh! Uongo usivyo na consistency yaani siku y a siku utakuja kujisahau una muwish last born wenu happy 38 Years!, Ukibanwa una kablock ka baby kako!, Mpendwa ulipo na msalaba wako upo yaani uko na wewe mpaka uchizikee! Yaani wapendwa kukwepa msalaba ni msalaba mzito sana!.

Wewe ujitwike msalaba wako kwamba mimi ni mkubwaa!, Millenium! I am fourty four (44) sawa nimechelewa kuolewa na sina watoto, watakao kupiga mawe  mzee acha wakupige, watakao fanya kalamu kusherehekea ugumu wako acha wafanye, Watakao kukubali hivyo hivyo ndiyo Mungu alikupa kwenye safari yako, Na wakao inuka dhidi yako acha wainuke acha wakusulubishe, Ukweli utakuweka sana huru!!!, Ukipata mwanaume mwambie ukweli kuwa nina miaka arobaini na nne (44), Kama anasepaa acha asepe mapema kuliko kupotezeana muda.

Wapendwa nina mwanangu alikuwa na miaka thelathini na sita (36) sasa kakutana na mkaka waka click, kuulizwa umri akasema nina miaka 28! ili kujiposition, Mind you aliomba karibu mwaka ndipo akaja huyu mwanaume sasa sijui alipanic baada ya kusema ishirini na nane (28), Mwanaume akapoteza interest kabisa!, kumuuliza mwanaume akamwambia ana miaka arobaini na nne (44) hivyo anatafuta mtu ambaye angalau ana miaka 36 hivi na ambaye alishamaliza ujana, yaani she is done with young and restless.

Sasa Mwanangu alichokifanya akabadili gia angani na kusema she is thirty six (36) Years Old yaani akatumia na NIDA, Mwanaume akamwambia kama umri tu umenidanganya utakuwa umenidanganya vingapi?, I’m so done with power and mind games, Mwanangu kajitetea wee, lakini wapi kilimramba, Nilimuhurumia sana she is not a bad girl just insecure.

Wapendwa ukificha msalaba na kukwepa shetani atakusaidia kuukokota na kuutumia dhidi yako wakati muafaka kabisa kukuharibia beyond repair. God Knows You are old!, He wont send someone to tormtent you on your age, Huwezi Muomba samaki akakupa nyoka, Mungu wetu hayuko hivyo, Yaani Ukiona mtu anakuja na kukaa juu ya msalaba wako hajatoka kwa Mungu, Akitoka kwa Mungu atakusaidia msalaba wako.

Yaani mtu una watoto watatu(3) una wa kana, Una waficha, Tumbo lina mishono mitatu (3), Wewe unakazi ya kuzima taa kabla ya mechi kuficha siri yako, Wewe crop top akhaa!, Ni full kuchomekea. Mungu hawezi kukupa ushindi kwenye misingi ya m mchongo mchongo kama hiyo, Mungu anajua unawatoto, Wewe mwenyewe unajua unawatoto, na Shetani anajua una watoto , sasa who are you kidding?, Hata Mungu akikupa Mume, Shetani atacheza Jokeri la watoto, Kuku discredit na kukuhakikishia unaonekana kituko.

Mpendwa wewe sema ukweli nina watoto watatu (3), Kama mtu katoka kwa Mungu atawakubali wanao na utapata amani, Na kama hajatoka kwa Mungu watoto watakusaidia kwenye vetting maana he may fool you but he can never fool the kids.

Mpendwa kokota msalaba wako ukikataliwa ukweni kisa watoto ndiyo vizuri maana umejua roho nyeusi mapemaa, Mtu stingy akiona ubahili kuwahudumia wanao unajua mapema na unasema bora sijakupa utamu mwanaume gani bahili kama nini. Kubali kusurubiwa ikiwezekana ku – uwawa kihisia na kiroho kwa abuse sawa lakini never ever deny your kids or gamble with them.

Mtu huna kazi , huna uchumi acha kujiegesha kwa wanaume za watu na kugawa gawa hovyo ili uishi maisha mazuri!, Msalaba haukimbiwi wala haukwepeki, hilo chocho lina ukomo wa umri na  ukomo ni miaka ishirini na tisa (29), Ukifika thelathini (30) sidechick gigs zina kukataa ushakuwa side ostrich!.

Usifosii! kuwa big girl, Ishi uhalisia wako wa chumba kimoja, Take junior positions, Earn Your Career Positions Godly, Jifunze kazi na fanya kazi kwa moyo!, Utabadilisha maisha yako in due time and process za watu wengi wanaanza na chumba kimoja wanakuja kujenga maghorofa.

Mpendwa kama unataka ushindi wa kweli kutoka kwa Mungu usiogope Kusulubiwa Msalabani wala kufa on the process, The version of you ambayo inapeleka mambo kimchongo mchongo can never win, There are many loose ends that devil will use against you to block that win.

Mimi mtu akiwa anakwepa msalaba wake akae akijua ni suala la muda tu shetani atautumia udhaifu wake kumchapia, Mimi mwenyewe kilish wahi nilamba na over years naona sana watu wanavyotolewa majokeri muda wa majeruhi!, Kama yule mtoto, najipanga na deliverance round mbili (2) kumbe kanaendekeza zinaa,Shetani kamkaribisha na jokei la mimbaz!!, yaani Kwisha kazi!!.

Most of times kwenye ufalme wa mbinguni you only win by losing!, Unaweza kuona unapoteza mapambano yaani unaona kwisha habari yako kumbe ndiyo unashindaa hivyo, Wapendwa njia za Mungu siyo njia zetu, Mwanangu ilitakiwa aseme tu ukweli, Yaani kwa udogo sana she is thirty six (36) Years Old yaani ingekuwa Done Deal!, Mungu kamleta Mtu suitable for her, Yeye kaleta ubabaifu, Shetani kamchapa jokeri na last card!.

Mpendwa hata wanandoa nawaambiaga being condecending and living lies can never make you a winner lather a slave to sins and your husband, sometimes for him to be  a changed man ina require wewe kwenda through separation and even divorce!, aone thamani yako in what he lost!.

Mpendwa ukiwaza kusulubiwa juu ya talaka una amua kuendekeza upuuzi, kuliko ufe umesimama, unaona bora umkosee Mungu na kuwafurahisha binadamu kwa kuishi umepiga magoti, and allow diabolical nonsense to go down on a daily basis, mkristo unakaa kama mke mwenza!!!??, Ndivyo dini inavyosema??, Ujue hawara wa mumeo na ujifanye mjinga wa mwisho kuliko wote mkachukue dose palestina hostital!, Holy Crap!.

Dini inasema mwanaume mmoja kwa mwanamke mmoja, The minute maandiko yanaaanza kupindishwa walk out!, Hata ukiwa na tatizo sawa, Lakini unawafundisha wanao stand up for themselves, You praise herouse at a grat cost lakini ulikuwa coward your sons will grow to be cowards who treat their women as shit!, Wa kike nao watakubali upuuzi wowote toka kwa wanaume its what they learnt from you, Take shit and More Shit than crap.

Sometimes ushindi unataka ufe siyo mara moja yaani several times, You live to die another day, Unaenda interview hata thelathini (30), Unakula not selected lakini hukati tamaa, unaenda tena na tena, Yaani kufa tena mpaka iseme selected.

Mimi mwenyewe nakufa kila siku, Kwenye biashara huko unakuta narogwaa, napotea na watu wanasherehekea kabisa kwamba nimeishaa, Na kuna muda hata mimi naona yamkini kweli hakuna marefu yasiyo kuwa na ncha labda hii ndiyo ncha lakini nazaliwa mara ya pili na na hit kuliko hata mara ya kwanza mwisho kabla sijafa kibiashara, Mpaka kuna watu wanahisi biashara yangu inaroho tisa (9) kama ya paka, Maana ikifa ni suala la muda tu inarudi kwa nguvu kuliko vile ambavyo ilikuwa  haijafa.

Sometimes before finding your prince you have to kiss  ten (10) frogs jitu linakuja vizuri tu na baadaye, linakuvunja moyo unajua kumbe lichuraa tu unalipiga teke kuliongezea mwendo wa kuliondoa kwenye maisha yako, na kisha unajirudisha sokoni ni suala la muda tu utamkiss  real prince charming!.

Uvivu wa kukiss frogs wa kutosha una manipulate mambo na kuamua kufosi ndoa na chura jambo amabalo huko mbele linakuja kukugharimu, Kelele za chura kuishi nazo mpaka kifo kiwatenganishe sio rahisi, Yaani utarudi sokoni na cheti chako cha mahakama ni taraka nginja nginja!.

What does being dead with christ actually mean?, Kufa na Kristo kwenye maisha yako ni kupotezaa kabisa, Hisia, Reactions wala mawasiliano yoyote baina yako na issue  inayokutesa. Mfano suala la ndoa limechelewa na watu wakikugusa ni angle hiyo, all hell will be let loose, Unaweza kunyonya mtu damu mchana kweupe, ” Flani ana miaka arobaini na tano (45) yaani hana mtoto wala mume ni ameolewa na career”, Aliyeropoka ukasikia safari za mkoani utazisikia kwa wenzie labda kama sio wewe HR, Promotion pia asahau!, Uzuri naye akiwa amebainika atawaza Yuda gani kamrudishia yale maneno jamani!!.

Dieing on the issue ni siku utakayo amua sababu Yesu anaishi ndani yangu na anaishi tena na alikufa kuniokoa hivyo hutakaa uumie juu ya issue ya kuchelewa kwa ndoa yako milele amina, Yaani hata waseme nini, Hata wakuseme mbele ya kanisa, No Network as good as dead, yaani huna reaction.

Mpendwa watu wazima waki kutest au kukupima imanmio umekufa kwelii!! au unajichetua tuu, Wakiona unaongea na hu-react! wanaanza kuja sasa uso kwa uso, mara wakutolee maneno kwa mfano mbele ya kanisa kukupima tu temperature, No reaction yaani you are good as dead, Remember! Unasema tu bwana Yesu nipe uvumilivu na unitetee wewe!.

Mpendwa utawashangaza maana all that they are after ni kukuona una fadhaika, Wanataka damu imwagike na pachangamke!, Wakiona udhaifu wako hauna nguvu tena dhidi yako wan anza kuhaha au Mungu Kashamjibu tayari nini?, anajiamini nini huyu kikongwe, Unaskia Bwana ananiambia soon utapata mwenzio!!.

Huyu hana kazi hana faida yoyote, Yaani huko chuo alienda kuzurura, Mwambie Bwan Yesu nakufa msalabani na wewe, Nipe uvumilivu na ustahimilivu, Washazoea wakikudochoa hivyo damu inamwagikaa, yaani huli siku tatu (3), Hutoki Chumbani, Lakini baada ya Kufa na Yesu Wakimaliza, Una waangalia macho kwa macho na kuwaambia ” Nawapenda sana na Mungu akinipa kazi soon kama aishivyo nitakwenda kazini!, Siku ya leo sita ikumbuka wala kuishikilia dhidi yenu, Kama Mungu aishivyo nimeisamehe na sitawaweka rohonio na nawaombea sana kwa Mungu kile nilichopunguza kwenye jasho lenu awarejeshee mara dufu” Una imba zako nyimbo za kusifu na kuabudu kama hakuna kitu!”.

Wapendwa sometimes una require another version of you, Stronger and Reliable Version!, Ushindi Unahitaji wewe wa zamani ambaye ni Dhaifu, Mbabaifu, Asiye na Maamuzi hana wala stamina na roho ngumu afe kwanza ili azaliwe wewe mpya ambaye sasa utakuwa capable kuupokea ushindi.

Ukifanikiwa kufa nyumbani kwenye gubu lao na manyanyaso, Oral Interview You will eat them alive, This new you is just dangerous, Hupepesi macho wala kope, Hubabaiki, Una waangalia macho kwa macho na kujibu maswali kama mshindi ambaye God has destined you to be, Nothing can stop you from being you, Umevua gamba.

Hata akama akija mwanaume yaani umenyooka nina miaka arobaini na tano (45), Nina watoto wawili (2) Nampenda Yesu, Nachukia zinaa, Na natafuta life partner, Je wewe unajiona uko kwenye direction moja MR?, Huogopi dudu wala mende, Haina kona kona, Huogopi Kuachwa, Huogopi kuonekana mzee, Sijui watoto itakuwaje, You have been there before, You have done that!, Now you know what you want!, You know your worth!.

Usichokijua tu ni mwenzio alikuwa anatafuta mtu kama wewe na kukupata anaona kama mioujizaa!, Maana watu kama wewe kwenye dunia ya zinaa washakuwa extinct!.

Mwanzo mwanaume akikaa na wewe siku tatu (3) tu inaanza world of lies, Fake life, Adultry who wants that for a wife?, Alafu unajiuliza mbona hawa ni owiii! Wewe kuweza kuishi na Mongo na Mhuni?

Mwanaume anaweza kuja kwako kwa nia njema kabisa ila nia kiabadilika kutokana tu anavyokukuta, Mwanzo anakuja na sera nzuri kabisaa, Nataka kukuoa, Hapo anajua akikuomba papuchi uta kataa si umeokoka, Anapima nguvu yako ya kupinga zinaa, Kamomba mara moja (1), Ya pili anavua chupi anaona unamfurahisha kumbe unamtisha, Kwamba hamna mkee! Maji mara mojaa?? yaani hapana! Siku mbili (2) nyingi ulisema una miaka ishirini na nane (28) unajisahau dada na kuropoka chuo umemaliza 2010!, Ni suala la muda tu baada ya kula mzigo anarudi magotini Mungu mbona kama Jezebel lile limwanamke jamani.

In reality, That is not you, ulikuwa una play character ya kufosi ndoa because you were too coward to stand with God, Too ashamed to be christian in 2024!, too naive to be yourself!, sasa kina kurambaa!.

Wewe ukinyooka na Mungu sawa mwanaume anaweza kuondoka kwa ukatili kweli muda huo akakuachia jaka Moyo lakini Mungu atamuonesha moto huko anapoenda, Picha linaanza anapata kaswende iliyo changanyika na ghonorea kudadeki, Anateseka nayo kidogo kifanyio kikatike, Anasema umalaya basii, Mademu wanao gawa gawa hovyoo stop engine!, Sitaki tena, Nirudi kwa Mlokole nimuoe nitulie kabla sijawa hanithi, Unashangaa anarudi na yeye ndio mpinga sex mkubwa mpaka una mshangaa Mungu.

 

2 Corithians 5:17

17.Therefore, If anyone is in christ, the new creations has come (a) The Old has gone, the nwe is here!

 

LORD FORGIVE MY UNBELIEF

Imani yako kwa Mungu ni kama mbegu ikimwagiliwa na kunyeshewa na kisha kupaliliwa ita chipua na kustawi sana, na ikikutana na jangwa itanyauka na kufa.

Mpendwa hata kama una imani haba ukikutana na mwenye imani thabiti atakuambukiza na ukikutana na mwenye jangwa la imani atakausha imani yako yotee. Hivyo mpendwa imani yako ni kitu cha kukilinda sana sanaa maana siyo kitu permanent ni kitu cha kupwa na kujaa, Mimi nakutana na watu wapo kijiweni miaka saba (7) yaani alishakata tamaa kabisaa, anashangaa mimi naamini vipi yeye ataenda kazini, anaanza kuamini sababu mimi naaamini yaani anakopa imani kwangu, na in no time anaenda kazini.

Mtu unakuta alishakata tamaa ya mahusiano lakini kwa sababu mimi nina amini atafaulu this time anakopa mtu imani mpaka akija mtu sasa ndiyo anaanza kuchepua imani yake kwamba ndoa inaweza kuwezekana.Mpendwa kutokuwa na imani au kupungukiwa imani ni kitu kibaya sana maana muda wa dhoruba lazima utafanya blander maana ushatoka kwenye reli.

Kuna muda things turn Gray hujielewi kama unaamini au huamini yaani upo upo tu, hii pia iliwatokea watu tofauti tofauti katika maandiko.

Marko 9: 14-24

14 Walipowafikia wale wanafunzi wengine, waliwakuta wamezungukwa na umati mkubwa wa watu na baadhi ya walimu wa sheria wakibishana nao.15 Mara wale watu walipomwona Yesu walistaajabu sana, wakamkimbilia, wakamsalimu.16 Akawauliza wanafunzi wake, “Mnabishana nini nao?”

Mtu mmoja katika ule umati wa watu akajibu, “Mwalimu, nimemleta kwako mtoto wangu wa kiume kwa maana anapagawa na pepo ambaye amemfanya kuwa bubu.18. Kila mara Pepo huyo amwingiapo mwanangu, humwangusha chini na kumfanya atokwe na povu mdomoni na kusaga meno, kisha mwili wake hukauka.Nimewaomba mwanafunzi wako wamtoe pepo huyo, lakini hawakuweza.”

Yesu akawaambia,”Ninyi kizazi kisichokuwa na imani, Nitakuwa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni huyo mtoto kwangu?”.20 Wakamleta, Yule Pepo alipomwona Yesu, alimtia yule mvulana kifafa, akaanguka chini akijiviringisha huku akitokwa na povu mdomonio.21 Yesu akamwuliza baba yake, ” Mwanao amekuwa na hali hii tangu lini?” Akamjibu tangu utoto wake. 22. Mara nyingi huyo pepo amemwangusha kwenye mtot au kwenye maji ili kuangamiza maisha yake. Lakini kama wewe unaweza kufanya chochote, tafadhali tuonee huruma, utusaidie.”

23. Yesu akasema, ” Kama unaweza??!, Kila kitu kinawezekana kwa mtu mwenye imani”.24 Ndipo yule Baba akasema kwa sauti,”Naamini, Nisaidie niweze kuamini zaidi.”.

 

Wapendwa hapa ndipo Password ilipo,  Zingatia mstari wa 23 na 24 na English Version imeweka vizuri zaidi kama ilivyo kusudiwa.

23. “If you can?” said Jesus. ” Everything is possible for one who believes.”.24.” Immediatelly the Boy father exclaimed, ” I do believe; help me overcome my unbelief”

“HELP ME OVERCOME MY UN-BELIEF”

Luke 17: 5

5. The appostles said to the Lord, “Increase our faith”

Mitume wenyewe na utume wao wanafika mahali wanaona mabo mbobmbongaf wanajilipua kumuomba Yesu kama vipi awaongezee imani.

Hivyo mpendwa kwenye safari yako kuna mudas kweli level za imani yako zitasoma chini mno na kuna muda kiukweli utataka matokeo ambayo imani ya kuyapata huna na ukicheza utayakosa kweli kweli.

Baba wa yule mtoto, mwanaye alikuwa nanteseka na pepo hatari, linamtupa kwenye moto mara sehemu hatarishi ilimradi tu tafrani. Sasa Baba anaulizwa unaamini yote kwa Mungu yanawezekana?, Yeye akaona huu siyo muda sahihi kupimwa imani yake, Chitoto kinateseka kama hataamini itakuwaje sasa?, Mbona mtego mbaya sana wanamuwekea?

Baba mtu akajiongeza kuongea kiutu uzimaa!!, Mimi naamini lakini kama kuna kutoamini au ubabaifu ndani yangu chonde chondee nisaidie huku kutoamini kwangu niweze kukushinda, ili niweze kufanikisha kumwokoa mwanangu dhidi ya pepo huyu mchafu, wa kifafa kuweza kumtoka wajameni.Nini Kiliendelea Mpendwa Soma  Biblia acha ubabaifu!

Hivyo hata wewe mpendwa ukipita wakati unaona kabiosa un-belief inaaanza kukula muombe Bwana Yesu akusaidie ku-overcome, The Un-Belief ufanikishe kiimani na kuvuka hapo. Mpendwa Youn need to spiritually address the un-belief in you first ili usipotezee! maana in no time utajikuta huna imani kabisa!.

Wapendwa mimi binafsi nikiona mtu hana imani namtemaa! kwa sababu ni suala la muda tu ataanza kunikausha imani yangu!! na imani ndiyo currency ya ulimwengu wa roho, Spiritual Transactions zotee zina angalia una imani kiasi gani, siwezi kukubali ani bankrupt spiritually.

Mimi mtu ambaye hajampokea Yesu hawezi kuwa close, Tutaongea nini? yaani atanikausha imani sio kwamba walokole tunapenda kubagua watu, tunalinda imani zetu maana tumezipata kwa gharama kubwa sana, kuwa dakika moja upo up there kwenye imani then dakika nyingine umerudia njia zako sio ajabuu!!!, Ni kama Crypto na Trading ya Faith!.

Mimi napenda nikae na watu walio-okoka kuliko mimi ambao wana manifestation kubwa sana, wana encounter kubwa zaidi wana mmulika Mungu kwa jicho kubwa zaidi la kiroho.

It challenges me and inspires me to seek God more, Nikiona Mungu kamtetea au kajithibitisha kwake kwa ukubwa naina kabisa my time is comming! Naona kabisa haya mambo yanawezekana mimi nafeli wapi?? Wewe unajiona kufunga saba (7) umetishaa unakutana na watu wanfunga arobaini (40) lazima utaona unajiaibisha usogee thelathini (30).

Lakini ukikaa na mijitu isiyofunga utaona umemaliza in the kingdom of blind, One eyed man is the king!, Mungu mwenyewe alimwambia Ibrahim ondoka uende nchi ya mbali kabisa na ukoo wa baba yake wapagani kabisa wale, alafu wewe you dwell among pagans mpaka na wewe umekuwa mpangani uliye changamka, lako lao na lao lako.

Of recent nimekutana na mdada anapess ndefuu, she is very popular, nikajua tu she musty have nasty attitude, It comes with money!. Lakini wapendwa yuko tofauti, unaweza sema ni malaika nini!!, She is muslim!! ana swali swala tano (5), yaani she doesn’t look down on anyone, anakutia moyo anaongea vizuri yaani mpaka unabakia unajiuliza ni huyu huyu nyamihela?? maana unaweza kujikuta  unahisi ndiyo unaela ana kuactia!!

Basi mwenyewe muda wote anawahimiza kusali na kumuomba Mungu inshallah kama zote!, kila kitu akiongea lazima amtukuze Mungu, kidogo lazima amshukuru Mungu mpaka unajua huyu yupo na Mungu 24/7. Wapendwa watu kama hawa ndiyo wakuchangamana nao wanakuchallange kiimani, na Mungu amewabariki na mumewe sio kidogo.

Sasa wewe kutwa kuketi vibarazani na wenye mizaha, Page unazo follow za ku-bully watu na kuwaombea watu wafilisike na kushuka chini kimaisha ndiyo yako, watu wadhalilishwe, sasa kwa mazingira hayo imani yako imani itakua saa ngapi?

Unakaa na washirikina kutwa kucha kuchoma udi na uvumba, story zao waganga na urogii, nakwambia ni suala la muda tu lazima na wewe ukashike manyanga kwa sangoma!.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top